*_______________________________________*
*SEHEMU YA KUMI NA MOJA*
Hali iligeuka kuwa nyingine kabisa, badala ya kutatua kesi kuhusu tope walijikuta wakibadilishana mate, romance yenye nguvu ya kupindukia iliibuka kati yao
Kama utani hivi lakini walianza kupunguziana nguo wakiwa sebuleni.
Dakika mbili hazikupita walijikuta wakiwa uchi.
Mguu mmoja wa Jamila ulishikiliwa kisha kazi ikaanza kufanyika.
Ilikuwa ni kama ndoto kwa mrembo huyu. Ni muda mrefu sasa umepita lakini hatimaye leo imekuwa.... hakuwa mzembe hata kidogo aliamua kuonesha kile alichojaliwa.
Sebule iligeuka uwanja wa burudani,
"Ahsante Jamila..." Chris aliongea
Jamila alionekana kutekewa hakuamini kama kaliwa sebuleni. Kuna namna alipoa ghafla.
Chris alilitambua hili alimnyanyua kisha akambeba.
Alimpeleka bafuni kwake akaanza kumuogesha
"Moyo wangu umevunjika tu ghafla, japo nimefurahia kitu tulichokuwa tunafanya wote lakini kuna namna nahisi huu ndio mwisho wetu...." Jamila aliongea ya moyoni
"Una maanisha nini kusema hivyo?...najua una hofia kuhusu Dorin lakini huyo ni Mshikaji wangu tu....kadiri siku zinavyoenda nina uhakika utaamini hiki nachokuambia" Chris aliongea
Jamila hakujua aongee nini.... alijikuta akimkumbuka Chris si kwa sababu anapenda ni kama alikuwa anabembeleza asije kutemwa
Isingekuwa rahisi kwake kulala hapa kisha amuache mdogo wake Ali.
Japo muda ulikuwa umeenda lakini Chris alimrejesha nyumbani. Na siku ya leo alivaa nguo za Chris pia.
Kuna namna aliona aibu baada ya kukutana macho na Ali.
"Sijafanya chochote kibaya kwanini unaniangalia hivyo...." Jamila alijihami
"Tisheti uliyovaa ni ya gharama sana....hicho tu ndio nilikuwa naangalia na si kingine" Ali aliongea kisha akajifunika shuka
Jamila alikaa kwa kujitupa kuonesha amechoka, siku ya leo Ali alikaanga karanga nyingi alijikuta akisikia uvivu kuzifunga
"Tangu ukutane na huyo Daktari umeanza kujiona tajiri...juzi ulifunga karanga katika kipimo kikubwa ukauza kwa mia tano. Leo nahisi utafunga mifuko mitatu tu uuze kwa elfu tano...." Ali aliongea akiwa ana mchungulia Dada yake kupitia kitundu kilichopo kwenye shuka
"Hizi mbona zina fungwa zote tena kwa ustadi mkubwa tu" Jamila aliongea yeye kama yeye ila mwili wake ulikuwa umechoka.
Aliishia kufunga karanga tatu usingizi ukapita naye.
"Sijui ni kitu gani umefanya ila inaonekana umechoka sana..." Ali aliongea pekee yake kisha akamfunika shuka Dada yake.
Alikaa chini akaanza kufunga karanga mwenyewe, zilikuwa nyingi lakini alipambana mpaka akamaliza.
"Huyu mtu kafanya kazi gani leo!" Ali alijiuliza kwa mara nyingine tena baada ya Jamila kuachia mashuzi ya kichovu.
Upande wa Chris alijikunyata kwenye blanket lake. Kila alipo kumbuka namna Jamila alivyokuwa anampandisha juu ya mawingu kwa kutumia kiuno chake alichanganyikiwa. Alijikuta akitamani show irudiwe tena.
Kulivyo pambazuka asubuhi alipigiwa simu ya dharula. Alikuwa radhi kwenda kazini bila kuoga lakini si kumuacha mgonjwa aendelee kuchungulia tundu la kifo.
Hakuwa na habari kuhusu Jamila, alipita gengeni kwake akiwa katika kasi ya 4G.
"Bila shaka kuna dharula kazini kwake...." Jamila alijisemea kisha akaifuta lipstick aliyokuwa ameipaka mdomoni mwake kwa lengo la Chris kuiona.
Kazi iliyokuwa mbele ya Chris ilikuwa ngumu.
Uhakika wa mgonjwa anayeenda kumfanyia upasuaji kuishi ulikuwa ni mdogo sana.
"Kwanini umekuwa na uoga ghafla.... Chris naye mfahamu Mimi hajawahi kuwa na uoga wowote linapokuja swala la kufanya operation yoyote ile, hakikisha unaokoa maisha ya huyo Mtoto..." Dorin aliongea kisha akaondoka
Chris alijishika mikono yake, hakuamini kabisa kama siku ya leo anatetemeka.
Kabla ya kuingia kwenye chumba cha operation alipanda gari lake akaenda gengeni kwa Jamila.
Jamila akiwa ana kusanya virago vyake asepe baada ya karanga kuisha ana shangaa baada ya kuliona gari la Chris
Chris alimfungulia mlango wa gari kumaanisha anataka wafanye mazungumzo.
Jamila alishangaa baada ya kuona Mwanaume huyu ana tetemeka mikono.
Japo si mjuzi sana wa mambo lakini alielewa mtu huyu ana kabiliwa na operation ngumu.
Alimkumbatia kwa hisia zote
"Kama utafanya vibaya nitaamini uwepo wangu maishani mwako ni mkosi.... naomba ujitahidi ufanye vizuri" Jamila aliongea kwa sauti ya kunong'ona iliyopenya vyema kabisa masikioni mwa Chris
*SEHEMU YA KUMI NA MBILI*
"Sawa nitajitahidi kufanya vizuri zaidi" Chris aliongea kisha akaondoa gari baada ya kipenzi cha moyo wake kushuka
Jamila aliishia kukodoa macho, hakuamini kama Chris anaweza kuja kwake kutiwa nguvu kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji
"Sijui hata ni maneno gani nimemuambia lakini naamini yalikuwa na nguvu..." Jamila aliongea kisha akaanza safari ya kuelekea nyumbani
Chris akiwa katika chumba cha Operation aliwekeza akili yake katika kichwa cha mtoto mdogo aliyekuwa na uvimbe.
Maneno ya Jamila yalizidi kujirudia kichwani mwake pale alipohisi kukata tamaa.
Alitumia saa moja kukamilisha hii kazi, kijasho kilimtoka na hata hakuelewa shida ni nini.
Wakati anatoka kwenye chumba cha Operation alikutana na Dorin
"Usiniambie ulikuwa unanisubiria..." Chris aliuliza huku akipokea maji anayopatiwa
"Nisingeweza kufuata ratiba zangu bila kujua hatima yako.... muonekano wa macho yako unatosha kuniambia umefanya vizuri" Dorin aliongea
"Ni mapema sana kujipongeza, acha nisubirie masaa mawili yapite...." Chris aliongea
Dorin alikubaliana naye, kwa pamoja walikaa katika benchi wakawa wanapiga stori huku wakisubiria masaa mawili yapite.
Upande wa Jamila alihitaji kujua kama Chris kafanya vizuri.
Aliingia bafuni akaoga baada ya kumaliza alitafuta nguo aliyoamini itamtoa vizuri kuliko zote.
"Vipi unaenda kwenye harusi....." Ali alimuuliza Dada yake
"Naenda hospitali kuonana na Chris, nafarijika kusikia nimependeza kama naenda harusini" Jamila aliongea
"Kila mtu utakayepishana naye atakushangaa si kwa sababu umetisha sana lakini watajiuliza unaenda kwenye harusi ya nani muda huu. Ingawa Mimi si mwanamitindo lakini naweza kusema sehemu unayoenda haiendani na hizo nguo" Ali aliongea kisha akaendelea kuchonga kinyago chake
"Kwahiyo nivae nguo gani...." Jamila aliuliza
"Vaa tu kawaida....hata hayo mapambo uliyoweka usoni mwako yafute. Hospitali ni sehemu yenye huzuni kwa asilimja kubwa. Utaonekana kichaa endapo utakuwa katika muonekano wa kula ubwabwa" Ali aliongea
Jamila alizingatia ushauri, alirudi ndani akabadili nguo zake.
Ali aliachia tabasamu kwa mavazi aliyovaa Dada yake kwa mara ya pili.
"Safari njema, umeonekana kama wa kishua hivi..."
Jamila alishtuka kwa sifa aliyopatiwa, alimuachia mdogo wake shilingi 2000 kisha akaendelea na safari yake.
Anafika hospitali akiwa hajui anaanzia wapi kumpata Chris. Anajilaumu ndani ya moyo wake kwanini hana namba za Chris mpaka sasa..... alianza kupita huku na kule akiamini ataonekana machoni kwa Chris.
Bahati nzuri au mbaya Dorin alikuwa wa kwanza kumuona. Hakutaku Chris amuone binti huyu
"Tumekaa sana hapa hadi nasikia kuchoka....twende ofisini kwangu. Tuna kama nusu saa ya kusubiria majibu ya Operation iliyofanyika" Dorin aliongea
Chris hakuwa na shaka, kwa pamoja waliongozana.
Jamila anafanikiwa kumuona Chris akiwa Dorin, kwa namna walivyokuwa wanatembea kwa kushikana mikono aligundua wawili hawa wanaelewana vizuri.
Hakuona sababu ya kuwaingilia aliondoka.
Baada ya Dorin kufika ofisini kwake alijitia ana dharula, lengo lake lilikuwa ni kuzungumza na Mlinzi wa getini na si kingine
"Hii ni hospitali kubwa nitafurahi kama utaweka mipaka kuhusu watu wanaoingia na kutoka. Endapo mtu hatakuwa na sababu maalumu inayomleta hapa naomba asiingie, huu ujumbe hauishii tu kwako nitawafikishia Walinzi wote" Dorin aliongea kisha akaondoka, mbali na kuwa Daktari bingwa wa mifupa ni Mjukuu wa Mmiliki wa hii hospitali.
Operation ya Chris ilienda vizuri, alijikuta akimbusu Dorin kwenye paji la uso sababu ya furaha.
Dorin alitekewa kabisa, hakutarajia kama Mwanaume huyu anaweza kumbusu.
Upande wa Jamila alirudi nyumbani akiwa hajielewi kama ana furaha au huzuni
"Mbwa mie ni kitu gani kilinipeleka hospitali...." Jamila alijisemea huku akiingia ndani. Kitu alichokutana nacho kilishtua moyo wake kupita kiasi
Itaendelea π₯
Full 1000
Whatsp 0784468229.