Mama mkwe akaniuliza ivi ni kweli wewe ni mchumba wake??
Mimi nikajikoolesha makusudi ili nisijibu lile swari nikawa kama nimejipalia ivi basi mama mkwe akasema pole pole nani anakutaja tena jamani dah.
Mimi tena nikaona tayari kashaingia king kama najipalia nikajishika mpaka kifua.
Chizi akaenda kuchukua maji akanipa kwenye kikombe uku anasema dear dear dear kunywa maji.
Nikachukua yale maji nikanywa chizi chizi tu akawa ananishika kifua mbele ya mama yake anasema hapa ndio panauma dear dear dear.
Mama mtu akaona makubwa haya akaingia ndani.
Chizi akaingia na mimi chumbani kwake.
Sasa mimi dah kuondoka nataka ila chizi nampenda sana na hii mimba ilinifanya nimpende zaidi nafanyaje swali najiuliza chizi ana kero ata kidogo kwenye mapenzi fundi na mahaba kama yote.
Chizi akatoka nje akachukua mihogo niliopika akamwita mama yake akamwambia mama kula chakura kapika dear dear dear wangu mimi.
Uku anajipiga piga kifuani yani anamaanisha au kwa lugha nyengine anaonyesha ishara ya msisitizo.
Mama yake akasema kimoyoni ivi kweli uyu binti ni mchumba wa mwanangu mbona makubwa kama kweli si itakuwa maajabu ya dunia aya bint mzuri kama uyu alafu sura yake sio ngeni nilimuona mjini au ndio dunia wawili wawili.
******************
Upande wa kisimani kukaanza zogo wanasema jamani uyu sio chizi wengine wanasema uyu chizi.
Mama mmoja akasema jamani Sisi ndio machizi sio yule.
Watu wakapaniki sasa wanaume wakaanza wewe mama tunakuheshimu kitendo cha kutuita Sisi machizi atukipendi sawa amani itavulugika hapa mbele ya mwenyekiti wa kijiji.
Mama yule akasema ivulugike tu yani munavyokasilika ndio mnazidi kuwa machizi.
Wanaume walitaka wamkamate yule mama wampige wagambo wakawazuia wakasema tulieni tumsikilize anamaanisha nini yeye kusema Sisi machizi na point yake IPO wapi.
Mama yule akasema kwanza kumbe neno chizi linakera kwanini mnalitumia kumwita yule kijana pili nyinyi mmekaa miaka mingapi hapa kijijini amjafikilia ata siku moja kuweka mfuniko kisima chetu tatu alichosema hapa cha kukataza wanawake kuoga kisimani mbona yeye kaongea mbele ya mwenyekiti nyinyi mnaongea pembeni nani chizi kati anaongea pasipo kuogopa na nyinyi mnaogopa.
mjumbe akasema mama basi inatosha ushaheleweka unachomaanisha kuwa yule kijana asiitwe chizi ilo limepita yule sasa babu yake yupo hapa ata sema tumwitaje.
Babu akasema kwanza nyinyi vijana mmekosa adabu tu mnamwita mjukuu wangu chizi mjukuu wangu ana miliki mwanamke mzuri kuliko wote hapa kijijini si mwenyekiti si mjumbe wote wanawake wenu wabaya mjukuu ana chombo kikari hahahahahaha.
Mjumbe akasema kweli yule kijana mzima machizi tunao sasa uyu mzee anaambiwa ataje jina la mjukuu wake yeye anakashifu wake zetu sasa kama si uchizi ni nini.
Mala chizi anakwenda kumwita babu kumwambia kuwa mama mkwe wangu kafika.
Alipofika pale akasema amjaondoka tu sasa sababu wote mupo hapa tufyekeni ichi kichaka chote kuwa kweupe tuone kama kuna mtu atakuja kuoga hapa aya tena tuanzeni kazi sio muda wa kuangaliana usoni.
Walipofyeka kichaka waliona kondom kibao chizi akacheka sana akasema mwanamke kweli achungungiki yani izi kondom wanaliwa wake za watu tusimung'unye mung'unye maneno akuna mtoto nasema wewe mwanaume unayekuja kumfanya mke wa mtu kisimani umekuwa auna tofauti na mchawi yani sehemu hii ndio tunachota maji ya kunywa wewe unakuja kufanya hapa ukimaliza lazima ushike nanii lako ujifute au ufutwe na uchafu wenu mnakuja kushika kopo hili linaingia kisimani amuwoni kama mulikuwa mnawanywesha watu uchafu.
Sasa nasema mwisho wa kuchota maji saa 12 jioni na funguo nipeni mukinikosa mimi nyumbani mtamkuta dear dear dear wangu atawapa wale wa asubuhi tu usiku akuna kuchota maji hapa nani anapinga aseme hapa nasema nani anapinga.
Wote kimya na wamebaki na mshangao tu wa neno dear dear dear.
Upande wa nyumbani wazazi wangu walikuja wakaonana na mama chizi wakasema waniite niseme ukweli kuwa chizi ni mchumba wangu au vipi.
Mama akaniita yani.....
ITAENDELEA
KWETU morogoro.