Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

DADA POA WA USIKU MMOJA _______________________________________ SEHEMU 01

7th Jul, 2025 Views 38

SIMULIZI :

MWANZO.......
Taarifa za kifo cha rafiki yake zilimshtua sana Osman, CEO wa Kampuni la DreamCloud linalo jishughulisha na uuzaji wa magodoro kama super Banco na memory foam.

"Ni jana tu nimezungumza naye kuhusu harusi yangu sijui unanisoma..." Osman alizungumza huku akimkunja shati bodyguard wake kana kwamba yeye ndio Malaika mtoa roho.

"Naelewa Boss, naomba utulize kichwa chako kila kitu kitaenda sawa" Asha alizungumza huku moyo wake ukivunjika kwa maumivu...siku zote hapendi kumuona Boss wake akipitia changamoto yoyote ile.

Katika moyo wake ana mtazama Osman kama Mwanaume anayetikisa hisia zake na si kama Boss wake.
Alijitahidi kumtuliza Osman mpaka akafanikiwa.

"Andaa tiketi, tutampeleka Boss nje ya Mji akapumzishe akili yake baada ya mazishi...". Asha alimuambia Victor (bodyguard mwingine) kwa njia ya simu.

"Hatuwezi kufanya hivyo, wiki ijayo ni harusi yake.... naomba unielekeze sehemu ulipo nataka kuja" Victor alifoka mara nyingi yeye na Asha huwa hawapatani linapokuja swala la kufanya maamuzi.

Asha hakuona sababu ya kuendelea kuzungumza na Victor alikata simu aliamini kwa vyovyote vile ni lazima mawazo yake yatafuatwa.

Kulivyo pambazuka alimuamsha Osman.

"Siku ya leo rafiki yako kipenzi ana pumzishwa naomba ujipige kifua twende...."

"Naelewa....lazima niende hata kama ni kwa kutambaa" Osman alizungumza huku akijaribu kusimama.
Mwili wake haukuwa na nguvu hata kidogo....
Asha alimkokota mpaka kwenye gari.

"Nimemuambia Victor aendae tiketi baada ya mazishi kumalizika tutaenda Jijini Dodoma... nahitaji upumzishe ubongo wako" Asha alizungumza.
Osman hakujibu chochote....

Mazishi yalifanyika watu walilia na kuomboleza....Asha alijitahidi sana kumficha Osman hakutaka watu wamkaribie hivyo msiba ulivyomalizika tu walielekea moja kwa moja uwanja wa ndege.

Asha anaachia tabasamu baada ya kumuona Victor, walimuingiza Osman ndani ya ndege.

Asha alimvalisha earphones masikioni kisha akamuwashia mziki.

"Ni mziki unaoupenda sana.... naomba u relax" Asha aliongea kisha akaenda kukaa nyuma na Victor.

Osman aliongeza sauti kisha akafumba macho, ni wazi kabisa mziki ulimkolea

🎵Mmm-mmm

I remember, years ago
Someone told me I should take
Caution when it comes to love, I did
And you were strong and I was not
My illusion, my mistake
I was careless, I forgot, I did🎵

"Hilda anataka kuzungumza na Mumewe mtarajiwa, kwanini simu ya Boss umeizima umekuwa nani wewe hadi unaipakata mikononi mwako!....ukiachilia mbali na Hilda, Mama yake mzazi anataka kuzungumza na mwanae" Victor alifoka.

"Kwa sasa furaha ya CEO ndio kipaumbele nipo tayari kukatwa kidole changu pindi tutakapo rejea Mwanza, kwa wakati huu naomba uniache nifanye nachotaka" Asha aliongea.

Victor hakuwa na namna aliweka earphones masikioni mwake akaanza kusikiliza mziki pia.

Asha alijikuta akiogopa zaidi baada ya kumkumbuka Sabrina (Mama yake Victor). Amenusurika kukatwa vidole mara nyingi sababu ya kufanya maamuzi bila kuuliza.
Kwa wakati huu ana uhakika atakatwa vidole vyote....lakini kwa ajili ya Osman hana budi kuvumilia.

Sabrina akiwa nyumbani kwake alionekana kukasirika sana kwa sababu namba za Osman hazikuwa zikipatikana.

"Hii ni kazi ya Asha, sielewi amekuwa nani mpaka anafikia hatua ya kuingilia mambo ya familia yangu...... naomba unitafutie mnoa visu maarufu hapa Mwanza, nataka aniandalie kisu kwa ajili ya Asha pindi atakaporejea nitaondoka na vidole vyake vyote..." Sabrina alitoa agizo kwa Dada wa kazi.

"Naomba harusi tuisogeze mbele sina uhakika kama Osman atarejea kwa wakati" Hilda alizungumza.

"Hakuna kitu kama hicho, awepo asiwepo harusi itafungika.... Mimi Mama yake nitalisimamia hilo swala" Sabrina aliongea.

"Mkwe...." Hilda aliita kwa mshangao.

"Na kumbuka siku ya harusi yangu Baba yake Osman alipata dharula ya ghafla.... harusi ilifanyika bila uwepo wake hivyo sitavunja ratiba yangu lakini katika hili lazima Asha apoteze vidole vyake" Sabrina alizungumza.

Hilda hakuongea chochote moyo wake uliingia shauku kubwa ya kumuona Asha, anaonekana kutopendezwa na matendo yake.

Ndani Ya Jiji La Dodoma
Osman alifikia kwenye hotel ya kifahari iliyojulikana kama 20 percentage akiwa na Walinzi wake.

Muda wote Asha alikuwa karibu yake akihofia huenda akajirusha afe kwa sababu mtu aliyepoteza maisha alikuwa zaidi ya rafiki kwake.

"Siwezi kujirusha kuwa na amani....kwanini tusishuke chini nataka kulewa" Osman alizungumza.

Asha alikubaliana na wazo la Boss wake, alimualika Victor kwa pamoja walianza kunywa pombe.

Asha alikuwa na mawazo mengi hivyo alilewa kupitiliza,, anampenda sana Osman lakini hawezi kueleza hisia zake kwani pindi atakapo fanya hivyo uhusiano wao utaharibika. Anabakia kula kwa macho

Osman hakuwa amelewa, baada ya kuona Walinzi wake wamelewa wote aliwatoroka.... alihitaji kuwa pekee yake na si kuzongwa zongwa.

Alitembea huku na kule.....kwa bahati mbaya alipita maeneo ya biashara za watu
Wadada warembo wenye uhitaji wa pesa walikuwa wakijiuza.

Isingekuwa rahisi kwa Osman kuvumilia kuwatazama alianza kurudi nyuma taratibu
Ghafla bin vuu aligongana na binti mrembo aliyekuwa kavaa nusu uchi.

"Huwezi kuondoka kirahisi namna hii bila kunipatia pesa....hivyo utake usitake tutaondoka wote" Anjeli (Dada poa) alizungumza.

Uzuri wake ulikuwa hauelezeki....Osman alibaki kumshangaa kwa sekunde kadhaa hakutaka kufikiria mara mbili mbili alimshika mkono wakaondoka. Aliamini mtu huyu atampunguzia mawazo yanayo msumbua kichwani mwake....

Lengo la Osman lilikuwa ni moja tu kufanya ngono na Anjeli.
Pesa haikuwa tatizo kwake.....vitu vyote alivyokuwa kavaa mwilini mwake vilikuwa vya gharama.

Baada ya kuchoka walilala, Anjeli aliingiwa na wazo la wizi aliiba vitu vyote vya Osman ikiwemo boksa pamoja na pesa.

Osman anaamka asubuhi akiwa kachoka, alishtuka kujiona yupo tupu.
Bahati nzuri mezani kulikuwa na simu aliandika namba ya Asha akampigia....

Asha alichanganyikiwa baada ya kugundua Boss wake yupo matatizoni. Alichukua pesa na nguo kisha akaelekea sehemu aliyoelekezwa.

"vaa nguo, naenda kumtafuta mtu aliyekutendea hivi..." Asha aliongea akiwa katega mgongo.

"Hapana usihangaike naye nisubirie hapo nje ..."

Baada ya kumaliza kuvaa waliondoka, Asha alitamani kujua nini kinaendelea lakini Osman hakumpa nafasi.
Wakiwa wanatembea, Osman alimshuhudia Anjeli akiuza nguo zake tena kwa bei ya hasara.
Kwa namna alivyokuwa kavaa nguo za heshima huwezi kudhania kama ndio yule aliyekuwa kavaa nusu uchi usiku wa jana.

Osman alijikuta akisikia hasira kwa namna nguo zake zilivyokuwa zinapigwa mnada.

Alijipenyeza kwa watu mpaka akamfikia. Alimshika mkono kwa nguvu.
Anashangaa baada ya kuona watu wote wamemshikia mawe isipokuwa Asha.

"Acha kumshika huyo binti kwa nguvu namna hiyo.... Mtoto wa watu yupo anajitafutia riziki, kama umeipenda biashara yake nunua!....anatafuta kwa shida sana" Mmoja wa Raia alizungumza.

Osman ndio alipata picha kamili kuwa Anjeli anaonekana Malaika kwa watu hawa. Anaonekana kama mnyonge anaye hitaji kutetewa muda wote. Ni wa kabisa sifa yake ya kujiuza haijulikani kwa watu hawa...........

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA
*__________________________________*
SEHEMU 02

ENDELEA.......
"unaonekana kuwa Malaika kwa hawa watu,,, niuzie vitu vyangu kwa bei yoyote utakayo, sijisikii amani kuona unavi zagaza namna hiyo..." Osman alimuambia Anjeli kwa sauti ya chini.

"Sikutarajia kama tutakutana mazingira haya... naomba tusikutane tena kuhusu boksa yako ipo ghetoni kwangu nitamzawadia boyfriend wangu siku ya birthday yake" Anjeli alizungumza kwa dharau huku akimtazama Asha aliyekuwa kavimba kwa hasira.
Osman alilipia nguo zake kisha akampa Asha abebe waliondoka.

"usifikirie kumuua...." Osman alimtahadharisha Asha kwa sababu ana fahamu ukorofi wake.

Anjeli aliingia mtaani akaanza kutafuta vitu vya kupika. Ndani ya moyo wake hakuwa na majuto yoyote kuhusu uhuni aliomfanyia Osman.

Upande mwingine, harusi iliandaliwa bila uwepo wa Osman, aina hii harusi ilishazoeleka hivyo si rahisi kwa watu kuuliza maswali kuhusu Bwana harusi.

Sabrina alikabidhiwa kisu chake kilichonolewa kwa wiki nzima.

Alimkabidhi Hilda pindi Asha atakaporudi akamkate vidole vyote kwa kuondoka na Mumewe.

Hilda alikipokea kisu bila kuzungumza chochote sumu aliyoihifadhi ndani ya moyo wake ni kubwa sana.

Harusi ilipendeza japo Osman hakuwepo....Hilda aliitwa Mke wa mtu rasmi. Alikabidhiwa funguo za chumba cha Osman
Jukumu Iake lilikuwa ni moja kumsubiria Mumewe.

Upande mwingine Osman aliagiza tiketi ziandaliwe tayari kwa kurudi Mwanza
Haelewi nini kimempata kwani alijikuta akitamani kumuaga Anjeli ingawa hakujua atampatia wapi. Alitamani kuuliza kuhusu boksa yake....

Asha alikuwa kambana sana anaamua kupotezea...alikuwa ni Dada poa wa usiku mmoja hivyo aliamua kumpotezea.

Alianza kupiga stori za hapa na pale na Victor, Asha anaachia tabasamu ndani ya moyo wake baada ya kuona CEO karudi katika hali yake ya uchangamfu.

Biashara kwa Anjeli zilikuwa ngumu sana siyo mchana wala usiku.
Mwanzo watu walikuwa wananunua karanga zake sababu ya huruma tu lakini kwa sasa wameamua kumsusa kabisa kwa sababu kipimo anachoweka kilikuwa kidogo sana ukilinganisha na thamani ya pesa yake.

Anaamua kuongeza kipimo lakini bado Wateja hawakuwa na habari naye. Karanga za jirani yake zilikuwa na ladha nzuri kuliko za kwake.

Biashara yake ya kujiuza ilikuwa ni ngumu pia, wadada wapya kutoka Tanga walivamia chimbo lao. Ilikuwa ni ngumu kwa wenyeji kupata soko.
Anjeli alijikuta akipagawa zaidi,
moyo wake unamuambia boksa ya Osman imegeuka kuwa mkosi kwake.
Anatamani kumrudishia mmiliki lakini haelewi atampata wapi.

"Mji....nga yule laiti kama ningejua ni mtu wa mikosi namna ile hata nisingemuuzia K yangu....kuna watu ukitembea nao mambo hunyooka lakini huyu niliyekutana naye Mimi huenda alizaliwa siku ya mikosi duniani" Anjeli aliongea pekee yake.

Alitaka kuzitafuna karanga zote lakini baada ya kufikiria biashara inahitaji ubunifu alianza kupita kwa Wateja wake wa zamani.

"Nakopesha karanga....karibuni sana" Aliongea huku akiachia tabasamu.

Hakuna hata mteja mmoja aliyekuwa tayari kuchukua karanga zake.
Na hata alipotaka kuwapa kwa bure hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari.

Anarudi nyumbani kwake akiwa mwenye huzuni mkubwa. Alipanda kitandani kwake akajifunika shuka.gubi gubi.

Baada ya kupumzisha akili yake alishika kalamu na karatasi, ni bingwa wa kuchora, dakika 20 zilikuwa ni nyingi sura ya Osman ilionekana kwenye karatasi.

Alianza kupita kwenye maofisi makubwa pamoja na hoteli.

"Kaondoka siku ya jana na ndege.... kaelekea Jijini Mwanza" Mfanyakazi wa uwanja wa ndege alimuambia.

"Atarudi lini...." Anjeli alijikuta akiuliza swali la kipuuzi.

"Inaonekana siyo mkazi wa Jijini Dodoma, sijui nini kimetokea lakini pole kwa sababu Wanaume wengi ni sawa na paka anayepita tu kwenye bakuli lenye samaki. Wakimaliza kula shwaaa hutowokeka" Mfanyakazi wa ndege aliongea.

"Ni heri iwe shwaaa tu bila kuachiwa mikosi!...shwaa na mikosi inaumiza sana" Anjeli aliongea kisha akaondoka akiwa mnyonge.

Alionekana kuchoka mwili na roho
Hakuwa na pesa za kumfikisha Mwanza pamoja na kwamba alikuwa anafanya kazi usiku na mchana.

"Sikutarajia huyo mwanaume atakuwa ana kaa nje ya Dodoma, bila shaka alikuja kuosha mikosi yake kwangu...." Anjeli aliongea pekee yake akiwa hajui atende nini.

Upande mwingine, Osman pamoja na Walinzi wake walirejea nyumbani.
Asha alikuwa na hofu kubwa moyoni mwake... Victor alilijua hili alichekelea ndani ya moyo wake kwa sababu siku zote Asha hujifanya mjuaji sana.

Baada ya Sabrina kumuona Osman (Mtoto wake) aliachia tabasamu.

"Karibu ndani Mkeo ana kusubiria, kila kitu kilienda sawa namaanisha harusi"

Osman alishangaa sana hakutegemea kama Mama yake angefanya mambo kwa haraka namna hii..... ITAENDELEA..........
Soma mpaka mwisho kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0781858056.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

DADA POA WA USIKU MMOJA _______________________________________ SEHEMU 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/dada-poa-wa-usiku-mmoja-_______________________________________-sehemu-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
OFFER YAKO IPO KWETU KARIBU
OFFER YAKO IPO KWETU KARIBU

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA🙈3~4

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 11.

majario rewards 100 Comments 0
 

GIGY MONEY DAH😭

majario rewards 100 Comments 0
 

YOUNG AFRICANS,

majario rewards 100 Comments 0
 

BAKORA VILLAGE

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 7...8

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA EPISODE 2

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE...5...6

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 3...4

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA 1

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈21

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈20

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 8

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 7

majario rewards 100 Comments 0
 

Life in a Year (2020)

majario rewards 100 Comments 0
 

Kenya, Tanzania, Congo

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 40

majario rewards 100 Comments 0
 

POSHY QUEEN:

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 39

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈19

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈18

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈17

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈16

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈15

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 05 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 04 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 03 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 02 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 01 ❤❤.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 34

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TUWASHUKURU KINA BABA

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest