Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Nilianza kukimbia kuondoka kwenye lile eneo... Inaendelea... Sehemu Ya 13

31st Jul, 2025 Views 6



Nilitoka lile eneo na kuanza kutafuta barabara, Nilifanikiwa kutokezea hadi sehemu ya barabara niliendelea kukimbia sababu ile barabara ilikuwa haina watu wengi, Nilikimbia huku naogopa wale watekaji wasije wakanikamata na kulirudisha, Bahati nzuri nikapata mtu wa pikipiki nikamuomba lifti akanisogeza hadi kwenye kituo cha kupandia gari, Kwakuwa kuna namba nilikuwa nimezikalili kichwani nikaona nitafute simu ya kuazima ili nipate msaada mapema nikatafuta simu ya kuazima nikapa nikajaza namba ya sakina nikapiga simu kwa sakina lakini hakupatikana, Ikabidi niweke namba ya baba kama hatopatikana nimpigie tina maana nilikuwa nimekalilii namba za watu watatu, Nikajaza namba ya baba nikapiga bahati nzuri baba akapatikana nikaongea nae nikamwambia anitumie nauli kupitia ile namba ya kuazima akasema hata mimi nipo huku kwa dada yako tumekutafuta sana, lakini sawa nafanya mpango sasa hivi nakutumia,

Nilikaa muda kidogo kweli pesa ikawa imetumwa kwenye ile simu niliyoazima ikabidi tuelekee kwa wakala nikiwa na yule mwenye simu, Tukatoa pesa nikamshukuru sana yule aliyenisaidia simu, Lakini kabla sijaondoka nilimpigia baba na kumuelekeza sehemu nitakayo shukia lakini itakuwa mida ya usiku, Sababu kule nilipokuwa nimetekwa ilikuwa ni mbali na mjini. Nilisubiri mabasi madogo ambayo yanaenda hadi mjini hatimaye basi lilifika nikapanda safari hadi mjini, Nilishuka katika kituo kidogo cha mabasi niliwakuta familia yangu yote wakiwa wamenisubiri, Mama baba dada pamoja na mume wa dada ambaye ni shemeji yangu,

Niliposhuka kutoka ndani ya gari mama alinisogelea na kuanza kunishika mwili huku akisema mwanangu kumbe ni mzima mbona niliambiwa umekufa... Mama alilia kwa sauti ya juu hadi akaanguka chini na kuzimia, Tulianza kumpepea lakini hakuzinduka ikabidi tuchukuwe usafiri wa haraka tumpeleke hospitali ili akapate huduma ya kwanza, Tulifika hospitali madaktar walimpokea mama na kumuingiza katika chumba cha matibabu. Lakini wakati mama yupo kwenye chumba cha matibabu, Alitoka daktar mmoja na kwenda kumuita daktar mwenzie, na yule daktar alipoingia kwenye kile chumba ambacho mama amelazwa, na yeye alitoka na kwenda kumuita daktar ambaye ndio mkubwa wa pale hospitali, Yule daktar wa mwisho alitoka na kutuambia mgojwa wenu inaonekana presha (pressure) ilipanda kwa kasi sana na amefariki muda mrefu kabla hata hamjamfikisha hapa hospitali.😭

Dada aliposikia kwamba mama amefariki na yeye alizimia palepale ikabidi tuanze kumpepea, Hakika ilikuwa ni maumivu ambayo sikutegemea na sitoyasahau, Kiukweli niliumia sana tena sana, Nilianza kujiona mimi ndio chanzo cha kifo cha mama yangu nilianza kujilaumu kuwa na mahusiano na sakina hakika nililia mno nilihisi kama vile ninamkosi, Niliona sasa mikono yangu imeanza kulowa damu.😭😭😭

Dada alizinduka ikabidi apelekwe kwanza nyumbani kwake harafu sisi wengine tukaanza kushughulikia masuala ya mazishi, Kwakuwa mama alikuja ugeni pale nyumbani kwa dada, ikabidi tufanye mpango wa kuusafirisha mwili wa mama ili tukamzike kule kijijini kwetu,

Tukatafuta gari la kubeba mwili wa mama pamoja na watu wengine ambao watatusindikiza msibani, Tukafanikiwa kupata gari lakini gharama ya usafirishaji ilikuwa ni milioni moja, Wakati huo mimi sina hata shilingi, Kiukweli nilikuwa naumia sana moyoni mwangu yani maisha na kila nilichofanya katika maisha yangu nilianza kuona hakuna kitu cha maana hata kimoja.

(Lakini wakati nahangaika na msiba wa mama tarehe za tina kuhitimu ndio zilikuwa zimefika)

Kwakuwa mimi sikuwa na pesa harafu pia ndio nimetoka kwenye matatizo ya kutekwa, Yule shemeji yangu ikabidi atafute mtu wa kuja kutudhamini ili atulipie pesa ya nauli harafu sisi kama wanaukoo tukimaliza mazishi tuchange ile pesa na tumrudishie mwenyewe, Mungu akawa ametusaidia akapatikana wa kuja kutulipia nauli, Kisha siku inayofuata tukaanza safari ya kwenda kijijini kwa ajili ya msiba.

Wakati huo wanakijiji na ndugu tayari tumeshawapatia taarifa za msiba, inamaana kule kijijini kwetu tayari watu wamekusanyikana kwa ajili ya kuja kuzika, Lakini pia watu wengi pale kijijini walikuwa wanajuwa mimi nina pesa kwahiyo watu walijaa wakiamini mtoto wa marehemu ni tajiri,

Tulipofika pale kijijini kwetu kila mtu alinishangaa kwanza nimekonda harafu hakuna ule mwonekano wangu wa kitajiri wala hakuna msafara wa magari ambayo watu walitegemea kuyaona, Tulifanya mazishi na tukamaliza, Kisha wanandugu wote tukakaa kikao kwa ajili ya kupata mchango wa kumlipa yule aliyetudhamini hadi tukapata usafiri, Lakini wanandugu na wanaukoo wote walikataa kuchanga pesa ya usafiri, Wakasema mimi kama mtoto kwa sababu nina pesa inabidi nilipe mwenyewe lile deni, Nilianza kulia na kujitetea kwamba mimi sina pesa nilipiga hadi magoti mbele yao na kuwaomba msamaha kama nilishawahi kuwakosea wanisamehe, Lakini hakuna aliyenielewa, Matokeo yake walianza kusambaa mmoja baada ya mwingine.

Baada ya ndugu kugoma kuchangia pesa ya usafiri ilibidi baba akate sehemu ya shamba na kuliuza ili tupate pesa ya kulipa kwenye usafiri, Mteja alipatika tukauza na kulipa kwa yule aliyetudhamini. Wakati huo mimi dada na baba ilibidi tubaki kwanza pale nyumbani kwa ajili ya maombolezo, Lakini Mawazo yalianza kunitesa nikafikia hatua hata kula sili harafu nikiangalia nimepoteza kila kitu Dah nilikuwa naumia sana, Sababu nilikuwa najaribu kutafakari ni nini nimefanya kwenye maisha yangu nakosa, Nikiangalia tina sipo nae, sakina sipo nae, pesa pia sina mbaya zaidi nimesababisha hadi mama yangu akafariki, Nilihisi sina sababu ya kuendelea kuishi,

Siku moja mida ya mchana nilienda nikanunua sumu ya kuulia wadudu kisha nikaiweka ndani mwangu mule ninamolala, Ilipofika mida ya jioni tulikaa mezani Mimi Baba Dada na kupata chakula cha usiku, Hakika nilionekana kama vile nimeshasahau yaliyopita tulimaliza kula kila mtu akaingia kulala, Nililala hadi ilipofika usiku wa manane nikaona sasa pametulia na hakuna mtu atakayesikia maumivu yangu,

Niliona sina sababu ya kuendelea kuishi, kwani nimeshakata tamaa ya kila kitu, Nilichukuwa ile sumu ya kuulia wadudu na kuishika mkononi mwangu...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Nilianza kukimbia kuondoka kwenye lile eneo... Inaendelea... Sehemu Ya 13  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-nilianza-kukimbia-kuondoka-kwenye-lile-eneo-inaendelea-sehemu-ya-13
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest