Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Siri Ya Mvuvi Na Bahari lakini huo ulikuwa ni mpango wa wizi... Inaendelea... Sehemu Ya 02

31st Jul, 2025 Views



...wakatupatia na sisi kama tulivyoelewa asubuh sisi tulitafuta mteja na kuuza wale samaki kisha tukapata pesa, tukaendelea na ulinzi tukamaliza mwenzi mmoja bila shida wala hasara, tukauanza mwezi unaofuata ambao ni mwezi wa pili tukiwa kazini, wale jamaa ambao tulifanyanao dili mara ya kwanza wakawa wamekuja tena, kwakuwa mara ya kwanza tulifanyanao dili na mambo yakaenda vizuri, wakaja tena kwa mara ya pili kuja kuchukuwa mitumbwi ili wakavue samaki, tukawauliza kuhusu hali ya hewa wakasema wao ni wataalamu na wazoefu wa baharini, tukawapa mitumbwi miwili kama kawaida na malipo ni baada ya wao kutoka baharini,

Wale jamaa waliingia baharini, lakini tulisubiri hadi ule muda ambao walipaswa wawe wamerudi lakini wakawa bado. Muda ukaenda hadi tukaanza kuwa na wasiwasi mbona masaa yanazidi na hawaonekani, baada ya muda wale jamaa walirudi kutoka baharini wakiwa hawana samaki hata mmoja, sisi tukahisi huwenda wametuchezea mchezo lakini wao wakasema ni hali ya kawaida ya bahari,sasabu kuna wakati unakuta bahari haijatulia hivyo inakuwa ni vigumu kupata samaki, tukawaambia kama ni hivyo basi muache kuwa mnakuja kuchukuwa mitumbwi sababu kutakuwa hakuna faida, harafu wenye mitumbwi wakigundua kwamba mitumbwi yao huwa inapelekwa baharini bila ruhusa yao itaonekana sisi ni wezi na hatuna uaminifu na tunaweza tukafukuzwa kazi,kama samaki hampati basi msiwe mnakuja kwetu. Wale jamaa wakasema kwakuwa samaki tumekosa lakini msijali tutawaletea pesa yenu, sababu tulikuwa kwenye makubaliano.

Asubuh palikucha salama lakini muda mwingi wa asubuh nilikuwa nautumia kulala sababu usiku kucha nilikuwa kazini, badae nikapata muda nikakutana na Latifa, nikamchukua kisha tukaelekea katika fukwe ya bahari. Mkoa wa pwani ni mkoa ambao unapatikana nchini Tanzania na umepakana upande wa kaskazini na mkoa wa Tanga,Dar-es-Salaam pamoja na Bahari ya Hindi. Mazingira ya fukwe ya bahari yalikuwa ni mazuri sana, lakini wakati tunatembea, Latifa aliniuliza nasikiaga huku kwenye fukwe ya bahari huwa kuna majini" nilicheka na kumwambia hapana hizo ni story za kutungwa wala hakuna ukweli kama huo" Latifa akaniuliza,tena nasikia umepata kazi kwa nini hukuniambia harafu kazi yenyewe ni ya usiku" nikamwambia hapa kwenye mji wetu imekuwa ni vigumu kupata kazi labda uwe mvuvi"

Tuliongea mengi na Latifa,lakini nilipoona muda umekwenda ikabidi nimsindikize Latifa hadi kwao kisha mimi nikaenda zangu nyumbani,kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini, baada ya muda nikawa tayari nipo kazini nikiwa na rafiki yangu Riziki, lakini ilipofika mida ya usiku wale jamaa zetu ambao mara ya mwisho tuliwapatia mitumbwi lakini hawakupata samaki, wale jamaa wakaja tena,na walikuja na pesa ya malipo waliyotuahidi hapo awali, wakatupatia kiasi cha pesa ambacho tulikubaliana mwanzo. lakini wakasema wanahitaji tena mitumbwi mitatu sababu walikuja wakiwa wameongezeka wawili inamaana kwamba walikuja wakiwa sita, kwahiyo kila mtumbwi watapanda wawili wawili, tukajiuliza na rafiki yangu tuwapatie mitumbwi au tusiwapatie, lakini tukaona kwakuwa hawa jamaa ni waaminifu na mara ya kwanza tumefanyanao kazi lakini wameleta pesa yetu, ikabidi tuwapatie mitumbwi mitatu lakini siku hiyo hali ya hewa haikuwa sawa,

Tukawapatia mitumbwi mitatu,ukiwemo na ule mtumbwi ambao ulipotea ghafla na kurudi ghafla, wale jamaa wakaingia baharini. Tuliwasubiri muda mrefu lakini hawakuonekana hadi tukaanza kuwa na wasiwasi sababu tukaona muda unazidi kwenda,harafu wavuvi wa ile mitumbwi huwa wanakuja asubuh sana na kuchukuwa mitumbwi yao kisha wanaingia baharini kwenda kuvua samaki.

Baada ya muda mrefu wale jamaa walirudi wakiwa na samaki wa kutosha, lakini mtumbwi mmoja hawana, tukawauliza mtumbwi mmeuacha wapi" wakasema wakati wanavua samaki ghafla hali ya hewa ya bahari ilianza kuwa mbaya na kupelekea ule mtumbwi kujaa maji, wakatuambia kwamba,kwakuwa walikuwa karibu na wenzao hivyo wakalazimika kuwaokoa wenzao na kuuacha mtumbwi hadi ukapotea, (Dah lakini mtumbwi ndio umeshapotea) tukaanza kupigizana makelele mwisho wale jamaa wakaondoka bila kutuachia chochote na mtumbwi mmoja wameupoteza, lakini mtumbwi uliopotea ni uleule ambao ulipotea na mara ya kwanza. tukajaribu kuutafuta maeneo yale lakini hatukuupata, ikabidi tusubiri vyovyote itakavyokuwa,

Baada ya wale jamaa kuondoka walikuja wale wenye mitumbwi yao ambao tunawalindia, kwakuwa tumepoteza mtumbwi mmoja yule mwenye ule mtumbwi uliopotea akasema kwakuwa tumepoteza mtumbwi wake inabidi tumlipe. Na kazi tukafukuzwa lakini tukaambiwa hakuna kusafiri na kutoka nje ya mji,hadi pale tutakapokuwa tumemaliza kulipa deni la ule mtumbwi uliopotea, tukaambiwa kila mmoja atalipa nusu ya gharama inayohitajika, ikabidi niongee na Riziki kama ana pesa ya akiba ili tufanye mpango wa kulipa pesa tuliyoambiwa, lakini Riziki akasema yeye hana pesa hata kidogo,

Mama alipopata taarifa akasema kwamba atatulipia lakini nikamwambia mama acha tutalipa wenyewe, mimi nilikuwa na akiba kidogo ya pesa ambayo nilikuwa na malengo ya kuiweka ili nikamilishe pesa ya mahari kwa ajili ya kumuoa Latifa, lakini nikaona siwezi nikabeba majukumu ya kulipa deni lote, ikabidi nichukue ile pesa yangu na kumpatia mama anitunzie harafu mimi na rafiki yangu Riziki tutaangalia namna ya kupata kazi ili tufanya mpango wa kulipa lile deni,

Ikabidi tuanze kutafuta kazi lakini wakati tunatafuta kazi tukakutana na wale jamaa ambao walikuwa wanakuja kuchukuwa mitumbwi wakati tunafanya kazi ya ulinzi, wale jamaa wakasema kuna wenzao wameondoka kwahiyo wamebaki wawili kama tunaweza tuungane nao tuwe wa nne na tuanze kazi, harafu tukipata samaki tutauza na kulipa deni lote tunalodaiwa, inamaana kwamba wanataka watusaidie kulipa deni sababu wao ndio walisababisha kupotea ule mtumbwi, wakasema kama tunaweza kuingia baharini inabidi tujiandae harafu jioni tutaenda wote kwenda kuvua samaki, tukawauliza ni maeneo gani" wakasema tutaona wakati ukifika"

Lakini mimi na rafiki yangu Riziki tukawa tunajiuza tuende au tuache sababu mimi na Riziki wote tulikuwa hatujawahi kuingia baharini kwa ajili ya kuvua samaki, tukaona bora twende mara moja kisha tukilipa deni tuachane na wale jamaa tuendelee na kutafuta kazi za nje na bahari,

Lakini mimi wakati huo mama alikuwa hataki niwe nafanya kazi ya uvuvi. ulipofika muda tukawa tumekutana na wale jamaa lakini tulikaa sehemu hadi mida ya usiku,lakini wakati tumekaa tukisubiri muda ufike wale jamaa wao walikuwa wanakunywa pombe muda wote,

Baada ya muda tukabeba kila kinachofaa kwa ajili ya uvuvi na tukatoka kuelekea sehemu ambayo tunaenda kuvulia samaki, lakini cha ajabu wale jamaa wakatupeleka kule ambapo tulikuwa tunafanya kazi ya ulinzi, tukawaambia sisi hapa tulifukuzwa na tukionekana tunaweza tukakamatwa na kesi ikawa kubwa, wakasema hakuna shida sababu sisi huwa ni wavuvi,lakini huwa hatuna mitumbwi ya kuvulia samaki, ikabidi twende hadi hapo na kuwakuta walinzi wengine ambao wamewekwa mbadala wetu,

Kama kawaida yao wakaongea na wale walinzi kisha tukaruhusiwa kwenda kuchukuwa mitumbwi miwili, Lakini cha ajabu ule mtumbwi ambao ulipotea tukauona upo palepale na wale walinzi wakasema tuchukuwe ule mtumbwi na tuangalie na mwingine...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Siri Ya Mvuvi Na Bahari lakini huo ulikuwa ni mpango wa wizi... Inaendelea... Sehemu Ya 02  >>> https://gonga94.com/semajambo/siri-ya-mvuvi-na-bahari-lakini-huo-ulikuwa-ni-mpango-wa-wizi-inaendelea-sehemu-ya-02
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest