________________________________________
“ mama siku ile wakati natoka shule, nilishuka kwenye school bus, nikamuona Yule mama ambae tulikuwa tunaishi nae, akanishika alafu nikalala, nimekuja kuamka naona nipo kwenye sehemu giza, nikajua ni usiku il Yule mama alikuwa na wanaume watatu wakawa wanasema “ huyu mpuuzi ndio amesababisha ndoa yangu ivunjwe anatakiwa auwawe ili mama yake ajute kucheza na watu asio wajua, nikaanza kulia mama, nikawa nawaomba msamaha wasiniue ila wakaanza kunipiga vibao na kusema kuwa nilazima wewe ujute, kwani umewakosea nini mama mpaka watake kuniua, naogopa mama, akawa anaongea mwanangu huku analia…
“ sijawakosea kitu , walikuwa wanataka kukuuwa kwa sababu tu wanaroho mbaya na sio kwa sabbau mimi nimewakosea, pole sana mwanangu na nitahakikisha unakuwa salama kuanzia leo, na hakuna mtu atakufanyua kitu chochote kile, nikasema kwa leongo la kumtia moyo…
“mama mimi sitatoka tena nje, na nitafutie mwalimu awe ananifundisha nyumbani, sitaki kufa mimi mamaa, akawa analalamika mwanangu na alikuwa anaonekana ana wasiwasi mkubwa sana…
“ mama yako na mimi baba yako tupo hapa kwa ajili ya kukulinda hakuna mtu yoyote Yule ambae anaweza kukudhuru kama sisi tupo hai, hivyo naomba uondoe mashaka mwanangu, kwa sasa bhivi hautataoka nje, ila baadae nikihakikisha Yule mama yupo polisi nitaanza kukupeleka shule mwenyewe na kukurudhisha na hautakuwa unarudi kwa school bus tena, akasema paul kwa lengo la kumtia moyo kijana wetu…
“ alafu mumpige na bunduki, akasema Jordan ..
“ usijali, tunampiga bunduki ya kichwa akufe yeye na sio wewe tena, nikasema na kidogo nikaona kama nimeanza kumpa moyo…
Paulina na wenzake walihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kujaribu kuuwa, na paul hakuwa anataka hatab kwenda mahakamani, alikuwa ananiambia kuwa anaweza kujikuta nay eye anafia polisi akiwaona…
Na Jordan kwa upande wake mambo yalikuwa magumu sana, ilikuwa ni ngumu sana mwanangu kuamini kuwa huko nje hakuna mtu ambae atamdhuru, maana alikuwa anamuona kila mtu kama adui, na alikuwa anaogopa sana kutoka nje, ikabidi tuanze kumtafutia mwanasaikolojia wa watoto…
Alikuwa anakuja nyumbani na kwa mieiz mingi kidogo Jordan akaanza kukaa sawa na akarudi shule kuendelea na masomo yake…
Kutokana na uoga ambao alikuwa nae Jordan ilikuwa inanilaimu mimi nilale nae na sio alale pekee yake kama iliovyokuwa awali, maana hakuwa anapata kabisa usingizi kwa sababu alikuwa anaota ndoto mbaya kwa sababu ya kilichomtokea huko nyuma…
Siku moja sasa Jordan kalala tu, paul akaja na kusema “ najua unanikwepa kwa sababu unadai mtoto hayuko sawa, ila usisahau kuwa mimi ni mume wako, hata kama kuna matatizo kiasi gani ila natakiwa nile chakula kila siku, ila nakuona kabisa unalengo la kuniua na njaa….
“ owww kumbe unasikia njaa, ngoja nikakupikie, nikaanza kueleke jikoni, nikashangaa navutwa kisha paul akasema “ weweeee unajifanya mjanja sana eeee, kwani si nimekula ugali muda sio mrefu sana, embu njoo hapa unipe haki yangu, baada ya kusema hivyo akaanza kunipa kiss kisha tukajikuta tunazama ukubwani…
Tumemaliza tukapitiwa na usingizi kwenye kochi, nakuja kuamshwa na sauti ya paul analia na kusema “ mamaa, mama upo wapi…
Tukakurupuka tukavaa vizuri kisha kila mmoja akapita njia yake, mimi nikaenda kwa mwanangu na paul akaenda jikoni akajifanya anaandaa chai..
ITAENDELEA ….