Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Siri Ya Mvuvi Na Bahari Sehemu Ya 01

31st Jul, 2025 Views 2



Mimi ni kijana niliyezaliwa mkoa wa pwani baba yangu alikwa akiitwa Samweli. Mkoa wa pwani ni mkoa uliopo katika fukwe ya bahari, nilizaliwa kwenye familia ya kawaida sana na ndipo nilipopewa jina la Saad, nilikuwa nikiishi na mama yangu ambaye anaitwa Isabella, wakati huo nilikuwa nikiishi na mama pekee bila uwepo wa baba, lakini mama yangu alikuwa akinisimulia kwamba baba alipotea katika mazingira ya kutatanisha,

Mama alikuwa akiniambia kwamba baba alikuwa ni mvuvi mkubwa sana wa samaki na alikuwa ni mtaalamu wa kuendesha mashua, lakini pia wavuvi wengine pale pwani walikuwa wanamtegemea sana kwenye uvuvi sababu baba alikuwa ni mtu ambaye anafahamu sehemu ambayo wanapatika samaki wengi kwenye eneo la bahari, lakini siku moja walikuja watu pale nyumbani na kumchukuwa baba kwa ajili ya kwenda kuvua samaki lakini ndio ikawa jumla na hakurudi wala kuonekana tena mpaka leo, hivyo wakaona huwenda alishafariki.

Nimeishi miaka mingi na mama hadi nimekuwa bila uwepo wa baba, sababu baba yangu inasemekana alifariki mimi nikiwa bado mdogo sana, na kifo cha baba yangu kilikuwa cha kutatanisha sababu baba alipotelea baharini,

Lakini mama alijitoa kunisomesha wakati huo nipo darasa la tatu, lakini nilikuwa wa mwisho kila mtihani, wakati mwingine ilinibidi kurudia darasa sababu sikukidhi vigezo vya kuvuka na kuingia darasa lingine, nilipofika darasa la nne nilianza kuota ndoto zisizo eleweka, mara niote naongea na baba yaani wakati mwingine naota ndoto za kutisha hadi naamka natetemeka, wakati mwingine nilikuwa namsimulia mama lakini yeye alikuwa akiniambia ndoto kama hizo maranyingi huwa zinatokana na kuwaza mambo mengi wakati wa kulala, hivyo mama akaniambia niwe nafanya ibada kabla ya kulala. Lakini wakati huo mama alikuwa anafanya kazi ya kuuza samaki,

Miaka ikasonga nikawa nimemaliza darasa la saba lakini kutokana na matokeo yangu mabaya hivyo sikuendelea na masomo, ikabidi niungane na mama kwenye kuuza samaki, lakini baada ya kuwa naenda na mama kwenye kuuza samaki nikawa natamani na mimi kwenda huko wanapovulia samaki, lakini mama yangu alikuwa ni mkali sana na hakutaka niwe mvuvi hata kidogo, lakini mimi nilikuwa namtoroka mama kisha naenda kuchezea mitumbwi ya watu, wakati mwingine wenye mitumbwi walikwa wakinikuta wananifikuza na kunifokea,

Miaka ikasonga wakati huo tayari nimefikisha miaka zaidi ya 20, lakini pia nikawa tayari nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na msichana anayeitwa Latifa, lakini Latifa alikuwa ni mtoto wa rafiki yake na mama kwenye biashara zao za kuuza samaki, baada ya mimi kuwa kwenye mahusiano na Latifa nikaona pesa ninayopata hainitoshi,

Nilipoona pesa ya matumizi hainitoshi nikaamua kwenda kwa rafiki yangu mmoja anayeitwa Riziki, nikajaribu kuongea na Riziki kama kuna sehemu naweza nikapata kazi, Riziki akaniambia yeye huwa anafanya kazi ya ulinzi inamaana kwamba huwa analinda mitumbwi isiibiwe yani wavuvi wanapotoka kuvua samaki huwa wanamuachia yeye awalindie mitumbwi yao, Riziki akawa ameniambia kama naweza niungane nae tuwe tunalinda wote lakini mshahara tutakuwa tunagawana sababu kila mwenye mtumbwi analipa pesa mwisho wa mwezi,na kazi itakuwa inafanyika usiku, nikaona kazi ya kulinda mitumbwi sio mbaya kwakuwa sina pesa harafu tayari nipo kwenye mahusiano na Latifa, hivyo ni muhimu kuwa na pesa,

Nikamwambia mama kwamba mimi nimeshapata kazi ya ulinzi na nitakuwa nalinda mitumbwi nikiwa na rafiki yangu Riziki, mama akaniambia kwa nini ufanye kazi za usiku wakati kama ni mtaji si bora useme nikupatie ili uendelee na kuuza samaki, nikamwambia mama kwa sasa nikubalie kwanza nianze kazi ya ulinzi kama itakuwa haina faida basi mimi nitaangalia kazi nyingine hapa pwani, mama hakuwa na namna ukizingatia pia wakati huo nimeshakuwa mkubwa ilibidi aniruhusu, lakini akaniambia nisije kusikia umeanza kwenda baharini. Nikamwambia mama mimi ni mlinzi na sio mvuvi. Kazi ya ulinzi ikaanza,

Lakini wakati naanza kazi ya ulinzi nilikuwa tayari nimeshaongea na Latifa kwamba nikipata pesa nikatoe mahari kwao harafu nimuoe, ila nilikuwa bado hata kwenda kujitambulisha kwa wazazi wake na walikuwa hawajui kama mimi nina mahusiano na mtoto wao, lakini mama yake na Latifa alikuwa ni rafiki yake na mama yangu,

Nimeanza kazi ya ulinzi siku ya kwanza ikaisha vizuri na siku ya pili pakakucha salama bila shida, lakini siku ya tatu tulipitiwa na usingizi kidogo kuja kuamka tukagundua mtumbwi mmoja haupo ikabidi tuanze kuutafuta usiku uleule na kila mmoja akapita njia yake tumetafuta wee mpaka tukachoka Mh tukaona bora tutulie tusubiri pakuche harafu tutaendea na kutafuta, ilipofika asubuh ghafla tuliuona ule mtumbwi ukiwa karibu na mitumbwi mingine, lakini kwakuwa ulikuwa kwenye maji kidogo tukaona huwenda mwenye mtumbwi alisahau kuufunga,

Tukaendelea na ulinzi hadi tukakaribia kumaliza mwezi zikawa zimebaki siku chache tupokee mshahara wetu wa mwezi, lakini wakati tunaelekea kumaliza mwezi ili tupokee mshahara, Lakini kabla hatujapokea mshahara, nakumbuka ilikuwa ni usiku tupo katika kazi yetu ya ulinzi walikuja watu wa nne na kutuambia kwamba tuwapatie mitumbwi miwili ya kukodi wao waingie baharini wakavue samaki harafu wakitoka watakuja watugawie na sisi samaki harafu sisi tutakwenda kuuza na kupata pesa, lakini huo ulikuwa ni mpango wa wizi...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Siri Ya Mvuvi Na Bahari Sehemu Ya 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/siri-ya-mvuvi-na-bahari-sehemu-ya-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest