"Nimepanga kutoroka siku ya harusi "
"Eeeee!?" tulishtuka kwa pamoja akajibu" Ndio sasa mnashangaa nini? wao siwanataka kucheza na maisha yangu sasa acha nicheze na akili zao "
Ney alisogea karibu zaidi na kumuuliza kwa sauti ya chini "Wewe Naira huoni kama hiki unachotaka kufanya ni kibaya?"
"Nikibaya kwamba wao wanachotaka kufanya nikizuri ? mfyuu embu niache huko "
"Hapana mimi sikushauri kwakweli maana utawatia hasara mbali na hasara Dully ataumia sana "
"Ney mdogo wangu nimeshaamua kama ni hasara nijuu yao na kuhusu huyo Dully ameyataka mwenyewe kwani nimara ngapi nimemwambia simtaki ila kihele hele chake akaona ajipeleke nyumbani sasa acha nimfunze kuwa na adabu mpuuzi yule."
Niliweka glass mezani na kuongea " Leo umejua kufikilia kitu kizuri, hapo nimekuunga mkono tena siku ya harusi nitakutorosha mimi "
Ney akajibu '" We Norah hapa unampoteza mwenzako hili jambo sio zuri jamani mimi siiungi mkono"
"Dada nampoteza kwamba kipofu au kilema wa ubongo, kingine ungekuwa wewe ungekubali au unasikia historia yangu basi unaona rahisi sana.
Ndoa za kulazimishwa zinashida asikwambie mtu ,usione nimetoboa ukajua kila mtu atakuwa hivyo mwenzako nimetunukiwa na Mungu ."
Amaira aliweka sm yake pembeni na kusema " Nyiee acheni kelele binti kashachukua maamzi ya kishujaa acha tuwanyooshe watu, Bi Naira sisi kama rafiki zako tume-support na tumelipitisha '"
Niliongea kwakumalizia "Haya jamani ajenda imepitishwa ,haya twende kwenye ratiba yetu"
Walikaa vizuri kisha kila mmoja akaweka koo lake tayari kwakuongea, mara nyingi tulikuwa na utaratibu wa kuweka mezani mambo yote yaliyotokea wiki nzima ili tuweze kushauria .
Basi Ney akaanza kwakusema "Okay tukienda kwenye lengo kuu , mimi bwana kilichonikuta wiki hii nimema tu kila kitu kiko sawa kazini mambo pia yako vizuri, na mahusiano nayo kama siku zote tu single as always "
Alimaliza kuongea Naira akaongea," Ulivyosema kulichonikuta nikajua umekutwa na kitu kumbe hamna ,haya jamani kwangu ndio hilo la hiyi ndoa basi"
Baada ya Naira kuongea ,Amaira akaongea " J mimi sina makubwa sana ila tu baba mtoto karudi jana usiku na kikubwa anasema anataka kurudiana na mimi "
Nilimuangalia kwa sekunde na kumuuliza "Wewe Zakayo huyu huyu au mwingine na imekuwaje arudi saizi miaka yote alikuwa wapi?"
"eeh Dada maswali yote hayo yanini ,we jua ndio hivyo karudi kwahiyo kazi ninayo"
"Nawewe umeamua nini sasa ?'"
"Achana na maswali we tuambie kimekukuta nini "
Nilichukua kinywaji na kunywa kisha nikasema "Mimi bwana wiki hii kila kitu kiko sawa ila tu ninamoja Nasra simuelewi nahisi kuna kitu anapanga "
Ney alikunywa juice na kujibu "Nilijua mama mkwe kumbe Nasra amefanya nini tena alafu kama jana nimemuona akiwa na wanao ."
"Ndio alitoka nao jana "
Basi tuliongea mengi kisha tukapata chakula na kuondoka majumbani kwetu.
Nilifika nyumbani nikakuta watoto wameshalala ,nikasalimiana na Selim kisha tukakaa mezani akala chakula huku nikinywa juice kumpa kampani.
Baada ya chakula nilitoa vyombo na kwenda kulala , tukiwa kitandani Selim akanambia "mke wangu tunaweza kuongea?" nilimgeukia na kujibu " Unanini mbona unanishtua ".
"Umeanza upuuzi wako sasa unashtuka nini?"
"Upuuzi wakati unanishtua"
"kukwambia nataka kuongea na wewe ndio ushtuke "
"Haya nambie maana moyo unaenda mbio kama nini sijui"
Alinisogeza na kunikumbatia kisha akasema " Nilichokuwa nataka kuongea na wewe ni kwamba nakupenda "
"Wempuuzi kweli kwahiyo umeona hicho ndio chakuniambia "
" khee Kwahiyo kukwambia nakupenda ni Upuuzi ?"
"We unaona ni nini ?"
"Norah wewe huyo leo unaniambia neno nakupenda ni upuuzi sawa fresh tu"
"Kwa hiyo umenuna ?"
Achana na mimi bwana "
"Haya tuyaache hayo nina ubuyu tena wamotooo" aliamka chap na kukaa kisha akasema " Kimetokea nini huko kwa shoga zako alafu nilikuwa nimesahau kukuuliza " nilicheka na kumwambia " Wewe tena unavyopenda umbea utakuja kusutwa shauri yako"
"Bwanaee weniambie kwani kusutwa nako kitu "
"Hahahahah baba yako anajua kama unapenda umbea?'"
"Norah unaongea au huongei maana unanichosha tu"
" Okay kitu chenyewe ni" nilikaa kimya kwanza kumuangalia namna alivyokaa kwa makini nikasema "Nakupenda" πaliachia sonyo hilo na tusi juuu nikajifanya kumkumbatia akanitoa na kugeuka upande wapili na kujifunika shwaaa
Itaendeleaaaaaa
KWETU morogoro.