Alex akauliza juddy amekuja kufanya nini huko mama ake akamwambia kwani we nini kimekuleta hapa kwani si ulisema hauta kuja tena hapaaaa
Alex akasogea akamwambia maama kwanini tugombane kwa mambo yasiyoeleweka??
"Et eeh hayaeleweki sio haya tokaa" mama alitufukuza mkavu kabisa
"Mamaaa!! Naomba tuongee"
"Kuhusu niniii??"
"Naomba tukae"
Yule mama akasogea mpaka kwenye kochi akaket muda huo huo alitoka na baba yake
Alitukalibisha vizuri tu nikasalmia wakatikia
Alex akasema Nimekuja kuomba Radhi kwa yale yaliyotangulia nyumaa
Baba ake akasema ni ilo tu au kuna linginee?? Kama la msamaha hilo limeisha lekebisha tu ulipokosea we ni kijana
Baba yake ndie alimuambia ,lakini mama yake alikuwa kimyaa tu muda wotee
Alex akasema ninalo lingine pia naomba juddy nae awe hapa!!
Ilibidi juddy aitwe , alex akawaambia
Mama na baba , naomba mnielewe mimi ni mtu mzima nina maamuzi yangu naomba mnielewe kwa hili
Kama juddy akijifungua mtoto na akawa wangu nitamlea mtoto kwa kila kitu kwa kila kituu atakuwa ni jukumu langu mimi ilaa sintamuoa naongea hili nikiwa na akili zangu timamu leo nasema juddy sintamuoa kabisaa "
"Kwasababu umetembea na Rafiki yake"
"Mama naona leo unaweza ukanisikiliza hautakuwa na hasira naomba unisikilize vizuri sanaaa
Juddy ni mwanamke niliekuwa nae mwenye mahusiano kwa miaka miwili , nilimpa kila kitu kama mwanamke wangu lakini hakuweza kunichukulia kama mwanaume wake bado sikuwahi kumtupa niliamini siku moja atauelewa tu moyo wangu ..
Huyu alifikia hatua ya kuniambia nisiende nyumbani kwake anaishi na mdogo wake kwahiyo akawa yeye tu ndio anakuja nyumbani kwangu ,nilipata taarifa kuwa anaishi na mwanaume na sio mdogo wake , ndio nikaenda hiyo siku baada ya mimi kuwa ndani alikuja mbaba tu mzima ndie akaanza kuniambia huyu ni mwanamke wake
Ulitokea ugomvi mwisho niliitiwa mwizi sikuwa na njia zaidi ya kukimbia mana wananchi walikuwa wengi sana hiyo siku ndio nilikutana na akanisaidia akanificha sikuwa namjua wala yeye hakuwa ananijua ilikuwa ndio mara ya kwanza kumuona japo aliishi mtaa mmoja na juddy abadani hawakuwahi kuwa marafiki
Sikuwahi kuwa na mahusiano na salma kipindi chote alikuwa rafiki tu, baada ya kuthibitisha hisia zangu ndio niliamua kumwambia na hapo nilikuwa nimeshavunja mahusiano na Juddy , anakuja kusema anamimba tayari sina mahusiano nae na umri wa mimba ni kweli nilikuwa nipo nae kwahiyo yeye anatumia hiyo kama fimboo "
Mama yake alishusha pumzi akamtazama juddy akamuuliza et ni kwelii?? Juddy akaanza kulia huyu dada hata aibu hana aisee akasema si kweli hakijawahi kutokea kitu kama hichoo aisee
Alex akacheka akasema mimi sijafunzwa uongo juddy ila wewe unaonekana ni mwalimu mzuri sanaaa eeh "
Juddy analia tu et anasema basi niitoe tu hii mimba mi siwezi kuzaa nikarudi nyumbani nitaolewa na nanii??
Huyu vipiiii??
Alex akasema hiyo juu yako sio mimi??
Mama yake na alex akasema embu tusiongee chochote kwa sasa mpaka juddy ajifungue ila mie huyu mschana hapana kwanza ni mwislamu na swala la wewe kubadili dini mi siliafiki kabisaaa
Alex akasema salma ameshabadili dini mama!! Juddy alishtuka mama akasema Ni kwelii?? Huku ananitazama nikasema ndio
Basi akanipongeza sanaa atleast leo niliona Tabasam lake ..
Alex aliwambia salma ni mjamzito anaenda kuwa mama wa mwanangu hivi karibuni wakanipa hongera ila ile ya shingo upande mana juddy alikuwa analia kweliii
Sie tukaondoka zetu tukaacha wanabembelezana hapo ...
Nilianza masomo Rasm alikuja mwanamama mtu mzima hivii akawa ananifundisha
Jamani mmhi mambo mengine ya aibu sana sana , jamani nilianza kufundishwa irabu na silabi mimi nina kichwa kigumu yaan kigumuuu sielewii sielewi kituuu
Ilipita wiki hakuna nilicho ambua, ikawa wiki ya pili wapiii hola tu
Yule mama akawa ananipa moyo sanaaa nitaweza tu ,nilijikuta nakata Tamaa hata zile ndoto nilikuwa naota kuwa nitaweza siku moja kusoma ile shauku ya kutamani kujua nikaona inaenda inaisha yotee kabisa
Nilikuwa namuonea hata haya alex mana alikuwa analipa pesa nyingi sana kwa ajili ya mimi kusoma
Ulipita mwenzi walai sina nililo shika kichwa kilikuwa kinaniuma mnoo yaan kama nikilazimisha nijue naumwa kichwa mpaka homaa , najikuta naachaa nikawaza hii nini mungu wanguu
Alex akienda akirudi ananiuliza vipi namwambia alex mi naona nisikutese alex kusoma sio sifa yangu akanambia hapana lazima kuna njia embu jitahidi siku yenyewe nikajitahidi nae yupo niliumwa mishipa ya kuchwa jasho likawa linanitoka
Nilikuwa hoiii , alex akamwambia yule mama basi asije tenaaa aache tu
Nilimuonea huruma maskini nimemuangusha alex wangu akanambia hata usijali salma ,huenda kuna shida ndio mana unaumwa hiyo sio.kawaida mmh sa naumwa nini?? Anajua mungu mke wangu
Nikamuuliza vipi unaenda nyumbani, akasema ndio ninaenda wapo sawa tu nikasema sawa ..
Niliacha kusoma nikawa nipo tu home ki mimba kikawa kinanisumbua sumbua tu
Siku yenyewe nakumbuka ilikuwa W/end , kule kazini huwa wanawahi kufunga , nikashangaa kumuona zakia nyumbani kwangu mmh nikamuuliza we mwanamke, hapo ni siku nyingi sana mimi na yeye hatujaonana , nilimkaribusha vizuri tu akanambia subira amenambia unaumwa nikasema nije kukuona kumbe ni mama k ??
Nikamuuliza we umejuaje kama mimi mama k akasema bwana unaonekana tu afu kila mtu anajua huko kazini nikacheka tu mana hata tumbo lilikuwa bado halionekanani vizuri
Tulikaa na zakia tunapiga story ananiambia siku hizi unanichunia sana nikamwmbia hapana mpenzi akasema kwelii naona siku hizi umekuwa boss ndo basi hata kucheka na mimi hutakii!!
Yaan alikuwa kama analalamika hivii , mi nikawa namshangaa huyu vipii ,mana ananifanya nione kama vile mimi najishauwa hiviii
Nikamwambia bwana we zakia wewe embu acha ujinga ,mi shoga ako lakini kwenye kazi tufanye kazi bwanaaa
Akasema sawa mi naenda basi nikasema sawa akaingiza mkono akanipa juice ya tende Akasema nilisahau juice hii nimekuletea zawadi mama kija nikachela nikaichukua ..
Nilimtoa mpaka getini nikamwambia mi hata siendi mbali, akasema haya ushakuwa mke wa boss wewe tenaa, mmmh nikasema huyu dada yaan kama amepanic flan hivi haya maisha yangu, nikasema acha bwana , wakati nataka kufunga get akanambia ndo usiitupe juice yangu unywe hapoo mi nimenunua kwa visent vyanguu ,nikamwambia usijali bwana ,Et eeh mana nyie mkishakuwa maboss ndo basi mmmh , nikafunga geti bila hata kumjibu kitu niliona huyu amekuja kunitukana huyuu
ITAENDELEA....
KWETU morogoro.