Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI* * *SSEHEMU YA 6 na 7

19th Jul, 2025 Views 42



Chris alijikuta akiboreka baada ya kukatishwa huu utamu, hakuwa na ratiba ya Mgeni siku ya leo.
Uume wake ulikuwa umevimbiana kupita kiasi.... isingekuwa rahisi kwenda akiwa katika hali hii.

"Nenda ukamsikilize nina uhakika ni yule Mama muuza matunda, mwambie sichukui..." Alimtuma Jamila

Jamila alijiweka vizuri kisha akaenda kufungua mlango.
Pozi lilimkata alipokutana na uso wa Dorin na si muuza mboga tena

"Karibu...." Jamila aliongea kisha akaondoka, hakutaka kuendelea kukaa hapa

Chris na Dorin wanatazamana baada ya Jamila kuondoka

"Karibu ukae ngoja ni kazungumze naye...." Chris aliongea kisha akamfuata Jamila kwa kumkimbilia

"Kwanini umeondoka, au ni kwa sababu uliyekutana naye si muuza mboga kama nilivyo kuambia" Chris aliongea

"Hapana, yule ni Daktari mwenzio bila shaka kaja mzungumze habari za kazi.... tutaonana siku nyingine. Na hata hivyo naweza kusema ni Malaika aliyekuja kuzuia anguko langu. Nadhani nilikuambia nipo katika siku za hatari..." Jamila aliongea kisha akaendelea na safari yake

Chris aliishia kukodoa macho ni kama alikosa cha kuongea.

Huku ndani Dorin aliendelea kukagua kisimu cha Jamila. Alijikuta akicheka kwa jinsi kilivyokuwa kimekaa kihuni huni. Anakirudisha mezani baada ya kugundua hakina maajabu yoyote.

"Nilitarajia mtarudi wote hapa, nadhani kasahau simu yake" Dorin aliongea

"Kama asipoirudia nitampatia kesho, enhe niambie kitu gani kimekuleta hapa bila taarifa, ujue umenikatisha utamu laiti kama ningejua ni wewe sidhani kama hata ungeingia humu ndani...." Chris aliongea kishikaji hakujua kama kuna namna Dorin kaumia

"Kwahiyo mlikuwa mnataka kufanya mapenzi hapa sebuleni!...." Dorin aliongea kwa mshangao

"Tuachane na hilo, niambie ni nini kimekuleta hapa..."

"Nimekuja kupika kwako, gesi yangu imekata halafu Mimi si mzuri wa kutumia jiko la umeme" Dorin aliongea

"Hamna shida nenda kapike..."

Wakati Dorin anaingia jikoni kupika, Jamila alirudi kuchukua kisimu chake. Japo kimechoka lakini kwake kina umuhimu mkubwa.

Muda wote masikio ya Chris yalikuwa makini kusikiliza hodi mlangoni.

Alisimama haraka akafungua mlango, alikutana na Jamila

"Nisaidie kisimu changu..." Jamila aliongea huku pua zake zikinusa harufu ya chakula kilichokuwa kinapikwa huko jikoni na Dorin.

Ndani ya moyo wake alimuona Chris kama bonge la tapeli. Alishukuru tu amenusurika kuliwa bahati mbaya.

"Naomba ni kusindikize... namaanisha naomba nikupe lifti..." Chris aliongea

"Unipe lifti Mimi!...." Jamila aliongea kwa mshangao kwa sababu alijua jikoni kuna mtu

Chris hakutaka kuongea chochote badala yake alimshika mkono Jamila wakaelekea kwenye gari. Dorin akiwa dirishani alishuhudia kila kitu. Kuna namna moyo wake uliumia.

Wakiwa ndani ya gari Chris aliishia kumshangaa Jamila, tangu amfahamu hakuwahi kujua kama ana kope ndefu siku ya leo ndio alijionea, alinyoosha mkono wake azishike.

Itaendelea πŸ’₯

*SEHEMU YA SABA*

"Unataka kufanya nini...." Jamila aliuliza akijihami
"Kope zako ni nzuri..." Chris aliongea huku akirudisha mkono wake

"Inaonekana wewe una roho nzuri sana...." Jamila alionesha hasira yake waziwazi

"Yule ni rafiki yangu, gesi yake imekata ni kawaida Mimi hapa kumsaidia kama Mshikaji wake..." Chris aliongea

"Kumbe na Madaktari hamna tofauti na wauza karanga....ni ajabu kuona mnaishiwa hadi pesa ya kujaza gesi!...vipi mitungi yenu inamaliza laki 5 au ni hizi hizi za 25 au 60" Jamila aliongea

Chris alijikuta akicheka kwa kauli ya Jamila.
Alielekeza mikono yake akashika usukani kisha akaondoa gari.

Jamila alibetua midomo yake kwa kitendo cha Chris kushindwa kujibu swali lake.
Habari za Dorin kuishiwa gesi nyumbani kwake hazikumuingia kabisa. Alijiahidi moyoni mwake pindi atakapo shuka kwenye gari hatakuwa na mazoea tena na Chris

"Naomba unishushie hapa njiani na si nyumbani.... sitaki mdogo wangu apate presha kwa vitu ambavyo havipo"

"Una maanisha nini kusema hivyo"

"Rudi kwa Mgeni wako, kuhusu kitu ulichoniambia muda mchache uliopita nitaufanyia kazi" Jamila anaamua kumtia moyo tu ili wasitumie muda mwingi kuzungumza

Chris alielewa kuna namna moyo wa Jamila umevunjika.
Hakuona sababu ya kuingiza habari za mapenzi tena, badala yake alianza kuongea vitu vingine.

Baada ya Jamila kufika nyumbani aliendelea kufikiria kwanini Dorin aende kupika kwa Chris

"Sitaki kuamini kama atokako hana majirani, okay nifanye hana majirani kwanini asingeenda kula hotelini. Inaonekana kazoea kupika kwa Chris!....tena si kupika chakula tu inaonekana huwa wanapika vyakula alivyotaka kunifanyia Mimi" Dorin aliongea pekee yake huku akifunga karanga

Muda wote Ali alikuwa ana muangalia Dada yake kwa kipimo kikubwa cha karanga ana choweka sababu ya stress

"Usiniambie kesho utauza hizi karanga kwa shilingi 500..." Ali aliongea kisha akageukia upande mwingine

Jamila ndio kushtuka, kama atasema kuzifungua upya atakuwa ameharibu vifuko pamoja na muda.

"Nitajitahidi ziuzike hata kama itanilazimu kutafuta Wateja bar...."

"Kitu gani kimekuvuruga, siku zote huwa unakuwa makini... usiniambie ni yule Mwanaume mwenye gari..."

"Ali kuna muda nakuogopa, unaongea kama Baba yangu hivi.... naomba tuishi kama washikaji" Jamila aliongea

"Nitafurahi kama siku moja utaolewa na Mwanaume mwenye mapenzi ya kweli hata kama atakuwa ni masikini kwangu itakuwa sawa tu kikubwa akupende wewe..." Ali aliongea kisha akafumba macho kumaanisha analala

Jamila alimgeukia mdogo wake kwa maneno anayo zungumza. Aliachia tabasamu lililojaa maumivu, kwa umri wake alipaswa ajifunze kuchora samaki na si kuzungumza vitu vigumu kama hivi.

Usiku wake ulikuwa wa hovyo hovyo hasa akimfikiria Chris, aliamini ni lazima atakuwa kakichapa na Dorin.

Kulivyo pambazuka asubuhi alienda kwenye kijiwe chake.
Gari la Chris lilipita shwaaaaa bila kusimama. Ingawa alivunga hajali lakini kuna namna moyo wake uliumia.

"Kuku tasa huyu! siku ya leo sionekani eeh" Jamila alijisemea huku akilisindikiza kwa macho gari la Chris

Biashara yake ilikuwa ngumu siku ya leo kutokana na kipimo alichoweka.
Akiwa katika hali ya kukata tamaa, Dorin akiwa na Daktari mwingine wa kike walinunua karanga zake zote.

Ile Dorin anataka kuondoka ndio alimkumbuka Jamila.
Hakutarajia binti aliyekuwa nyumbani kwa Daktari Chris ni muuza karanga

Alimrudia kwa macho makubwa yaliyojaa shauku ya kumpeleleza
JE NINI KITAENDELEAAA!
FULL 1000
SIMULIZI HI IMEKAMILIKA MPK MWISHO KABISA
BEI NI 1000 TU
WAHI WHATSAPP 0755090082.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI* * *SSEHEMU YA 6 na 7  >>> https://gonga94.com/semajambo/biashara-ya-karanga-ilinipa-mume-daktari-ssehemu-ya-6-na-7
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest