"Noo!! Salma ni usiku huwezi kwenda peke yako ,naomba twende wote"
"Asante inno" siwezi kwenda na wewe nilimpisha Pembeni nikapita kuelekea barabarani nikachukue boda"
Nilifika pale barabarani nikawa nimesimama nasubiri boda,gafla nikashikwa mkono nilipo tazama alikuwa alex ,nikatamani kumkumbatia ila pembeni alikuwepo inno nikakausha tu..
"Sorry salma, umeniahidi tunakwenda wote??" Alex akaniuliza huku bado amenishika mkono ,nikamtazama inno mungu wangu hata sijui nasema nini ,kwa vile inno nilimkatalia nikaona wacha tu na huyu nimgomee"
"Hapaana alex acha tu niende tutaonana siku ingine" nikauvuta mkono wangu lakini moyo unaniuma hatari, nikicheki Alex alivoumia amechafuka dam afu et nimuache peke yake dah nitawezaje kumuacha na hii hali?"
Nilipiga hatua moja tu Alex akanifuata nyuma akaniambia salma Siwezi ,siwezi kukuacha ukaenda mwenyewe" baada ya alex kunizuia inno alichukia sana aliondoka mpaka lilipo gari lake
Akapanda kwenye Gari akaondoa Gari kwa kasi kama vile anaenda kwenye mashindano aisee , alex alimtazama afu hakuonesha kama kujali chochoteπ₯΅
Baada ya inno kuondoka mi nikaona nimepata mwanya nilimgeukia Alex nikamkumbatiaπ«π©πnikaanza kumuuliza kama yuko sawaπ₯Ήβ€οΈnikawa namkagua nampangusa pangusa maana alichafuka vibaya mnoo
Alex alinibembeleza sana tuondoke wote nikamwambia sawaaβ€οΈβ€οΈtuliongozana hadi kwenye gari hapo watu wanatushangaa vibaya mnooπtuliondoka zetu kuelekea nyumbani..
Usiku ulikuwa mkubwa kibaridi nacho kilikuwa kimetaradadi kidogo, alex aliv ua ile shat yake akaniveka kwa juu ye akabaki na singlend..niliishia kumtizama tu alivojaaliwa yule mwanaume ila kila nilipokumbuka ile kauli yake
Et hana hsia zozote juu yangu niliishiwa nguvu nikabaki nimetulia tu roho ikawa inaniuma vibaya mnoo..
Safari ilitawaliwa na ukimya wa hali ya juu kila mmoja alikuwa anajiwazia ya kwake moyoni..
Tulifika kwenye mjengo mmoja hivi aisee nyumba nzuri afu kubwaaa ,Alex alishuka kwenye gari akanifungulia mlango nikashuka na mie..
"Aliniangalia machoni akaniambia..Karibu sana hapa ndo nyumbani π₯°"
"Nilitabasam nikajibu asante akaja akanishika mkono mpaka ndani ,nyumba ilikuwa ya kisasa nzuri haswaa,"
"Alex aliingia jikoni akaniletea maziwa fresh ya moto akanambia kunywa utoe baridi ngoja nikuandalie chumba nikasema sawa , alipo niacha tu nikachukua simu yangu.. "
Nilikuta missed call na msg nyingi sanaa kuna baadhi ya msg zilitoka kwa inno moyo ulishtuka sana baada ya kuziona msg za inno
yaan huyu kaka mi sasa hivi sina imani nae nilitamani nijue alichoniandikia ni kitu gani..,
niliforwad sms kwa dogo afu nikampigia nikamuuliza imesemaje hiyo mdogo wangu??akasema imeandikwa (Samahani kwa kuonesha tabia mbaya mbele yako salma)
Jamani kwanza nikatamani hata na kucheka nikamwambia dogo nijibie hiyo sms nikamwambia na maneno ya kujibu..akaandika
(Usijali inno Samahani pia nimefanya sikuyenu imekuwa nzito) mdogo wangu
Baada ya kunitumia nilicopy nikatuma kwa inno..
Hazikupita hata sec ikaingia sms ingine yaan inno alijibu muda huohuo nikasema kazi ipo aisee ,niliituma tena kwa mdogo wangu
(Upo wapi) ndo inno aliniuliza hee nikasema haya namwambia nini miee nipo kwa alex auu??
Nikasema hiyo sms hata siijibu nilichofanya nilizima tu simu , haya mengine hata hayamuhusu
Alex akawa amekuja nae nilikuwa nishamaliza maziwa akaniuliza kuhusu kula nikamwambia hapana mi tumbo bado limejaa akaniomba Samahani kwa kile walichofanya na mdogo wake nikasema sawa,
sa nitasemaje mi hata sielewi maisha yao hawa wawili , nikamuuliza tu kuhusu kuumia akasema atakuwa sawa amesha tumia dawa za maumivu
Alinipeleka kwenye chumba ambacho natakiwa kulala mimi ,nikajimwagia maji akanipa pens yake na tshirt ili nivae niwe mwepesi kidogo .
Usiku wangu ulikuwa mzuri lakini sikupata usingizi kichwa kilikuwa kizito sana Akili yangu karibu robo tatu ilikuwa inamuwaza sana alex kama hana hsia na mimi kwanini namuona kama mtu anaenijari sanaa??
Hata macho yake anavyonitazama sio kawaida afu anasema hana hsia na mimi au mimi tu ndio namtafsir kiupendo?? kwanini sasa mara zote yupo karibu sana na mimi??
Au nihamishie akili kwa inno ,lakini uuuh inno hawezi kunipenda mimi hawezi ππsijui hata nifanye nini mbona nawaza sana mungu wangu dah nilihisi kuchanganyikiwa kwahiyo nikajikuta nipo hovyo hovyo tu ..
Asubuhi nilichelewa kuamka mda ulikuwa umeenda kidogo ,niliamka baada ya kuhisi nagongewa mlango nikajua alex huyo ,
nilipo fungua nilikutana na mdada tu wa makamo akanisalimia akanipa supu akanambia aliambiwa na Alex ikifika sa tatu aniletee supu mmh nikamuuliza ye yupo wapi?? Akasema sijui mi alinipigia tu simu, nikasema sawa
Nikachukua zangu supu nikarudi chumbani ,nikaiwasha simu yangu , haukupita muda alex akapiga simu
"Ooh nimekuacha bila hata kukuamsha!!" Mi nikacheka afu nikamwambia Asante nimepata supu akasema vizuri si unanisubiri narud jioni nipo kibaruani kwangu,"
nikasema hapana naenda home tutaonana wakati mwingine alex akanibembeleza kweli nimsubir mpaka jioni akirudi ndio anipeleke nyumbani.
Siku hiyo mi nilikuwa na ratiba zangu za kutafuta dalali ili nipate eneo la biashara, niliona Bora nipambane kulikuo kuendelea kulala nyumbani najichelewesha tu mwenyewe,
nikamwambia kuna issue muhimu sana lazma leo nikaifanye yaan lazima kwahiyo lazima niondoke akasema Sawa basi kuna mtu namtuma anakuijia nikasema poa ..
Baada ya muda alikuja mlinzi akanambia kuna mtu ananihitaji nje nilipo toka nikamkuta mkaka tu hivi akanambia ameambiwa na alex aje kunichukua nikasema poa ,nilijiandaa fasta fasta nikatoka akanipeleka nyumbani.
Nilipofika mtaani kwetu nilikutana na habari kila kona Juddy kayazagaza salma hajui kusoma kajipeleka kwenye party za wasomi kaishia kuaibika ilikuwa kama ndo story et dah..
nikasema atajua mwenyewe , hata zakia alipo kuja kunipa habari hizo nikamwambia bwana wee mi na mambo mengi ya kufanya sio kukaa namuwaza mtu mmoja kwa ujinga wake ,
sikutaka maneno yao yanitoe kwenye mstari hata kidogo ,kweli sijui kusoma hayaa nimekufaa?? Sawa sijui kusoma ye anaejua kusoma ana kipi bora kunizidi mimiii?? Aende huko sijui kusoma sijui kusoma mpuzi niniii!!!
Nikafanya zangu kazi zangu ili nitoke kwenda kutafuta eneo kwa ajili ya biashara , simu yangu iliita namba ilikuwa ngeni,
"Waoooh,umepokea mapema kuliko nilivyotegemea" ilikuwa sauti ya kiume nilijaribu kuivuta taswira lakini sikuitambua hata
"We nani"
"Hahah mi kama wewe tu, mpelelezi uliekuwa unawachunguza kaka zako, hujambo Cinderella "
Baada ya hayo maneno nikamjua yule dishi anaitwa bruno "
"Sijambo vipi"
"Usiku nimejikuta hata siwezi kulala wallahi nimekuwa napitia picha zako tu za kwenye cctv camera karibu mpaka kuna kucha"
Nikasema moyoni hayaa kumekucha balaa lingine hili hapa
"Upo wapi salma naomba kuongea na wewe please "
"Sina muda Samahani '" sikutaka hata anizoee niliikata ile simu nimblock sijui hata namba alitoa wapi mshnz huyu"
Nilitoka nikaenda kutafuta dalali nikampata , nilimuelezea shida yangu ,akanambia twende ana maeneo kama matatu ya Biashara hiyo ,nilikuwa nataka eneo la kuuzia chakula ..
Eneo la kwanza halikuwa mbali sana hata na nyumbani hili lingekuwa rahisi lakini sikulipenda palikaa kiswahili sanaaa ,akanipeleka sehemu ingine hapa palikuwa na bar nyingi zimezunguka napo sikupaelewa mana kuuzia walevi waweza shikwa tak kila siku na hakuna kitu utamfanya..
Dalali alinambia hiyo sehemu ya mwisho tukaenda ilikuwa mbali na mitaa ya nyumbani lakini ni sokoni yaan ndani ya soko aisee pachafu afu ni zile banda za mabati
Tulizunguka hiyo siku na dalali akaniunga kwa dalali wenzie ,mpaka nikachoka sehemu zingine nilikuwa nakupa pazuri ila bei yake mmh ikawa inanishinda .
Alex alinipigia simu akaniuliza nilipo nikamwambia tu kuna sehemu nipo akanambia nielekeze nije ,nikawaza huyu si alisema anatoka kazini usiku huyuu ,nikawa nimemuelekeza akaja kweli
Aliniuliza natafuta nini mana alinikuta na dalali ,nikamuelezea nahitaji kufungua sehemu ya chakula ,nifanye kazi akasema waooh umewaza vizuri nimependa we ulikuwa unataka hiyo sehemu iweje nikawa nimemwambia, akauliza mtaji wangu shingap?
Nikatamani kudanganya na kweli bwana nikamwambia mimi nina laki nne tu akasema ndo ya kila kitu nikasema ndio, akamlipa hela dalali akamwambia aende tu atuache sikumuelewa lakini nilikausha kwanza nilikuwa nishachoka kutembea hatari
"Naskia njaa ,naomba tule kwanza!!"
"Sawa" tukakubaliana tukale kama alivyonambia tukaenda kwenye mgahawa mmoja wa kisasa wa kishua kweli ,pazuri pako simple
Akaagiza chakula ,wakati tunakula akawa ananiuliza
"Unataka kama hapa au pawe pakubwa "
"Mmmmh uwezo wangu huku pakubwa sana mi nataka pa kiswahili ty"
Alex akacheka akasema haya sawa mwamuzi ni wewe nikasema ndio π₯°
Akanambia hiviii salma naomba nikuulize Samahani lakini usinielewe vibaya mamaa..
Mmmmm moyo ulilipuka nikajiuliza Alex anataka kusema nini??
Itaendeleaaaaaa
KWETU morogoro.