Max alifika karibu na dala kabla hata ya salamu Dala akasema.
" Ehee unasemaje na wewe?
" Mbona unanipokea kwa ukali?
" Usinipotezee muda nina mambo mengi ya kufanya .
" Mmmm punguza jazba kwanza waungwana wakikutana wanasalimiana alafu mambo mengine yanafuata. Habari yako.
" Salama.
" Dala naomba unipe muda tuongee.
" Huoni kama huu ni muda wa kazi?
" Naweza kulipia ilimladi tuongee tu.
" Siwezi kurudia kosa.
" Najua nilikukera sana siku ile lakini nitakupa hela yako pia kuna swala lingine naomba tujadili tukikubaliana nitakulipa laki 5 kwa mwezi.
Dala alishituka na kumuangalia max usoni alipotajiwa hiyo hela.
" Kazi gani hiyo ya kulipwa laki tano kwa mwezi?
" Nipe muda tuzungumze. Ni jambo serious sana.
Dala alimuangalia huku akiwa anatafakari kitu .
"Kumbuka nipo kazini.
" Naelewa ila naomba unipe muda kidogo tuzungumze .
Dala alikubali waliondoka wakaenda kukaa sehemu iliyotulia kwaajili ya kuzungumza.
Max alitoa kiasi cha shilingi laki mbili akampatia.
" Hayo ni malipo ya kuwa na mimi ule usiku.
" Khaaaaa pesa zote hizi na hatukufanya chochote?
"Usijali. Hata hivyo sikuwa na nia ya kukufanya chochote.
Dala alizichukua zile hela na kuweka ndani ya mkoba wake.
" Asante.
" Dala naweza kukuuliza maswali mawili au matatu?
" Ndio wewe uliza tu.
" Kwanini unafanya kazi ya kujiuza?
Dala alimuangalia kisha akainamisha macho yake chini.
" Najua wengi hawapendi kufanya kazi kama unayofanya ila kuna sababu unaweza niambie sababu yako ni ipi?
" Ni ugumu wa maisha, pia nilikwambia ukweli hautaweza kuniamini.
" Unaweza kinaelezea kwa kirefu?
" Naishi na mdogo wangu, ana miaka 13 sasa, hatuna wazazi na mimi ndio tegemeo lake hivyo natakiwa kufanya kazi na kujituma kwaajili ya maisha yake nataka asome sitaki aje kuishia kama mimi . Kusema ukweli sijawahi kuuza mwili wangu siku ile ilikuwa mara ya kwanza na nilifanya vile sababu ya kutafuta ada ya shule ya mdogo wangu.
" Kwahiyo hufanyi biashara ya kujiuza?
" Ndio , kazi yangu ni kuuza bar tu.
"Pole sana.
" Unamuda gani kwenye tangia umeanza hiyo kazi ya bar?
" Huu ni mwezi wa pili.
" Nilihisi kuwa sio mzoefu kwenye hiyo kazi ya kujiuza maana wasichana wa nafanya hiyo kazi wanajulikana tu. Sasa nikikupa kazi utaweza kuifanya?
" Kama inamalipo mazuri nitafanya.
" kama nilivyosema mwanzo ni laki 5 kwa mwezi.
" Ni kazi gani ambayo unataka nifanye?
" Kuwa mama wa mtoto wangu.
Dala alishituka akawa kamkatoa macho kwa mshangao, Max aliangalia chini kwa sekunde kadhaa alafu akasema
" Yani namaanisha mke wa kukodi.
Dala bado aliendelea kushangaa.
" Hilo ni jambo geni sana kwangu inawezekana vipi? Sijawahi kusikia wala kuona.
" Haya mambo yapo sana sema kwako ndio mageni. Upo tayari kufanya hiyo kazi?
" Unamaanisha kumlea tu na kuigiza kama mama?
" Ndio ipo tayari kufanya hivyo?
" Ndio nipo tayari lakini kabla sijaamua hiyo kazi unatakiwa kunipa maelekezo ya kutosha.
" Ok, ni binti yangu anaitwa shalon nimeishi nae tangia alipokuwa na miaka miwili, alikuwa na matatizo ya kuona ila siku tatu zilizopita alifanyiwa upasuaji na hivi ninapoongea na wewe bado yupo hospitali. Tamanio lake kubwa ni kumuona mama yake baada ya kutolewa bandeji.
" Kwani mama yake yuko wapi?
Max alishindwa kujibu swali la dala. Dala alihisi huenda mama yake Shalon amefariki.
" Samahani haikuwa dhamira yangu kukukumbusha yaliyopita , naelewa ni uchungu kiasi gani kuondokewa na watu tunaowapenda kwani kuna muda hata mimi napitia hali hiyo ninapowakumbuka wazazi wangu.
" Tuachane na hayo , upo tayari kuanza kazi kesho?
" Nipo tayari kufanya hiyo kazi.
Max alitoa kadi yenye namba zake za simu na kumpatia Dala.
" Hizi ni namba zangu za simu naomba kesho Mida ya saa nne asubuhi unitafute.
" Sawa.
" Kwaheri.
Max aliaga akaondoka .
" Afadhali nimepata kazi nzuri sasa Shakira atasoma shule nzuri na kupata mahitaji mengine bila shida yoyote.
Kesho yake Mida ya saa nne Dala akimtafuta Max.
" Hallow Dala.
" Umejuwaje kama ni mimi?
" Hakuna mtu mwingine ambae nilikuwa nina miradi nae zaidi yako pia sauti yako haiwe kunipotea. Uko wapi kwa sasa?
"Nipo nyumbani.
" Unaweza kuja Tumaini hospital
" Sawa nafika hapo muda sio mrefu.
" Sawa chukua usafiri wa binafsi ili ifike haraka.
" Sawa.
Dala alichukua usafiri anaelekea Tumaini hospital.
Alipofika alimpigia simu max akatoka nje kwenda kumpokea.
" Tulikuwa tunakusubiri wewe shalon anatakiwa kufunguliwa nacho yake .
" Lakini sijachelewa sana.
" Huu ndio muda tuliopanga hivyo haujachelewa.
Walielekea kwenye wodi aliyokuwa kalazwa shalon wakamkuta Irene anamnywesha juice Shalon.
" Habari.
" Salama.
Dala na Irene walisalimiana na Shalon aliposikia sauti ya Dala akauliza.
" Huyo ni mama yangu? Shalon aliuliza.
" Ndio ni mama yako amefika. Alijibu max
Shalon aliachia tabasamu kisha akauliza
" Mama yangu anaitwa Hilda mbona sasa mnamuita Dala?
" Hilo ni jina lake lingine.
" Nimekumiss mama nataka kukuona.
Dala aliwaangalia Irene na Max. Max alimuonyesha ishala apite na kwenda kuungana nae. Dala alimpita na kwenda kukaa pembeni ya shalon alimkumbatia na kumbusu.
" Mwanangu Shalon nilikumiss pia binti yangu nakupenda.
" Nakupenda mama , doctor aliniambia nitaona nataka kukuona wewe kwanza
" Nipo hapa pembeni yako kipenzi utaniona. Hata mimi natamani kuona macho yako mazuri .
Shalon alitoa kicheko kikubwa alionekana mwenye furaha mno. Hali ya Shalon kuwa na furaha ilimfanya Max ajisikie vizuri maana hakuwahi kumsikia akicheka kwa sauti zaidi ya tabasamu tu.
Baada ya muda mchache kupita doctor alifika kwaajili ya kumfungua Shalon. Kila mmoja alikuwa makini kuangalia , Iren alikuwa na wasiwasi endapo Shalon utagundua kuwa dala sio mama yake itakuwaje.
" Max itakuwaje kama shalon akigundua kuwa huyu sio mama yake?
" Sio rahisi maana haijui sura ya mama yake.
Baada ya shalon kufunguliwa alipewa kioo ajiangalie.
Shalon alijiangalia huku akitabasamu.
" Huyo mrembo unaemuona ni wewe shalon.
Shalon aligeuka kuwaangalia wote waliokuwa wamesimama kisha akarudisha macho yake kwa Dala na kumuabgalia kwa makini . Irene alimfanya Max alijua kila kitu kinaharibika.
" Nilikwambia anaweza ahisi sio mama yake.
Mapigo ya moyo ya max yalianza kudinda kwa kasi.
" Mwanangu unaona?
Dala aliuliza na shalon akatingisha kichwa akimaanisha ndio.
" Mama....
Shalon alimkumbatia na kusema
" Niambie hautaondoka na kuniacha mimi na baba.
Dala alimkumbatia vizuri na kusema
" Naanzaje kumuacha mtoto wangu mzuri hivi.......
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
OFAAAA KUPATA YOTE NI 1000 TU
NJO....
WHATSAP 0755090082.