Mkononi mwangu kisha nikainywa nilianza kupata maumivu makali ndani ya tumbo langu, Nilianza kuhisi misumali inachoma pembeni ya tumbo langu, Nilikuwa nahisi utumbo wangu unakatikakatika, Niliona leo kweli nakufa, Alikuja baba na kuanza kugonga mlango huku anapiga makelele dada nae aliamka na kuanza kuita watu hatimaye watu walikuja kusaidiana na baba hadi walifanikiwa kubomoa mlango na kuingia ndani baba alipoona mabaki ya sumu ya kuulia wadudu aliomba mtu mmoja aende akatafute maziwa, Aliyeagizwa kwenda kutafuta maziwa alitoka huku anakimbia kwenda kutafuta maziwa wakati huo dada analia na watu wengine wanahangaika kutafuta usafiri wa kunipeleka hospitali,
Baba alianza kulia akinililia ni kwa nini nataka kujiua, Nilikuwa nikiyatazama machozi ya baba naona kama nimelaaniwa kutokana na kifo cha mama.
Yule aliyeenda kutafuta maziwa kwakuwa ni kijijini hakuchelewa akaja na maziwa, Nikanyweshwa maziwa na baba, Kisha wakaleta usafiri wakanibeba na kunipeleka hospitali, Nilifikishwa hospitali nikiwa hoi nikapatiwa matibabu ilipofika asubuh nikaruhusiwa kurudi nyumbani sababu hali yangu ilikuwa inaendelea vizuri,
Baada ya kutoka hospitali baba alitaka kujuwa ni kwa nini niliamuwa kunywa sumu, ni kipi kinafanya hadi nataka kujiua, Niliwaficha lakini nikaona hata nikiwaficha haina tena maana, Nilisema ukweli mwanzo mwisho tulivyoanza mimi na sakina hadi pale nilipotekwa na kufanya biashara ambazo sio halali. Baba akasema atauza shamba ili anipatie mtaji nianze biashara, Niliona ninapoelekea nitamfirisi na baba yangu, Nilimwambia baba asiuze lile shamba lakini nitapambana mwenyewe kupata mtaji, sababu pia kule mjini pembeni mwa mji kuna nyumba yangu nilinunua.
Nilikaa siku kadhaa pale nyumbani dada yangu akawa ameondoka tukabaki mimi na baba. Lakini wakati huo tina alikuwa tayari ameshamaliza masomo na hakurudi nyumbani kwao bali aliendelea kuishi kulekule mjini, sikujuwa kama amepata kazi au anaishi vipi, Lakini pia nilikuwa sijui chochote kuhusu sakina,
Nikaona pale kijijini sina hata kazi ya kufanya niliamua kurudi mjini ili nikaanze maisha yangu, Lakini nilikuwa bado nampenda tina lakini kuhusu sakina kitajulikana hukohuko mjini, Nilipanda gari na kuamua kurudi mjini, lakini pia kuna kiasi kidogo cha pesa alinipatia baba kwa ajili ya kuanzia maisha nikifika mjini,
Nilipofika mjini sikutaka kwenda kule garage wala kule nilipokuwa nimepanga, Lakini nilienda kwenye ile nyumba yangu ambayo niliinunua kwa siri, Nilianza kuishi huko bila mtu kujuwa, Ilibidi niwe naweka mabox na kulala, Nikanunua na ndoo kwa ajili ya kuogea. Lakini pale karibu na nyumba yangu palikuwa na eneo dogo jirani yangu alikuwa amelima mihogo, Siku moja nimeamka nikawa nimemuona mdada mmoja anachimba mihogo, Nikamsalimia na kumtania, Dada naomba namimi mihogo, Yule mdada akanijibu kama utani Nikaipike kwanza,ikiiva nitakulete si utakuwepo? Nikamjibu ndio nitakuwepo. Yule mdada baada ya muda akaniletea mihogo iliyochemshwa, Dah mimi nilimtania kumbe mwenzangu kaniletea kweli, Bas niliipokea ile mihogo na kumshukuru. Kwa mwonekano alikuwa ni mdada flani hivi ametulia kiaina, Mazoea ya taratibu yakaanza kati yangu na yule mdada, tukafahamiana yeye anaitwa Edina, Lakini mimi ilibidi nimtajie jina langu la David, Maana niliona hili jina la sadiki silielewi.
Nimekaa siku chache nikaona akili imetulia sasa naweza hata kumtafuta tina, Lakini kabla sijamtafuta tina nikaona ni vyema nikaangalie kwanza pale garage kama pako salama, Sababu nilikuwa na share/Shea biashara na sakina hadi account ya bank nilikuwa natumia ya sakina sababu nilimuamini sana, Nilipofika pale garage/kuoshea magari, Nilikuta palishabomolewa na harafu kuna jengo kubwa linajengwa maeneo yale kwa ajili ya biashara. Dah nikaona hapa niangalie utaratibu mwingine,
Nikaanza kumtafuta tina nilimtafuta sikumpata lakini nikawa nimepata taarifa kwamba tina baada ya kumaliza masomo alipata kazi kwenye kampuni moja kubwa pale mjini lakini pia ana mchumba wake ambaye huyo mchumba wake ni mtoto wa boss mwenye kampuni anayofanyia kazi, Niliona kwakuwa siwezi kuonana na tina kirahisi ilibidi niende kwenye ile kampuni anayofanyia kazi tina,
Nilipofika pale anapofanyia kazi tina wakati naingia pale getini nilikutana na sakina akiwa ndani ya gari, Sakina alishusha kioo cha gari lake na kunitazama kwa dharau kisha akaniambia nimekuona siku nyingi ukihangaishana na tina lakini kwa sasa muda wa kuwa na tina umeshapita kwahiyo fanya kumsahau lakini kama unahitaji msaada utanitafuta, ila zingatia neno langu achana na tina. (Sikumjibu chochote) Sakina aliendelea na safari mimi nikaingia ndani,
Niliingia na kuelekea sehemu ya mapokezi maana jengo lilikuwa ni kubwa nilipofika sehemu ya mapokezi nikaomba muhusika anielekeze kwenye ofisini ya tina, Yule muhusika wa pale mapokezi akaniambia hakuna ruhusa ya kuonana na tina,kama unataka kuonana na tina lazima upite kwenye ofisini ya boss, Nikaelekezwa kwenye ofisini ya boss ikabidi nipande lifti sababu ilikuwa ni ghorofa ya nane, Nilifika hadi kwenye ofisini ya boss nikagonga hodi na kuingia,
Nilipoingia niliogoapa baada ya kumkuta tule mzee ambaye aliniteka na kunilazimisha nimfanyie kazi yake ya kumtakatishia pesa. Nilitaka kuondoka mzee akaniambia...
Itaendelea...βπ»
~Daudi~.