Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

NILIPOFUNGA NDOA NA MAITI UKU NALIA Sehemu ya kwanza.

27th Jul, 2025 Views 25



Naitwa Daudi nakaa mkoani kaka yangu anakaa mjini anaitwa yusuph kaka alinipigia simu mdogo wangu mimi kazi ninayofanya bado miaka miwili nistahafu sasa nimeambiwa nimchague mtu wa kumwacha kwenye hii kazi mimi nimeona wewe ndio unafaa kukuachia hii kazi unasemaje??

" Mimi nikiangalia maisha magumu na kazi siku izi ndio fashion yake kujuana.

Nikamwambia kaka nakuja mimi najuwa kaka anafanya kazi hospital ila sijui kitengo gani yeye ananiambia hii kazi ina malupu lupu tofauti na kazi zengine yani anaisifu na mimi nina shida nikasema sawa nakuja kaka.

" kweli nilifika mjini nikafikia kwake anakaa peke yake nililala kesho yake akaniambia twende sasa kazi ukaanza kuchukua uzoefu mdogo mdogo.

" nikaenda hospital sasa tuliingia kwa mganga mkuu neno mganga mkuu lilinistua kidogo maana mimi nilikuwa najuwa mganga ni yule mwenye tunguri akanitambulisha.

Mganga mkuu yule akamwambia kaka mpeleke wodini akazijuwe wodi zote.

" mimi moyoni nikasema kazi ya uku naisi kufagia hospital kwenye wodi sasa najiuliza ata kazi za kufagia nazo ni ngumu mpaka tulisishane alafu anasema ina malupu lupu hii kazi mmm kaka kaniingiza chaka ayo mawazo yangu kimpango wangu.

nashangaa tunaingia kwenye wodi wagonjwa wamenuna wote kuna mzee mmoja akasema uyu bundi kafata nini uku jamaa akija yeye lazima Leo usiku afe mtu.

" kaka ananielekeza mwanzo wa wodi mpaka mwisho kama yale maneno ayasikii.

Mimi nikashangaa wodi zote wanamwita kaka bundi sijui maana yake ila sababu nataka kazi nikasema nitajuwa tu.

Basi mtihani ukaja tukaenda monchwali tukaingia ndani yeye ana ata uoga ndio kwanza anamwambia mwenzie mwanangu nipe ata posho Jana nasikia neema imekudondokea maiti za ajari kama zote.

" yule mwenzie anasema subili mwanangu Jana kweli walikuja kama wote ila dokta masawe kaleta michongo ya tamaa wale maiti pesa kajifanya awajakufa kumbe kaenda kuwavua Pete kwanza zote za ndoa kazingua kinoma yani mimi nimewavua viatu ndio nimempa mshikaji wetu yule ajaludi akiludi oya oya.

" moyoni nikasema kumbe kuna kinachoendelea kwenye aya maisha yapo nyuma ya pazia yani maiti zinavuliwa viatu zinavuliwa Pete mimi aya siyajui mule ndani natetemeka kwa uoga lakini wao wenyewe wanaongea awana shida.

" kaka akasema dokta masawe asilete michongo ya tamaa yeye anawapiga sana kule kwenye upasuaji akiwachoma sindano nusu kaputi anapita na Pete sana sasa asije akajifanya anataka mazoea na uku kila mtu ale ofisini kwake akaniambia mimi daudi chukua kiti ukae tushafika.

" dah moyoni naogopa lakini kaka yeye ana ata uoga ananiambia acha uoga naisi kama unaogopa sasa unaogopaje maiti awa washakufa awana kazi yoyote wanayoweza alafu mdogo wangu hii kazi ina pesa sana alafu ukiwa mtu wa pamba mwezi wa 12 na wa 9 utapiga pamba mpaka watu wakushangae.

" mimi nabaki njia panda pamba napigaje na humu ndio tunasinda na izi maiti mpaka muda wa kuondoka au.

" jamani nilikuwa naogopa kaka kumbe anafanya kazi monchwali na mimi inatakiwa nifanye kazi monchwali ili kaka akistahafu mimi nashikiria usukani akanipa koti akanipa glox tukaenda kubeba maiti wodini.

Mimi naogopa kweli lakini sitaki nimuonyeshe kaka kuwa naogopa.

Nilishangaa maiti za jinsia mbili tunazipakia kwenye tololi moja alafu tunazibandanisha.

Tukaenda nazo monchwali tukaziweka akaniambia nenda kanywe chai uje.

Sasa nilipoenda kunawa maji jamani nilimwaga maji mengi kusafisha mikono mpaka jamaa mmoja akaniambia ndugu yangu mikono unamwaga maji ivyo je kuoga inakuwaje??

" sikumjibu sababu ajui najisikiaje kwenye moyo wangu.

" nikaenda kula.

Naludi nakuta kaka yupo peke yake anasoma gazeti ananiambia yule jamaa ndio kaondoka kwaiyo kaamishwa hapa kitengo tumebaki mimi na wewe kesho nitakufundisha jinsi ya kupiga pesa humu monchwali kwa siku unatoka na pesa nyingi sana upaswi kuogopa awa maiti kuna vitu nyuma ya pazia ya dunia hii utayajuwa kupitia maiti izi.

" mimi naogopa kimya kimya.

" basi tulikaa mimi namtegemea yeye sina ujanja wa kusema mimi nimezoea wale maiti sasa usiku ulipofika kaka akaniambia kaa hapa ngoja mimi nikachungulie nje nikaweke mitego yangu ya pesa.

" basi nilikaa pale kiuwoga uwoga sasa kaka alipotoka nje tu umeme ukakatika we we nikaanza kumwita kaka kakaa.

Nasikia nimeshikwa mkono jamani nilipiga kelele kama kichaa alafu kaka asikii namuona kwa nje kule anaongea nashangaa umeme umekatika umu tu monchwali yule mtu aliyenishika ananipapasa kwenye shingo kama anatafuta koromeo alifunye sijui alifanye nini jamani nilipiga kelele tu maana kukimbia naogopa giza chini kuna maiti nitazikwaa nizidondokee.

Yule mtu akanikamata koromeo jamani jamani dah sijui niseme nini yani.....

NINI KITAENDELEA USIKOSE EPISODE YA PILI
ITAENDELEA

KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NILIPOFUNGA NDOA NA MAITI UKU NALIA Sehemu ya kwanza.  >>> https://gonga94.com/semajambo/nilipofunga-ndoa-na-maiti-uku-nalia-sehemu-ya-kwanza
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest