Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

Sɪᴍᴜʟɪᴢɪ﹕ 𝙈𝘼𝙋𝙀𝙋𝙀 SEHEMU YA TATU

19th Jul, 2025 Views 53


_Mtaalam Star7_
*_______________________________*

**
Mpaka inafika saa kumi na moja jioni ,tulikuwa bado hatujafanikiwa kuipata namba moja iliyofutika na sasa zimebaki namba mbili za mwisho, ilibaki namba nane na namba Tisa.

"Weka namba nane" (ilikuwa ni sauti ya john akiniambia Mimi)

Niliweka namba nane kisha nikapiga simu,simu ikaanza kuita na baada ya kuita mara kadhaa mhusika akapokea siku,sikuwa na amini baada ya kusikia sauti ya Sunita jai.

"Halo" (sauti ya sunita jai)

Nikaachia tabasamu kidogo
"Halo sunita jai,ni Mimi muuza madafu,namba yako nimechukua ofisini kwako"

"Ofisini kwangu?"

"Ndiyo"

"Si nilikupatia namba yangu ama?"

"Kadi uliyonipatia ni ya ofisi"

"Samahani,nilikosea kutoa kadi nisamehe"
Kumbe sunita jai wakati ananipatia kadi alikosea,badala ya kunipatia kadi yake binafsi ananipatia ya ofisi.

"Haina shida dada,nimekupigia kuuliza sehemu gani niwe nakuletea dafu,na unahitaji kiasi gani?"

"Nitakuelekeza baadae kwenye meseji,kwa sasa nipo bize ndugu yangu"

"Sawa"

Sunita jai akakata simu,john alifurahi kuona nimeongea na sunita jai.
"Haya ndo mambo sasa,inatakiwa umpate huyu mrembo,usipende kukaa singo siku zote"

Nilishusha pumzi kisha nikakaa,nikamtazama john
"Siwezi kuwa na mahusiano tena" (kauli yangu ilimshitua john ikambidi akae karibu yangu)

"Kwanini?"

"Yaliyonikuta miaka Minne iliyopita sitamani yajirudie tena,sunita jai atabaki kuwa bosi wangu na wala siyo mpenzi wangu,nitajitahidi kuzishinda hisia"

John akatazama huku na kule kisha akaniuliza.
"Kwani kevo kuna jambo gani kubwa ambalo limeshakukuta na kukufanya usitamani kupenda tena?"
John anafahamu historia ya maisha yangu kwa ufupi,kuhusu suala la mahusiano hafahamu kabisa ingawaje niliwahi kumgusia juu juu kipindi tumelewa,ila hakumbuki kwakuwa siki hiyo tulikuwa tumelewa chakali.

"Nenda kwanza kaongee na Mteja" (nilimwambia John badala ya kuona Mteja yupo ofisini kwake)
John akaenda kuongea na Mteja,akamhudumia halafu akarudi nilipo.

"Ehe,nieleze ndugu yangu"

Nilivuta pumzi nikaibana kifuani kwa takribani sekunde kumi ndipo nikaishusha,nikamtazama rafiki yangu John na kusema.
"Miaka minne iliyopita nilitengana na mpenzi wangu niliyekuwa nampenda sana,Mpenzi wangu aliishia kidato cha nne,Mimi niliendelea mpaka elimu ya chuo kikuu".

John akauliza
" mlikuwa mnasoma darasa moja?"

"Ndiyo,tulikuwa darasa moja kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne,yeye alifeli hivyo hakuweza kuendelea na kidato cha tano,tuliahidiana kuoana nikimaliza masomo yangu,nilienda kidato cha tano mpaka chuo kikuu nikamaliza,kwa bahati nzuri baada ya kumaliza masomo yangu nikabahatika kupata kazi kwenye kampuni moja lililopo Jijini Mwanza,ikanibidi nimchukue mpenzi wangu nianze kuishi naye huko huko mwanza"

"...Mimi na mke wangu tulianza kuishi maisha mazuri sana,kampuni ikanipatia nyumba Pamoja na Gari ya kutembelea,lakini maisha yangu ya Furaha hayakudumu hata mwezi mmoja Kwani,kuna vita iliibuka kutoka kwa ndugu zangu,vita yenyewe ilikuwa ni vita ya Mapenzi"

"Unamaana gani kelvin?" (John aliniuliza kwa umakini)

"Kaka yangu mkubwa alikuja kunitembelea,hii ilikuwa ni wiki moja baada ya kupata kazi,kipindi hicho kaka hakuwa na kazi yoyote ile hivyo akawa anabaki nyumbani na shemeji yake ambaye ni mke wangu Berther"

"Kila siku asubuhi nilikuwa natoka nyumbani narudi usiku,na nilikuwa najaribu kumuunganisha kaka yangu kwenye kampuni ninalofanyia kazi ili nayeye apate kazi"

John akaniuliza tena
"Wewe na kaka yako mmesoma kozi moja?"

"Hapana,Mimi nimesoma biashara ,lakini yeye amesomea masoko"

"Aah sawa"

Nikaendelea kumsimulia john
"Kwa bahati nzuri kaka akafanikiwa kupata kazi pale pale ninapofanyia kazi,kampuni ikampatia nyumba lakini hakupewa Gari,kwakuwa nyumbani kwangu na kwake palikuwa karibu,nikawa nampitia kila siku tunaenda kazini"

"..siku moja ya jumamosi nilikuwa nimekaa sebuleni natazama runinga,mara simu ya mke wangu aliyoisahau sofa la pembeni na nilipo, ikaanza kuita.Simu ya mke wangu iliita ila sikutaka kuipokea kwakuwa sina mazoea ya kupokea wala kuchunguza simu yake,mpigaji aliendelea tena na tena,ikabidi niichukue simu ya mke wangu niangalie nani anapiga"

"Macho yalinitoka baada ya kukuta namba ya kaka yangu ameisevu 'Mi Amor'(kipenzi changu),nikatazama mlango wa jikoni nikagundua mke wangu alikuwa bado anapika,nilijikuta natamani kufahamu kwanini mke wangu kamsevu kaka yangu 'mi amor'"

"Labda nisingelifungua meseji walizokuwa wanachati huenda Leo hii nisingeliumia zaidi,nilikuta mke wangu na kaka yangu wanachati jumbe za Mapenzi,cha kushangaza zaidi nilifahamu mke wangu anaujauzito wa kaka yangu,nilizidi Kusoma meseji zao mpaka pale nilipofika kwenye meseji moja kutoka kwa kaka yangu ikimtaka mke wangu aniache"

"Pole sana rafiki yangu,sasa kwanini uliacha kazi?au kwa sababu ya hicho?"

"Hapana,sikuacha kazi bali wanitengenezea njama ya kuacha kazi"

"Njama ?akina nani hao?

" nilipogundua mke wangu anatoka kimapenzi na kaka yangu tena mke wangu anaujauzito wake ambao Mimi najua ni wangu ,niliamua kumfuata kaka,nikajaribu kuongea naye lakini akanijibu majibu ya dharau,nakumbuka kaka aliniambia yeye na mke wangu walianza mahusiano baada ya Mke wangu kufeli kidato cha nne,miaka yote ambayo nilikuwa nasoma,wao walikuwa wanamahusiano"

"...kaka hakutaka kumuacha mke wangu,alidai mke wangu ana damu yake tumboni, nilitamani kuwaeleza ndugu zangu nikashindwa,ilinibidi nijaribu kuongea na mke wangu Kama atanielewa,Mke wangu na yeye hakutaka kuachana na kaka yangu,aliniambia yeye na kaka yangu wanapendana Sana,tena walikuwa wanasubiri kaka apate kazi ndio waoane"

"Mke wangu akaniacha akaanza kuishi na kaka yangu, maumivu ya Mapenzi yalipelekea nikawa sifanyi kazi kwa ufanisi,nilijikaza nikaendelea kufanya kazi ila kila nilipomuona kaka yangu niliumia Sana,sikuwa na namna kwa sababu Mimi na yeye tunafanya kazi kampuni moja"

"...kaka yangu na aliyekuwa mke wangu wakanichongea kwa Bosi,nikaonekana nafujisha Mali za kampuni, Bosi aliniachisha kazi mara baada ya kupokea maneno kutoka kwa kaka yangu"

John akashusha pumzi
"Bosi alikuwa anajua Kama nyie ni ndugu?"

"Hakuwa anafahamu"

"Pole Sana,kwahiyo kaka yako na aliyekuwa mkeo bado wapo Pamoja?"

"Sifahamu,ninasiku nyingi sijawasiliana na ndugu wala jamaa wa karibu,nimeamua kuyaanza maisha mapya"

"Huyo kaka yako ni mnyama kabisa,inawezekana vipi umuibe mke wa mdogo wako?tena mdogo wako amekutafutia kazi baadae unamlipa hivyo?"

Niliinamisha kichwa chini kwa masononeko
"Huenda Mimi ndiye nilikuwa nalazimisha Mapenzi kwa Berther"

"Usiseme hivyo kelvin,kumbuka mlikuwa mnapendana tangu kidato cha kwanza,kila uliporudi likizo ulimkuta ,kwanini asingelikuambia mapema kwamba anatoka na kaka yako?hata kaka yako kwanini asingesema?"

"Kwa alichonifanyia kaka yangu sitamani hata kurudi nyumbani"

"Sasa kwanini usirudi na wakati wao wapo mwanza na kwenu ni Mara?"

"Kipindi nakuja dar sikuwaaga,kaka yangu akatumia nafasi hiyo kunisingizia kuwa nimemtelekeza mke wangu,familia nzima kuanzia mama yangu marehemu na ndugu zangu wakajenga chuki dhidi yangu,niliamua kuanza upya kutafuta maisha ili siku moja nirudi nyumbani nikiwa na pesa, bahati mbaya mama yangu alifariki mwaka Jana nikashindwa hata kwenda kumzika"
John akanigusa bega
"Sikuwa nafahamu haya ndugu yangu,hebu nikuombe uwe jasiri na kutokukata tamaa,naelewa msongo wa mawazo ulionao kila ukikumbuka maisha uliyokuwa unaishi na haya ya sasa"

"Kwa sasa mawazo yamepungua,ila mwanzo nilikuwa natamani hata kujiua"

"Dah aise"

Maongezi yangu na john yalikatishwa na Mteja aliyekuwa anaulizia dafu,nikaenda kuuza dafu na kumuacha john akiwa amekaa kwenye kiti.

Itaendelea......
💥Mke wa kevoo alitoka na kaka yake,wakamtengenezea kesi akafukuzwa kazi,kutoka kuwa mfanyakazi wa kampuni kubwa ,Leo hii amekuwa muuza Madafu.
Sɪᴍᴜʟɪᴢɪ﹕ 𝙈𝘼𝙋𝙀𝙋𝙀
SEHEMU YA NNE
_Mtaalam Star7_
*_______________________________*

**
Saa tatu usiku ndani ya nyumba moja nzuri ta kifahari anayoishi sunita jai na familia yake,kulisikika malumbano baina ya Baba na Mwana.
Baba yake na sunita (Mr Jai),alikuwa anamlazimisha mwanae kuolewa na mwanaume wanayemtaka wao.
"Sunita utake usitake lazima utaolewa" (Baba yake na sunita aliongea kwa hasira)

"Baba Mimi simpendi huyo mwanaume"

"Mama sunita kaa na mwanao umweleweshe,haiwezekani asiolewe na mtoto wa kiongozi,hivi unategema biashara zangu zitaendaje pasipo kudumisha uhusiano na viongozi?"(Mr jai aliongea mpaka mishipa ya shingo ikawa inamtoka)

Kipara cha Mr jai kililowana jasho,alikuwa anazunguka zunguka sebuleni akitamani kumpiga Kofi mtoto wake sunita.

Mama yake na Sunita anayefahamika kwa jina la Esha alikuwa amesimama pembeni na mwanae.
" mwanangu usijibizane na baba yako,hebu kaa kimya"

Mama sunita alikuwa anamtuliza mwanae ambaye alikuwa anatokwa na machozi.
Mr Jai akaingia chumbani kwa hasira akawaacha sebuleni watu wawili ambao ni mke na mtoto wake.

"Mwanangu naomba uketi tuongee" (Mama sunita alimbembeleza mwanae)

Sunita akakubali ombi la mama yake,kwa masononeko makubwa akaketi chini.
"Mwanangu pole Sana,ila naomba nikuulize maswali kadhaa"

Sunita akajifuta machozi halafu akamtazama mama yake
"Una mpenzi yeyote ambaye mmewekeana ahadi ya kuoana?"

Sunita akatikisa kichwa
"Hapana sina"

"Sasa Kama hauna kwanini usikubali kuolewa na mtoto wa Mbunge ili sisi biashara zetu ziende vyema?"

"Kwahiyo mama mnataka niolewe kwa sababu za biashara?hamuangalii mateso kiasi gani nitayapitia huko!,mama nilijua wewe ndio utakuwa mtetezi wangu kwenye hili kumbe na wewe unakuja kunididimiza!" (Sunita akaanza kulia)

Mama sunita akashusha pumzi.
"Nadhani unamjua baba yako,atafanya juu chini mpaka apate sababu inayokupelekea ukatae kuolewa,hapa nimekuuliza kwa upendo tu,Kama Una mpenzi niambie lasivyo yatakayowakuta Mimi Simo"

"Mama sikutegemea utaniambia hivyo,kwahiyo mnanitishia Sasa ama?Mimi ni mtu mzima mama siyo mtoto tena,nimesoma chuo nikamaliza ,huu ni muda wangu wa kujisimamia Kama mtu mzima"

Mama sunita akaanza kwa kuguna.
"Mh naona umekuwa mkubwa Sasa,siku hizi hautaki kabisa kusikia maneno kutoka kwa wazazi wako,Sasa nikuambie jambo moja,hiyo ndoa utafunga iwe kwa kutaka ama kulazimishwa,unadhani tulivyokupeleka chuo Kusomea biashara tulikuwa tunatumia pesa zipi?kampuni inahitaji umoja baina ya familia mbili,kupitia mtoto wa mbunge kuna mengi tutayavuna" (Mama sunita akasimama na kuanza kuondoka)

Mama sunita na mume wake walikuwa na jambo moja linalofanana,kila mmoja alitamani sunita aolewe na mtoto wa mbunge ili waweze kufanya biashara zao bila kupata pingamizi lolote, lakini pia mbunge huyu ni miongoni Mwa wafanyabiashara wakubwa jijini dar es salaam.

Sunita alibaki peke yake sebuleni akiwa analia,kitendo cha wazazi wake kumchangulia mume wa kumuoa kilimuuma sana,swali lake kubwa ni kwanini wamchagulie kwa sababu za kibiashara?kitendo hiki kinaonekana kama sunita ni chambo ama daraja la mafanikio ya familia yao.

Ingawaje sebule na Vito vilivyopo sebuleni ni vya thamani na kuvutia,lakini sunita hakuacha kutokwa na machozi,hakuna hata kitu kimoja ambacho kingelimpatia Furaha.

Sunita alianza kuongea peke yake.
"Nilipokuwa masomoni India walikuwa hawataki niwe na mahusiano, kila mwanaume niliyejaribu kuweka ukaribu naye walituma vijana wampige,nimemaliza masomo wakaniambia nije nchini kuendeleza kampuni ya Baba,hata mwaka haujaisha limeibuka jingine,kwanini wanapenda kunipelekesha ilihali Mimi ni mtu mzima?"
(Sunita alijifuta machozi kwa upindo wa shati lake).

**
Wakati sunita anaugulia maumivu nyumbani kwao,Mimi nilikuwa nimejilaza kitandani nikiwa na simu yangu ndogo,mawazo yangu yalikuwa mbali Sana.Siku ya Leo nimejikuta nikikumbuka maisha yangu ya zamani.

Nakumbuka kipindi naelekea kujiunga na masomo ya kidato cha tano,kaka na mke wangu(Berther) walinisindikiza mpaka stendi,kabla ya kuondoka nikamuomba kaka ahakikishe anamlinda berther maana ni mwanamke ambaye nilimpenda Sana na tuliwekeana ahadi nyingi.Nilizidi kuumia kwa sababu nilimkabidhi fisi bucha.

Tukio lingine ninalokumbuka ni siku ambayo nilitoka kazini mapema nikamkuta kaka na aliyekuwa mke wangu wakiwa wamekaa sebuleni kwa mikao ambayo sikuielewa,mke wangu alijifunga kanga halafu kaka yangu alivalia bukta nyekundu,waliponiona wakaonekana kushituka,laiti ningelijua mapema nisingeliteseka Kama Leo.

Usaliti wa mke wangu kwenda kuolewa na kaka yangu ndivyo vilinifanya nisitamani kupenda tena,Mapenzi yamesababisha undugu wangu na kaka yangu kuvunjika,sitamani hata kuiweka sura yake mbele ya mboni za macho yangu.Labda angelinidanganya kwa kutumia msemo uliozoeleka kwamba 'amepitiwa na shetani',huenda ningewaelewa na kusamehe.Lakini,kaka yangu hakutaka hata kuomba msamaha na badala yake Mimi nikaonekana ndiye mwenye makosa.

Kaka yangu wa toka nitoke aliuumiza Moyo wangu,vidonda alivyonipatia kupona kwake siyo Leo.
"Malipo yote ni hapa hapa duniani" (niliongea kauli ile huku nikilalia ubavu wa kulia)
Nikiwa najiandaa kuutafuta usingizi ,Simu yangu ikaanza kuita,nilipoitazama nikakuta namba ya sunita.
Niliipokea Simu kisha nikaiweka sikioni.
"Halo sunita"

Upande wa pili wa Simu akajibu kwa sauti inayotoka kwa mtu anayelia
"Halo kelvin,za wakati huu"

"Salama sunita,mbona Kama unalia kuna shida?"

"Mafua yamenibana wala siyo kitu kikubwa,nimekupigia kukuambia usiniletee dafu nyumbani,Mimi ndiye nitakuwa nazifuata hapo kijiweni kwako".

"Kuhusu hilo wala usijali,kwangu Mteja ni Mfalme"

"Asante Sana"
Sunita akakata Simu,ukweli ni kwamba sunita hakutaka nionekane karibu na nyumba yao kwa sababu Baba yake ameahidi kuwafanyia jambo baya wale wote wapo karibu na mwanae,sunita hakutaka kuniingiza matatizoni.

Kwakuwa sikuwa nafahamu kinachoendelea kwa sunita,nikachukulia ni jambo la kawaida kwangu.

**
Nilipitiwa usingizi mnono,lakini ilipofika saa nane usiku nikaanza kuota ndoto ya kutisha,ndoto hii ilinifanya niweweseke kitandani mpaka kuanza kutokwa na jasho.
Nilikuwa naongea peke yangu ndotoni,hii ndoto ninayoota ndiyo ilipelekea haya yote.

"Hapana ,hapana" (ilikuwa sauti yangu nikiwa kitandani)

Huenda Kama kungelikuwa na mpita njia anayepita nyuma ya dirisha la chumba changu,basi angelitamani kujua ni kipi kinachonifanya niseme hapana.

"Muacheni huyo,uwiii" (nilizidi kuongea peke yangu)

"Mamaaaa" (yalikuwa ni mayowe baada ya kushituka kutoka usingizini)
Nilikuwa nahema juu juu,kifua changu kilipanda nakushuka Kama dayaflamu ya hewa,nilipapasa kitandani nikachukua Simu,nikawasha taa yake kisha nikaelekea ilipo swichi ya kuwasha taa za chumbani nilizokuwa nimezizima,nikatupa macho ilipo ndoo ya maji ya kunywa ,nikachukua kikombe na kuchota maji.

Nilianza kunywa maji huku nikitafakari ndoto niliyotoka kuiota muda mchache uliopita.Nilimaliza kunywa maji, nikarudisha kikombe mahala pake.
Nilisimama kwa takribani dakika mbili nikiwaza maana halisi ya ndoto niliyoiota
"Au kwakuwa sijasali wakati wa kulala? Au niweke mkaa chini ya kitanda?"
imani nyingi za watu huwa wanasema ukiweka mkaa chini ya kitanda hauwezi ota ndoto za kutisha.

Nilitafuta mkaa nikauweka chini ya kitanda upande ambao naegesha kichwa, nikapiga magoti na kusali,nilipomaliza kusali nikajilaza kitandani na awamu hii sikuzima taa.
Baada ya nusu saa kupita tangu nilale kwa mara ya pili,nilijikuta napatwa na ndoto ile ile niliyoota muda uliopita,nikashituka kitandani huku macho yakinitoka.

"Hii ndoto ina maana gani?kwanini niiote mara mbilimbili?kuna nini?" (Maswali yangu hayakuwa na majibu)

Usiku wa Leo umekuwa usiku mrefu Sana kwangu,ndoto mbaya zilizojitokeza mara mbili ndizo zimeninyima usingizi,ilinibidi nibaki macho mpaka kutakapo pambazuka.

Itaendelea......
💥NDOTO GANI AMEIOTA KEVO?
Soma mpaka mwisho kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Sɪᴍᴜʟɪᴢɪ﹕ 𝙈𝘼𝙋𝙀𝙋𝙀 SEHEMU YA TATU  >>> https://gonga94.com/semajambo/s-mapepe-sehemu-ya-tatu
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

TREVOR CHALOBAH 🫡

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 28💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

🌹I MISS YOU 🌹

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 22💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest