Endelea ๐ป
"Una maanisha Sultana ndio Boss wako?" Liam aliuliza
"Ndiyo....."Vivi alijibu akiwa ana tiririka machozi
Bi. Fatma, Ali na Liam walishangaa sana kwa namna Sultana anavyonekana mtakatifu machoni kwao
"Na yeye ndio sababu ya Meli ya Star kuzama.... Polisi Tee alimuingiza kwa siri ndani ya mabehewa ya mizigo ili tu asafirishe madawa ya kulevya!....Meli ni sawa na chupa huwezi kulazimisha kuijazia chai ilihali unaona imejaa, sababu ya ujinga wako watu 280 wamezima kama mshumaa" Sona aliongea akijitia kuchanganyikiwa kupita kiasi
Alisahau kama si yeye kumuweka Dada yake ndani ya mabehewa ya mizigo, Meli isingezama.
Sultana hakuonesha kupaniki hata kidogo, kama kawaida yake aliachia tabasamu. Muonekano wa macho ya Vivi ulitosha kumuambia mtu huyu ni mateka....
"Ile siku anaingia hapa akijitia amelifananisha jengo hili na hekalu nina uhakika alikuja kutubu dhambi zake kwa kumuua Marmar" Sona alizidi kumkandamiza Dada yake
"Imetosha...." Liam alimzuia Sona kuongea kisha akamgeukia Sultana
"Naomba tusikie maelezo kutoka kwako....kwanini ulimuua Marmar na kwanini uliingia kisiri siri kwenye Meli ya Star" Liam aliuliza
"Kila kitu kaeleza Sona, pengine unataka kusikia direct kutoka kwangu nitarudia" Sultana aliongea kisha akasimama
"Nilimuua Marmar kwa sababu alikuwa ni kikwazo kwenye biashara zangu.... Meli ya Star imezama kwa sababu nilihitaji kusafirisha madawa ya kulevya bila kusumbuliwa na watu wa usalama si ndiyo hivyo Mhe. Polisi" Sultana alimuuliza Mdogo wake
Sona alisimama akamtia kibao Dada yake kwa namna anavyoongea kwa kujiamini.
"Hakuna haja ya kumpeleka Polisi.... naomba mniruhusu ni mnyonge mbele ya picha ya Marmar" Sona aliongea
Pamoja na ushahidi kutolewa lakini bado moyo wa Bi. Fatma pamoja na Liam uligoma kuamini kama binti huyu mrembo ndio mhusika.
"Ni kweli hatuwezi kumpeleka Polisi, kila kitu tutakimaliza wenyewe....Ali nenda ukalifungue tundu la Simba, kama kweli Sultana ni kahaba na Muuaji hatatoka salama lakini kama vyote hivi ni uongo atatoka salama" Bi. Fatma aliongea
Watu wote walishtushwa na uamuzi wake, kulingana na imani yao ya dini tundu la simba ni mzani unaopima utakatifu na uhalifu.
Sona aliachia tabasamu ndani ya moyo wake, baada ya tundu la simba kufunguliwa alimshika mkono Dada yake akampeleka...watu wengine walisimama hatua kumi nyuma
"Dhambi yako ya Ukahaba ndio itakujengea kaburi tumboni mwa Simba hao na si ushahidi wa Vivi....kosa lako ni kutembea na Liam" Sona aliongea
"Sona.... naomba ukumbuke maisha yako yote kama si Mimi kupoteza bikira yangu nikiwa na miaka 16 ungekufa ukiwa na miaka 10.....kwa sababu yangu Mimi upo hai na hata unapendeza katika sare za Polisi" Sultana aliongea kisha akajitosa mwenyewe ndani ya tundu la Simba.
Sona alifunga kisha akampatia funguo Bi. Fatma
"Huenda hizo kelele ni za hofu za kuona Simba au minofu yake ipo ina tafunwa. Kesho saa kumi na mbili asubuhi tutakuja kujionea nini kinaendelea" Bi. Fatma aliongea kisha akaondoka
๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป
Mida ya usiku Liam hakuweza kupata usingizi....moyo wake uligoma mara 1000 kuamini kuwa Sultana ana husika kwa lolote
Hata ile siku anamueleza kuwa yeye ni Kahaba hakuamini na hata kama ni kweli basi anafanya hivyo kwa sababu maalumu.
"Familia yako itakuwa salama kama wewe utakufa.... nisamehe kwa kwenda kinyume na makubaliano yetu lakini sina imani na wewe" Sona alimuambia Vivi kisha akampiga risasi ya kichwa
"Sultana....ha...wezi kufa kwa sababu ni chaguo la Marmar, ni lazima ataolewa na Liam..." Vivi aliongea
Sona hakuwa tayari kusikia maneno yake alimuongezea risasi nyingine kisha akamtupa kwenye mto uliokuwa una mwaga maji yake katika bahari kuu ya Odes
Alirudi ndani ya Jumba La Dhahabu kusubiria kupambazuke
Saa kumi na mbili kamili watu wote walikusanyika karibu na tundu la Simba.
Bado walikuwa wanasikia miungurumo hii ilitosha kuwaambia huenda Simba wanamalizia mifupa ya Sultana
"Nenda kachungulie ndani ya tundu la Simba kisha utupe majibu...." Bi. Fatma alimpatia funguo Ali
Sona alimkwapua alihitaji kuleta majibu yeye lakini alinyanganywa ufunguo
"Hata Malaika huwa wanapeana zamu ya Ulinzi....safari hii atafungua Ali" Bi. Fatma aliongea
Sona alituliza komwe lake....Ali alichukua funguo kisha akapiga hatua.
Alifungua tundu la Simba taratibu, kitu alichokutana nacho kilimshtua.
Aliwageukia watu wote kutoa majibu....
Itaendelea ๐ฅ.