Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani
Mawasiliano: 0763 595006
Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y
*ONYO*
Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.
KARIBU
Nanah aliingia uwani kwake na kufumba macho yake huku akijitizama kwenye kioo kidogo.
"Nimefanya nini mimi? Kwanini nimefanya hivyo? Ni kwaajili ya kumkomoa Brown au ni nini sasa? Bieber atanionaje? Nimejirahisisha sana kwake wallah".
Nanah alibaki akijisikitikia alichokifanya na wakati huo Bieber alikuwa macho kitandani akitabasamu kwani alikuwa akimuona anachokifanya uwani.
Aliinuka kutoka kitandani na kuvaa nguo zake kisha akaondoka na kwenda kwake.
Nanah alitoka uwani baada ya nusu saa na hakumkuta Bieber pale kitandani zaidi ya ujumbe wa Nimeondoka.
"Ameondoka? Mbona hajaniaga?" Aliuliza Nanah na kuweka kile kikaratasi chini kisha akaanza kwa kuvuta shuka lililokuwa kitandani na kulipeleka uwani kwenda kuliroweka usiku ule.
Bieber alikuwa amesimama kama kawaida yake kwenye kibaraza chake na kumtizama.
Nanah alitoka uwani akatandika shuka jingine na kujitupia zake kitandani.
Bieber alisimama pale kwa nusu saa zaidi na alipohakikisha Nanah amelala aliingia sasa ndani akiufunga mlango wake wa upande ule na kuingia bafuni kwaajili ya kuoga na hapo naye alilala.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Palipambazuka asubuhi na Nanah aliwahi kutoka kwake kwelikweli akiwahi tax aliyoikodisha kwani hakutaka kabisa kukutana na Bieber kwa siku hiyo.
"Vipi kuna mahali unawahi?" Aliuliza Bieber aliye ingia ndani ya tax ile na alishaamka mapema sana akiwa anafanya mazoezi huku anatizama chumba cha Nanah na alishangaa kwanini leo ameamka mapema hivyo na hapo aligundua Nanah anataka kumkimbia na kuona haya kwa kile walichoweza kukifanya jana usiku.
"Ooohh Bieber" aliita Nanah akijifanya anashangaa kumuona.
"Yes".
"Nimeamka leo mapema kwasababu nataka nikaanze kushona nguo".
"Oohh vizuri sana, nitakusaidia kwenda kuchagua baadhi ya vitambaa. Hope utaniruhusu".
"Mmmh hahaha ndiyo" alijibu Nanah akijichekesha na kugeukia upande mwingine.
"Aibu gani hii jamani" alijilalamikia mwenyewe na kugeuka upande aliopo Bieber kisha akamchekea.
Bieber alitabasamu akimtizama Nanah kiaina hivi.
Nanah alitizama mbele na kukaa akitulia.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Jana ulimaanisha nini ulipomwambia mama mimi ni mwongo?"
Brown alimtizama Shalha pasina kumjibu na wakati huo walikuwa mezani wakipata kifungua kinywa.
"Brown hivi kwanini unani hukumu kwa matukio yaleyale ya zamani".
Brown bado hakumjibu kitu kabisa.
"Brown nazungumza na wewe" alisisitiza Shalha
"Embu niache basi, unataka nini wewe?"
"Kuna nini tena asubuhi asubuhi?' Aliuliza Bi Everline.
"Hamna mama" alidakia Shalha juu kwa juu na kutabasamu
"Nikuongezee juisi kidogo mume wangu?"
Brown alimtizama pasina kumjibu kabisa kisha akaendelea zake kula.
"Ila mwanangu una gubu wewe, yani unaulizwa vizuri lakini kimya kama vile hujasikia jamani".
Brown aliinuka na kuacha kifungua kinywa mezani.
"We Brown jana usiku ulifanya hivi hivi, unataka kupata Madonda ya tumbo eee?" Alihoji Bi Everline na Brown hakumjibu chochote kile zaidi ya kuingia chumbani kwake.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Nitalipia mimi" alizungumza Bieber akitoa wallet yake na Nanah alijibu Sawa
Kisha akarudisha pochi yake na kutaka kuanza safari
"Subiri usiende mahali"
Nanah alisimama na kuanza kutizama watu wachache ambao wameshaanza kuingia kwenye kampuni.
Bieber alitoa kitambaa chake mfukoni na kukisokota vizuri kisha akamsogelea Nanah na kupeleka mkono wake shingoni akisogeza kola iliyokuwa fupi.
"Unataka kufanyaje?"
"Kufunika love bite 🫦 yangu" alijibu Bieber na Nanah aliweka mkono shingoni mwake.
"Toa bhana kamkono kako".
"Inaonekana?"
"Toa basi mkono".
Nanah aliutoa taratibu na Bieber alimfunga vyema kitambaa kile shingoni.
"Uko sawa sasa" alisema hilo Bieber na Nanah alijishika pale alipofungwa kitambaa.
"Asante".
"Unapaswa kunisaidia mimi"
"Baadae nitakwambia, twende ndani".
Bieber aliweka mkono wake mfukoni akitangulia huku Nanah akiwa ametoa mkono wake akiamini Bieber alitaka kumshika mkono.
Aliurudisha mkono wake chini na kumfuata Bieber nyuma akiwa ameishilia kuishika tu pochi yake kwa mikono miwili.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Brown alifika kwenye kampuni na alipokuwa akipita alitupia macho yake kwenye ofisi anayofanyia kazi Nanah.
Alitabasamu alipomuona Nanah akifanya kazi zake asubuhi ile alipotaka kuongeza hatua zake kwenye kumsalimia alimuona Bieber ofisini kwake akiwa yuko busy anamtizama Nanah kwa tabasamu pana sana.
Aliishia kuwatizama tu na kuondoka akienda ofisini kwake.
"Za asubuhi jamani" alisalimia Bob aliyefika pale na kum busu Nanah shavuni kama vile mashoga kindakindaki.
"SALAMA, vipi wewe umeamkaje?"
"Salama kabisa. Nataka nikuonyeshe mchoro wangu yani sijalala usiku kucha nilikuwa niki design" alizungumza hilo Bob na kuutoa mchoro akimuonyeshea Nanah.
Nanah aliutizama kwa mshangao kidogo kwani ni mchoro ule ule ambao jana tu aliukamilisha.
"Una uonaje?" Aliuliza Bob.
"Vizuri ume design vizuri sana" alijibu Nanah akitabasamu.
"Yani na nimeuona ni mzuri nataka nikamuonyeshe Mr Handsome"
Bob alitabasamu kinafiq na kwenda ndani kwa Bieber.
"Good Morning Mr Handsome"
"Good Morning" alisalimia na yeye Bieber.
"Yani sijalala kabisa usiku kucha embu ona namna macho yangu yalivyo".
"Pole sana Bob"
"Asante" alijibu Bob na kuutoa mchoro akimuonyesha Bieber aliyeushangaa na kumtizama Nanah aliyempa ishara ya asiseme chochote.
Alimtizama Bob Risky aliyekuwa akisubiri majibu kutoka kwake.
"Umefanya vizuri sana, nimeupenda unaweza kwenda kuushona sasa"
"Waoooo ahsante Mr Handsome. Yani nilijua tu kwa mchoro huu lazima unipe nafasi Asante sana" alijibu Bob na kutoka akiwa na furaha alimfuata Nanah na kumuonyeshea ule mchoro.
"Mr Handsome amenikubalia na kuniambia nianze kuushona".
"Jamaniiii, hongera"
"Asante ngoja niende nikawaonyeshe na wengine design yangu".
"Sawa" alijibu Nanah akitabasamu na Bob alim busu akatoka mbio mbio.
Bieber alimuita Nanah ofisini kwake kwa ishara ya mkono wake mmoja.
Nanah aliinuka na kwenda.
"Ile design imefanana na yako, yani ni vitu vichache tu ndo vimebadilika pale".
"Najua lakini hujamsikia Bob alivyosema? Usiku kucha amekuwa akiiandaa"
" mmmmhhh haiwezi kufanana namna hiyo bwana, kuna kitu pale"
"Angekuwa Doy au Kurwa ningesema wameniibia lakini ni Bob hawezi kufanya hivyo"
Bieber alibaki akimtizama.
"Bado nina michoro mingine miwili nita iandaa hii"
"Sawa kama ndo unataka hivyo" alijibu Bieber.
"Asante".
"Nanah" aliita Bieber
"Abeee".
"Usimuamini sana huyo shoga kama ameweza kuchukua design yako na kujifanya ame design yeye basi anaweza kukufanyia vitu vingine vya hatari".
"Bob Risky hana shida niamini mimi".
"Hapana sitaki" alijibu Bieber
"Hutaki?"
"Kuwa makini naye na nina maanisha hili sawa?"
"Sawa asante kwa kujali" alijibu Nanah na kuondoka zake.
Bieber alibaki akimtizama kwa nyuma na hapo alimuita.
"Nanah"
"Abeee"
"Umependeza".
"Asante " alijibu Nanah na kuondoka zake.
Itaendelea In Shaa Allah.