Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

KATIKATI YA CHUMBA CHANGU KUNA KABURI SEHEMU YA 14

1st Aug, 2025 Views 20

........

ANZA NA LIKE KISHA SOMA VIZURI.......Kupambazuka kwa siku mpya kulienda sambamba na mimi kurudi zangu nyumbani, sikutaka kukaa sana katika eneo lile isipokuwa nilimuahidi Mzee kwamba kama nikikamilisha kile ambacho nimekidhamiria basi ningerudi kumpa majibu, naye alinipa baraka zote. Niliondoka kwa Mzee majira ya saa moja asubuhi ambapo nilipitia nyumbani kwa Debora na kuweka mazingira sawa kama ilivyokuwa ada yangu.

Siku hii sikutaka kuweka makazi mengi sana, nilijiambia kwamba natakiwa kusafisha kuhusu kupika halikuwa suala la muhimu sana bali jioni itakapoingia ndio nitarudi tena kupika na kama ingewezekana basi ningelala mahala hapa ili siku inayofuata niwahi kwa mganga. Baada ya kuhakikisha kwamba kila kitu nimeweka sawa, nilifunga safari ya kurudi nyumbani kwangu.

Hatua katika ardhi niliingia barabarani na kukatisha baadhi ya chochoro hatimaye saa nne asubuhi nilifika nyumbani lakini nilikuta nyumba ikiwa imetulia mno. Hakukuwa na sauti yoyote ambayo nilikuwa naisikia. Nikajiuliza watu wamekwenda wapi au kuna kitu ambacho wanakijua kinaendelea. Nilikuwa ni mtu mwenye mawazo kiasi lakini baadaye nikajiambia kwamba acha niweke mambo yangu sawa ili muda wa kazi utakapofika nikamilishe kila kitu.

Macho yangu hayakuacha kutazama saa yangu katika simu hadi naingia chumbani, nilikuwa ni mtu ambaye nakwenda na muda sana. Sikutaka kupoteza ama kwenda kinyume na masharti. Nikiwa chumbani nilienda katika dressing table kwa mara nyingine na kutazama nini nitakiona lakini bado sura ya Mama mkwe ilijitokeza. ‘Nitakuwa nimefanya jambo la maana sana kama mama mkwe nikifanikiwa kumuua, sababu huyu ndio ameanza kutembea na mtoto wake, ndio mpango wangu unakwenda kukamilika sasa” nilisema kisha nikatupa macho kitandani.

Nilihisi kama kulikuwa na utofauti hivi katika kitanda, nikawekeza umakini wa hali ya juu. Niligundua kwamba kulikuwa na maji maji, pia harufu ya marashi ikapita katika pua yangu ‘Itakuwa kuna mtu aliingia enh?” nikajiuliza pasi kupata jibu. Nikatazama katika kabati, niliona baadhi ya nguo zikiwa zimadandazwa mno. Nikapekua kutazama chupi zangu kama zipo, niliziona lakini zilikuwa zina maji maji pamoja na harufu ya marashi. Nikahisi jambo huenda zilikuwa zimebebwa na mtu ambaye aliingia ndani.

Sasa nikajiambia kwamba kwa namna yoyote ile sitakiwi kukaa pale kitandani hata iwe vipi. Kama nilikuwa nimeoteshwa hivi, kumbe ni kweli wao walikuwa wameingia na kitu cha kwanza kukifanya ilikuwa ni kunyunyuzia dawa ili nitakapolala basi nife chelewe kuamka na mpango wao ukamilike.

Kwa hili ‘walifeli’ maana sikudiliki hata kukigusa kile kitanda hata zile chupi niliziacha na kujiahidi kwamba sitakuja nivae hata moja katika maisha yangu. Basi, niliinama uvunguni na kuchukua kisu ambacho nilipewa na yule mganga kisha nikatoka nje ambako nilikaa kwenye bustani huku macho yangu yakiwa getini kutazama wanaingia saa ngapi? Nilikaa kwa lisaa la kwanza yaani ile saa nne ikaisha, kisha lisaa la pili likaingizana lakini kuingia kwa lisaa hili yaani saa tano kuliambatana na wingu nzito ambalo lilitanda na kufanya jua lisionekane.

Nikaona nakwenda kushindwa kukamilisha mpango wangu maana ili nipate kivuli basi ilihitajika kuwaka kwa jua. Nilikaa pale nje hadi saa sita kamili muda ambao walirudi kina Sofia akiwa yeye, Mume wangu pamoja na Mama mkwe wakiwa ni watu wenye furaha mno. Mama mkwe na mume wangu walishikana mikono, kibaya ni kwamba pindi waliponiona walipigana hadi mabusu huku Sofia akiwaiga na picha.

Walifurahia kile ambacho walikifanya, walifurahi kwa kuona kwamba wapo sahihi. Jua limezama na hakuna kitu ambacho naweza kukifanya. Nilijikuta nikiwa ni mtu ambaye nimejawa na hasira kuliko kawaida, niliomba Mungu aweze kuleta jua lakini haikuwa hivyo. Hadi muda ambao niliambiwa nifanye tukio ulipopita sikuwa nimechoma kivuli, saa saba kamili ikwa mbele yangu pasi jua kuwaka. Nilibaki na kibarua kizito ambacho sikujua nafanyaje ili niweze kukimaliza.

Nilirudi zangu ndani nikiwa nimenyong’onyea mno, moyoni mwangu nilikuwa na hasira. Nikatamani nichukua maamuzi mkononi kwa kumchoma choma mama mkwe ili akili imkae sawa lakini nilihisi nitazidisha matatizo. Nilipofika sebureni nilimkuta Sofia akiwa ni mwenye furaha kupitiliza. Alinitazama kisha akasema.
“Mjini tumekuonesha sisi ulikuwa hujui hata chipuputa ilipo halafu unataka kujifanya kuwa mjuaji, lipo wapi jua sasa?” maneno yake yaliniumiza sana, nikatamani kumjibu lakini mdomo uliweza kufunguka ila ubongo hakuwa tayari kuzalisha maneno. Nikajiambia bora nipige zangu kimya ili kumuacha yeye aendelee kuzungumza.
“Kama huna radha unataka Mama asile, wewe vipi bwana” Sofie aliendelea kunitemea shombo.

Maneno yanauma, maneno yanazalishwa na ulimi ambao umezungukwa na meno 32 lakini yanaweza kuwa makali na kuutesa moyo kuliko hata meno yenyewe. Siku hii niliumia kuliko siku zote kwani nilipopiga hatua kukaribia katika chumba changu, nilisikia miguno ya kimahaba kutoka katika chumba cha mume wangu. Walikuwa wakifanya mapenzi, walikuwa wakikamuana katika kitanda changu ambacho nilienda mwenyewe kwa fundi na kumwambia nataka kitanda cha aina fulani.

Masikio yangu yalipitisha sauti za change ambazo zilikuwa zikilalamika mno. Mama mkwe alikuwa akilalamika kama mtoto mdogo, alisifia utamu wa mwanae hata mume wangu naye alikuwa akilalamika kwa kugumia. Ndio, walikuwa wanafanya mapenzi, walikuwa wanakamilisha hitaji lao. Walikuwa wanautaka utajiri na njia pekee ilikuwa ni hii ya Kazumar kufanya mapenzi na Mama yake.

Miguno ilipozidi kuzama katika masikio yangu, ilienda kuvukua hasira ambazo sikupanga kuzionesha lakini ilinibidi. Awe! Awe! Awe! Kwa jinsi ambavyo alikuwa akilalamika unadhani hata nilivumilia kwa kuingia chumbani kwangu, labda sikuwa mimi.

Kwanza nilienda kugonga mlango kisha nikasimama kwa pembeni, mkono wangu wa kulia ulishika kisu vizuri kwa ajili ya kumchoma yoyote yule ambaye angetokea. Kijasho kilinitoka huku nikiwa na hasira kiasi kwamba hadi nilihisi nataka kupasuka. Bora ufumanie kwa meseji kuliko kuona moja kwa moja, inauma, inaumiza na inavujisha moyo damu. Nilikuwa njia panda nisiwe uongo. Nilikuwa nipo tayari kubeba kesi ya mauaji na kama walikuwa wabishi kufa basi ningeona siku hii ingekuwaje kama wangekufa ama lah.

Nikiwa mahala hapa nasubiri yoyote atokee mara alikuja Sofia ambaye alinitazama kwa dharau kisha akatingisha makalio yake madogo na kusema.
“Huna nyota ya utajiri, huna bahati ya kushika mimba, unatazama wenzako wakilalamika si ndio? Nawe unataka? Hahaha! Nenda kasafishe nyota mama, upo hapo?” chambo lake lilinifika kunako, nyongo yangu ikatibuka mithili ya ngisi aliyeona adui, nikasema huyu kiumbe labda hanijui vizuri. Nikashika kisu vizuri na kupiga hatua kumsogelea.

Sofia alijua sasa nimekasirika, alitambua kwamba huenda lolote lile lenye kumdhuru lingemfika. Nilimuoa akirudi nyuma kisha akashika kitu kama kombe sijui ni nini lakini kilikuwa na rangi nyekundu kisha akachora msitari akasema.
“Mwanamke wa shoka si ndio, vuka sasa kama kweli wewe mwanamke na uchezwa unyagoni”
“Sofia nitakuua! Cheza na vyote lakini sio mimi, nitakuua Sofia” nilizungumza kwa jazba, kusema kweli kuvuka nilitamani ila uwoga ulikuwa nyuma yangu. Nilikuwa na hofu mno maana ule msitari ni kama kuna nyakati ulikuwa ukimelemeta hivi.
“Vuka si unajifanya umekomaa mavuzi, si unajifanya umeanza kukojoa mkojo wa kuchimba. Vuka sasa kama sitakuzika ukiwa mkavu ka….” Hakumaliza hata kuzungumza.

Nilinyoosha mkono wangu na kumshika ‘brauzi’ yake kisha nilimvuta aje kwangu, kwa bahati nzuri alifanikiwa kuvuka ule msitari akaja upande ambao mimi nilikuwepo. Nilimwangusha chini na kumshika vyema kisha nilimkalia kwa juu na kuanza kumpiga ngumia ya kwanza, pili, na tatu hivi. Unajua Sofia hakuwa na nguvu licha ya mikwara yote, alikuwa ni lelemama ambaye amejaliwa kuwa na mdomo wa kukutisha na kuogopesha. Nami nilihakikisha kwamba nampiga huku kisu kikiwa kimedondoka kwa pembeni lakini nilifanikiwa kukiokota.
‘Sofia nakuua, nenda kawasalimie kuzimu Malaya wewe” Nilisema kwa kufoka huku nikishika kisu vizuri
“Niache! Mama ananiua” Sofia alilalamika baada ya kuona nimeshika kisu. Nikafumba macho kwa ajili ya kumchoma, nilifanya hivyo nisiwe muongo.

Nilichoma visu mara nne katika eneo la kifua chake, nilichoma kiasi kwamba damu zilikuwa zikirukia katika mwili wangu nami sikujali lolote lile. Sofia ambaye alikuwa jeuri, mjuaji na mtu ambaye aliongea maneno ya shombo. Alikuwa ni Sofia ambaye anaaonja mauti, anaonja kufa na anaonja maumivu makali ya kuchomwa chomwa na kisu. Mdomo wake uliruhusu kutoa damu, pumzi akazivuta kwa shida. Nikazamisha kisu katika jicho lake na kukiacha. Hasira zilinifanya kuchukua maamuzi ambayo hayakuwa sahihi, hasira zilinifanya nimchome Sofia ambaye alikuwa chini akigaragara hivi nadhani sijui ndio alikuwa akifa hata sielewi maana kwa wakati ule nilikuwa nimechanganikiwa na mwenye hasira mno.

Nikiwa ni mwenye hasira sasa nilikumbuka kuhusu kauli ambazo niliambiwa na Mganga wa kwanza kwamba mchawi hafi kwa kuchomwa chomwa na visu lakini siku hii Sofia alionekana kabisa kuelekea kibra, sijui unanielewa naposema kibra yaani namaanisha kwamba alikuwa akipoteza maisha. Mara ghafla. Niliona Mama mkwe akitoka vangu wangu huku akiwa na chupi
kilichokaa pembeni pamoja na sidiria ambayo haikufunga vizuri.
“Mungu wangu! Umeua?” Alisema kwa sauti kubwa. “Mwanangu mimi! Mwanangu mimi, mwanangu” Mama Mkwe hakuacha kulia tena kwa sauti mno.
“Mama! Nani kafa?” sauti ya Kazumar kutoka chumbani nikaisikia.

Niliona sina sababu ya kuendelea kukaa katika eneo lile badala yake niliingia chumbani kwangu kisha nikafunga mlango na kukaa katika dressing table. Kilichofuata ilikuwa ni macho yangu kuingia mkataba wa muda na machozi, nililia kwa yanayoendelea. Nililia kiasi kwamba hadi kichwa changu kiliwaka moto, mwili haukuwa wangu kabisa. ‘Mungu wangu najua mimi sijadhamiria hili lakini ningefanyaje? Kama nakosea masharti nisamehe mimi! Nimefanya haya yote kwa ajili ya Debora sikuwa na jinsi ningefanyaje sasa kama mtu ananiambia mambo ya kipuuzi. Ningefanyaje unadhani Mungu wangu, ona nateseka na Debora, nateseka na maisha ya hapa nyumbani kwanini usinipumzishe, nateseka Mungu wangu nateseka” nilizungumza maneno haya huku machozi yakiendelea kunitoka.

Nilikuwa katika wakati mgumu, nilikuwa katika kipindi ambacho nilimuhitaji sana Mungu kuliko kitu chochote katika maisha yangu. Njia panda ilikuwa mbele yangu, sikujua ni kweli kama Sofia amepoteza maisha ama lah lakini kwa wakati ule nilisikia vilio vikiendelea kwa nje nikajua kwamba wafiwa walikuwa katika msiba. Huyu ndio nilikuwa Zamda mpya, Zamda ambaye walimtengeneza wao wenyewe.

Nikiwa adondosha machozi, taratibu nilipeleka macho katika dressing table. Nilikutana na sura ya Mama mkwe bado ikiwa nyuma yangu. Nikawaza ‘inamaana bado natakiwa kumuua na sio Sofia au nimekosea masharti?’ swali hili liliendelea kunisumbua mno. Nikapiga hatua hadi katika dirisha kisha nikatazama kwa nje kama kulikuwa na jua lakini halikuwepo badala yake ni mvua ya rasharasha ama manyunyu ndio ilikuwa inaanza.

Nikawaza na kuwazua kipi nikifanyaje? Wazo pekee ambalo niliona lingenifaa ni mimi kurudi kwa Debora kisha kufungia kuku na baada ya pale nielekee kwa Mzee kumpa majibu ya kile ambacho nimekifanya. Basi niliona ni muhimu kufanyia kazi mawazo haya mawili. Niliondoka nyumbani nakumbuka ilikuwa saa tisa kisha nikaenda kwa Debora ambako nilipika na kula, nikaoga na kubadilisha nguo ambapo nilivaa nguo za Debora huku nikisubiria muda ufike ili niende kwa Mzee.

Vuta picha haya maisha ambayo nilikuwa naishi, yafikirie maisha ya mwanamke Tajiri ambaye alikuwa anaishi katika jumba nzuri lakini amani ya kumiliki jumba hili hakuwa nayo. Vuta picha ya mwanamke ambaye ana kila kitu katika maisha yake lakini hakuwa anavitumia, vuta picha ya mwanamke ambaye anapambana na uchawi ili kuwa huru. Vuta picha ya mwanamke ambaye hana thamani mbele ya mume wake na familia yake. Kisha vuta picha ya mwanamke ambaye alimtoa mwanaume katika umasikini hadi kuja kuwa Tajiri halafu niweke mimi hapo kisha niambie nilikuwa na hai ya kupitia haya. Halafu vuta picha ya mwanamke muuaji kisa tu alikuwa akijitetea anakuwaje, basi huyo ndio nilikuwa mimi.

Wakati haya napitia hakukuwa na mtu yoyote ambaye alikuwa akifahamu katika upande wa kina Debora hasa mumewe ambaye ni zaidi ya miezi saba sasa amesafiri na kwenda Uingereza kibiashara maana alikuwa ni mtu wa biashara sana. Sikujua atarudi lini ijapokuwa Debora aliwahi kuniambia mara kadhaa kwamba huenda mume wake angerudi muda wowote ule.

Kumbe siku hii ndio alikuwa akirudi ambapo wakati nikiwa nimejiandaa vizuri kuondoka kuelekea kwa Mzee, mlango wa getini ukagonga. Nami nikataka kujua ni nani? Nilinyanyuka na kwenda kufungua, macho yangu yakakutana na mume wa Debora ambaye alikuwa akiitwa Frank Patrick. Wawili hawa walifunga ndoa miaka miwili nyuma lakini hawakubahatika kupata mtoto.

Frank sikuwa nimezoeana naye kwa sana, mara chache sana ungekuta nazungumza naye. Sasa siku ile alikuwa mbele yangu, kibaya ni kwamba alikuwa akifahamu baadhi ya mambo ambayo aliambiwa na majirani kwamba mke wake hayupo pale nyumbani lakini kumekuwa na mtu ambaye amekuwa akiingia asubuhi kisha anaondoka jioni, mtu mwenyewe ni mimi.
“Shemeji!” nilijisemesha huku nikimtazama Frank aliyekuwa ameshuka katika Taxi
“Mke wangu yupo wapi?” swali la kwanza ambalo nilitakiwa kujibu kushujaa lilikuwa mbele yangu, kwanza nilimeza fundo kubwa la mate kisha nikamtazama kuanzia juu hadi chini.
“Yupo kwa mganga ila naomba twende” Nilisema hivyo, unajua nilijiamini sana kwa sababu niliona kwakuwa nimemuua mtu mmoja pale nyumbani basi kila kitu kitaenda sawa na huenda hata Debora atakuwa yupo salama kama sio kupona kumbe sikujua kwamba yule ambaye nilikuwa namuua pale nyumbani kwa kudhani ni Sofia alikuwa ni Debora…...Weka Like... Weka Kopa.... Weka Love Emoj......

Unasoma kipande kimoja kila siku, huchoki? Njoo ununue kwa bei yako mwenyewe. Sikupangii. WhatsApp, namba ni 0717255498..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

KATIKATI YA CHUMBA CHANGU KUNA KABURI SEHEMU YA 14  >>> https://gonga94.com/semajambo/katikati-ya-chumba-changu-kuna-kaburi-sehemu-ya-14
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest