Basi haikuchukua muda sana kama muvi ya kihindi ndani ya nusu saa tu tukafika mtipesaa , nikaagana na shogile wangu mama kibonge mie huyoo kila mtu akapita njia zake
Maana yeye kidogo maisha aliyawezea japo anauza supu ya mapupuπ€£π€£π,kajitahidi mwenyewe shoo wangu anakaa kwenye chumba cha afu thelethini kina umeme japo wa mawazo ila sio ligi langu mimi nipo na kachumba ka afu ishirini cha gizaaa na bado natamba mwanamke kujiamini π€£π€£
Kama kawaida nikawa nasokota kwato naelekea nyumbani kwanguuu ,njiani watu wote walikuwa wakinitazamaaa mie naskia rahaa balaa
Jamani nimenunua mcheleee kilo 15 staki wageni lakiniπ€£π€£,mimi sina siri jamani khaa basi mtaa mzima ukajua kua nimenunu mchele tena si kununua tu bali nimenunuliwa na danga langu jipyaaa
Dakika kumi tu zilinitosha nikawa tayari nimefika nyumbani
Da kibo nikupokee mchele??jirani mpambe aliniulizaa
Weee koma babu peleka njaa zako huko ,mwanamke usie jua kujituma weye kutwa kupanua miguu na kazi za maana zipo usije niharibia bajeti bure na miezi miwiliπ€£π€£
Hee da kibo yote hayo kisa mchele tule jirani aliongea
Hehehhehehe ntafute la undani nikupe yako ya ndani huo mchele unao??
Unataka ushindane na boss kibogaa??π€£π€£
Nikampandisha nakumshusha huyo nkachanja kwato hadi chumbani kwangu
Ukiachana na jinsi nilivo ila hii ngoma kuonewa ni no tena big NO sjui nipo sawa maana hili neno nililisikia kwenye muvi
Mie naitwa njoo kiumane aka mbabe wa mtaa
Basi na uchovu wangu mie nikatua mzigo nikajipandia kitandani kulala ,ilikuwa saa tisa hioo nkaja kushtuka saa 12 jionii tena simu ndo iloniamshaa mie pono
Haraka nikaiokota simu maana hata sikumbuki niliitupa wapi
Heeee jamani kiswaswa kiko wapi ?basi vurugu mechi ikaanza humo ndani tafuta tafuta hakunaa
Ikabidi nifungue kiroba cha mchele nikaingiza mkono ndo nikaipataπ€£π€£ππama kweli mmmmmmmh aaaaah
Muda huo ilikuwa imeshakata basi nikaangalia nani aliepigaaa nikagundua ni namba ngeni mfyuuuuuππππnikasema sipigi wala nini kama ana shida atapiga tena we ushaona wapi star kama mimi nikamnyenyekea mtuπ€£π€£π€£
Nikaitupa simu huko nikachukua ungo nikapima mchele kilo moja nikaanza kuuchambua huko sina stress najua nna gesi hivo
Japo nilikuwa naskia joto kutokana na mtembeo wa asubuhi ila nikiwaza foleni la chooni uwiiii naishiwa poziππππsi mnajua nyumba za uswahilini π€£π€£π€£π€£choo kimoja nyumba kumii
Basi nikamaliza kuchambua mchele nikawasha gesi mweeehππππpozi likaniisha kumbe gesi sinaaa sasa ntafanyaje na mchele nshauoshaa
Nikawaza mara mbili mbili ,nkapata akili nkatoka zangu hadi kwenye mianziii nikaokota vikunikuni ,nikatoka nnje ya nyumba ,nikakoleza moto mie nikaaanza kupikaa
Siku hio mtaa mzima ulijua kama mimi napika wali π€£π€£π€£na nilivo na sifa nilienda kupika kati kati ya njia watu wote wajue nini napika sinaga jambo dogoπ€£π€£π€£we usawa huu kupika wali mchezooiπ€£π€£
Basi buana wali wangu ukaivaa nikanunua na viutumbo vya mia tano nikachukua sufuria langu huyo ndanii
Nikaanza kutafuta sahani sasa kama tano hivi,nikapakua wali mkavu nikaanza kuupitisha chumba kimoja hadi kingine kwa wale wapangaji wenye midomo na roho za husda na mie ndo kiboko yaoooπ€£π€£π€£πππ
Nikaziweka kwenye sinia nikatoka hadi nnje kwenye kordoo
"Majiraniiiiiii majiraniiiiiiiii nawaita mara mbili ya tatu ni ndoto tena ya alinacha"
Walivosikia hivo tu wotr wakatoka nnje
Aya shoga zangu nimepika ubwabwa kama mjuavo dogo sina ,sahani hizo mkimaliza zirudi safii
Piga kelele kwa dada kibooo wakeeeeeπ€£π€£nikaitikia weuweeeeeeee
Labda tu niwahadithie nyumba nilopanga mimi wapangai wenzangu wote ni madada poa nadhani mnawafahamu na danguro lao lilikuwa huko kinondoni na hivo juzijuzi limevunjwa tu ,basi wapo nyumbani hoi hawana mbele wala nyumaa maana katikati wanapo
Hivo hata ukiwapa ugali mkavu kwao sherehe,sembuse waliii unaopita hata kwa chaiππ
Basi dada kiboga mie nikarudi ndani nikalala zangu mie sikutaka stress maaana nilikuwa nshashiba nilikula wali kidogo tu na vishombo vyanguuu
Usiku sasa majira ya saa tano nasikia simu inaitaa bwiiiii bwiiii bwiiiiiiiiiiii na vile kiswaswa kinavojua kukeraaa ukizingatia spika mbovi uwiiiiπ€£ππ
Nikajivuta nikapokea japo nina wenge ka usingizi hatariii
Haloooo??haloooo?
Kimyaaaaaaa loooooh yani kuna watu mnajua kupoteza vocha yani mtu unapiga halafu huongei ndo nini sasa ovyoooo na mie sijui kubembeleza acha nijilalie zangu
Basi nikajitupa zangu kitandani mtoto wa watu staki shida na ninavokoroma sasa kama koroboi bovuπ€£π€£π€£
Tukutane sehemu inayofuataaa
DADA KIBOGA NA MJEDA : 04
Hayawi hayawi sasa yakawa hatimae asububi ikafika kama kawaida yangu dada kiboga nikaamka nikaelekea hadi chooni
Uwiiiiπ€£π€£π€£ππjamani sjui foleni litaisha lini jamani khaa hapa bila ubabe sitoboi
Aya manirani nipisheni nioge mie, ila wali wa jana si ulikuwa pambe enheeee??
Sanaa tu dada kiboga tunae na tunatamba nae
Mie nikajibu teeeenaπ€£π€£ππhuku naingia bafuni kuogaa halooo
Basi nikakaa hukoo chooni nkajisugua haswa nilipotakata nikarudi zangu chumbani mie
Leo nikaamua nivae suruali na crop top nyeupeee huku kachuluari kangu keusi
Japo sjawahi kusifiwa ila najijua buana nikivaa dera haliwi kama kanzu kama tufudenge..... Au basi simtaji
Kisuruali kangu kalinikaa tako likajichora haswaa halooo nikafunga zangu mlango huyoo safari ya kuelekea kibaruani ikaanza
Dada kibogaa ni wewe kweli huyooo??? Mama kibo huyooo kashaanza na kuropoka zake maana huyu haongei huwa anakunya kwa kupitia mdomo
Sio mimi , ni bibi yako huyuuuu na kufuli kichwaniπ€£π€£π€£halooo mama kibo alicheka hadi akakaa chini
Mwendo wangu wa maringo sasa yaani ukiniona tu kama rijali unadindisha mwenyewee chezea wewe
Njiani nikakutana na ugomvi wadada watatu wanamchangia mdada mmoja si unajua mtaani tena watu walivyooo
Nikawaangalia kwa maneno waloyatoa nikajua pale kama hawajafumaniana si bureee
Enheee wadada mchana kweupe jua la utosi hili hapa mnaanza kumchania mwenzenu madera na alivomweupe hivi mumtie makovu kisaaa??? Kama desturi yangu nikavaa dera lisilonihusu , π€£π€£nqjitia mwamba ngoja nipigike limshuke shuu
We sijui dada kiboga sjui kibo tobo la mlima kilimanjaro usizani sisi yunakuogopa wanaokuogopa wa huku sio sie fata hamsini zako tufate zetuu, vile vidada viwili visivyokuwa na nyama za usoni wala matakoni vikanijibu
Kwanza nikavitazamaa juu chini pembeni katikati , nikawapandisha nikawashushaa, nikawapima kwenye mzani wangu wa kilo tano nikaona hata moja hawafiki, π€£π€£π€£
Kwanza asanteni kwa kunitambulisja bila kujitaja hqloooooo hehehehehehe, nadhani hamnijui vema mnanisikia kwenye redio tu ila bado tv hamjanunua
Sasa sikieni huu mtaa ugomvi mwiko hapo amueni muondoke mniachie huyo dada au tulipigee!, nikawakazia macho kwelikweli wanipe majibu mieπ€£π€£π€£kama mtu kweli
Hatukuogopi bibi weeeh kama vipi tuzichapeee pambee tu
Kusikia lile jibu nikapandisha mizukaa kwanzaaa , nikavua crop topu yangu nikabakia na kitopu tu na surualiππ
Nikawasogelea acha niwavute nywele vuta vutaaa, niliwapiga makonde ya maana walijuta kunifahamu nakwambia
Nilipomaliza kila mtu akawa ananishangilia dada kiboga dada kibogaa mie tena bichwa hilo kam sufuria la msibani
We nae nyanyuka hapo chini umepoa kama uji wa dona usio na sukari loooh, nikampa mkono yule dada tukaondoka zetu haoo
Nikamtembeza dada wa watu haraka hadi tukafika saluni kwangu nikafungua kisha nikampa kiti akae
Aya shoga nambie nini kilikukuta hadi ikawa vileee
Yaani dada we acha tu , wale wamenikuta nyumbani kwangu na bwana angu wakaingia wakanivutaaa wakanikokota hadi pale eti wanasema ni bwana wao jamani
Pole shoga angu na wewe tuliza kibampuli hiko na kwanza sifanyi kazi buree nisafishie saluni ndo uondoke
Sawa dada
Basi mdada wa watu akasafisha kisha alipomaliza akaondoka
Nikabaki mwenyewe sasa kama kawaida siku ilikuwa mbaya hatarii wateja hamna na watu wa mtipesa wa bahili hata akija atasuka nywele ya mia tano kamaliza kwao rasta wanaziita nywele za maitiπ€£π€£π€£
Wakati nimekaa zangu saluni kwa mbali nikaiona gari kali imepakii nikasema hiii tena fursaa jamani tajiri tajiriiii
Khaaaa !!!!! Si akatoka mjeda buanaa kwenyw garii na ajabu akawa kaongozana na yule kaka niliyemtapeli afu hamsini yake nikasema uwiiiii leo ukisikia kuisha ndo huku kama sio kupatikanaπππππππ
Itaendelea
Soma mpaka mwishooo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.