Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI* SSEHEMUYA 16* NA 17

27th Jul, 2025 Views 79


Chris alisimama kisha akamkumbatia Jamila

"Naomba uvunge kama hujasikia chochote, Mimi na hao tuna fahamiana hivyo nitajua namna gani nitamalizana nao"

"Maneno yao yana ukweli, dunia ya sasa inahitaji watu wenye uwezo wa kusaidiana na si kupeana mizigo, naomba ulifikirie hili swala vizuri. Naomba niende nyumbani kwangu, siku ya kesho nitarudi gengeni ni lazima nijiandae" Jamila aliongea kisha akaondoka

Chris alijitupa kwenye kochi, alionekana kufikiria.

Upande wa Jamila akiwa mwenye nguvu mpya aliingia sokoni akanunua karanga.
Zilikuwa ni nyingi sana lakini alijitahidi akazikaanga zote kisha akazifunga kwenye vifuko.

Kulivyo pambazuka asubuhi, alibeba biashara yake akaelekea gengeni kwake.
Kwa bahati mbaya pikipiki iliyokuwa na haraka ya kwenda kumchukua mgonjwa ilimpitia. Karanga zilienda kulee,

Watu walijaa kujua nini kinaendelea, hali ya Jamila ilikuwa mbaya sana.
Mguu wake haukuwa na mawasiliano kabisa ni kama uliumia ndani kwa ndani.

Taratibu za kumpeleka hospitali zilifanyika.
"Anatakiwa kukatwa mguu..." Daktari wa zamu aliongea

Chris hakuwa tayari katika hili, aliamini hili swala limo ndani ya uwezo wa Dorin.
Tukumbuke huyu binti ndiye Daktari bingwa katika swala zima la mifupa katika hospitali ya St. Peter

"Daktari aliyemhudumia yupo sahihi ni lazima akatwe mguu..." Dorin aliongea huku akiandika

"Hapana, nina uhakika hili swala limo ndani ya uwezo wako tafadhali sana naomba unisaidie" Chris aliongea huku akitia huruma

"Ni kitu gani nitapata endapo nitamsaidia..." Dorin aliuliza

"Lakini ni kazi yako kama Daktari kuokoa maisha ya wagonjwa wanaofika kwenye hii hospitali" Chris aliongea

"Na ndio maana nimependekeza akatwe mguu.... tofauti na hapo sina msaada mwingine, ukitaka niende nje ya uwezo wangu kabisa itakulazima unipe kitu ambacho Mimi na Babu yangu tunataka" Dorin aliongea

Chris hakuwa na namna kwa ajili ya Jamila hakuwa na ubishi.

Dorin alivaa mavazi yake kisha akaingia kwenye chumba cha Operation.
Akili yake yote aliiwekeza kwenye mguu ya Jamila.
Ilikuwa ni kazi ngumu sana, alifumba macho yake kwa dakika kumi kadhaa kisha akaanza kushughulika na Jamila.

Huku nje Chris alikuwa ameishikilia karanga ya Jamila.
Alijikuta akiikumbuka mara ya kwanza wamekutana.
Muda ulizidi kusogea bila Dorin kutoka katika chumba cha upasuaji.

Akiwa katika hali ya kukata tamaa, Dorin alitoka akiwa ana tiririkwa jasho usoni mwake.

Chris alimpatia maji pamoja na kitambaa.

"Ilikuwa ni kazi ngumu sana, hakikisha unatimiza maneno yako..." Dorin aliongea kisha akaelekea ofisini kwake

Alijitupa kwenye sofa, chozi lilimdondoka kwani kama angekosea kidogo tu Jamila angekatwa mguu.

Chris aliingia wodini alipolazwa Jamila.
Anaachia tabasamu baada ya kumuona amelala.

"Naomba unisamehe, Mimi na wewe hatutaweza kuwa kitu kimoja tena, nitamuoa Dorin..." Chris alijisemea ndani ya moyo wake kisha akaondoka.

Siku iliyofuatia Jamila alifumbua macho yake akiwa anajisikia vizuri.
Alijikokota taratibu akakaa, nesi wa zamu alikuja kumtoa akawa ana msaidia kufanya mazoezi

"Mshukuru sana Daktari Dorin, ilikuwa ukatwe mguu lakini kwa juhudi zake hujakatwa...." Nesi aliongea

"Vipi kuhusu gharama!... naomba unisaidie nitoroke sina uhakika kama nitaweza kulipa" Jamila aliongea

"Usiwe na shaka kila kitu kimelipwa, sijui nani kakulipia lakini hudaiwi na ndio maana nakusaidia hata kufanya mazoezi..." Nesi aliongea

Jamila alikosa kitu cha kusema, akiwa anasaidiwa kufanya mazoezi aliachia tabasamu baada ya kumuona Chris, cha ajabu Mwanaume huyu hakuonesha tabasamu. Ni kama alikuwa hamfahamu hivi

"Hatimaye Chris anaoa, nafurahi kuona anamuoa Dorin....wawili hawa wanaendana sana" Nesi aliongea

Jamila alishtuka kusikia Chris anaoa, lakini kwa namna moja au nyingine alifurahia kwa sababu hana uwezo wa kumsaidia Mwanaume, tofauti na k hana kitu kingine cha kumpa.

Alikaa hospitali kwa wiki mbili hatimaye akaagwa, wakati anatoka nje ya geti la hospitali alikutana na Chris akiwa na Dorin. Pete zilizokuwa kwenye vidole vyao alielewa watu hawa ni wanandoa tayari. Isingekuwa rahisi kwake kuwapita kwa sababu ni watu anao wafahamu....alisimama ili wasalimiane cha ajabu walimpita kama hawamfahamu hivi

Jamila aliachia tabasamu lililojaa kejeli kisha akaendelea na safari yakeJE NINI KITAENDELEAAA!
FULL 1000
SIMULIZI HI IMEKAMILIKA MPK MWISHO KABISA

BEI YA OFAAAAA WAHI INBOX NA 500 YAKO TU UMALIZE MPK MWISHO
NAMBA YA MALIPO 0755090082 JINA LA USAJILI ZAINABU SUNGITA MPESA

UKISHALIPIA WAHI...
WAHI WHATSAPP 0755090082.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI* SSEHEMUYA 16* NA 17  >>> https://gonga94.com/semajambo/biashara-ya-karanga-ilinipa-mume-daktari-ssehemuya-16-na-17
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest