Mwandishi Salma Rasheed
Mawasiliano: 0763 595006
Jiunge na Group Langu La WhatsApp
https://chat.whatsapp.com/DxN0OOf9UJvCM1IMJrkAEX
Channel zangu za Youtube
1️⃣. https://www.youtube.com/@Simulizizasalma
2️⃣. https://www.youtube.com/@Salmasimulizi
*KARIBU SANA*
"Oh poleni sana"
Brown hakuitikia asante ya maneno zaidi ya kutikisa kichwa chake akimtizama mama yake ambaye anafaham ni mdhaifu sana kwenye mambo yanayowakuta watu hasa ya huzuni.
🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️
Bi Dorah akiwa mahabusu, aliambiwa ana mgeni wake ambaye anapaswa kwenda kumtizama.
Alitoka taratibu sana akiwa anawaza nani kaja kumtizama.
Alishangaa alipomuona Mkuu wa Kituo Shekiombo.
"Nikusaidie nini?" Aliuliza Bi Dorah.
"Unidaidie nini? Kweli Bi Dorah!!! Hilo swali nani anapaswa kumuuliza mwenzake kati ya mimi na wewe?"
Bi Dorah alibaki akimtizama tu pasina kumjibu
Anyway nimekuja kukwambia ya kuwa majibu ya yule maiti yametoka na hakuwa Salome.
"Niliwaaambia lakini, sihusiki na chochote kile lakini hakuniamini"
"Hahah hapana Bi Dorah itakuwa hujanielewa, ni ukweli kwamba mwili haukuwa wa Salome lakini bado ulitoka katika kituo chako umesahau hilo"
"Lakini kwanini nikamatwe mimi tu? Mule tunaishi zaidi ya watu 10 ambao ni watu wazima"
Mkuu Shekiombo alimtizama na kuona swali hilo kama lina maana lakini kwa mbali hivi.
"Ni kweli na vipi kuhusu madawa ya kulevya?"
"Sijui chochote mim, sihusiki na chochote kwanza wakati mna search sikuwa huko mnawezaje kusema madawa ni yangu"
"Unamaanisha kwamba askari wangu alikuwekea madawa wewe au mimi ndo sijakuelewa?"
"Kama mmeweza kunisingizia kumuuwa binti ambaye sikuweza kufanya hivyo tangu alipokuwa na miaka 6 , mtashindwa kunisingizia madawa ya kulevya? Nataka nikwambie kitu niko serious na hili na wakili wa kituo changu atalifuatilia kwa makini kabisa tuhuma hizi zilizopo juu yangu, pia usisahau ya kuwa kituo changu kimefadhiliwa na watu wakubwa. Kwahiyo haitakuwa rahisi kwenu. Cha kuwashauri2 mtafuteni anayehusika"
Mkuu wa kituo Shekiombo alimtizama na kutabasamu kwa dharau ishara ya kwamba aliyoyasema hayajaweza kumuingia akilini hata kidogo.
"Nakusikitikia sana Bi Dorah kwasababu bado hujafahamu uzito wa kesi uliyonayo, yani hufaham mashtaka yako yana uzito kiasi gani mpendwa"
Bi Dorah alimtizama na hakumjibu kingine chochote kile.
"Askari nimemaliza hapa, na kwa siku nyingine sitahitaji kumuona mgeni kama huyu zaidi ya mwanasheria wangu tu"
Aliinuka akaondoka huku akimuacha Mkuu wa kituo Shekiombo akimtizama kwa hasira.
🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️
"Umemfaham yule aliyeenda kule kukagua maiti?" Alirudi Shekiombo akiwa na jazba na jazba zake alimshushia Juniour.
"Unamaanisha Mkuu?"
"Namaanisha?" Aliuliza Shekiombo akimsogelea na kumuliza.
"Labda mimi ndo nikuulize wewe kama Unamaanisha kuniuliza hilo swali mpumbavu wewe? Hivi unajua kwamba Bi Dorah ana wakili?"
"Eeeeeh!!"
"Umewaza kwamba labda huyo wakili wake ndiye aliyemtuma huyo aliyeenda kuukagua mwili?"
"Lakini Mkuu unajua kabisa hakuna ushahidi wowote hakuna hata pa kuanzia unafaham kabisa ya kuwa mimi sijawahi kuwaga mzembe hata mara moja".
"Hata mara moja? Hivi nilichokwambia umekisikia kweli? Sema hili ni kosa langu kufanya kazi na watu wajinga, na hao wapuuzi wawili badala ya kuuleta mwili wa huyo Salome wametupatia mwili wa mtu mwingine yani wao ndo wameharibu kila kitu.... nataka niwaambie2 pakiharibika kokote basi ni nyie mtawajibika".
🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️
"Mwanasheria wake? Una appointment naye?" Aliulizwa Abby ambaye alikuja kivingine kabisa akiwa amevalia wigi lililomfanya akaonekana hana asili ya nchi za watu. Aliweka miwani yake vizuri na kumtizama aliyemuuliza lile swali huku akiwa anatoa kitu kwenye briefcase lake.
"Kuna nini?" Aliuliza Askari aliyetokea ndani.
"Kuna wakili hapa kaja kumuona Dorah Frank"
"Aaaaa Bwana wakili, ingia alikuwa anakutegemea hata hivyo"
"Asante" alijibu Abby ambaye hakukuwa na chochote cha maana ndani ya briefcase ile aliyokuwa akijifanya ya kuwa anatoa kitu.
"Haya mwanasheria wako uliyetaka kuonana naye ameshafika"
Bi Dorah alitoka ndani ya sero yake na alikuwa na uhakika Abby lazima tu aje.
Alifika na kuketi.
"Nilijua lazima uje hapa, nakwambia ukweli kabisa. Sijahusika na chochote kati ya hivyo wanavyo visema yani sijui chochote"
"Nataka kukuamini Bi Dorah!! Alisema hilo Abby akitoa makaratasi na kuweka pale mezani ya uwongo na kweli.
Ila ushahidi ambao uko mezani unakuelekea wewe moja kwa moja tuanze na hili, kwanini ulichoma picha ya Salome?
Bi Dorah alishusha pumzi yake na kusema
"Sikuwa na nia yakuchoma picha yake, nilikuwa nikihangaika kuchoma ushahidi ambao unaonyesha vitu ambavyo sikuwa nikivifanya sahihi katika kile kituo, nilivifanya kwa miaka mingi sana na yule Askari aliponipatia taarifa ya kuwa atakuja kufanya uchunguzi pale nilijua tu kama nyaraka zile zitapatikana basi nitakuwa kwenye matatizo makubwa sana.....hivyo nilizibeba nyaraka zile bila kutambua ya kuwa ndani yake kulikuwa na picha ya Salome na kwenda kuteketeza ushahidi"
"Hakuna mtu aliyethibitisha kwamba alimuona Salome akitoka pale kituoni na kwenda chuoni, unatambua hilo"
"Ni kwasababu Salome siku hiyo aliondoka mapema sana tofauti na muda wa kawaida"
"Muda gani?"
"Aliondoka saa 12, wakati mara zote huwenda chuoni saa 2, lakini pia hakuwa sawa ni kama mtu ambaye alikuwa na wasiwasi"
"Kivipi?"
"Sijui nikuelezeeje lakini Salome, ni kama kuna kitu kilikuwa kikimtatiza huko chuoni"
"Kwanini umesema hivyo?"
"Kuna siku niliingia katika chumba chake na niliikuta nguo yake ya shule ikiwa imechanika ni kama kuna mtu alimfanyia unyanyasaji"
"Unyanyasaji?" Aliuliza Abby.
"Salome alikuwa mtu ambaye anaficha yale yanayo muumiza yeye mwenyewe pasina ku share na mtu mwingine kabisa, ila nahisi chuoni kuna mtu alikuwa akimfanyia unyanyasaji.... kuna jambo nahisi pia chuo huwenda wakawa wanalificha ili kutokuharibu sifa ya kile chuo"
"Unamaana gani?"
"Uuuuhhhh, siku moja kabla ya yeye kupotea nilimkuta akiwa na sumu mkononi mwake ni kama alitaka kuinywa ila aliponiona alijifanya kuna panya ndani. Niliichukua na kuondoka nayo na ndiyo kesho yake alipoenda chuo hakurudi tena"
"Unamaanisha nini?"
"We fuatilia hilo" alijibu Bi Dorah na kumwambia
Nakuhakikishia kabisa ya kuwa, sijahusika na chochote kile kuhusu Salome, fuatilia na utajua.
Itaendelea In Shaa Allah.