Yule kaka alikaa kwenye siti kisha akanambia umelalaje sikitu ? ππ Huyu kajuaje jina langu! Niliwaza
Basi nikajichekesha pale .......aah niko salama kaka....okay is time for lunch you are welcome.......π³nilibaki nimemkodolea macho nisijue anaongelea nn niliishia latatu D sikujua chochote kile.....alichonisaidia nikaelewa alinipa mfuko uliokuwa na vyakula hapo ndo nikajua amenikaribisha kula.....aaah hapana kaka kile cha asubuhi bado hakijayeyuka kwahyo bado nimeshiba......okay chukua umwage dirishani π³kha huyu kaka kama siyo mchawi atakuwa mwanga π€£nilijisemea moyoni......nilichukua ule mfuko na kuufungua nilikutana na vyakula vitamu balaa kuku chips ndizi Rost matunda pamoja na pepsi ya kopo ya baridi sana ........soda soda soda nakuita mara tatu ......daah nakumbuka niliwahi kunywa soda aina ya fanta pashen siku ambayo mtendaji wa kijiji chetu alipokuwa anamuozesha kijana wake nilikua na miaka nane tu sikuwahi kunywa tena mpaka miaka yangu 20 ......nilikula kile chakula mpaka nikabakisha π€£sikuwahi kubakisha chakula kabla......wakati wote nakula yule kaka alikua amevaa zile headphone zake anasikiliza music kwenye simu yake hakuwa na time na mimi kabisa.......aaΓ sh jmn ni mweusi mzuri tu kama roho yake ilivyo nzuri..... nilikunja ule mfuko vzr nikauweka nitakula badae tenaπ€£π€£umaskini huu asikwambie mtu......basi bwana. Gari ilitembea hatimae ilikuwa ni saa mbili usiku.....abiria jiandaeni mkachimbe dawa...ilisikika sauti ndani ya gari....tukachimbe dawa awa gani hiyoπ³π³nilikuta nimeropokq kwa sauti kubwa .....watu walivunja mbavu ndani ya gari yule kaka jirani yangu alivunja mbavu nilijiskia unyonge sanaπ₯ nikajiinamia kwenye mfuko wangu nikaanza kulia.......hasira zangu mara nyingi zinaisha nikishalia tu ......yule kaka kuona Malia alininyanua kichwa na kusema usijali nyamaza sipendi kuona machozi ya mtoto wa kike ....nipishafuta sana machozi ya mama yangu hivyo naomba usilie mbele ya uso wangu tafadhali...kuchimba dawa ni kwenda kujisaidia.......alinieleza walau nikajihisi yupo mtu wa kunitetea.....tulishuka abiria wote wote tukaenda kuchimba dawa kisha tukarudi lkn nilipofika kwenye siti yangu nilikuta tayari jirani yangu ameshafika .........nilitaka kukaa lkn pale kwenye siti yangu palikuwa na kitu kama mkufu hivi .......kaka hii ni yako umeisahau hapa ........nilimwambia ......oooh chukua ni zawadi yako kuwa huru........mmh kwanini anipe zawadi nikawaza kichwani ....hapohapo nikaona sura ya mamdogo inanijia jichunge mwanangu fanya kilichokupeleka mjini.......nikachukua ule mkufu nikauficha na kujiambia hawezi kujidanganya bwana mimi nina akili nyingi .........usingizi ilitupilia wote tulikuja kuamshwa na sauti ya makelele ...... waaaaaaao tayari tulishafika jijini Dodoma.......hello tutaonana siku nyingine take care...yule kaka aliniaga akanisogelea akanibusu kwenye paji la uso heeeeeeeeπ³π³π³π³ sijawahi kuhusiana kabla roho ilienda mbio ndundundu ........yule kaka wala hakujali akashuka chini na mimi pia nikashuka nikaelekea upande wa buti ili nikachukua begi langu nilichukua na nilipogeuka nikimuona yule kaka upande wa pili wa barabara akiwa na mdada ambaye alikua ameshikilia mtoto mkononi na mwingine amembeba mgongoni ....walikumbatiana kisha wakabusiana na kuingia ndani ya tax wakatokomea zao........nilikaa sehemu ya abiria kumsubiri mwenyeji wangu....
.Nilikaa pale stendi kwa muda mrefu sana ........nilishikwa begani ...za saiz ...salama tu ...wewe ndo sikitu...ndio....alikua ni mdada mrembo sana alinichukua na tukapanda bodaboda kisha tukatokomea
ITAENDELEA.
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
NAMBA YANGU YA WHATSAPP NA KULIPIA PIA NI 0715906120 MTANDAO YAS JINA LA USAJILI FLORA.