Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMMπŸ’˜πŸ’πŸ’˜ SEHEMU YA (36)

27th Jul, 2025 Views 89



Nilitoa ile karatasi ya Ultrasound nikampatia afu nikasema Tadaaa ,surprise haya fumbuaa akafumbua anaitazam akaniuliza hii nini nikasema mmmmmh yaan kwa kudeka ile ileee
"You Gona be a Dadyyyy!! For my own child!!!!"

"Serious?????"

"Mhuuuu" Alex alichekaaaaa akanikumbatia alinipiga mabusu kidogo ninuke mate akanambia kumbe unajua kingelezaa hahaha nikasema ungejua navyo kaliliii hahahah basi tuuu

Alinibeba juu juuu chumba chotee anazunguka akanambia salma wanguu jamani salmaaaaaa we salmaa wewee nikupe ninii mie mke wangu??

Nikamwambia naomba moyo wako nipe moyo tuuuu huo ndio nautaka akaniuliza vipi kuhusu bandama na filigisi yaan we hata inni beba na figo zake salmaa moyo wangu unatembea naoo , hivyo vingine mpe mwanangu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… nilichekaaa alex alikuwa kama kachanganyikiwa kichwa chake muonee

Nililala nabusiwa tumbo jamani hiyo siku nikijigeuza tu kidogo anasema vipi ,nikusaidie mke wangu hahaha nikacheka namwambia embu acha bwanaa jamani..
asubuhi naamka ile Alfajir akanambia mmmh huendi popote pale lala bwana sa hizi baridi mtoto ujue, nikamwambia zamu yangu usafi jamani akanambia nielekeze wapi na wapi nitafanya mwenyewe hee jamani nikacheka namwambia we tulia nilikuwa najua utani ,wapiii alikataa kabisa hakuna kuamka asubuhi asubuhi wala kuinama

Alex aliinuka mwenyewe akadeki Choo na bafu , akafagia uwanja mpaka barabarani, nilikuwa najishtukia majirani na vile nyumba yetu inawatu kama kijiji hee nikawa naona aibu mie sijazoea haya jamani

Akapika chai na mayai, akanifata ndani nilikuwa hata havikaliki hapo tayari sa mbili nikamuuliza kwenda kazini akasema huenda kule ,itabidi uwe unaenda tu jioni kupiga hesabu tafuta mtu wa kupokea pesa unaemuamini , nikasema jamani mi mbona nipo sawa akasema we unajiona upo sawa lakini hapo ulipo ni mgonjwa we jiandae twende hospital ..

Mtoto wa kike nikajianda vizuri tukaondoka hapo mpaka hospital akanipima tena huku ananiomba Samahani et sio kama sikuamini mke wangu hapana nataka kusikia tena na tena hata mara elfu , namwambia hata usijali kipenzi changu .
Aliulizia vyakula navyotakiwa kula , kazi gani nisifanye muda wa kupumzika , vitu kibao yaan , ndo tukarudi nyumbani , hapo kwenye Bamzii gari inaendaaa taratibu hataki nipate mitikisiko

Tulifika nyumbani, alex akanambia salma kuna kitu nawaza hapa nikamwambia nambie mpenzi

"Ila naomba usinielewe vibaya "

"Usijali hata!!" Nilimjibu huku najiweka makin kumsikiliza mana aliongea akimaanisha ni muhimu sana akanambia kuwa

"Salma mke wanguuu"
Nami nikaitia abee mume wanguu

" kuna mtu niliongea nae ,nahitaji upate mwalimu urudi darasani tena ,unajua we bado bint kesho utasimama kwenye nafasi kubwa sana nahitaji hata kama sipo usipate mtu akakuadhibu kwa udhaifu wako ,nakuomba unielewe mke wangu please "

Nilijifikiria huku roho inaniuma alex ukweli ananipenda kaka wa watu hata asipo sema naelewa kupitia macho yake na Care zake
Nilimwambia kwanza nashkuru kwa kila kitu bado unanipa nafasi kubwa sana kwako unanipenda nashkuru bado unanipigania Alex baba wa wanangu chochote mimi nitafanya we sema tu hakuna haja ya kuniomba mpenzi wangu

Alinikumbatia akasema sawa basi kwa vile Subira anamaliza aende kusimamia ofisini mimi nianze kwenda kusoma akasema huyu mwalimu atakuwa anakuja hapa hapa nyumbani nikasema sawa ila akanambia anahitaji tuhame hapo unajua tunaenda kuwa na familia kwahiyo inatakiwa kuwa na nyumba yenye nafasi nikasema chochote baba angu mi nipo tayari akasema sawa ..

Nilimuita Subira akaja nikaongea nae ,kuhusu kusimamia pale kwenye mgahawa mimi nitakuwa nakwenda usiku kupiga hesabu na kulipa watu akasema sawa haina shida , inno baada ya kusikia mimi ni mjamzito alifurahi sanaaa yaan alikuja akanipa hongera akasema Alex inatakiwa mmalize tofauti na nyumbani Alex akasema freshiii yupo kwenye huo mchakato
Basi siku enyewe alex alinambia kuna nyumba imepatikana mbezi beach, tulienda kuitazama ilikuwa nyumba nzuri nzuri kweli niliipenda na ilikuwa hakuna wapangaji pangaji , akanambia nikae huko huko nisirudi kule , ye akaenda kufunga mizigo yangu yotee akaleta na gari akasema hakuna nilicho acha nikasema poa

Asubuhi yake alileta Furniture mpya afu za kisasa tanda la maana masofa ya kisasa yaan nyumba ikawaka gafla kwelii,
Oooh nilijiona kweli nimekuwa mwanamke tena mwanamke kamili kabisaa
Akanambia nakutafutia dada aje kuwa anakusaidia nitaongea na dalali nikasema sitakiii we mambo ya mdada wa kazi sitaki miee tena sitaki kabisaa najiweza akanambia huniamini mmh nakuamini lakini simuamini mfanyakazi miee akacheka nikasema mi mwenyewe nimepokonya mtu je nikipokonywa sitaki bwanaa akanambia basiii simlet mie nitakuwa mfananyakazi wako ..

Zilipika siku kadhaa Alex akanambia kuna sehemu anataka twende aliniletea nguo nikaona mbona kama hii safari ni special sanaa nikamuuliza kwani alex tunaenda wapii??

Akanambia salma naomba uniamini mpenzi wangu nakuomba nahitaji kwenda nawe nyumbani nataka wajue hali yako huyo ni mjukuu wao lazima tu waelewe kuwa ni mjukuu wao hakuna njia ingine zaidi ya kukupokea ,chochote kitakacho kuwa naomba uvumilie sijajua watapokea vipi hii taarifa lakini vumilia tu nilikubali hakuna shida

Nikajiandaa vizuri , tukawa tumeondoka , nilifika nikamkuta juddy yupo bize kweli yaaan hana hata wasi wasi , Alex akamuuliza we mbona upo hapaa?? Akasema ndio au hutakii
Alex hakumjibu mama yake nae akawa ametokaaa
Alishtuka kutuona tupo wote ,
"Karibunii!!" Alitukaribisha kwa sauti ya mladi tu aongee

"Salma keti hapo,, mama huyu anafanya nini hapaa??" Alex akamuuliza mama yake akimaanisha Juddy ....

KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMMπŸ’˜πŸ’πŸ’˜ SEHEMU YA (36)  >>> https://gonga94.com/semajambo/nilizani-mwizi-kumbe-mmmm-sehemu-ya-36
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest