Baada ya kuondoka kwa kina Rasma pale nyumbani, nyumba ilitulia kidogo, vurugu zilipotea kabisa. Walibaki watu wawili tuโMama na mtoto wakeโwakiwa sebuleni, kila mmoja akimtazama mwenzake ๐.
Garma hakuwahi kufikiria kwamba kumpoteza Mayner kungekuwa na athari kubwa kiasi hicho, lakini alihisi ametimiza wajibu wake.
Kwake, hakupenda kudharauliwa. Kitendo cha Mayner kwenda kwa mganga, ilhali tayari alikuwa amemkataza, kilimvunja moyo na kumvunjia heshima ๐ค. Kama mwanaume, alihisi inampasa kuonyesha kuwa yeye ni nani.
Mama yake alimtazama kwa sekunde kadhaa, kisha akasogea hadi alipokuwa na kusema:
"Usijali, kila kitu kitaenda sawa. Yule hakuwa mwanamke wa maana wa kusema unataka kumuo..."
Kabla hajamalizia, aliona kitu kama chupa chini ya meza ๐ณ.
Akasita kuzungumza, kisha akainama na kuichukua ile chupa.
"Si umeona? Umeona huu ni uchawi wake. Wale wanga haki tena!" alisema huku akimkabidhi chupa hiyo kwa mtoto wake.
Chupa hii ilikuwa ile ile aliyopewa Rasma na mganga, sehemu ya dawa. Kwa bahati mbaya, wakati wa ugomvi wa Mayner na kaka yake, Rasma aliidondosha bila kujua ๐.
Mama alidhani ni dawa ya Mayner.
"Nimepata nywele yake na hii dawa... mbona namkaanga mchana kweupe! Huyu lazima awe chizi! Haiwezekani aniabishe kiasi hiki," alijisemea moyoni.
"Kwahiyo ni nini sasa?" Garma akauliza.
"Ukisikia libwata ndio hili! Huu ni uchawi mbaya sana. Hapa kama ungerogwa, kila kitu ungemuandikisha yule mpuuzi!" ๐คฌ
"Mh! Bora Mama umeniokoa aisee. Ubarikiwe sana, Mama. Ndiyo maana nakupenda. Ngoja niivunje kabisa!" Garma alisema huku akinyanyua chupa hiyo.
Mama yake akamzuia haraka.
"Hapana! Naomba usivunje. Itakuwa kama ushahidi. Nikae nayo mimi hapa."
"Sawa," alisema Garma na kukabidhi chupa hiyo. Kisha alianza kuondoka kuelekea chumbani. Lakini alipopiga hatua nne, alikumbuka jambo ๐ค.
"Mama, yule mwanamke ameolewa?"
"Yupi?"
"Yule uliyemleta, Ninnah."
"Aolewe wapi? Bado anakusubiri tu."
"Basi kesho tutaongea vizuri, na kama ikiwezekana tutaenda kwake."
"Sawa, hakuna shida," Mama Garma alitikia, akimtazama mwanawe akiondoka kwa bashasha ๐.
Ndani ya moyo wake, kulikuwa na furaha isiyoelezeka ๐. Alifurahia kwamba amefanikisha kumtoa Mayner pale nyumbani na kupata nywele pamoja na dawa aliyokuwa amepewa Rasma na mganga.
Furaha iliongezeka alipoona mtoto wake ameanza kumuulizia Ninnah ๐.
"Hapa sasa mambo yamekaa sawa! Ndoa muda si mrefu, ebu ngoja..." alisema kwa sauti ya chini na kuelekea chumbani kwake.
Alipofika chumbani, hakupoteza muda. Alipiga simu kwa Ninnah kumpa taarifa.
"Mama kuna nini?" aliuliza Ninnah kwa sauti ya kushtuka.
"Umejiunga na kifurushi cha ndoa yako!" Mama Garma alisema kwa tabasamu pana ๐.
"Mama jamani! Hapo unazungumza kama huduma kwa wateja! Hebu niambie, kuna nini kinaendelea?"
"Kapigwa! Katiwa mateke na kafukuzwa kama mbwa!" ๐
"Weeee! Usiniambie!"
"Kakwenda na aibu! Mabegi juu juu. Sijui kaenda wapi ila kesho tutakuja kwenu."
"Kunini tena?"
"Wewe naye! Kuna kingine zaidi ya ndoa?" ๐
Ninnah akashikwa na butwaa.
"Mama, nina furaha sana! โค๏ธ Moyo wangu una amani! Nakupenda sana! Mwaaah! Mwaaah! Mwaaah!" ๐
"Hahaha! Sawa mwaya, ngoja nimkaange mtu hapa. Nitakutafuta kesho nikiamka," Mama Garma alimalizia na kukata simu.
Akapiga magoti uvunguni mwa kitanda, akatoa ukaango mdogo uliokuwa na maji meusi sana. Aliweka kidole, maji yakapotea kama kwa uchawi ๐ฎ. Akaweka nywele aliyoitoa katika khanga, akaichanganya na dawa, kisha akajisaidia mkojo humo ๐ณ.
"Kesho nitadili naye," alijisemea huku akijifuta mikono.
---
Asubuhi ilipofika, pirika pirika zilianza. Kwa upande wa Garma, aliamua kuvunja ratiba zote ili kwenda kwa kina Ninnah kufanya mazungumzo.
Akiwa kitandani, alijiangalia:
"Mwanamke angeniua huyu! Kumbe ni mchawi hivi?" alijisemea na kwenda kuchagua nguo ya kuvaa ๐.
Baada ya masaa mawili, wote walikuwa tayari na waliondoka nyumbani. Dakika 45 baadaye, walifika kwa kina Ninnah. Ninnah aliwapokea kwa upendo wa dhati na tabasamu la furaha ๐.
"Sidhani kama Mama hajakuambia kila kitu?" Garma akauliza.
"Mama ataongea na Mama, lakini mimi bado. Kuna nini?" aliuliza Ninnah.
Mama Garma akaamua kueleza kila kituโkuanzia sababu ya ugomvi, mpango wao juu ya ndoa, hadi mipango ya maisha ya baadae.
Wakaafikiana kwamba ndoa itafanyika mwezi ujao ๐, hivyo maandalizi yaanze mapema.
Kila mmoja alijawa na furaha ๐. Garma aliamini Ninnah ni chaguo sahihi kwani alichaguliwa na Mama yake.
---
Wakati huohuo, upande wa pili...
Wakiwa kwenye meza ndogo ya chakula iliyojaa maboga na mamungโunga ๐ฅฌ, mazungumzo yalikuwa kati ya Mayner na Rasma.
"Hapa ndipo mimi na wewe tutaishi. Si sehemu nzuri, lakini tutaishi kwa amani," alisema Rasma, huku akinywa chai โ.
"Asante. Hakuna ubaya katika dhiki. Kikubwa ni kupambana tu. Najua tutafanikiwa... ingawa moyo wangu bado unamkumbuka Garma," alisema Mayner, huku akifuta chozi ๐ข.
Rasma alimtazama kwa maumivu, akasema:
"Najua unaumia. Lakini tunapaswa kukubaliโkuna watu sio sahihi maishani. Ukiwapoteza mwanzoni itauma, lakini baadaye utapata amani."
"Sijui nitayaweza maisha ya upweke. Na siku Garma atakapoamua kuoa, nitaweka wapi sura yangu?"
"Wanasema wakati mgumu ndio wakati wa kujifunza..."
Kabla hajamaliza, ghafla akatetemeka! ๐ณ
"Dawa yangu iko wapi?"
"Uliweka wapi?"
"Ngoja kwanza..." alisema huku akitikisa kichwa chake. Baada ya muda alitulia.
"Nina wasiwasi nimeidondosha sehemu..."
"Wapi?"
"Kwa kaka!"
"Kwahiyo?" Mayner akauliza kwa hofu ๐ฐ.
Rasma akasita kidogo, halafu akasema kwa uthabiti:
"Naenda kuichukua!"
"Nikusindikize?"
"Hapana! Wataweza kugundua mambo ya kwako. Acha niende mwenyewe..."
Wakaendelea kula, lakini Rasma alikuwa na hofu kubwa.
Je, ataikuta dawa? Au imechukuliwa tayari...?
Ukiwa mjanja utajua namna gani nakupa uhuru wa kununua kutokana na kipato chako. Tazama, simulizi nzuri kama hii unanunua kutokana na vile unajisikia. Njoo WhatsApp namba ni 0717255498 Niambie una Tsh ngapi, nikupe simulizi usome..