Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

NIPE YOTE DADY* *SEASON THREE* *41~45*

27th Jul, 2025 Views 195


_______

Haya haya wale ndugu zangu wapenzi wangu na maadui zenu Norah ndani ya nyumba kwa mara nyingine, najua mnanifahamu so sina haja ya kujitambulisha mmh ila ngoja nijitambulishe huenda kuna watu wapya hamnifahamu.

Okay naitwa Norah Khalid aka Mrs Selim aka kiboko ya mama mkwe πŸ˜‚ ukitaka kunifahamu sana soma story yangu kuanzia mwanzo season one huko kuna mengi ya kufurahia na pia utanifahamu kwa upana zaidi, huu msimu wa tatu ndio msimu wetu wa mwisho..

Sasa tuendelee ,asububi moja niliamka mapema na kuandaa chai kisha nikaweka mezani na kwenda kuwaaamsha waanangu , niliingia chumbani na kukuta SONAM (doto) amalala ila Sonaksh hayupo huyo Sonaksh ni kivuruge ,msumbufu ,mkorofi yani huyu nimejizaa mwenyewe ila amezidi sijui ndo ile vya kurithi vinazidi ?.

"Haya chaupole wa familia ndugu yako yuko wapi?" nilimuuliza Sonam huku nikimuangalia usoni kwa kumkazia macho haka katoto nikapole lakin nikaongo kuliko nani sijui hivyo ukimuuliza kitu ukiwa unamchekea chekea hasemi ukweli, basi akawa nafikicha fikicha macho kwa wenge la usingizi na kujibu hajui, nilimwambia aamke akapige mswaki kisha nikatoka nje kumtafuta huyu kivuruge wangu.

nilizunguka nyumba nzima sikuona mtoto nje kote hayupo nikajisemea huyu nikimkamata leo atanijua mimi ni nani , baada ya kumtafuta nakamkosa nilienda kumuamsha Selim .

"Selim amka wee Selim "

"We mwanamke vp ndio uamshaji gani huu wenzako wana waamsha wame zao kwa mahaba wewe unaniamsha kama unamuamsha mtoto aende shule "

"Mahabaaa mahaba bongo kwanza hao wanaowaamsha wame zao kwa mahaba we umewaona wapi ?"

"Kwenye tamthilia "

"Kwa hiyo na sisi tuko kwenye tamthilia au umeanza kudata mtu wangu , alafu kabla hujashuka kitandani leo jioni nitatoka na nitachelewa kurudi hivyo itabidi usiku uwepo , hilo ni moja pili binti yako hayupo na sijui ameenda wapi".

"Binti gani ?"

"nikikutukana utanuna siku nzima we una mabinti wangap humu ndani"

"Ndio ni wawili ila Sonam hawezi kutoka nje ya hapa "

"Sasa kumbe unajua kivuruge ni nani alafu unanichosha kuniuliza yako ya ajabu"

"umemtafuta ukajua ameenda wapi?"

"Kwenu"

"Norah hii tabia yakunijibu short utaiacha lini ?"

"Ulinikuta nayo alafu unategemea niiache alafu kuna tabia mama yako anaianza siku nikimfumua nisilaumiwe "

""Mmeanza na maugomvi yenu hivi unajua unanichosha ."

""Uchoshwe na ndoto zako za utotoni alafu unakuja kuniambia mi ndo nakuchosha una shida wewe" Nilimjibu na kuchukua nguo za kuvaa ili nijiandae tayari kutoka nilivyoweka nguo tayar nikataka kuingia bafuni mara Selim akaniita .

"We unaenda kuoga umeshampata mtoto ?"

"Kwani amepotea ?"

"We siumetoka kuniambia kuwa hayupo na umemtafuta ukamkosa "

"Ndio hayupo"

" Sasa kama hayupo unapata wapi nguvu ya kwenda kuoga hivi ulizaa kwa uchungu kweli au ulipiga chafya"

"Nguvu uchungu vyote hivyo vinahusiana nini ? alafu Sona sio mtoto anajua njia ya nyumbani kwao akichoka kudhurura atarudi ila akirudi niyamuonesha yasiyo onekana "

"Umuoneshe nini wakati umemfundisha wewe ,mtoto mdogo akili kubwa yani huyu alieweka mfumo wa watoto kuchukua silimia 60 ya akili za mama yao sijui alikuwa anawaza nini ?"

"Kwa hiyo unataka kuniambia mimi ndo nimemuharibu?"

"aaa sio wewe makalio yako embu kaoge haraka nataka nioge na mimi"

"Oooh nikikujibu mimi unasimamisha nywele za puani ila wewe unanijibu poa tutakutana "

"ulitaka nisimamishe za kwapani embu nitokee hapa naona unaniimbia matoronya tu"

"Mmm!haya, alafu hii tabia ya kusema kaoge kwanza na mimi nataka kuoga imeanza lini shoga yangu umepata danga jipya ee ?"

"We koma eti shoga yako nani shoga yako "

"Hujajibu swali langu unadanga jipya "

"Hata nikiwa nalo we inakuhusu nini kwanza dini inarihusu kw hiyo kaa kwa kutulia "

"Haki ya nani nahisi unataka kufa ukiwa umegonoa yani unizalishe na kunichakaza juu alafu ukatembeze hizo kubu na miambili zako kwa madanga , nadhani huu ndio utakuwa mwanzo wa wewe kuuona upande wangu wa pili"

"Sio watatu?"
"Selim we haya " niliingia bafuni nikiwa na hasira kwanza nikasema ngoja nimfanyie drama tuone kama hatukuja kuoga , eti oga haraka nataka nioge na mimi shenzi kabisa .

Nilikaa huku nikisugua miguu taratibu akaita wee mwisho akaamua kuingia nilimuangalia chini juu kisha nikaoga fasta na kutoka moja kwa moja nikaenda kufunga maji alafu nikakaa mezani na kanga yangu moja 😎.

Unajifanya kichaa mwenzako nimetoroka milembe , nilimimina chai na kuanza kunywa hapo Sonam yuko ananiangalia anajiuliza huyu mama vip , nikiwa naendelea kunywa chai mara akaingia mama mkwe akiwa na binti yangu kivuruge .

Kwanza niliweka kikombe mezan na kugeuka nikawaangalia vizur,huyu mama amekuja kumchukua mtoto sanagp na hii tabia nimeshamwambia Selim aongee nae hasikii .

Yani anatabia anakuja mda wowote anamchukua mtoto bila kutoa taarifa anaondoka nae na kumrudisha mda anaojisikia yeye, sasa naona mwanae hakumwambia kifuatacho uchungu wa mwana aujuae mzazi.

Nikitabasamu kinafki na kumkaribisha ,mara Selim akatoka chumbani na mipovu πŸ˜‚ bahati nzuri alifunga tawel kwa akili zake hachelewi kuja uchi,basi alifika na kuanza kufoka " We Nora kwa hiyo umeamua kunizimia maji si ndio unajua iko siku nitakupiga wewe shikamoo mama"

" πŸ˜‚πŸ˜‚ ngoja kwanza mama aitikie salamu, mh tayar sasa rafiki yangu kuzaliwa kote tanzania na kuishi humu bado hujui kiswahili tangia lini maji yakazimwa sema hivi kwann umefunga maji sio kuzima sawa mwanangu"

Alitaka kutukana akasita baada kuangalia watoto, alitoka moja kwa moja hadi kwenye koki zilipo akafungua na kupita kwa hasira bila hata kuongea mara mama mkwe akasema.

"Hivi Norah nilini utakuja kumuhesimu mumeo huoni kama unakosea alafu unakaa kichwa wazi mbele ya watoto unategemea kuwafunza kitu gani haswa"

nilichukua chai nikapiga fundo moja na kumjibu.............

Full 1000
KWETU morogoro
Whatsapp 0657171961.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIPE YOTE DADY* *SEASON THREE* *41~45*  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-season-three-41-45
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

gonga94 official track
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest