Mzee wa Jambia anasemaje kuhusu usajili huu?
Labda Simba Sports wameshindwa Kumnunua Kiungo ambae tayari wanae ndani ya Yusuph Kagoma? ..Just Maybe.✍️
Ukipitia hizi takwimu hapa utaona Moussa Bella Conte amempiga Kagoma Kwenye Usahihi wa Pasi na ubora Kushinda mipira ya Juu.
Usahihi wa Pasi ni 81% Kwa Conte na 72% Kwa Yusuph Kagoma.
Ubora wa Kushinda mipira ya Juu pia unaelewa Kwasababu urefu wa Moussa Bella Conte ni 1.86m wakati Kagoma ni 1.80m.
Hizo takwimu zinaonyesha Bella Conte ana 100% ya Kushinda mipira yote ya Juu wakati Kagoma ana 90%
Maeneo Mengine yote Yusuph Kagoma ni Mchezaji Mzuri Kuliko Moussa Bella Conte. Kwa mfano
Ubora wa Pasi ndefu ✅
Kwenye Kuwania mpira wa chini ✅
Kutunza Mpira ✅
Tackles ✅
Interceptions✅
Key Passes✅
Kumbuka timu ya Moussa Bella Conte CS Sfaxien ilimaliza nafasi ya Mwisho na Points 3 Kwenye Kundi ambalo Simba Sporta aliongoza Kwa Points 13
Kwenye Ligi ya Tunisia CS Sfaxien walimaliza nafasi ya 7 tofauti ya Points 22 dhidi ya bingwa Esperance.
Nimesema Just maybe,sijamaliza Maneno .Kwamba Inawezekana Simba Sports wamemkosa Kiungo ambae wanae ndani ya Kagoma?
Au inawezekana Moussa Bella Conte alitakiwa Kuchukua nafasi ya Fabrice Ngoma?
Lakini bado Ngoma anamzidi Kwenye Ubora wa Mipira ya Juu na Kupiga Pasi sahihi.
Na hii sio Kusema Moussa Bella Conte hatafanikiwa Yanga Africa. Anaweza Kufanya Vizuri Sababu bado Kuna Fursa pengine ya Kukutana na Mazingira mepesi Yanga Kuliko Yale ya Tunisia na CS Sfaxien.
What Do you think?
@Mzee wa Jambia
Mchambuzi wa michezo.