Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

SAMIRA πŸ’‹ πŸ§šπŸ»β€β™‚οΈ 08___9 (Nimeshindwa kusamehe)

27th Jul, 2025 Views 33



BY DIANA STORIES

WTSP 0768328909

Nilirudi chumbani kwetu lakini bado sikuweza kujizuia kilio changu kwa jinsi nilivyokuwa nalia kwa hisia na maumivu ya hali ya juu nilimtisha sana dada Salome alinibembeleza mno. A mwisho nililitiwa na usingizi hakupata hata nafasi ya kunuiliza kuwa nalia nini.

Majila ya usiku tulipata chakula tulipo aliza da Salome akazungumza mbele y kila mtu

"Mama leo samira Amelia sana lakini pia sikuweza kujua ni kwanini analia "

Mama mwenye nyumba ile alinigeukia na kuniangalia kisha akaniuliza

"Ulikua unalia nini ??"

Niliangalia chini na kujikuta machozi yakinitoka tena na kisha nikajibu

"Nimejikuta nawakumbuka sana wadogo zangu na ndugu zangu niliowaacha kule kwa anko rafiki "

"Oooh jamani ni kiasi gani uko na upendo lakini pia uko na shukran, usilie unajua mimi samira wapo watu ambao wametoka kwenye kituo kama wewe lakini hawakumbuki chochote wala shukran hawana "

Alizungumza baba mwenye nyumba

"Lakini usijali jumamosi hii tunaenda kuwatembelea na sio kuwatembelea tu tunaenda kuka anao siku nzima kwahiyo usijali "

Ingawa nilidanganya kuhusiana na kilio changu lakini taarifa hizo zilinipa furaha sana.

Siku ilipowadi tulifungasha zawadi za kutosha hadi mimi nilifungasha zawadi kutokana na pesa yangu ya mshahara niliyolipwa, safari ilianza kuelekea kwenye kituo cha anko rafiki kwanza nilikuwa naona kama nachelewa jamani kuna muda nilikuwa naona mama gari haitembei vile nilipofika walinikimbilia kwa shahuku sana sana ilionesha ni kiasi gani walikuwa wakinikumbuka, lakini pia tulikuta kuwa kuna sherehe kubwa sana kuna mdada alikuwa mkubwa latika iko kituo alikuwa anaitwa Irene siku hiyo alikuwa akifunga ndoa na anko rafiki alisimama kama baba katika ndoa hiyo, labda niwaelekeze haikuaa ndoa kama ndoa, ndoa ilishafungwa lakini siku hiyo waliiweka kwaajili ya kumuaga Irene kabla ajaondoka na kwenda kuanza majukumu yake kama mke.

"Na wewe dada samira utaolewa na kufanyia sherehe yako hapa ??"

Aliniuliza kijana flan hivi nilibaki nikicheka

"Utaolewa na maiko ??"

Bado aliniuliza kijana huyo lakini nilikaa kimya na muda huo huo samiry akajibu

"Ataolewa na mimi na sherehe itafanyika hapa "

"Yeeeeeh πŸ™Œ dada samira ana......."

Alinza kushangilia kwa sauti mtoto huyo chap nikamziba mdomo

"Anakutania mdogo wangu Sawa haya nenda kacheze "

Aliondoka nikamgeukia samiry

"Hivi unaakili gani wewe unakera sana ujue "

"Lakini kila kitu kiko wazi kipi ujui ??"

Niliondoka na kumuacha akijiongelesha tuwenyewe me nilikuwa najionea mambo meusi. Niliendelea na shughuli za uku na uku nilikuaa bize sana yaani lakini pia da Salome hakuwa mwisho katika kusaidia shughuli za pale.

Siku hiyo nilionjoy sana nilipata muda mzuri na familia yangu lakini pia nilipata muda wa kuongea na anko rafiki.

Muda ulifika nasi tukarudi nyumbani kwaajili ya mambo mengine.

Majila ya kama saa 5 usiku hivi nilijikuta nikikosa usingizi nikatoka nje na kukaa kwenye ngazi za nje nikiwa nacheza gemu langu la nyoka kwenye kisimu changu cha kitochi

"Ujalala unajua umechoka sana "

Nilisikia sauti ikiongea nyuma yangu na nilishajua kuwa ni sauti ya samiry

"Sina usingizi hata sijui nawaza nini ??"

"Nahisi unafikilia siku ya leo na kila kitu kilichofanyika "

"Nahisi hivyo, samirt hivi uko na miaka mingapi ??"

"Ahaha achana na miaka yangu ila jua kuwa mimi ni mkubwa kwako ni vile wanaume atukuwi "

"Nimeuliza swali moja nimepata maelezo lakini bado jibu sijapata πŸ˜‚ yaani unajua nimekaa hapa nawaza wewe ni mkubwa lakini mama yako hakutafutii ata mdogo wako yaani amewezaje kuwa na mtoto mmoja ikiwa umri unaruhusu, lakini na wewe ni mkubwa mno "

"Sijui umewaza nini lakini mama yangu anaitaji mtoto leo kesho wameshaangaika na madaktari wa kutosha na hakuna aata mwenye tatizo sio baba sio mama "

"Mmmh we umejuaje kuwa ameangaika "

"Samira mimi ni rafikiwa wa wazazi wangu na wanapenda Sana kunishirikisha kila kitu chao...."

Tuliendelea kupiga zogo za ukweli na uongo,

"Nimechoka tuingie ndani me naenda kulala"

Alizungumza samiry tukainuka na kuingia ndani tulipofika sebuleni alinikisi kwenye shavu chap na kuingia chumbani kwake

Nilibaki nikiwa nimeshikilia shavu langu yaani kama nimepatwa na ugonjwa wa chekelea nilikuaa nikifurahi tu moda wote 😁 samira mimi jamani haya.

Siku iliyofuata nilikuwa nashindwa hata kumtazama usoni nilitamani kumkwepa lakini ndo ilishindikana kwani nyumba ni moja na tunazunguka uku na uku.

Niliendelea tu na shughuli zangu

"Samira....."

"Naaam "

Yaani tabia ya kuitika naam sikuacha kabisa muda huo niliitwa na mama wa nyumba hiyo ambaye aliruhusu mimi kumuita mama na nilikuwa najisikia furaha sana

"Mama, niko hapa "

Nilizungumza hivyo baada tu ya kufika sebuleni

"Aaah vaa mavazi yako vizuri uwende sokoni nimekuandikia orodha ya kila kitu "

"Lakini mimi sipafahamu mama "

"Usijali utaenda na samiry "

"Sawa mama "

Nilijibu tu lakini nilikuwa na wasiwasi Sana yaani amjui tu lakini sikuwa na uwezo wa kukataa, baada ya muda tulianza safari na kaka samiry sikuwa muingeaji muda wote nilikuwa nikitazama nje tu sikutaka ata kumuongelesha au kutazamana nae

"Samira....."

Aliniita nikaitika pasipo na kugeuka

"Mbona kama uko na wasiwasi sana "

"Hakuna naangalia mazingira tu ya nje "

"Mmmmh "

Aliguna kisha akaendelea kuendesha gari na kuwa bize zaidi na nilitamani sana aendelee kuniongelesha lakini ndo hivyo aibu ilionekana kushika upande wangu nilikaa tu kimya.

Tulifika sokoni nikanunua mahitaji ambayo niliagizwa kisha nikarudi kwenye gari lakini sikumkuta na alikuwa amelifunga gari nilikaa Sana pale nje ya gari nikiendelea kupigwa na jua, baada ya muda alirudi kwenye gari alikuwa akifurahi tuh tukapanda kwenye gari kisha nikamuuliza

"Mbona unafurahi sana kuna nini ??"

"Unapenda kuniona nikiwa nina uzuni au ??"

"Yaishe"

Nilijibu hivyo na kukaa kimya akanipatia mfuko ambao alikuja anao

"Hii ni kwaajili yako"

Nilipokea na kutaka kufungua lakini alinizuia.....

ITAENDELEA.

SAMIRA πŸ’‹ πŸ§šπŸ»β€β™‚οΈ 09
(Nimeshindwa kusamehe)

Nilipokea mfuko ambao alinipatia samiry lakini nilipotaka kufungua alinizuia

"Nimesema ni kwaajili yako hivyo basi utafungua kipindi ambacho sitakuwepo "

"Sawa......"

Tulitembea kwa mwendo mrefu na hatimaye tukafika nyumbani kabla ajaingiza gari ndani ya geti kazungumza

"Samira, nikuulize kitu ??"

"Niulize "

Nilijibu chap nikitaka kusikia swali lake

"Hivi umeshawai kuwa kwenye mahusiano ??"

"Nani mimi ??"

Yaani najua kabisa nimeulizwa mimi lakini kwaajili ya wenge nilijikuta nikiuliza kama sijui vile

"Hapana naongea na huyo wa nyuma yako "

"BhanaaπŸ˜‚"

Hapo ndo hata nilicheka yaani tangu safari imeanza

"Nijibu basi "

"Hapana....."

"Hapana nini maandazi kitumbua, yaani hapana utaki kunijibu au hapana kwamba hujawai kuwa na mahusiano "

"Ndo hivyo hivyo "

Nyie aibu ilikuwa ya hali ya juu mpaka majibu yangu yakawa hayaeleweki

"Nashindwa kukuelewa "

"Sijawai.....πŸ™ˆ"

Nilijibu na kugeukia pembeni, akawasha gari na kuondoa kabisa eneo lile yaani hata ndani hakuingiza

"Uku wapi tena "

"Nataka tuongee kila kitu tumalize huku, maana nahisi hatutaweza kukaa karibu kwa kipindi hiki chote maana mama amepatiwa likizo ya week mbili kazini sijui kwa nini lakini atakuwa nasi hapa"

"Sawa...."

Nilijibu kwa ufupi

"Tunaweza tukaongelea hapa si ndio ??"

Aliniuliza nikaitika kwa kutikisa kichwa

"Nitakuwa mbinafsi kama nitauliza kuhusu wewe kama wewe hautajua kuhusu mimi "

😳 nilimtumbulia tu nikimtazama anavyozungumza kwa busara

"Samira, sijui kwanini lakini nimevutiwa sana na wewe tangu siku ya kwanza nilipokuoa kule kituoni, nikafanya kila njia mpaka wewe kuja kukaa nyumbani kwetu, lakini kwa sasa nataka kubakikisha kuwa haukai nyumbani kwetu "

Nilistula sana baada ya kusema kuwa haukai nyumbani kwetu kwa jazba nikauliza

"Kwahiyo unataka nirudi kukaa kituoni .?"

"Sijamaliza samira, naomba nisikilize "

"Sawa....."

"Nilitaka kusema kuwa sitaki uishi tena kama mfanyakazi Bali uishi kama mke halali wa samiry....."

"Mke ?? 😳

Nilishtuka zaidi

"Unafikili ndoa ua maisha ya mke na mume ni mchezo ??"

Nilimuuliza kwa jazba zaidi

"Lakini umesema ukuwai kuwa na mahusiano lakini mshtuko wako ni kama umewai kuolewa hivi halafu ukaachwa "

"Mmmh maisha ya ndoa, unajua anko rafiki amenifunza mengi sana amenifanya mimi ni binti yake anazingumza na mimi kama ambavyo mzazi anapaswa kuzungumza na mwanae aswa binti ambaye anatalajia kuanza maisja yake au kijana wa kiume anayetalajia kuanza maisha yake, lakini sio ilo tu maisha ya ndoa ya wazazi wangu ambayo sikuwai kuyashuhudia lakini nimeyasikia kutoka kwa baba yangu yananifanya nione kuwa ndoa ni hatua kubwa sana "

"Nakuelewa na nafurahi kuona kuwa samira wewe ni muelewa mno "

Nilitabasamu baada ya kusifiwa yaani mda ni kama mbichwa unataka kupasuka ile misifa yaani

"Tukiachana na mambo ya ndoa tuanze na uchumba ili kujuana zaidi "

"Mmmh "

Niliguna ule mguno ambao ujui utoe jibu gani yaani ukubali au ukatae

"Samira kwahiyo wewe ni bikra....??"

Aliniuuliza

"Naomba twende nyumbani "

Sikutaka kujibu swali lake ilo

"Nitakupa majibu tukifika nyumbani ila nipatie muda wa kila kitu "

Tulifika nyumbani nikakabizisha vitu nilivyonunua kwa mama baada ya hapo nikapata ruhusa ya kwenda kupanga kwenye fliji baada ya kuona kila kitu kimekamilika

"Samira......"

Nilisikia jina langu likiitwa tena kutokea sebuleni

"Naaam mama....."

Niliwai chap kwa haraka

"Naona umechukua miguko yote kasoro huu "

Alizungumza mama na ulikuwa mfuko ule ambao nilipewa na samiry kama zawadi

Majila ya usiku da Salome alikuaa bize na kuchati nami nilianza kuangalia zawadi zangu, jamani katika vitu napenda basi ni chocolate 🍫 na ndio kitu cha kwanza kukikuta kwenye mfuko huo, nilifungua zaidi na kukuta nguo za ndani (chupi) hata sijui kwanini lakini haraka nimazirudisha kwenye mfuko na kusikumia uvuni mwa kitanda na musa huo nilikuwa nikimtazama da Salome kama ananiangalia

"Mungu wangu amewezaje kuninunulia kitu kama hiki huyu "

Nilijikuta tu nikitetemeka bila sababu za msingi

"Itakuwaje da Salome akiziona na kujua kuwa nimenunuliwa na samiry ? Lakini pia atajuaje kama samiry ndo ameninunulia "

Nilibaki nikijiuliza na kujijibu mwenyewe, mwisho wa siku nilisogea na kulala.

Asubuhi na mapema nilikuwa wa kwanza kuamka niliamka na kutoa ule mfuko nikachukua zawadi zangu na kuziweka kabatini vizuri kabisa nilifurahia lakini sasa kuhusu nguo za ndani nilikuwa nikihisi aibu mno

"Hata hivyo itabaki kuwa siri yake na yangu "

Nilijipa moyo kisha nikaingia kwenyw kutimiza majukumu yangu ya kila siku, baba wa familia hiyo aliamka akiwa ameshajiandaa nilimuandalia kifungua kinywa kwani yeye ndio alikua akienda kazini.

"Samira, anko rafiki analalamika sana kuwa haumpigii simu mpaka anajua kuwa tunakupatia kazi nyingi sana "

"Oooh sikuwa na salio lakini leo nitajitaidi nimpigie"

"Fanya hivyo "

Niliendelea na shughuli zangu sikusahau kumpigia anko rafiki ambaye kwa kipindi chote nilikuwa namuona kuwa ni familia yangu kabisa, lakini pia mawazo kuhusiana na samiry yamekuwa yakinitawala sana amekuwa akinitumia ujumbe kila siku wa kutaka kupata jibu lake.

Majila ya usiku niliamua kutoka nje ili niongee na anko rafiki ambaye hakuwai kunificha kitu kuhusu maisha

"Umesema amekuambia kuwa anakuitaji sana .."

"Ndio anasema anataka niwe mkewe "

"Mmmh na wewe unamuonaje anamuelekeo au ??"

"Hata sifahamu "

"Samira binti yangu mzuri kwa upande wa mimi baba yako naweza kusema kuwa Nina furaha sana kuona kwamba lile UA ambalo nimeliweka mbolea na kulitunza vizuri kuna watalii wameliona na kuliitaji, lakini wasiwasi wangu je UA liko tayali ?? Lakini nikiachana na UA vipi kuhusu muhitaji atataka kulitunza UA katika maisha yao yote ? Mmmh binti yangu samira wewe ni mkubwa na unamaamuzi juu ya maisha yako, lakini pia ujakosea kuniambia mimi kama anko rafiki lakini pia baba na mama kwako nikupe muda wa kumchunguza na kumjua vizuri huyo kijana kisha uje uniambia majibu yako yatakupa muongozo wewe pia "

"Sawa baba, uwe na usiku mwema "

"Na wewe pia binti yangu hakikisha unapata yule ambaye atafanya UA license liendelee kuchanua na sio kunyauka"

Nilipokata simu tu nilihisi mtu akinishika kwa nyuma nilishtuka sana na kugeuka kwa jaziba.......

Ipo full mpaka mwisho karibu ujipatie kwa bei ya ofa kabisa
WhatsApp namba 0768328909
Namba za malipo 0768328909 jina Diana John ni voda karibu.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SAMIRA πŸ’‹ πŸ§šπŸ»β€β™‚οΈ 08___9 (Nimeshindwa kusamehe)  >>> https://gonga94.com/semajambo/samira-08___9-nimeshindwa-kusamehe
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest