Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

KISASI KILICHOZAAA MAPENZI🥰🥰 EP 02

27th Jul, 2025 Views 33


Story na Nash

Tsap 0773792227

Wakati Mariah akikazana kucheza alishtuka ndani ya moyo wake baada ya kumuona Max.😬😬

Watu wengi waliachia tabasamu kutokana na aina yake wa wimbo😅😅😅.

Simu ya Max iliita🤨, anaamua kuikaushia baada ya kugundua mpigaji ni Mama yake😌.

Sandra (Mama yake Max) ni mtu wa kujali sana kuhusu Kijana wake😒😒. Baada ya kuona simu yake haipokelewi aliamua kumtrack ili afahamu sehemu alipo🙌🏾.

Anaachia tabasamu baada ya kugundua Kijana wake yupo kwenye Casino la IVY🤔🤔. Aliingia kwenye gari kisha akaweka gia ya mwisho kabisa🙌🏾.

"Ahsanteni kwa kuja kwenye Casino letu😊, muda si mrefu atakuja mwimbaji mwingine endeleeni kufurahia😅😅" Mariah aliongea baada ya muda wake kuisha🙌🏾.

Ile anataka kuondoka alishangaa baada ya Max kumpa ishara ya kusogea🤌.

Mariah alipiga hatua akamsogelea🤥, Max alitoa ishara akalishe makalio yake🤔.

Mariah anakaa akiwa katika uso wa kujiamini kupita kiasi🤨🤨.

Muonekano wa simu ya Max ulimpandisha hasira🤨🤨. Ilikuwa ni simu ya gharama sana kama si Sandra kuteka akili za Baba yake huenda hii simu ingekuwa yake😫😫😫.
Hata muonekano wa ngozi yake ulipaswa uwe wa kwake😫😫.

"Nimefurahishwa na wimbo wako🤔....kwanini hiyo chai ya maajabu iliyogundulika ina wafaa tu Matajiri☹" Max aliuliza

Namna yake ya kuongea ilikuwa ni ya kipekee😌, pamoja na kwamba Mariah alikuwa na chuki na huyu mtu lakini alijikuta akiduwaa kwa namna Max alivyokuwa akiongea🤥🤥.

"Nikiwa jukwaani🤥, nyimbo huwa zinakuja tu zenyewe.🤔🤔...naweza kusema sielewi hata nini nilikuwa naimba🙌🏾. Kitu pekee nacho zingatia huwa ni tabasamu la Wateja🤨" Mariah aliongea

"Itapendeza kama tutapata chakula huku tukizungumza😌😌...agiza chakula chochote nitalipia🤨" Max aliongea

Mariah aliamua kukomoa, aliagiza chakula cha bei kubwa sana😅😅.
Haikuwa shida kwa Max, pesa alizonazo zinatosha kuwalisha watu wote wa Kigali milo mitatu kila siku bila kulalamika😅😅.

"Naamini unapata changamoto kubwa sana kutoka kwa Wateja hasa wa kiume😒..." Max aliongea

"Kazi zote zina changamoto😫, asilimia kubwa ya Wateja wanaokuja hapa huwa wana msongo wa mawazo🤔🤔, wengi ni watu wazito huko mtaani hivyo kazi yangu huwa ni kupunguza stress zao😫😫..... muonekano wako unatosha kuniambia umevurugwa na Wafanyakazi kazi wako huko ofisini🤨🤨" Mariah aliongea

Max aliachia tabasamu,😊 Mariah alijikuta akimkodolea macho kwa jinsi dimpozi zilivyo bonyea na kumfanya aonekane kama Mwanamke😅😅😅.

Max anashindwa kuelewa kwanini Mariah ana mtazama namna hiyo bila kummaliza🤨🤥.
Kabla hajamuuliza chochote Sandra alimfikia🤌

"Sitaki kuamini unapuuzia simu yangu kisa huyu Mwanamke🤨🤨🤨!"

"Nisamehe, lakini sijaona simu yako🤔.... nawezaje kumdharau Mama yangu🤨🤨" Max alijitetea huku akitumia hisia kufuta call history yote

Macho ya Mariah yaliekea kwa Sandra🤔🤔, hakuamini Mwanamke huyu ndio Mama wa Max🙌🏾.
Kama ukiwaona basi utasema ni mtu na Dada yake🤥🤥.
Hakuwa na dalili ya kuzeeka ukilinganisha na Paulina (Mama yake). Kitu hiki kilimuuma sana😫😫😫....aliamini huu muonekano ulipaswa uwe Mama yake.☹☹

Alijikuta akikunja ngumi yake bila wao kumuona🤥🤥

"Hiki chakula kimegharimu laki tatu na nusu kama sikosei🤨.... sielewi ni kitu gani huyu Binti kakufurahisha lakini jitahidi kuwa na matumizi mazuri ya pesa,🙌🏾" Sandra aliongea huku akisogeza meza Kijana wake apite🤨

Max alimuachia Mariah business card bila Mama yake kujua🧐.
Kabla ya kuondoka alilipia pesa ya chakula cha Mariah.😒

Mariah aliitazama business card kwa umakini mkubwa kisha akaiweka kwenye pochi yake😒😒.
Alikula chakula chapu chapu kisha akaelekea nyumbani.🙌🏾

Mara nyingi huwa hapendi kupanda daladala au bajaji hivyo alijiadhibu kwa kutembea kwa miguu.😫

Tamaa ya kuliona Kampuni la Green tea linavyokuwa mida ya usiku ilimuijia🤥🤥.
Alitembea taratibu mpaka alipolifikia😒.

Alijikuta akijiona akiwa amevalia suti huku nyuma akifuatiwa na Walinzi wapatao kumi😥😥.
Wafanyakazi wote walimsifu kwa utendaji wake mzuri wa kazi🙌🏾

Honi ya gari ndio ilimshtua katika ndoto aliyokuwa anaota🤥🤥, aliipisha kisha akaendelea na safari yake.🤔

Baada ya kufika nyumbani alimkuta Mama yake akisoma gazeti🙄

"Kwani Sandra (Mama yake Max) na wewe nani ni mkubwa🥺🥺" Mariah aliuliza baada ya kusalimia

"Nadhani tunalingana, kwanini umeuliza hivyo! vipi mmeonana🤨🤨?" Paulina aliuliza maswali mawili kwa wakati mmoja

"Imetokea tu tukaonana katika Casino🙌🏾, anaonekana kuwa mdogo wa amri☹" Mariah aliongea

"Pesa za Baba yako ndizo zinamfanya aonekane vile😫😫....acha kuongea zaidi kuhusu muonekano wake🙌🏾" Paulina aliongea akionekana kuumia

Mariah alimpatia Mama yake nyama waliokaangwa kisha akaelekea chumbani😌😌😌.

Alifungua begi lake baada ya kukumbuka kuhusu business card aliyopatiwa na Max😌.

Upande wa Max aliendelea kushikiria simu yake🤌, ni kama alikuwa anasubiria atafutwe na Mariah😒

"Hello...Mariah hapa🤔"

"Kata simu nikupigie😊😊" Max alionekana kufurahi kupita kiasi😅.

Mariah anakata simu kisha anaizima😅😅😅, haikuwa bahati mbaya alihitaji kumchanganya tu Max na si vinginevyo🙌🏾.

Max alipiga simu zaidi ya mara ya tano haikuwa inapatikana🙌🏾, anaamua kulala pia.

Kila akikumbuka wimbo wa Mariah unaongelea chai ya maajabu maalumu kwa Wanaume wenye pesa tu aliachia tabasamu😅😅😅.

Kulivyo pambazuka asubuhi alielekea kazini kwake😒.
"Hello..." Aliwasalimia Wafanyakazi wake aliopishana nao🙌🏾

Mezani kwake kulijaa files, alimtazama Secretary wake Jose

"Yaani files zote hizi zinanisubiria Mimi😫😫😫! umeshindwa kupunguza hata moja🙄🙄?"

"Wote hao wanataka kuongezewa mshahara🙌🏾"

"Mshahara? kwanini?🤔"

"Kazi zimekuwa nyingi🤔, halafu watenda kazi ni wachache🙄, nadhani kuna haja ya kuongeza Wafanyakazi wengine🤥🤥...." Secretary Jose aliongea

Kabla Max hajajibu chochote alisimama dirishani akasogeza pazia😌😌

"Unajua.... unajua..." Max aliishia kuongea hivi baada ya kumuona Mariah kupitia dirisha🧐🧐

Alijikuta akikodoa macho zaidi🙄🙄, upepo mwanana uliokuwa unavuma asubuhi hii ulizipeperusha nywele zake na kumfanya aonekane Mrembo zaidi🤔🤔.

Secretary Jose alisogea dirishani🧐, alitaka kujua ni kitu gani kinamfanya boss wake apoteze kumbukumbu ya kitu alichokuwa ana zungumza😅😅

"Mwanamke🙄?....leo umepata wapi nguvu za kushangaa Mwanamke😅😅!.. usiniambie umekula karanga zilizo changanywa na mayai ya kuku aliyezeeka😅😅🙌🏾!" Secretary Jose aliongea huku akitupia utani😆

"Nisaidie kufanyia kazi haya mafaili yote🤔🤔" Max aliongea kisha akaondoka kwa kukimbia alihitaji kuzungumza na Mariah☹

Ile Mariah anataka kuingia kwenye duka linalouza viatu vya kike alishtukia akishikwa mkono wake😫.
Akigeuka kwa haraka aone mtu anaye mpunguzia mwendo☹☹.

Mapigo ya moyo wake yalianza kusikika puuuh puuuh🧐🧐 puuuh hasa baada ya kukutana na tabasamu la Max😊😊😊

Itaendelea
Nash stories
Tsap 0773792227

Full 1000.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

KISASI KILICHOZAAA MAPENZI🥰🥰 EP 02  >>> https://gonga94.com/semajambo/kisasi-kilichozaaa-mapenzi-ep-02
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

gonga94 official track
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest