Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

SASHA (nauchukia mlango wa siri 09___10😭)

19th Jul, 2025 Views 34



Nash stories

Tsap 0773792227

Sikuona sababu ya kufikiria kuhusu msamaha sikuwa nimekosea chochote... niliendelea kufanya mambo yangu. Sikutaka kujua kuhusu mambo ya Biden na Mgeni nilielekea kazini.

Secretary wangu alinikabidhi barua nyingi kutoka vitengo mbalimbali. Nilizifanyia kazi....moja ya barua ilinitaka ni safiri tofauti na hapo nisingeweza kutoa jibu linalotakiwa kwenye barua hii.

Mwanangu hakuwa akinyonya tena hivyo nilimuacha na Dada wa kazi. Ilikuwa ni safari ya siku tatu. Nilimjulisha Biden kwa njia ya ujumbe.

"Uwe na safari njema....na safiri pia kwa wiki mbili sitakuepo" Biden alinitumia ujumbe

"Sawa.." Nilimjibu kisha ni kajiegemeza kwenye kiti cha gari

Nilisafiri kama Mkuu wa chuo na si Mke wa Rais, hivyo nilijisitiri uso wangu kuepuka macho ya watu
Baada ya kufika sehemu niliyo dhamiria tulikaa kikao ili niwapatie jibu linaloeleweka kwa lugha nyingine nilihitaji kuonyesha msisitizo.

Mazingira ya huku yalikuwa ya kijijini hivyo swala la mtandao lilikuwa ni changamoto. Ilitulazimu kufanya vikao hadi usiku ili siku ya kesho niondoke.
Tulikubaliana chuo kingine kwa ajili ya Wanafunzi wenye ulemavu kijengwe sehemu hii.

Asubuhi na mapema sana, Nilianza safari ya kurudi nyumbani kwangu. Baada ya masaa manne kupita nilifika. Nilikuwa nimechoka sana hivyo nililala bila hata kuvua viatu.

Nikiwa nimelala nilikumbuka kuna chumba cha siri mahali hapa kwa kuwa Biden hayupo nilihitaji kujionea kwa macho yangu vitu gani vimehifadhiwa kwenye chumba cha siri.

Nilifungua mlango wa chumbani kwetu kisha ni kaufunga nilifanya hivyo kama mara tatu ndipo mlango wa chumba cha siri ulifunguka pia. Niliingia haraka..... moyo wangu ulivunjika baada ya kukuta chumba alichokuwa amekaa siku moja Biden na Donald kimefungwa.

Niliangaza nione kama kuna kitasa hakikuepo.... mlango kama huu niliwahi kukutana nao kipindi nikiwa chuo Nchi za nje. Niliupapasa mlango mara tatu ukafunguka.
Niliangaza macho yangu huku na kule nione kama kuna camera zimetegeshwa sikuona.

Kilikuwa ni chumba kidogo tu hivyo niliweza kukagua kwa muda mfupi. Sikuambulia chochote.....wakati nataka kutoka nilikumbuka kuna funguo niliiona.

Niliishika funguo kisha ni kajiuliza moyoni hii funguo inafungua wapi. Kwa sababu hakukuwa na kabati wala mlango mahali hapa.

Nilikitazama chumba vizuri kwa mara nyingine. Nilifanikiwa kuona sehemu ambapo funguo inatakiwa kupita. Ilikuwa ni sakafuni kwani baada ya kutoa zurulia niliona kitasa.

Nilikitekenya kisha kikafunguka. Huku chini kulikuwa na handaki... niliingia nikiwa na hofu ya kukamatwa
Hofu yangu ilikata baada ya kukutana na picha kubwa ya Mwanamke ikiwa ukutani. Alikuwa ni Mwanamke wa kawaida sana lakini kwa sababu yupo na mapambo alionekana mrembo.

Sikuelewa kwanini hii picha ipo hapa na ina maana gani.

Niliisogelea karibu ilikuwa imeandikwa jina la Mariah
Niliangaza huku na kule nilifanikiwa kuona diary, niliishika ni kaanza kuisoma...kadri nilivyozidi kusoma machozi yalizidi kunitiririka

"Mariah ahsante kwa kuniruhusu nitimize ndoto yangu....kitu kinachoumiza moyo wangu ni kimoja tu, kumpenda Mwanamke niliyechaguliwa na Wazazi wangu kisha ni kakuacha wewe kwa sababu isingewezekana kuwa wote.... "

"Najaribu kukusahau lakini inashindikana.... nisamehe kwa sababu muda si mrefu nitakutafuta ili nijue unawezaje kufurahia maisha bila Mimi"
Haya ni baadhi ya maneno ambayo Biden alikuwa ameandika kwenye diary yake. Nilirudisha vitu kama vilivyokuwa kisha ni karudi chumbani.

Hakuna siku nililia kama siku ya leo....eti ananipenda Mimi kwa sababu ni chaguo la wazazi wake
Mlango uligongwa kisha nikapewa taarifa kuhusu ujio wa Mke wa Rais Golden.

Niliingia bafuni nikanawa uso, sikutaka afahamu kama nilikuwa nalia. Baada ya kumaliza nilielekea bustanini.

Mama Biden alikuwa ana cheza na Collin... niliachia tabasamu kwa jinsi walivyokuwa wanacheza kwa upendo

"Macho yako yamevimba usiniambie bado una usingizi au ulikuwa unalia" Mama Biden aliniuliza
"Nina usingizi siku ya jana sikulala vizuri" Nilijibu kisha ni kakaa
"Hapana ulikuwa unalia...." Mama Biden alisisitiza
Sikuona sababu ya kubishana naye nilimuacha ashinde katika hili

"Ndoa ndivyo zilivyo mwanangu kuna muda zinakuwa tamu na kuna muda zinakuwa chungu....sijui ni kitu gani unapitia lakini naomba usikilize hadithi yangu kwa ufupi" Mama Biden alizungumza kisha akambeba vizuri Collin
Nilitega masikio nisikilize kwa umakini kitu nachotaka kuambiwa

"Rais Golden alinioa kwa sababu Wazazi wangu walikuwa na ushawishi mkubwa katika Siasa.... alikuwa na Mwanamke anayempenda lakini ililazimika anioe Mimi ili atimze ndoto zake....Biden aliulizwa kama ana Mwanamke ndani ya moyo wake alikataa kata ndipo tulipendekeza akuoe wewe kwa sababu familia yako ni marafiki zetu wakubwa" Mama Biden alizungumza kisha akanishika mkono

Sikutaka kuzungumza nilichokiona kwenye chumba cha siri.... nilitamani Mama Biden aondoke ili niendelee kulia.
"Sasha, naomba uzungumze chochote ukikaa kimya unanipa wasiwasi" Mama Biden alizungumza kwa mara nyingine

"Hakuna Mama anayependa kusikia mabaya ya Mwanae.... ahsante kwa kujali kuhusu Mimi ni kweli nilikuwa nalia sababu ya Biden. Naomba tusizungumze sana" Niliongea

"Sawa, kama huna majukumu mengine naomba twende wote Supermarket kuna vitu nahitaji kununua kwa ajili ya Collin" Mama Biden alizungumza
Nilikubali hivyo nilienda ndani kujiandaa baada ya hapo tuliondoka, Mama Biden alimpakata Collin miguuni kwake hivyo niliendesha gari.

Tuliingia Supermarket moja inayoaminika kwa ubora wa bidhaa zake. Tulianza kuchagua vitu...Collin alikuwa anatembea tulimuacha awe huru ili kama kuna kitu kitakuwa kimemvutia aseme tumchukulie.

Nikiwa naendelea kuchagua vitu nilimsikia Collin akisema "nataka"...nilisogea karibu nione kitu gani anataka. Ulikuwa ni ubuyu wa pilipili....nilichukua ni kampatia aushike moyo wake uridhike.
Wakati nainua hivi kichwa nilifanikiwa kumuona Mariah Mwanamke aliye andikwa kwenye diary ya Biden. Nilitamani ni muongeleshe japo niijue hata sauti yake
Yeye pia aliniona, alinipa heshima bila shaka ni kwa sababu Mimi ni Mke wa Rais. Nilitikisa kichwa kuashiria nimepokea salamu yake... aliendelea kuchagua vitu.

Tulikutana tena sehemu ya malipo, watu walisubirishwa sababu yangu na ya Mama Biden. Niliamua kutenda wema kwa kuwalipia watu wote walionunua vitu. Hata Mariah nilimlipia pia.... walinishukuru huku kila mmoja akinitakia maisha marefu.

"Hivi ndivyo siasa inakuwa hakika umeupiga mwingi" Mama Biden alizungumza
Niliachia tabasamu la uongo.... hakika ndani ya moyo wangu nilitamani kuzungumza na Mariah na si vinginevyo.

Baada ya siku mbili kupita nilimpeleka mwanangu Clinic.... niliamua kwenda hospitali za kawaida lengo langu lilikuwa ni kuona namna huduma zinavyotolewa.
Hospitali yote ilichangamka baada ya kugundulika nipo hapa. Nilisikia watu wakisema siku ya leo wanapatiwa huduma kama Wafalme
Kwa kuwa nilikuwa nimechelewa sikutaka kuwa wa kwanza kupata huduma niliwaacha niliowakuta wapate huduma.

Zamu yangu ilifika, nilishtuka ndani ya moyo wangu baada ya kuona Mariah ndio anatoa huduma. Nilijifanya sielewi kama najua yeye amewahi kuhusiana na Biden. Yeye pia hakuonesha kushtuka badala yake alinikaribisha na kunipongeza kwa kuhudhuria Clinic katika hospital yao.

Baada ya kupatiwa huduma niliondoka, nilimuita Nesi mmoja aliyekuwa kabeba bahasha...tulifuatana mpaka kwenye gari
"Vipi unafurahia kufanya kazi hapa" Nilimuuliza
"Natamani ningefanyia hospital ya kati kwa sababu hapa kuna changamoto nyingi lakini ndio hivyo si rahisi kupata uhamisho" Nesi huyu alizungumza
"Bila shaka una mfahamu Mariah.... naomba unitafutie hadithi nyingi zinazo mhusu yeye.... ukifanikiwa njoo katika chuo kikuu cha Mini....nitakuhamisha sehemu hii pia utapata zawadi zingine" Nilimuambia Nesi huyu huku ni kimhimiza azuie mdomo wake asije kuzungumza kwa watu kazi niliyompatia.

Nesi huyu aliahidi kuwa msiri tuliagana kisha Mimi nilielekea nyumbani. Nilishangaa kumuona Biden kwa sababu wiki mbili zilikuwa hazijatimia.
Alinikumbatia huku akisisitiza kanikumbuka. Sikujua ni kitu gani napaswa kumuambia hasa nilivyo kumbuka maneno aliyo andika kwenye diary yake kuhusu Mariah eti atamtafuta ajue anawezaje kufurahia maisha bila yeye

"Kichwa changu hakipo sawa naomba nipumzike" Nilimuambia Biden huku ni kimtoa kwenye mwili wangu
Biden alinielewa alinipandisha kitandani kisha akanifunika shuka.... hakutaka kuondoka alilala pembeni yangu.
Nilimtaka aendelee na mambo yake, alidai siku ya leo hana kazi nyingi hivyo atakaa pembeni yangu mpaka nitakapojisikia vizuri

Sielewi ananipenda au ni analazimisha moyo wake kwa ajili ya usalama wa ndoto yake. Kifua changu ni kidogo sana niliamua kumuuliza swali ambalo sina uhakika kama alitegemea nitawahi muuliza

"Biden, kabla ya kuwa na Mimi umewahi kumpenda mtu mwingine" Niliuliza

ItaendeleaWhtsp 0773792227
Nash stories
Full 800

SASHA (nauchukia mlango wa siri 10😭)

Nash stories

Tsap 0773792227

Biden aliamua kukaa kabisa kutokana na swali nililomuuliza
"Sasha ni kitu gani kimetokea mpaka uulize kuhusu ex wangu" Biden aliuliza kwa sauti iliyojaa msisitizo

"Nataka kujua tu unajua Mimi na wewe tulioana bila kuzungumza mapito yetu" Niliongea

"Hili swali ulipaswa uniulize siku ya kwanza nilivyo zungumza hisia zangu kwako. Ni utoto kuzungumzia mtu anayeitwa ex pengine kama kuna sababu za msingi....ni weke wazi kama kuna sababu za msingi" Biden alizungumza akiwa bado kanikazia macho

"Huenda bado unampenda ex wako ndio maana hutaki kumzungumzia" Nilijikuta ni kizungumza
Biden alicheka kwa sauti kubwa kisha akanisogelea

"Bila shaka umechoka kutimiza majukumu yako ya ndoa.... Mwanamke anayependa ndoa yake hawezi kuzungumza hizi habari" Biden alizungumza
Sikujali kuhusu maneno yake, moyo wangu unaniambia hii ndio nafasi ya pekee kuzungumza kuhusu kila kitu nachokijua
Nilimuambia kuhusu chumba cha siri.... nilizungumza pia kuhusu picha niliyoiona pamoja na maneno aliyoyaandika ndani ya diary yake.

Niliona Biden katoa macho kwa mshangao mkubwa... niliendelea kusisitiza aongee chochote kuhusu Mariah ili moyo wangu uwe na amani

"Sasha, siku zote najua mlango wa siri na ufahamu pekee yangu na Donald kumbe hata wewe una ufahamu?" Biden alizungumza
"Mimi ni mkeo napaswa kujua kila kuhusu wewe, kumbuka likitokea tatizo kwako Mimi ndio nitakuwa mtu wa kwanza kuulizwa na si Walinzi wako...hivyo sioni kama kuna kosa Mimi kuufahamu mlango wa siri, sielewi kwanini hukunieleza kuhusu hili" Nilizungumza

"Chochote kibaya kikinitokea mtu wa kwanza kuulizwa ni Donald, kisha Walinzi wangu halafu atafutia Daktari wangu sina uhakika kama utaulizwa kuhusu changamoto zangu zaidi ya kupatiwa pole" Biden alizungumza

Nilijikuta ni kicheka baada ya kuona nafasi yangu haijatajwa nilijihisi kudhalilika... nilitaka kuzungumza lakini Biden alinizuia tena kwa ukali
"Na kumbuka ulisema haujisikii vizuri naomba upumzike...." Biden alizungumza kisha akaondoka
Moyo wangu ulibaki kutapatapa baada ya kujua chochote kikimpata Biden Mimi siwezi kuulizwa chochote zaidi ya kupewa pole. Nilijikuta ni kilia....majibu yake yalikuwa makali sana.

Usiku uliwadia lakini Biden hakurudi nyumbani.... nilikuwa bado na hasira hivyo sikuona sababu ya kumtafuta.
Yeye pia hakunitafuta hivyo kwa usiku mzima Mimi na yeye hatukuzungumza.... kulivyo pambazuka nilienda kazini. Kwa namna fulani hasira ilikuwa imeisha, nilishika simu ni kamtafuta Biden lakini simu iliita mpaka ikakata. Nilitaka kurudia kupiga lakini ujio wa Secretary wangu ulinikatisha

"Profesa, kuna Mgeni katokea hospital ya Mama na mtoto kadai una taarifa zake hivyo anaomba mzungumze" Secretary alizungumza
"Mruhusu aingie....." Niliongea

Yule Nesi niliyempatia kazi kuhusu Mariah aliingia, alinipatia heshima kisha ni kamruhusu akae

"Mariah hana maajabu yoyote....anaishi maisha ya kawaida. Mpaka sasa hajaolewa na wala hayupo kwenye mahusiano" Nesi alizungumza
"Hapana, hujachunguza vizuri...." Nilimuambia Nesi baada ya kuona anaongea upuuzi
"Huenda nikawa sijachunguza vizuri lakini hizi habari ndizo nimeruhusiwa kuzungumza kwako....kuna mambo mengi na fahamu kuhusu Mariah lakini asubuhi ya leo nimepigiwa simu na mtu asiyejulikana kanipa vitisho" Nesi alizungumza kisha akaondoka
Hakusubiri hata nimuulize mambo mengine,

Akili yangu inaniambia Biden ndio anamkingia kifua Mariah ili nisipate kujua kuhusu mambo yake. Mimi ni Boss mahali hapa hivyo nina mamlaka ya kutoka sehemu hii muda wowote ninaotaka, nilihitaji kuonana na Mariah ilikuwa ni busara zaidi kwenda na Secretary wangu.
Nilimtuma aingie hospital aulize kuhusu Mariah endapo atampata basi amlete kwenye gari, sikuweza kuingia ndani ya hospital kuepuka macho ya watu.

"Mariah ni mgonjwa ana ruhusa" Secretary wangu aliniletea majibu
"Usijali, Mlinzi wa getini atanipeleka nyumbani kwa Mariah" Nilizungumza
Secretary wangu alitikisa kichwa kuashiria ameelewa.... alizungumza na Mlinzi wa getini.
Mlinzi alitupatia mtu atupeleke nyumbani kwa Mariah.

Akili yangu inaniambia huenda Biden atakuwa nyumbani kwa Mariah. Hivyo niliongeza kasi ya gari.
Baada ya kufika nyumbani kwa Mariah sikuona dalili zozote za uwepo wa Biden nilimtaka mtu aliyetuleta aondoke kisha Mimi na Secretary wangu tuliingia ndani
"Nadhani unaelewa Mimi ni nani hivyo naomba ukae kwa kutulia, nitakagua kila sehemu mpaka niridhike moyo wangu" Nilizungumza kwa ukali
Mariah hakuwa na shida aliniruhusu ni kague.... nilifanya hivyo nikiwa na hasira, harufu ya perfume niliyowahi kuinusa kwa Biden enzi za mgeni wa siri nilikutana nayo chumbani kwa Mariah.

"Naomba uniambie bado una husiana na Biden" Niliuliza kwa ukali
Marian alitoa macho ya mshangao
"Vipi ulihisi sitajua!" Nilijikuta ni kianza kujijibu mwenyewe
Mariah hakuzungumza chochote....aliniacha ni kaongea pekee yangu. Hasira zilinijaa nilijikuta ni kimpiga vibao pamoja na kumshushia matusi mazito.

Nilimuamuru Secretary wangu tuondoke baada ya kuona Mariah si mtu wa vita....nilivyotoka nje nilimkuta Biden kasimama, alikuwa kavaa nguo za kawaida pamoja na kofia. Sina uhakika kama Secretary wangu alimtambua. Kwa namna nilivyokuwa na hasira nilimpita kama simfahamu hivi. Nisingeweza kurudi kazini, ilinilazimu kurudi nyumbani ni kapumzishe akili yangu, nilimsihi Secretary wangu achunge mdomo wake kuhusiana na kila kitu alichokiona.

Niliingia chumbani kisha ni kajifungia, nililia sana kwa sababu naelewa Biden atambembeleza Mariah na mwisho wataishia kufanya ngono.
Najuta kwanini niliingia chumba cha siri, sidhani kama ningefahamu kuhusu Mariah kwa sababu Biden hakuwahi kuzungumza

Mida ya usiku Biden alirudi, alikuwa kavaa vizuri... kabla hata hajazungumza na Mimi nilimpongeza kwa kufanya ngono na Mariah
"Naona umekuwa mwepesi.... Mariah kakuchagulia nguo nzuri, hakika umependeza" Nilizungumza

Biden hakuzungumza chochote badala yake alipiga magoti, sikuelewa anataka kufanya nini hivyo nilikuwa mtazamaji...

"Katika siri zote ulizowahi kuzitunza naomba usije ukazungumza kwa watu, Wazazi au mtu yoyote wa karibu yako kuwa Rais Golden na Mkewe siyo Wazazi wangu wa damu. Naomba uifiche sana siri hii kwa sababu hata wao hawajui kama Mimi ninaishi na ukweli huu, nilifanya makosa makubwa kuandika siri hii nzito kwenye diary" Biden alizungumza

Macho yalinitoka, ile siku sikuimaliza kuisoma diary kwa sababu maneno niliyokutana nayo mwanzoni tu yaliniumiza. Nina uhakika Biden anahisi nilisoma mpaka mwisho.

"Kuhusu Mariah naomba umuache kadri unavyozidi kumfuatilia ndivyo unazidi kunikumbusha kama nimewahi kumpenda kupita kiasi. Kuanzia sasa naomba tuishi kama Mume na Mke na si kama marafiki.....nimekupigia magoti nikiwa na maana kubwa sana, naomba uuchunge mdomo wako kwa ajili ya mwanao.....siku utakayo funua mdomo wako kuzungumza siri yoyote iliyotoka mdomoni mwangu kwa mtu mwingine sitakusamehe" Biden alizungumza kisha akasimama

Alinisogelea kwa ukaribu
"Sijafanya ngono na Mariah, tangu ni kuoe wewe sijawahi kuonana naye. Ikitokea nimemkumbuka huwa najipulizia perfume anayoipenda. Nadhani tumeelewana Mke wa Mimi" Biden alizungumza kisha akaondoka

Nilibaki nimesimama, kuna aibu ilipenya moyoni mwangu. Niliona kama nimemkosea Mume wangu, nilitoka chumbani ni kamkimbilia ili tuzungumze lakini tayari alikuwa ameingia kwenye gari.
Nililikaribia gari ni kagonga dirishani afungue lakini haikuwezekana. Nilivyozidisha kuwa msumbufu dirisha la gari lilifunguliwa.
Nilimshuhudia Biden akiwa anatokwa machozi, kioo kilipandishwa kisha gari likaondoka.

Niligundua nimemkosea sana Mume wangu, lakini kuna sauti niliikumbuka kutoka kwake eti akimkumbuka Mariah huwa anapuliza perfume anayojipulizia Mariah ili kupoza moyo wake. Hapana, nilihitaji kujua ni kitu gani Mariah alimtendea Biden mpaka awe ana mkumbuka

Itaendelea.......

Malizia simuliz hii kwa 500 tuπŸ™ŒπŸΎ sitapost tena.
Whtsp 0773792227
Nash stories.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SASHA (nauchukia mlango wa siri 09___10😭)  >>> https://gonga94.com/semajambo/sasha-nauchukia-mlango-wa-siri-09___10
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest