Macho ya mwalimu Rashid yalibadilika ghafla. Aliangalia uso wa Romeo kwa umakini kana kwamba anajaribu kusoma maneno yaliyoandikwa kwenye moyo wake.
“Unamfahamu vizuri Nasra?” aliuliza kwa sauti ya chini lakini yenye msisitizo.
Romeo alimeza mate, akihisi joto la mwili wake likipanda. “Kidogo tu mwalimu,kwa sababu ni mwanafunzi mwenzangu” alijibu kwa upole, huku macho yake yakikwepa yale ya mwalimu.
“Kidogo tu?” Rashid akakariri, sasa akijisogeza karibu zaidi na Romeo. “Au unampenda?” alimuuliza kimtego.akitaka anase ili akione cha moto.....
Swali hilo lilimchoma kama sindano ya sindano ya kalyo . Romeo alijikuta akiduwaa.
“Mwalimu… mbona unadadisi sana ,” alisema kwa sauti ya kukatika.
Rashid alitabasamu kuzuga. “Mioyo yenu nyie vijana... Siku zote mnadhani mnajua kupenda kuliko sisi, kumbe hamjui hata kupenda kivuli cha upendo.”
Romeo alishusha pumzi nzito. Alijua sasa hana la kujitetea.
“Ni kweli mwalimu,” alisema baada ya kimya kifupi. “Nampenda Nasra. Lakini nampenda kama mwanafunzi mwenzangu ambaye tunashirikiana tu kwenye masomo na si vinginevyo...
" sio una mtaka awe demu wako Romeo?
" mmmmmh hapana mwalimu sijawahi kumuona hivyo sababu hata sheria za shule haziruhusu . Ila sijuwi huenda akawa na mtu wake?"
Alicheka sana Rashidi na kupigs hatua
Rashid alimsogelea karibu sana.na kusema “Na kama huyo mtu ni mimi?”
Romeo alipigwa na butwaa. Akatazama uso wa mwalimu wake kwa mshangao, akijaribu kuelewa kama ni mzaha au kweli.
“Mwalimu, wewe?”
“Shule hii ni zaidi ya unavyoiona Romeo... Kuna mambo mengi yanaendelea nyuma ya pazia.”
" lakini ondoa wasiwasi kijana wangu wewe kazana kusoma ukiwa kama sisi warembo utawafanya utakavyo unadhani si tungecheza tungefika hapa . Epuka mapenzi ni hatari kwa afya sawa?
Rashid akageuka na kuondoka, huku akimwacha Romeo amesimama pale ameduwaa. Moyo wake ulikuwa umejaa maswali kuliko majibu.
Kwa upande wa Kelvin, bado alikuwa jikoni, lakini hata harufu ya mchuzi wa maharage haikumsisimua kama kawaida.
Aliendelea kuchokonoa sufuria huku machozi yakimlengalenga, kumbukumbu za Nasra zikiwa kama sinema akilini mwake.
Alikumbuka maneno yake ya mwisho:
“Sitaki mapenzi na wewe kelvin .. ukurasa nimeufunga.”
Lakini moyoni alijua ulikuwa uongo. Kwa sababu bado anampenda. Na hakujua kwanini alimuumiza kiasi hicho, huku akiwa na nia ya kumlinda.
Akatikisa kichwa kwa huzuni. “Labda Nasra alimbusu Rashid ili kunilinda... au ndio kweli hanijali tena na kayahamishia mapenzi kwa Mwalimu wake ?”
Huku akiwa na maswali hayo, mara mlango wa jikoni ukafunguliwa taratibu. Alidhani ni mwanafunzi mwingine, lakini alipofungua alishtuka.
Ilikuwa Neema naye kaja kujaribu bahati.
“Samahani Kelvin,” alisema kwa sauti ya adabu. “Naomba niongee na wewe kidogo... siyo kwa niaba ya Nasra, bali kwa sababu ni rafiki yake.”
Kelvin alitulia, akaegemea mlango, uso wake ukiwa hauna furaha wala hasira bali ni huzuni ya wazi.
“Sema.”
Neema akavuta pumzi. “Kelvin... Nasra hajawahi kumpenda mtu kama alivyokupenda wewe. Alifanya alichokifanya kwa sababu mwalimu Rashid alimtishia atakufanyia mpango wewe na Nasra mfukuzwe hapa.
Ila zaidi alipanga aanze na wewe kwanza ni bahati tu Nasra ndiyo akajikuta analazika kufanya hivyo ili kukulinda wewe na hata kujilinda mwenyewe.
Hakuwa na namna. Alijitoa sadaka kwa ajili yako lakini nashangaa unavyomhukumu kelvin ujuwi jinsi gani anavyolia hosteli,jatibu hata kuiona thamani yake ata kama ni kidogo ..”
" hakuna kitu kinauma kama kumpenda mtu ambaye hujuwi moyoni kakuwekaje sijuwi mlianzaje ila nachojua Nasra anakupenda sana Kelvin . Lione hili swala na ulipe uzito tafadhali" kisha akamtazama machoni
Kelvin alishtuka. “Umesema?”
“Alijitoa... kwa ajili yako,” alirudia Neema huku machozi yakianza kumtiririka.
“Leo alilia mpaka tukashindwa kumfariji. Ametetemeka, amevunjika moyo, amepoteza kila kitu lakini bado moyo wake upo kwako.”
Kelvin alifumba macho, pumzi ikawa nzito. Hakujua afanye nini, aende, amtazame, amkumbatie... au akae tu hapo na aendelee kuumia kimya kimya.
Alifungua macho yake polepole, akamuangalia Neema kwa macho ya shukrani.
“Niambie yuko wapi,” alisema kwa sauti ya upole.
Neema akajibu, “Bwenini. Chumba namba nne.”
Kelvin hakusema neno lingine. mwambie nimemsamehe leo jioni aje pale kwenye historia ya mapenzi yetu. Nitakuwa namsubiri saa 3 kamili usiku .
Neema alitoka mbio mbio kuelekea bwenini baada ya kujua tayari rafiki yake kasamehewa kabisa na kipenzi chake kelvin.Angalau hata bwenini watarudi kuwa na furaha kama mara ya kwanza ...
Akiwa anaelekea bwenini alikutana na Romeo akiwa kabeba begi lake kanyong'onyea
" kheee Romeo shida ni nini?
" mapenzi neema "
" mapenzi??? Kwa nan?
" kwa rafiki yako Nasra"
" mmmmh pole sana "
" pole ya nini tena "
" kumpenda asiyokupenda ninayekupenda hunitaki"
Aliondoka Neema na kuelekea bwenini sio kwamba Neema ni mbaya sema kana ujings fulani hivi ambao unamkera Romeo. Neema akiwa anaenda bwenini
" mmmh shoga nyota imewaka wanaume watatu wanampenda mimi nipo tu anigawie hata kipande cha nyota"
Aliingia Bwenini, Nasra alikuwa bado kalalia kitanda, uso wake umefichwa kwenye mto. Jeska alikuwa pembeni,
Mara mlango ukagongwa.
Nasra alishtuka. “kama una habari mbaya kaa kimya kama ni njema nakusikiliza "
Neema akatabasamu kwa huzuni. “Hapana, za leo ni za moto .”
" za moto kivipi? Wakati kelvin kanikataa jeska si kaenda ?
Neema akainua kichwa. na kutabasamu akaanza kupiga makofi na kusema kwa sauti
" kakusamehe kasema historia ya upendo muda saa tatu ...
Nasra alitabasamu na kusema “kweli Neema? ......mpaka machozi yanamtoka
ITAENDELEA...
FULL 1000
0699286085.