.
Usiku wa saa sita na nusu ndani ya jiji kubwa la Dar es Salaam, giza ndilo lilikuwa limetanda huku likidhibitiwa na mwanga mkali wa taa za umeme barabarani na kwenye majumba ya watu pia.
Ghafla sana sauti ya milipuko sita ya mabomu ikasikika, na mwanga mkali ukali pasua anga la jiji kutoka ardhini mpaka juu angani.
Mwanga huu ulisababisha Watu wengi waliokuwa kwenye pilika pilika zao za kila siku kushtuka sana kufuatia milipuko hiyo sita mikubwa iliyolipuliwa muda mpufi tu uliopita.
Watu wakaingiwa na hofu kuu, kila mmoja akatafuta upenyo wa kuiokoa nafsi yake mwenyewe.
Dakika zikasogea binadamu wakiwa mbali kabisa na eneo hilo ambalo muda mfupi uliopita ilikuwa imesikika milipuko mikubwa ya mabomu..
Lakini ambacho kilikuwa kikiwashangaza ni ile hali ambayo ilikuwepo, licha ya mabomu kulipuka lakini baada ya mabomu hayo kulipuka, ukafuata ukimwa mkubwa sana.
Shauku ya kutaka kujua nini kinaendelea ikajaa ndani ya nafsi ya baadhi ya watu ambao waliingiwa na sintofahamu baada ya ukimya mkubwa kutawala, watu wakaongozana kufuatilia eneo ambalo milipuko mikubwa ilikuwa imesikika..
Baada ya muda mfupi kama dakika mbili hivi Watu walikuwa wengi sana eneo la tukio.
Kila mmoja alibaki mdomo wazi maana milipuko hiyo imelipuliwa eneo la wazi ambalo hakuna watu kabisa, hakuna majeruhi wala aliyepoteza maisha.
Watu wakaanza kucheka na kuhisi hisia mbalimbali, mfano baadhi ya watu walianza kuhisi itakuwa Tanzania wapo watu ambao wameanza kutengeneza silaha za moto hivyo walikuwa kwenye majaribio ya silaha zao, huku wengine wakisema labda ni mabomu yalilipuka bahati mbaya, ila ukweli kila mmoja hakuwa na majibu sahihi ya kile ambacho alikua akikiwaza kuhusu milipuko hiyo ya mabomu.
Muda wa takribani dakika kumi na tano tu ulitosha kabisa kumfanya kila aliyeisikia milipuko hiyo kufika eneo la tukio, tayari walikuwa zaidi ya watu elfu mbili eneo hilo, kila aliyefika alileta mtazamo wake juu ya milipuko hiyo na kila aliyeleta mtazamo wake alikuwa akipata sapoti ya watu wengine, hivyo mtazamo ulikuwa ukijadiliwa mpaka upatikane mtazamo mwingine.
Watu wakashindwa kuondoka kuendelea na shughuli zao za kila siku, badala yake wakaona kuwa ni eneo ambalo wanaweza kupiga soga na kufahamiana zaidi, maana walikuwa watu wengi sana na kila dakika ya saa ilipoisha watu walikuwa wakiongezeka badala ya kupungua, Ile hali ya kuogopa ikatoweka kwa kila aliyefika eneo hilo..
Kitu ambacho kilikuwa kikishangaza sana na kilikuwa ni kitu cha ajabu sana, mpaka mda huo hakuna polisi aliyekuwa amefika eneo la tukio, licha ya kituo kidogo cha kati cha polisi kuwepo karibu kabisa na eneo hilo, lakini hakuna hata polisi mmoja aliyesogea mahala hapo.
Darcrown Hotel ni hoteli kubwa sana mjini Dar es Salaam, ilikuwa ikimilikuwa na tajiri mkubwa tu ndani ya nchi ya Tanzania.
Hoteli hii husifika kwa ukubwa wake na wingi wa vyumba vya thamani sana, hivyo hukaa na hupangwa na watu wenye nyadhifa kubwa Serikalini..
Ilikuwa hoteli yenye ghorofa 22 kwenda juu, jengo lefu la mraba lenye upana wa futi 12..
BIM Company limited, ni kampuni kubwa ya madini Tanzania, kampuni hii nayo ilikuwa na ghorofa 22 kwenda juu, ndani ghorofa hizo walikuwa wameweka frem mbalimbali kwaajili ya wafanya biashara..
Hivyo wafanya biashara wamekuwa wakikodisha vyumba kutoka kwenye kampuni hiyo, kwaajili ya kuendesha biashara zao..
BIM Company limited na Darcrown Hotel, zilikuwa zimetengwa na barabara ndogo ya mtaa huo..
Mlipuko hiyo ilikuwa imetokea katikati ya kampuni ya BIM Company limited, na ile hotel ya Dar crown Hotel, hivyo binadamu ambao tayari walikuwa wamesogea eneo hilo la tukio walikuwa hawana hofu wala mashaka kabisa bila kujua wanajichimbia kaburi wenyewe..
**********************
Juu kabisa ya jengo la BIM Company limited anaoneka mwanaume ambaye alikuwa amekamata macho ya shetani au kwa kiswahili fanisi darubini, hii ilikuwa ni darubini ndogo ya mkononi ukiachana na zile za kusimika kwa stendi.
Kwa kutumia kifaa hicho cha kuona mbali akawatazama kwa makini watu waliokuwa chini kabisa ya kampuni hiyo..
Mwanaume huyo alikuwa amekamata kifaa kilichokuwa sikioni kwake kisha akasema.
"Mkuu sasa tageti yetu imeenda vizuri sana naona wapo zaidi ya watu 1700 hapa, kwa ruhusa yako naweza kufanya Tanzania ilie muda huu, vile vile kwa ruhusa yako naweza kusubiri waongezeke zaidi?"
Hiyo ilikuwa sauti ya mwanaume huyo ambaye alikuwa amefunika sura yake kwa maski nyeusi na kuacha macho pekee yaonekane, ili aweze kuona vizuri.
Mwanaume huyu alikuwa juu ghorofani akitazama kundi kubwa la watu lililokuwa chini kabisa, na aliweza kuwaona vizuri sana kwa kutumia kifaa chake cha kuona mbali,( darubini)
Maneno hayo aliyasema huku akiwa ameshika kifaa fulani cha mawasiliano kilichokuwa sikioni kwake.
"Unaweza kusubiri na wasiongezeke baadala yake wakapungua, fanya tukio ambalo litamshitua kila atakaye sikia juu ya kifo chao, zingatia asiondoke hata mmoja"
Hayo ni maneno ambayo yalisikika kutoka kwenye kifaa kile cha sikioni, ikimpatia ruhusa muuaji huyo aliyefunika sura yake kuwa afanye hayo mauaji.
"Sawa mkuu"
Alisema hayo muuaji huku akiweka mabomu yake vizuri ili kushusha bomu moja baada ya jingine mpaka watu wote wapoteze maisha.
***
Baada ya muda mfupi akanyanyuka na kurusha bomu la kwanza ambalo lilienda na kuziba njia upande wa kulia wa majengo hayo makubwa mjini Dar es Salaam, mwanaume hakuridhika akatupa bomu lingine ambalo lilienda na kutua eneo lilelile na kufanya moto kuongezeka zaidi baada ya mlipuko mkubwa sana kutokea.
Moto uliowaka baada ya milipuko hiyo ukaleta taharuki kwa kila mmoja, haraka wakaandamana kukimbia wakielekea upande ambao haukuwa na moto ili waondoke eneo hilo.
Ghafla mbele yao ikaibuka milipuko mitatu ambayo ilipelekea watu zaidi ya mia tatu kufa pale pale kwa mshituko wengine kuunguzwa na moto wa mabomu hayo, yaani ulikuwa ukatili mkubwa sana uliofanyika ndani ya dakika moja au mbili hivi.
***
Milipuko saba ikafuatana kufuatiwa na moto mkubwa katikati ya kundi la watu, harufu kali sana ya nyama ya kuchoma ikapasua anga.
Si nyama ya mbuzi au nyama ya nguruwe, au pengine kuku Bata na jamii yote ya ndege, hapana, hii ilikuwa harufu ya miili ya binadamu kama mimi au wewe ambao walijikuta walichomwa kama mishikaki wakiwa hai tena wanapumua vizuri sana.
Moto ulikunja ngozi zao wakiwa wanatazama, hatimaye wakaanza kubabuka wakiwa wanatazama, kilio na yowe havikufaidia kitu kabisa, kila mmoja aliteketea kwenye moto huku maumivu makali sana akiyahisi bila chenga.
Harufu ya nyama zao zilizoungua na kuiva kwenye moto wao wakitazama ndio ilipasua anga na kuingia kwenye pua ya kila aliyekuwepo eneo la karibu.
Zaidi ya watu elfu 1700 wakafa palepale kikatili sana, hakuna majeruhi wala mtu aliyepona, wote walikuwa wameshindwa kuendelea kuivuta hewa ya kwenye huu ulimwengu wa maovu, tena kifo cha kuteketea kwa moto na miili yao kuungua kikatili sana
***
.
Siku iliyofuata polisi wakafika eneo la tukio, baadhi ya watu waliokuwa wakishuhudia miili ya ndugu zao machozi yalikuwa yakiwatoka, ukiacha polisi na baadhi ya waandishi wa habari kila mmoja alikuwa akitokwa na machozi kwa jinsi miili ilivyokuwa imejaa eneo hilo na kuchomeka kikatili..
Polisi hawakuweza kulia maana hawakuwa wakiruhusiwa lakini laiti wangeruhusiwa basi na wao wangetokwa na machozi maana ilikuwa inasikitisha sana..
Waandishi wa habari wakasogea eneo la tukio ili kukusanya maudhui ambayo yangewafikia raia siku hiyo..
Kwa siku ya kwanza midia ndogo zikafika eneo hilo, hatimaye zikakusanya taarifa kwa video kuonyesha miili ya watu walio ungua kwa moto, wale ambao walionekana walizuiliwa wasipaishe maudhui hayo ya kutisha, ila wengine wakawa wagumu na kuondoka zao huku wakitambua kuwa, hiyo ni sehemu ya Fursa ambayo inaweza kuzisaidi midia zao kujipatia umaarufu na kukua zaidi, hatimaye zikamudu vyema soko la media mtandaoni.
Taarifa hizo zikapasua anga na kusambaa kwa kasi ndani na nje ya nchi ya Tanzania, kila aliye zipata taarifa hizo alisisimka mwili mzima na wengine kushindwa kuwa na uvumilivu, machozi ya maumivu yakapenya katikati ya mfereji wenye kutenganisha pua na mashavu na mwisho machozi yale ya laana yalikuwa yakishuka chini ardhini, na kinywa cha mtu huyo kujikuta kikisema,
"Ulaaniwe kila mkono ulioshiriki juu ya vifo vya hawa watu wasio kuwa na hatia'
***
Zaidi ya watu 1700 walikufa ndani ya usiku mmoja, huku wauaji wasiache hata ushahidi mdogo eneo hilo, hakuna mtu ambaye alifanikiwa kufahamu muuaji alikuwa amekaa eneo lipi kati ya hayo maghorofa mawili, maana camera hazikumnasa muuaji wakati anaingia wala wakati anatoka.
Siri ikawa ya mbingu, ardhi na muuaji mwenyewe, huku polisi na serikali ikikosa eneo la kuanzia uchunguzi wao..
Hakika Mungu azilaze nafsi hizo mahara panapostahili sema ameni kwenye comment...
********
****
*
KAHAMA SHINYANGA
Siku iliyofuata ikiwa ni majira ya saa 7 : 45 mchana..
Waziri mkuu wa nchi ya Tanzania mheshimiwa Dr Fabian Sunda, alikuwa kwenye ziara yake ambayo alikuwa akimuwakirisha Mh. Rais wa nchi.
Alikuwa akizungumzia masuala ya uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya, akawa anaelezea kuwa inatakiwa kupoteza na kutokomeza ufisadi na uuzazi wa madawa ya kulevya ndani ya macho ya nchi ya Tanzania.
Mheshimiwa Dr. Fabian Sunda akawa anaelezea mpaka madhara ya kutumia madawa ya kulevya, akagusia mpaka lile tukio lililotokea mjini Dar es Salaam, huku akiwahakikishia wananchi kuwa serikali ya Tanzania itawatia mbaloni wahusika wote wa vifo vya watu wasio na hatia..
***
Kando ya mkutano huo wa waziri, kulikuwa na ghorofa refu sana kwenda juu, ghorofa hili lilimilikiwa na kampuni moja maarufu ya film Tanzania, hivyo jengo hili likawekwa kama hoteli mjini hapo.
Juu kabisa kwenye froo za mwisho ndani ya ghorofa anaonekana mdunguaji (sneipa).
Mkononi alikuwa amekamata silaha hatari sana ya masafa marefu, alikuwa ana jitahidi kumuweka mh. Waziri mkuu kwenye tageti za kilengeo chake, ili aweze kutoa uhai wa Waziri huyo Mkuu wa nchi.
Kwa muonekano mdunguaji huyo alifanana sana na yule muuaji aliyehusika na mauaji kule mjini Dar es Salaam usiku wa jana yake.
Alikuwa amevaa nguo nyeusi kuanzia juu mpaka chini na kuifunika sura yake kwa maski nyeusi tii!, ila siku ya leo hakuwa na macho ya shetani bali mkononi alikuwa amekamata silaha hatari sana ya kulenga masafa marefu.
Huku tageti yake akiwa ameielekeza aliko mheshimiwa waziri mkuu wa nchi ya Tanzania.
.
(N.B Simulizi hii ni ya kubuni haihusu matukio yaliyowahi kutokea hapa duniani, wala haimhusu mtu yeyote wala kiongozi yeyote yule, bali ni simulizi ya kubuni ili kuburudisha kufurahisha zaidi kuelimisha)
.
Mara baada ya kuweka tageti zake vizuri akatoa kidole chake kwenye triga kisha akaachia silaha na kurekebisha kifaa kilichokuwa sikioni kwake.
Baada ya tukio hilo akakamata vizuri sana bunduki yake kisha akaingiza kidole chake kwenye triga, akavuta kidogo triga nakusema
"Good"
Baada ya kusema hayo kwa sauti ya chini sana akaachia tabasamu jembamba na kusema,
"Mkuu nipo kwenye tageti"
Baada ya kusema hayo akanyamanza, mara sauti ikasikika kwenye kile kifaa cha sikioni ikisema
"Vizuri sana, sasa kazi imebaki mkononi kwako, hakikisha haponi, maana amenusurika kufa kwenye tageti za wadunguaji wengi"
Muuaji aliposikia hivyo, alitabasamu na kusema,
"Siwezi kufeli boss, maana mimi ni mzoefu na kazi yangu, Dr Strange kama jana tu nimeangamiza zaidi ya watu 1700 kwa wazo langu moja iweje huyu nyumbu mmoja anishinde!? namuamgamiza wala usijari mkuu"
Muuaji huyo alisisitiza, huku akijinadi na kunyamanza kidogo kisha ikasikika sauti ikisema
"Kazi njema"
"Nashukuru mkuu"
Baada ya kujibu hivyo akakamata bunduki yake ya masafa marefu na kuvuta triga ili kuruhusu risasi kutoka, alipo achia risasi ikachomoka kwa kasi sana, akatoa ganda la risasi na kuweka risasi nyingine, alikuwa Fasta sana hata kabla risasi haijafika kwa muhusika alikuwa tayari ameweka tageti nyingine.
Risasi ile ikasogea na kuzama kwenye kifua usawa wa moyo wa mheshimiwa waziri mkuu wa nchi ya Tanzania.
Muuaji baada ya kufanya tukio hilo akasema
"Dili Dani"
Akakamata bunduki yake, akaiachanisha, magazine akaiweka kando na bunduki, kisha akaikunja haraka na kuihifadhi kwenye begi lake jeusi baada ya hapo akagusa mfukoni na kutoa karatasi akaandika maneno baada ya kuandika akaiacha karatasi hiyo pale alipokuwa na kuanza kuondoka kawaida kama vile sio yeye aliyehusika, alipofika mlangoni akageuka na kuitazama karatasi ile kisha akarudi na kuiweka eneo zuri ambalo askari watakapo ingia wataiona kwa haraka...
*****
Polisi nao wakaanza kupanda ghorofani maana walikuwa wameelekezwa eneo risasi ilikotokea.
Polisi wakazuia kila mtu kutoka nje ya jengo hilo, lengo lao walitaka kumkamata muhusika wa kifo cha Mheshimiwa waziri mkuu wa nchi.
Baadhi ya askari walikuwa wakiwakusanya watu sehemu moja ili msako uendelee.
Walipanda mpaka juu ghorofani, wakafanikiwa kuingia eneo ambalo alikuwepo muuaji, hawakukuta mtu wala ushahidi wowote zaidi ya karatasi iliyokuwa na maneno.
Kiongozi akaikamata ile karatasi na kusoma kilichokuwa kimeandikwa mle, baada ya kusoma ujumbe ule hapo akashituka sana.
Akakamata karatasi ile kwa nguvu sana kisha akawaamuru askari kutoka nje haraka kabla yaliyoandikwa kwenye karatasi hayajatimia.
Askari wakafuata amri na kushuka haraka ngazi, wakatoka mpaka nje kabisa na kusimama mbele ya mlango mkuu wa jengo hilo.
Bila wasi wasi muuaji akatoka nje na kukamata pikipiki yake, akawatazama sana wale polisi akatabasamu na kuanza kucheka sana tena kwa dharau ya juu.
Muda huo huo wanajeshi wakafika, wakashangaa kuona muuaji anataka kuondoka kwa dharau mbele ya polisi.
Haraka kiongozi wa jeshi akataka kuamrisha kikosi chake kumkamata mtuhumiwa ila kabla hajafanya hivyo akamsogelea kiongozi wa askari aliowakuta na kusema
"Muuaji anaondoka unatazama"
Yule kiongozi hakuwa na maneno mengi akatoa karatasi na kumpatia hapo akashituka na kusema
"Huyu mjinga anataka kuua watu wote hawa"
Alisema kwa sauti lakini cha ajabu yule muuaji akawajibu kwa sauti akiwa mbali kuonyesha anawasikia vizuri sana.
"Watu waliopo hapa hotelini ni wachache sana, vipi niliowaangamiza huko Dar es Salaam?"
Hapo akafanya hasira kuongezeka kwa yule kiongozi wa wanajeshi, akaanza kumfuata kwa hasira, ila akashituka baada ya mlipuko mkubwa sana kutokea ghorofa ya juu.
Alipomtazama muuaji alikuwa na limoti mkononi kwake.
Hapo akakumbuka kilichoandikwa kwenye ile karatasi
"Natoka mkiwa mnanitazama, na kama mkitaka kunikamata naangamiza kila mtu aliye kwenye hoteli hii na wale walio kwenye mkutano wa waziri mkuu, maana huko kote nimetega mabomu na limoti ninayo mimi, kwahiyo mkileta jeuri nalipua moja baada ya nyingine nanyi pia mkiwemo"
Maneno hayo ndiyo yalikuwa yameandikwa kwenye ile karatasi, yakamfanya kiongozi huyo wa wanajeshi kurudi nyuma na kusimama kando.
"Kama hamuitaji hawa watu wapoteze maisha basi hakikisha hamni fuatilii maana kama mkinifuatilia hata mmoja nitajua,, na nikijua sitaongea kama ninavyofanya sasa bali nitafanya kwa vitendo, nitaangamiza watu wote walio katika eneo hili"
Baada ya kusema hayo muuaji akawasha pikipiki yake akiwa anajiamini sana bila hofu huku akicheka.
Mmoja wa askari akakosa uvumilivu kabisa akafyatua risasi ambayo ilienda na kumpata muuaji kisogoni.
Ila ajabu muuaji akasimamisha pikipiki badala ya kuanguka kisha akawageukia na kusema
"Hilo ni kosa sana, na kwa taarifa yenu mimi mwili mzima nina vifaa vya kuzuia mwili wangu kudhurika, mnacho takiwa kufahamu hakuna panganga au mjinga yeyote anayeweza kuniua kwa risasi hata kama mngemimina, mimi kufa kwa risasi ni ndoto ya mchana"
Baada ya kusema hayo akagusa kisogoni na kuitoa risasi ambayo ilikuwa juu ya maski aliyokuwa amevaa, kisha akaitazama na kucheka.
Palepale akabonyeza rimoti.
Ukasikika mlipuko katikati ya watu ndani ya jengo hilo.
Mlipuko huo ukapelekeaa watu kurushwa kama karatasi kutoka juu ghorofani kwa kupitia dirishani na kutupwa chini wakiwa wameiva kwa moto, huku moto mwingine ukionekana dirishani na kupotea baada ya mlipuko kumalizika.
Askari polisi aliyefyatua risasi ili kumzuia muuaji huyo kuondoka na kufanya watu wengi sana kupoteza maisha, hatimaye hukumu ikampata ndani ya moyo wake na kufanya maamuzi magumu sana ya kujipiga risasi, maana aliona amefanya makosa makubwa sana na kusababisha vifo vya Watu kwa kosa la kutofuata amri ya kiongozi wake.
Watu waliumizwa na kile kitendo cha kinyama kilichofanywa na muuaji huyo asiye julikana, machozi yakawatoka maaskari na wanajeshi ambao walikuwa wamejiapisha kulinda nchi na watu wake, vile vile ule ujasiri wa kujizuia kulia ukawashinda kabisa maana walitokwa na machozi ya maumivu sana, hasa hasa ni hili tukio lililotokea muda mfupi uliopita watu kufa mbele ya macho yao na muuaji kuondoka kwa dharau sana huku akiacha watu wakiwa wamefariki kikatili.
"Nani ambaye yupo nyuma ya pazia?"
Kila mmoja alikuwa anajiuliza swali hilo..
UVS COURAGE DAR ES SALAAMU.
Ni majira ya saa 8 : 15,
UVS courage Dar es Salaam ni chuo kilichokuwa kinapatikana nchini Tanzania, chuo hiki kilikuwa kikifundisha coz mbalimbali ikiwemo coz ya kompyuta.
Isabella na Alexander walikuwa miongozi mwa wanafunzi walio kuwa wanasoma katika chuo hicho, mpaka sasa imepita miaka mitatu tangu waanze kusoma katika chuo hicho cozi ya kompyuta.
Uhusiano wao ulianzia kwenye urafiki mpaka baadae wakajikuta wameingia kwenye ulimwengu wa mapenzi, hatimaye kwa sasa wapo kwenye ulimwengu mzito wa mapenzi, walikuwa wanapendana sana.
Isabella alikuwa binti mzuri sana na mwenye kuvutia, vijana wengi walikuwa wakimuhitaji lakini hakuna ambaye alifanikiwa kugusa hata kifua cha mtoto wa kike.
Aliyekuwa na bahati alikuwa kijana ambaye anafahamika kuwa hana kipato kabisa, na vile mkopo wa bumu nao ulikuwa haujatiki upande wake basi ndio akawa hana pesa mazima, Alexander ndilo jina lake.
Uzuri wa binti ulikuwa ukiwapagawisha vijana wengi sana pale chuoni, wengine wakawa wanatumia pesa lakini hakuna hata siku ambayo waliweza kupata hitaji la moyo wao, wala hakuna siku ambayo Isabella alipokea pesa kutoka kwa kijana yeyote yule.
***
Dickson alikuwa kijana mwenye pesa nyingi sana pale chuoni, alisifika kuwa hakuna kitu alichokitaka asikipate, kama akitaka mwanamke akakataa pesa basi alitekwa na alienda kumfurahisha kinguvu na pesa hapewi, kwahiyo mabinti wakatambua kama binti hata mmoja akiitwa na Dickson inatakiwa aende ili apewe hata pesa baada ya kufanya kile alichoitiwa na Dickson.
Siku hiyo Dickson akiwa anatoka kwenye kipindi, mbele ya macho yake akakutana na sura nzuri sana ya kuvutia, kila alipokumbuka kama amewahi kukutana na binti mzuri kama huyo moyo ukakata kabisa.
Tangu awepo kwenye chuo hicho Dickson, miaka mitano sasa imekwisha na ndio alikuwa anachukua shahada yake ya mwisho ya biashara na mauzo, ila hakuwahi kabisa kumtia machoni mtoto mzuri sana kama huyo.
Isabella ndie ambaye alikuwa mbele ya mboni za macho yake binti ambaye hakuwahi kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine zaidi ya mwanaume ambaye watu wanamdharau kwamba hana kitu.
"Huyu binti ninamuhitaji mda huu, nataka nimkute geto, iwe kwa nguvu au kwa pesa yoyote atakayoitaka"
Akatoa amri na kuondoka zake kurudi alikokuwa anaishi yeye na kikosi chake, alipofika ajabu akawakuta vijana wake wamefika mda sana.
"Naona kazi ilikuwa nyepesi sana"
Akasema hayo huku akishangazwa kwa jinsi walivyokua wamevimba.
"Unamaana hamja mleta"
Dickson akauliza kwa hasira sana.
Wale vijana hawakuongea neno badala yake wakatoka simu na kumuonyesha video ya kile walichokutana nacho baada ya kwenda kumkamata binti huyo.
Dickson akachukua simu ili atazame kilicho kwenye video ile.
Alishangaa sana kwa alicho kiona.
"Kwahiyo huyu binti anapiga kiasi hicho?"
Wale vijana wakati kisa vichwa kisha mmoja akasema
"Huyu mwamke ni mtu hatari sana mkuu"
Alijibu hayo kijana wake mmoja..
"Ila hakijaaribika kitu lazima nimpate ikiwezekana nitaomba msaada kwa baba."
Alisema hayo Dickson huku akiwa anazidi kuwatazama vijana wake kwa zamu..
Itaendelea...
Usikose Sehemu ya pili.
Ukajue majibu ya maswali haya.
Je polisi watafanikiwa kumpata muuaji?
Ni kwanini mauaji yamekuwa mengi sana Tanzania.
Muuaji kabla hajamuua Mh. Waziri mkuu alitamka jina la Dr Strange, je huyo mtu ninani?
Je huyo Isabella ninani kwa nini wamuite mtu hatari kiasi kwamba Dickson awaze kuomba misaada kwa baba yake?.
Usikose...