MTUNZI; LIZY MICA
Ukiyaangalia vizuri macho yake utagundua hayana tofauti na yale ya Simba jike.
Kama angezaliwa Mwanaume basi angeitwa Jemedari wa vita.
Wakati mabinti wengine wakiwatazama Wanaume kwa aibu, yeye aliwakodelea macho bila kupepesa kana kwamba anaangalia movie ya kusisimua.
Songa nayo 🌻
Jina lake anaitwa Sultana, akiwa na miaka 16 alipoteza usichana wake ili tu aokoe maisha ya mdogo wake.
Tangu hiyo siku aliisahau ndoto yake ya kuwa Rubani wa ndege aina ya Airbus A320
Aliamua kujikita katika biashara ya kutembea na Wanaume tofauti tofauti bila kujali umri wao.
Kitu pekee alichokipa kipaumbele kila alipokutana na Wanaume ilikuwa ni pesa. Jina lake lilikuwa maarufu ndani ya Kijiji cha Odes kuliko zao la tumbaku
🩸Sijivunii kuwa na Dada kama wewe....matukio yako yamekuwa ni ya kutisha kuliko hata ya watu wasiojulikana. Nahitaji kutimiza ndoto zangu hivyo kuanzia sasa nitakaa mbali na wewe, kama hatutaonana tena katika ulimwengu huu naomba usihuzunike sana ipokee kama hatma yetu🩸 Mara nyingi Sultana huwa anayakumbuka maneno ya Sona (mdogo wake wa kike) hasa akiwa amelewa. Japo ni miaka kumi imepita sasa lakini anahisi ni kama jana
Siku yake huwa inaenda vibaya kuliko kawaida.....upendo alionao kwa Sona hauwezi kupimika na mizani ya Mangi
Shauku ya kumtafuta mdogo wake ilimuijia ghafla, aliamini sehemu pekee atakayoweza kumpata Sona ni Jijini Odes, hivyo alifunga virago vyake akaelekea stendi kuu kusubiria magari yanayoenda Jijini Odes.
Pumzi nzito kama mtu aliyetua mzigo zilisikika miongoni mwa Wamama na Mabinti baada ya kusikia Sultana ameonekana maeneo ya stendi.
Ni wazi kabisa alikuwa tishio kwao kuliko hata tetemeko la ardhi.
Waliiomba miungu yao isimrudishe kabisa Kijijini kwao, adhabu ya kifo au kupotea kusikojulikana ingemfaa zaidi.
Baada ya Sultana kukaa siti ya dirishani, alifumba macho yake.....hakufurahishwa na namna watu walivyokuwa wanamuangalia.
Safari ya kuelekea Jiji la Odes ilianza, watu wengi akiwemo yeye walionekana kuwa na shauku ya kufika.
🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
Ndani ya Jiji la Odes;
Katika jumba la kifahari lililojulikana kama Jumba la dhahabu, ukimya ulitawala kwa sababu ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Marmar.
Binti huyu alipoteza maisha siku moja kabla ya harusi yake.
Ripoti ya Daktari ilithibitisha kifo chake kimetokana na sumu aliyoivuta kwa njia ya hewa.
Ingawa ni miaka miwili imepita sasa lakini imekuwa ngumu kusahaulika katika Jumba la dhahabu.
"Liam yupo njiani, naomba kila kitu kiwekwe vizuri....hakikisha rangi nyeupe inatawala ukumbini na si hizo mlizoweka....msisahau kutakuwa na wageni pia" Bi. Fatma (Mama yake Liam) aliongea
Wafanyakazi walifanya kama walivyoagizwa....kila kitu kiliwekwa katika mpangilio mzuri.
Kabla ya Liam kwenda nyumbani kwao, alipita katika Casino lililojulikana kama "the night watchman"
Kuna mtu alihitaji kuonana naye kwanza kabla ya kwenda kushiriki kumbukumbu ya kifo cha Marmar, aliyesalia kidogo kuwa mke wake
"Sielewi kwanini umewekeza nguvu nyingi kuchunguza kwa mara nyingine kitu kilichokwisha kuthibitishwa na Daktari bingwa miaka 2 iliyopita, kama ningekuwa ni wewe nadhani ningefunika kombe mwana haramu apite..." Sona (mdogo wake Sultana) alishauri
"Naomba uniambie hicho ulicho fanikiwa kupata kwa kipindi chote nilichokuwa nje ya Odes..." Liam aliongea, ni wazi alitaka kusikia matokeo na si ushauri
Sona alimpatia bahasha iliyokuwa na ushahidi wa kila kitu
Liam hakuwa na subira, alichana bahasha ajionee kitu kilichopatikana.
Mapigo ya moyo wake yalizidi kwenda kasi kutokana na taarifa aliyokutana nayo
"Marmar alikufa kwa sababu alianza kufatilia kesi iliyofungwa muda mrefu...." Sona aliongea
"Nahitaji kumjua Muuaji na si chanzo cha kifo chake hilo ndilo lilikuwa lengo la Mimi kukuachia hii kazi....." Liam aliongea akionekana kutofurahishwa na taarifa alizopatiwa
"Alikuwa ni rafiki yangu, alinikaribisha Jijini Odes nikiwa sina sehemu ya kwenda...kwa pamoja tulitimiza ndoto zetu za kuwa Polisi. Kila kitu kitafahamika ni swala la muda tu naomba uniamini" Sona aliongea huku machozi yakimlenga lenga kwa kushindwa kufurahisha moyo wa Liam
"Nisamehe, umejitahidi kwa kiasi chake" Liam aliongea baada ya kuona Sona ana dalili ya kulia
Kwa pamoja waliingia kwenye gari, walihitaji kwenda kushiriki kwenye kumbukumbu ya kifo cha mpendwa wao Marmar.
Watu wote walidondosha machozi baada ya kumuona Liam, tabia yao ya huruma ilimfanya ajisikie maumivu.
Fatma (Mama yake) alilitambua hili hivyo alimtuliza kwa kumkumbatia.
Muda wote Sona alimtazama Mwanaume huyu kwa matamanio....alijipa matumaini ipo siku atakuwa Mkwe katika Jumba la dhahabu.
"Iliandikwa wewe ufe ili Mimi ni bakie na Liam.... naomba usinichukie sana, hakukuwa na njia nyingine tofauti na wewe kufa kifo kile " Sona alijisemea ndani ya moyo wake huku akiitazama picha ya Marmar
"I wish urudi kwangu kama Mzimu...." Liam alijisemea akisogeza mdomo wake auzime mshumaa lakini kabla hajafanya hivyo
Watu wote waligeuka baada ya kumshuhudia mtu akija usawa wao akiwa amevalia mavazi meupe sawa na yao
Itaendelea 💥.