Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMM💘💐💘 SEHEMU YA (05)

1st Jul, 2025 Views 55



Ilifika mida ya saba hivi usiku watu washalala mtaa upo kimyaa Alex akanambia mi naondoka sasa nahisi sasa hivi ni salama nikasema sawa😣😔

Alichukua simu akampigia inno akamuelekeza amfate .

Wakati anamsubiri akaniuliza

"Hivi salma!!"

"Abee"

"Mbona haujaniuliza chochote kilichonikuta jana kwaniniii??"

"Hahah afu we bwana, wewe si ulinambia sio mwizii?? Na hauonekani kama mwizi hayo mengine mi hayanihusu" nikamjibu simple yaan kama vile sijali ,

Kumbe mwenzie umbea wote ninao , upo full nikawa namchora tuu .

"We wa ajabu, utakuja kuweka wezi huku ndani hayaa"

"Kwahiyo unanichambaa eeeh"

"Sio bwanaaa nakutania"

"Sitakii "akachekaa😍😍alafu akaniangalia mmmm mimi hapo sijielewi kimvutano fulani hivi kikawa kinaendelea😌😌basi Alex aliniita

"Salmaaaaa ,naomba basi nikukumbatie please mamyyyy!!!" mmmmmm Kabla hata sijajibu alinikumbatia dah🫂😩nilissmkaaaaaaaaaa

"Asante salma Ubarikiwe sana bint omar una pepo yako ujue" mmm niliishia kumwangalia tu machoni dah😍😍😌

Simu yake iliita muda huo huo akaitoa alikuwa Inno akapokea inno akamwambia nimefika , basi tukatoka mie mbele naangalia mazingira nyuma Alex

"Sante bint" inno akanambia huku anatabasam jamani huyu kaka nyie mzuri afu wanafanana kweli na Alex

"Alex aliniambia inno ni pacha wangu , Rafiki yangu kaka yangu yaan huyu ndio kila kitu kwangu" aliongea huku anamshika bega Inno

"Ndo mana mnafanana ni mapacha kwelii??" Nikauliza namie huku nacheka cheka tu

"Yeah ,huaminiii" inno akanambia

"Hapana naamini bwana "

"Nitakutafuta Bint eeeh" inno akanambia jamani hawa watu wanameno meupe yaan gizani lakini unaona vizuri kweliii

Mi nikacheka tu wala sikujibu kitu , Alex akaniaga akaingia kwenye gari mi nae nikaingia ndani ndo wakaondoka zao kwao..

Niliingia Chumbani nakiona chumba kimekuwa kipweke kweli yaan nilijiona mnyongee ,nikapanda zangu kitandani ,haya masaa sijui mangapi ya kukaa na Alex nimejikuta nimemzoea nikaona kama kuna tisha kuwa peke yangu..

Niliamka asubuhi na mapema kama kawaida kugombea dala dala za kariakoo niwahi kibaruani,

Nikaoga zangu chap chap nikavaa baada ya kumaliza sasa kila kitu nikawa nachukua zangu funguo juu ya Kabati ili nifunge mlango niondoke,

Ile nachukua funguo nikashangaa naona hela nyekundu nyekundu juu pale mmh kwanza nikaguna hizi hela mi akiba yangu huwa hata elfu 30 haifiki ndani tena vibuku buku kibao ..

Sasa hizi nyekundu afu mpyaa kabisa zimetoka wapi??,ooooh nikakumbuka pesa nilizopewa na Inno jana zilikuwa hivi kama zimetolewa bank mana hata harufu yake ilikuwa inaonesha.

"Itakuwa amezisahau Alex" nilizitoa sehemu zilipokuwa huku najiwazia kwa sauti mungu wangu ni nyingi itabidi nimtafute Alex nimwambie ile nawaza kumpigia ghafla nikaona kiujumbe kwenye karatasi..

( Salmaaa ,nimeona aibuu kukupa hiyo pesa mkononiii naomba upokee kidogo chungu ila sio kama nimekulipa Noo!! Yaan hata sijui niiwekaje ila naomba upokee Mwaya💘 )

Nilicheka tu , na hizi shida nilizo nazo nikajitupa kitandani huku nacheka cheka , Hapo naona Uvivuu kwenda kugombea dala dala ,yaan pesa bwana yaan niende nikagombane na wateja hukooo kariakoo kwanza wasumbufu wanadharauuu afu napewa ka Elufu 7 tu!!!?

Huwezi amini ujinga wangu nikaanza kuziona tabu nyingiiii za kariakoo wakati zamani sikuziona😂baada ya kuona kile kibunda cha pesa akili ikaanza kuona kero za kariakoo dah😂😂

Nilizishika vizuri zile pesa nikazihesabu mara mia mia yaan siamini Nakumbuka zilikuwa Laki sita ,we Huogopi?? Laki 6 yaan ushike afu umezoea mwisho 10000 hiyo elfu 50 ukiipata sherehee ..

Nilizikumbatia zile pesa nikarudi kulala😂😂huko kariakoo napigwa jua kusambaza vyakula afu jioni nalipwa elf saba tu bora niachane na huo utumwa nitafute kibiashara nijifanyie na hii pesa..

Nilishtuka kumekucha tena niliamshwa na simu inaita nilipo itazama alikuwa boss wangu ,nikapokea

"We salma unachelewa sana siku hizi sijui upoje mkifukuzwa kazi mnasema tunaroho mbaya hambebeki kabisaaa"

Mama yule akaanza kunitokomeza maneno afu waga anamdomoo ,nikamsikilizaaa mpaka alipo maliza nikamwambia

"Mama mi mbona nishaacha kazi mwaya "

"Nini 😳😳???"

"Mi kazi nishaachaa"

Niliamua tu kuacha kazi ,yaan hapo najiona mie nina pesa nyingi sanaaa kama boss lady tu vile yaani hahahaaaa

niliamua nitafute biashara yangu mwenyewe nikimbize ,hivi ulishawahi kulala maskini afu ukaamka umekuwa tajiri??

Ndio mimi hiyo siku niliona kama hii kwangu ni miujiza ,nilitamani kumwambia Alex Asante,nilitamani nimwambie kitu kilichokuwa moyoni mwangu ,furaha niliyokuwa nayo ilikuwa imepita kiwango , lakini sikujua ninampata vipi hata , nikabaki tu kumshukuru moyoni..

Iyo siku sikula wala kusogeza kali😌o nilishinda kitandani naitazama ile pesa nifanye niniii??

Mpaka sa nane inafika ndo nikahisi tumbo kukwangua kwa kasi ,si ndo nikakumbuka sikula tangu asubuhi, nikajiinua taratibu,

nilichukua begi langu la nguo nikaweka zile pesa chini kabisa nikapanga nguo juu vizuri, unajua ile hata ukiwa la laki mtu akikufata nyuma unahisi ni kibaka ndo mie hapa mwenzenu,

nilienda Gengeni nimefunga mlango kabisa na Funguo nimebeba lakini nilikuwa natembea huku nageuka nyuma asije shoga kuingia akazipitia ..

Kuna muda nilihisi labda zinawezakuyeyuka humo ndani ,nilikuwa napika kidogo nakimbia kuzitazama zipo , nikiziona naomba mungu anilindie mana hela nimezipata kimiujiza zisije ondoka tena kwa miujiza hivyo hivyo...

Nikampigia simu mama angu baada ya kumaliza kula, nikamuhadithia kila kitu hata kupewa hiyo pesa, kwanza alipanic akanichamba niache tabia ya kukaribisha watu hovyo

nikamwambia mama jamani basi nisikilize kwanzaaaaa!!!! ndo akatulia nikamuelezea habari ya pesa wacha aanze kusema ni jambazi ,mtu wa kawaida hawezi kuacha pesa nyingi hivyo hawezi ,

jamani ilibidi nianze tenaa upyaaa,kumuhadithia kuhusu fumanizi yaan mama yangu mbona nilikomaaa ..

Baada ya kujilidhisha kabisa ndo akanambia embu tulia kwanza hela ya kutumia si unayo nikasema ndio ipo akasema haya kaa utulie kwanza najua hujawahi kushika hiyo pesa hapo ulipo una kitete kwelii!! Nilichekaa mana ni kweliii natetemeka hatariiii

Niliamua kufata ushauri wa mama, nikatoa vi akiba vyangu vyotee ,nikapiga hesabu ,ipo elfu 20 , nikawaza hii pesa inanitosha kula mie hili wiki lote mpaka wiki ijayo nitakuwa tayari nimejua nini cha kufanya zaidi ..

Nakumbuka ilikuwa kama siku ya pili yaan ukiacha ule usiku wa Alex kuondoka ,ile jumatatu ikapita ikapita jumanne , juma tano nilipigiwa simu na namba ngeni ilikua mchana nipo zangu ndani nimejilaza sina hili wala lile nipo tu nacheck movie kwa raha zangu ..

Nikapokea ilikuwa sauti ya mwanamke

"We nanii??" Akaniuliza mie ,wakati yeye ndie amepiga

"Jamani we si ndo umepiga sasa"

"Aah sorry sijui nimekosea namba ,Nilikuwa namtaka mwenye simu"

"Mi ndo mwenye simu!!"

"Sorry ni naniii" sasa alikuwa anaongea kwa ustaarabu kweli ,si nikajichanganya nikasema mi naitwa Salma

"Salmaaaa ,embu we ni salma wa hapo kwa mama ziadaa???" Moyo ukashtukaaa mana huyo mama ziada ni mama mwenye nyumba wetuu

Sa nikasema huyu mtu ananijua nilisita kidogo naitafuta sauti kama niliwahi kuiskia mahala lakini ilikataaa

"Ndio mie ,we nanii???"

"Mh , hii namba ulimpa nani atumie??" Sikuelewa swali lake nikabaki najiwazia

"Sikuelewi kwani we nani"

"Mi juddy" moyo paaah ,nusu nizimie

"Wa wapiii" nilikuwa nishamjua vizuri sana ila nikajiulizisha tu ili nipate nafasi ya kufikiria mengine

'"Mh inamaana sio tu inno, na alex pia?? Niambie ukweliii salma I'm Serious " wee nikasema nimeyatimba mungu wangu miee nafanyajee??

"Sikuelewi unaongea ninii??" Nikajifanya nundaa

"Utanielewa upo wapi sasa hivii??"

"Kwanguu"

Si nikajichanganya miee ,najutaa bora hata ningesema sipo , baada tu ya jibu simu ilikatwa , nikaanza kutetemeka huyu mwanamke namwambia nini miee

Baada ya dakika chache tu Nikasikia mlango wangu unagongwa nilishtuka moyo paa , nilitetemeka huku nachungulia dirishani mama weeeeeeeeeeee🥵..

Itaendeleaaaaaa

KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMM💘💐💘 SEHEMU YA (05)  >>> https://gonga94.com/semajambo/nilizani-mwizi-kumbe-mmmm-sehemu-ya-05
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

GIGY MONEY DAH😭

majario rewards 100 Comments 0
 

YOUNG AFRICANS,

majario rewards 100 Comments 0
 

BAKORA VILLAGE

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 7...8

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA EPISODE 2

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE...5...6

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 3...4

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA 1

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈21

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈20

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 8

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 7

majario rewards 100 Comments 0
 

Life in a Year (2020)

majario rewards 100 Comments 0
 

Kenya, Tanzania, Congo

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 40

majario rewards 100 Comments 0
 

POSHY QUEEN:

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 39

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈19

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈18

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈17

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈16

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈15

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 05 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 04 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 03 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 02 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 01 ❤❤.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 34

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TUWASHUKURU KINA BABA

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest