MTUNZI; LIZY MICA
Endelea ๐ป
Sona alimshikia Dada yake bastola huku uso wake ukiwa umekunjamana
"Usiku wa leo nitautumia vizuri kuwatafuta wauaji wa wageni kutoka Israel.....hivyo kutakapo pambazuka asubuhi naomba uondoke na kamwe usije kurudi Jijini Odes, endapo utaenda kinyume na makubaliano yetu nitaachia risasi bila kujali ulipoteza bikira yako ukiwa na miaka 16 kisa Mimi" Sona aliongea kisha akairudisha bastola yake kwenye koti
Sultana alibakia kukodoa macho, kila kitu alichokuwa ana kiona na kusikia ilikuwa ni ndoto kwake
Sona alitaka kuondoka lakini aliijiwa na wazo jipya kichwani mwake
"Utalala nyumbani kwangu usiku wa leo....kutakapo pambazuka asubuhi nitakurejesha mwenyewe Kijijini Odes..." Aliongea kisha akaanza kukusanya virago vyote vya Sultana pamoja na pesa zake, alimshika mkono kisha wakaondoka
"Pindi CEO wa Star ships atakapouliza kuhusu huyu binti mwambie kaondoka na Mwanaume mwingine.... Mama yako ni msafirishaji mzuri wa madawa ya kulevya, endapo utazungumza tofauti na maagizo yangu itanilazimu nianze kufatilia hatua zake" Sona alimchimba mkwara Dada wa mapokezi kisha akasepa na Dada yake
Wakiwa ndani ya gari, alimfunga Dada yake kitambaa cheusi machoni
"Kwanini unanitendea hivi kama mateka" Sultana aliuliza
"Sitaki ufahamu sehemu ninayoishi....ni hivyo tu" Sona aliongea
Sultana aliachia tabasamu, dimpozi zilizokuwa mashavuni kwake zilimfanya aonekane mrembo ingawa macho yake yalikuwa yamefungwa.....Sona alijikuta akiumia ni kama alikuwa anamuonea wivu Dada yake kwa muonekano aliojariwa, aliendesha gari kwa kasi kana kwamba ana fukuzana na majambazi
Nyumba yake ilikuwa nzuri kuliko kawaida..... Sultana alifurahia mafanikio ya mdogo wake baada ya kutolewa kitambaa
"Nisamehe lakini nitakufunga mikono na miguu ili usije kutoroka...." Sona aliongea, safari hii alimzimisha Dada yake kwa kumpulizia madawa ya usingizi.
Alimfunga mikono na miguu, baada ya kumaliza alielekea sehemu aliyoamini ataweza kuwa kamata Wauaji.
Upande wa Liam, anarejea Burj Al hotel akiwa kabeba zawadi kwa ajili ya Sultana. Anashtuka ndani ya moyo wake baada ya kukuta chumba kimepangwa vizuri kana kwamba hakukuwa na mtu.
Alirudi mapokezi kujua ni kitu gani kinaendelea
"Ooh, baada ya wewe tu kuondoka kuna Mwanaume mwenye asili ya kiarabu alikuja kumchukua....nadhani ni mpenzi wake" Dada wa mapokezi aliongea
Moyo wa Liam ulivunjika kwa namna fulani, hakuona hata maana ya kuondoka na zawadi alizokuwa kamletea Sultana, alimuachia Dada wa mapokezi
๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป
Kulivyo pambazuka asubuhi, Sona anarejea nyumbani akiwa na jeraha mkononi mwake.
Alimfungulia Dada yake mikono na miguu....
"Kabla sijaelekea kazini nitakupeleka Kijijini Odes...." Sona aliongea
Sultana alinyoosha mkono wake taratibu akalishika jeraha lililokuwa mkononi kwa mdogo wake
"Hii si kitu, huna haja ya kupata presha" Sona aliongea, hakujali kama Dada yake ana njaa au la...alichotaka yeye ni kumtoa Jijini Odes
Wakiwa ndani ya gari aliijiwa na wazo jipya
"Kama nitamrudisha Kijijini Odes nina uhakika atarudi kunitafuta....haonekani kukata tamaa kuhusu Mimi" Sona alijisemea kisha akabadilisha uelekeo wa gari
Alihitaji kuiwahi Meli iliyokuwa inaelekea China....
Hakutaka kusikia nasaha za Dada yake hivyo alimzimisha kwa kuipiga shingo yake kwa nguvu
"Kama atapatikana hana uraia au kibali maalumu cha kuishi Nchini humo hukumu yake itakuwa ni kifo....kuliko umpeleke huko ni heri umtupe baharini afe" Polisi mmoja aliyekuwa anaelekea China aliongea
"Siwezi kumuua.... nina uhakika uzuri wake utamuokoa pindi atakapokuwa China hastahili kukaa Jijini Odes wala Kijijini kwetu.... safari njema" Sona aliongea kisha akaondoka...ndani ya moyo wake hakuonesha kuumia.
Aliwahi kazini haraka kukabiliana na Waharifu aliowakamata.
Sultana anarejesha fahamu akiwa kwenye mabehewa ya mizigo.....kabla hata hajafikiria vizuri alisikia kelele za watu wakiomba msaada
"Usijiokoe pekee yako.... hakikisha unasaidia watu wawili na zaidi huo ndio Uzalendo wa watu wa Jijini Odes.... Meli inazama" Sauti ilisikika kupitia kipaza sauti
Sultana alichanganyikiwa..... alianza kufunua huku na kule akimtafuta Sona, hakuwa tayari kujiokoa pekee yake kama tangazo lililivyo sikika
Ghafla mlango wa mabehewa ya mizigo ulivunjwa.
Sultana alibakia kukodoa macho
Itaendelea ๐ฅ.