Usiku ulikuwa umetanda, kimya kilitawala kama vile dunia yote imelala. Saa ilikuwa saa nne kasorobo usiku, lakini mke wangu hakuwa amerudi kazini. Alisema ana kazi ya dharura hospitalini, lakini kila dakika iliyopita, moyo wangu ulizidi kuchafuka.
Nilipokuwa nimeshika glasi ya maji nikielekea sebuleni, mlango wa chumba cha wageni ukafunguka. Mdogo wa dada yangu, Sabrina, alitoka akiwa na kitenge kilichombana mwilini, kifua kikiwa wazi kidogo na miguu yake myeupe ikiangaza kwenye mwanga hafifu wa taa ya ukutani.
“Unalala?” aliuliza kwa sauti ya chini, macho yake yakiwa yamenitazama moja kwa moja, kama mtu anayetafuta kitu zaidi ya jibu.
“Siwezi kulala mke wangu bado hajarudi,” nilijibu kwa haraka, nikigeuza macho kuepuka ule mtazamo wake wa hatari.
Alikaribia. “Una hakika unajisikia salama kuwa peke yako?” aliuliza kwa sauti ya kunong’ona, mikono yake ikishika bega langu.
Nilihisi joto mwilini. Harufu ya mafuta ya nazi na sabuni ya ‘Dove’ ilitanda puani mwangu. Alikuwa karibu mno.
“Ninajua uko kwenye ndoa… lakini,” alinyamaza kwa sekunde, “mbona unajitesa bure? Mke wako hataki hata kukupa muda wake. Wanaume kama wewe mnahitaji kitu kingine... usiku kama huu.”
Moyo wangu ulidunda. Nilimsogelea kisha nikamwambia kwa sauti ya kutetemeka, “Sabrina… usifanye hivi. Mimi ni mme wa mtu.”
Lakini kabla sijamaliza, alishika mkono wangu na kuuweka kwenye kiuno chake. “Sema tu ‘hapana’ kama hutaki,” alisema kwa sauti ya mtego, akiinama kidogo na kuniangalia kwa jicho lililolegea.
Kimya. Nikabaki natetemeka. Mlango wa mbele ukagonga.
Niliruka kama mtu aliyeamshwa kutoka usingizini.
Sabrina akaniangalia, akatabasamu. “Una bahati leo... lakini usiku bado ni mrefu.”
Aliingia tena chumbani kwake kwa mwendo wa majaribu. Nilibaki nimesimama kama sanamu, nikihisi vita ya tamaa, uaminifu, na hatari ikichafua akili yangu..