Baada ya kushtuka usingizi 😳Nilimkuta yule mkaka amelala shuka ipo pembeni amebaki na ile nguo ya ndani pekee na inavombana wee mbele pametuna na alivobarikiwa mmm😍💕nikabaki nimegandiza macho yangu hapo...
Basi wakati namwangalia nae akashtuka nikajidai kuvunga napepesa macho huku na kule ila mmmm kijana kabarikiwa huyuuuu
"Mbona hujaondoka??" Nikamuuliza huku nainuka kitandani mi nilikuwa na dera langu
"Aah hata sijui nimelala vipi"
"Chukua nguo zako uende" nikamtupia nguo zake
"Khaaa!!! Nitoke watu wananiona hapo unataka nifeeeeee😢😢😢??"
"Lakini mwizi anatakiwa kuu awa eeh"
"Mi sio mwizi sister nakuapia ujue"
"Kwahiyo watu siku hizi wamechanganyikiwa wanakimbiza tu watu hovyo na kuwaita wezi , haya kwanini usisimame nawe unakimbia kabisa kama sio mwizi??"
"Nakuapia dada angu mi sio mwizi nimekupa kitambulisho changu hichi huniamini tu???"
"Sikukwambia sijui kusoma au"
"Embu acha utani ba....."
Aliacha kuongea baada ya mlango wangu kubishwa hodi
"Nanii.." nikauliza huku nasogea mlangoni
"Bwana Zakia embu fungua" mmmh nilisita kidogo afu nikamtazama yule kaka yaan ni muoga jamani khaa,
"Nakuja nisubiri huko" niliona nisije kumkosesha amani huyu kaka nikamwambia zakia anisubiri huko nje nikatoka ,huyu ni shost angu tu wa hapa mtaani mara nyingi j2 kama hivi siendi kibaruani huwa anakuja tunashinda wote
"Shog jana ulivusha niniii??" zakia aliniambia wakati nipo nawasha moto ili nitenge chai hapo tupo nje unajua nyumba za kupanga uswahilini watu wamejazana nje asubuhi tu
"We umeyasikia wapi watu wambeaa"
"Mwenzangu, mama Jack alinipigia simu,,, sasa ndo utoke hapa ukamwambie nimekwambia sitaki mabalaa kabisa sitaki "
"Bwana weee unanificha hadi mimi best yako?"
Nikamsikiliza zakia hapo akajimaliza dada mbea huyu et ananiuliza kwahiyo shemu bado yupo fanya ututambulishe shogaaa, nikamwambia bwana zakia embu nenda mi nina kazi zangu..
Nikaweka chai yangu baada ya kumfukuza zakia nikaingia ndani nikachukua pesa nikafata chapati jirani tu hata sio mbali, nilipo rudi tukanywa chai wote kimyaa hakuna hata anaemsemesha mwenzie ..
Baada ya chai nikaenda zangu kujimwagia maji nikamwambia mgeni mi naenda zangu kusuka hapo karibu sio mbali akasema sawa mi nitakaa humu ndani ,
nikamwambia kaka angu ole wako uniibie yaan mie nitakutafuta hata ukiwa nje ya dar nitakupata ole wakooo , akabaki anacheka kweli yaan nilimpiga mkwala utafikiri naweza mpata akiniibia
ila nilikuwa najihami tu ukweli sikuwa namuamini hata kidogo ila kumfukuza tena najikuta siwezi kabisa ,nikiwaza kumfukuza nafs inasema mbona haonekani kama mwizi kaka wa watu .
Nikaenda zangu kusuka mtaa wa nyuma tu na pale napoishi , wakati nimefika nilikuta yule mama msukaji kuna mtu anamsuka nikakaa pembeni kusubiri foleni yangu ,nikakuta mada inayoongelewa ni kuhusu mwizi wa jana sijui walianzia wapi mi nilikuta kati kati tu
"Yaan yule kaka jana anamungu wake hakiamungu alikuwa anakufaa yaan" yule mama msusi aliongea huku anachukua chanuo akate mstari
"We mama bela unajua nimeskia yule kijana hakuwa mwizi😳😳 yani angeweza kuu awa hivi hivi aisee"
Mmh nikatega sikio vizuri kusikiliza lakini kwenye maongezi yao yote sikuona ninalo taka kulisikia ikabidi tu nichangie mada
"Sasa kwanini walitaka kummaliza kama hakuwa mwizi"
"Hee we Salma we wa wapiii, hujapata tu habari "
"Nazipatia wapi mie shg anguu"
"Huyo kijana ni Bwana ake Queen wa mtaa sasa naskia anakujaga humo ndani kila siku wanafanya yao ila jana ndo amekutwa na Sponsor wa Queen ndo kaitiwa mwizi😂😂"
"Sponsor mwenyewe mnamjua.? ni yule mzee Amos yeye ndo sponsa wa Queen yani hii dunia ina siriii"
kheee Nikapata ubuyu mpyaa kwanza nikajitengeneza vizuri mana huyo dada wanaemwita Queen wa mtaa ni bint mmoja hivi anaitwa Judy sa huyo judy ni mdada flan hivi matawi hatari
yaan ananata sio poa hata sio mzuri ni vile tu anavihela na amejipata anavaa nguo za bei bei yaan hivyo umaridadi ndio unao mbeba ..
Huyo dada anamiliki pay point huko maeneo ya posta , amepanga nyumba nzuri yenye hadhi hapo mtaani ila ni mdada ambae anasifa ya kubadili wanaume wenye vihela hela sa hapa ndo nashangaa kumbe anatembea na huyo mbaba ambae ni Amos .
Huyu baba anafamilia yake kabisaaa afu anauwezo yaan hela za kubadili mboga zipo afu ni jirani na juddy, Nyie wanaume hawa mmh nilibaki nimeduwaa huyu baba anawatoto wakubwa kabisa tena wanakazi zao haogopi kutembea na kitoto cha 2000
Mke wake ni mwanamama anaepambana yaan anakazi yake nzuri ni mtu mzma lakini anakwenda na wakati sasa anaenda kutembea na juddy ni kama bint yake afu jirani hee makubwa nilishika mdomo
"Sa mke wake jamani hajajua ,nyie huyu babaaa!!!!" Niliendelea kustaajabu ya mtaa
"Eeh we mwanamke anadharau yulee , hata hajaonekana nje."
"Sasaaa ilikuwaje" nikataka kujua story nzima si unajua wambea tena nami nataka nipate umbea mana hii story kwa asilimia mia inanihusu mie , moja ya sababu kubwa huyu kaka yupo getoni kwangu .
"Yaan huyo kaka ambae ni mwizi sasa, navyosikia ndo anamuweka mjini Shostiii , na anakujaga hapo sema ndo hivo bishost anawachanganya wote wawili ila ndo hivo jana wamekutana wote ndo sponsa akaamua kumuitia kijana watu kwa madai et ni mwizi"
"Heheheh kwahiyo anatunzwa na wotee"
"Na sio hao tu ,mtoto anaitembeza huyooo hee hatari, inachapwa kila siku we fanya mchezo nini ,hehehehe !!!"
"Yaan tunacheka kama mazuri enhee ndo ikawaje??"
"Basi bwanaa , kumbe huyu Amos anawinda kila siku kumjua mwanaume anaekula mali yake ,naskia huyo baba amepagawa na naniliu ya juddy hasikii haambiwi yaan hata mke wake navyosikia anajua na wanamagomvi kwa sababu ya Juddy ila mzee amos hasikii lolote..
"Sasaaa ndo jana huyo bwana akajitosa kwa mpnz wake ,kumbe amos yupo mawindoni bwana , hajawavamia ndani, baada ya kuingia ndani ndo wakapigana mikwala hapo ,
juddy akasema ye hamtaki mzee amos shost anataka dogo dogo yake inayomfikisha mlima kilimanjaro hahahaaa mnaelewa bwana mambo ya kileleni,heheheh!!!!
Mzee ndo kupanic hapo kuanzisha ugomvi hataki kukataliwa! akamtoa nje huyo kaka akamwambia aondoke la sivyo atamfanya vibaya huu mtaa ni wake anaujua vizuri,
Handsome boy nae akajifanya nunda tena anasema ye haondoki si ndo akaitiwa mwiziii hahaha unajua kutimua mbio ,jamani kwenye kuf kuna mbio ha ha ha"
"Ha ha ha we ufe kisa kitumbua haaah hata mimi naosha "
"Mpaka akaacha na gari fa mchezo nini , nasikia gari mzee amos amevunja vunja viooo hatar sa we jiulize mwizi anakuja kuiba na gari tena ni gari haswa sio la bei ndogo"
"Wamemfanyia vibaya kaka wa watu jamani"
"Ndo hivyoo, akirudiana tena na Juddy aah nitaamini juddy naniliu yake ina asali itabidi nimtafute kwakwel he he he!!!"
Story zikanoga hapo hata nikawa najiuliza wenyewe wamejuaje jamani ila sikuuliza mladi nishapewa umbea tena Full duh ,
moyoni nikasema halali Juddy amchague huyu kaka mana ni Gentlemen wa maana anamwili mzuri na tumidomo afu anaonekana yupo vizur hahah hata sijui nawaza nini .
Nikamaliza zangu kusuka nikarudi nyumbani ,nikamkuta yule bwana amelala, hata sikumwamsha nilipitia gengeni nikapika zangu ugali, baada ya kumaliza ndo nikamsemesha ili tule zetu
"Kumbe umerudi??"
"Mda sanaa, umelala tu unaweza kuibiwa we ugenini unalala hivyo"
"Ha ha ha , huogopi tena wewe kuibiwa namie"
"Aah yamepita hayo bwana" nikajibalaguza si nishasikia story yake hapo yamenishuka kweli , ila nilikuwa namtazama ni mkaka mzuri kweli namuwaza na Juddy mmmh nasema kuna watu wanabahati kwelii
"Mbona unanitazama kwa wasi wasi " nae akanishtukia akawa ananiuliza sasa..
"Nanii, mimiii??? Sa kwanini nikutazame??"
"Ha ha ha nakutania bwana, Ila Asante sana kwa Fadhira zako umenisaidia hata hunijui umeruhusu nilale ndani mwako bila shaka, sitasahau wema wako dada angu ubarikiwe sanaa"
Moyoni nikasema ungejua usiku nilishindwa hata kulala ungetulia tu aisee..
"Kwani umeshiba?? Au ugali umekushinda" Mi hata sikumjibu baraka zake nikamuuliza mana nilimuona kasi ya kula imepungua..
"Ugali mtamu sana huu naeza sema sijawahi kula kama huu hauwezi kunishida"
"Okay"
"Naitwa Alex"
"Una jina zuri ila unamambo ya ajabuu!!"Nilimjibu huku nachukua vyombo vyangu kutoa nje baada ya kumaliza kula
nikamuacha anacheka afu kingine nilichogundua huyu mkaka ni mkaka poa sana yaan yupo Charming any time anacheka tu , afu akicheka anapendezaa anavimeno vyeupeee na dimpo moja hahah mi mbeaaa
sijui ndo nishaanza kumpnda mkaka wa watu hata sielewi na hapo sitamani hata aondoke sijui itakuwaje..
KWETU morogoro.