Nilikuwa zangu kituo cha daladala nasubiria usafiri..
mbele yangu alikuwepo jamaa mmoja ni kama kuna mtu alikuwa akimsubiri pale kituoni..
Basi katika hali isiyo ya kawaida alikuja mwanaume mmoja nahisi ni konda
Alikuwa na kopo la maji ya kunywa mkononi alipokaribia sehemu aliposimama huyo mkaka
konda alimtupia kopo mgongoni kisha akawahi kwenye gari na kuondoka
Yule kaka baada ya kupondwa na kopo aligeuka akiwa amekunja sura aliniangalia kwa hasira zisizo za kawaida
Niliogopa nikamwambia siyo mimi wakati namnyoshea mkono kumwambia kuwa ni konda ndo alompiga na kopo
Yule kaka aliushika mkono akanivuta pembeni kidogo ambapo hakuna watu wengi..
Akaanza kunitukana na kunigombeza kwa sauti ya juu iliyojaa ukali usioelezeka.. ujinga gani huu umefanya??
Samahani siyo mimi..
Ni wewe😡😡
No siyo mimi ni konda
Hivi unathubutu kuongea uongo mbele yangu?? Unaji uza siyo??
Kwa taarifa yako mimi sinunuagi ma.... na...tafadhali hebu acha upu mbavu nani mal..y??
Nikutake wewe kwa kipi?? Nakwambia siyo mimi nilokuponda na kopo unanilazimisha hivi unajikuta nani??
Oh unataka kujua mimi ni nani sasa subiri nitakuonyesha mimi ni nani..
Usinitishe bwana hebu peleka ujinga wako huko yani wanaume weupe mna tabia za ki ke mnafikiri kila mwanamke anawataka mxiiuu
Kauli yangu ilizidi kumpandisha hasira alitaka kuninasa kibao nikainama kibao kikanikosa
Yule mkaka alitoa simu mfukoni kwa hasira akapiga police wakati nashangaa shangaa mara nikashangaa difenda hilo
Ile nataka kukimbia nikazingirwa🥺🥺ile nataka kujielezea nikawekwa chini ya ulinzi mungu wangu
Hivi huyu kaka ana akili kweli??
Sasa unaniitia police mimi nimekufanyia nini??
Msikilizeni alivo na mdomo mchafu hakikisheni mnamshikisha adabu..
Alitoa kauli hiyo na kisha akaondoka nilipigwa pingu nikapakiwa kwenye difenda msobemsobe mpaka kituo cha police..
Niliwekwa lokapu hakuna cha maelezo wala nini yani police ni wanamtii yule kaka kupita maelezo nililala kituoni siku tatu bila kuruhusiwa kutoa taarifa nyumbani..
Siku ya nne alikuja Yule jamaa nilivomuona tu nikaanza kusonya na kubinua midomo
Mbwa zingine sijui huwa zinajikuta nani kuna mbwa nazichukia mimi eh Mungu nifundishe kunyamaza maana bila kuninyamazisha naweza nikajikuta naozea lumande
Niliongea hivo jamaa akanisikia alitaka kuninasa kibao akaishia kupiga kwenye nondo nilianza kucheka na kumwambia umepata kiboko yako..
Alizidi kupandwa na hasira police mmoja aliekuwa karibu alimtuliza kisha akanifokea na kunitaka nifunge domo langu..
Yule mkaka alimwambia police hakikisha huyu mshnzi hatolewi hapa mpaka awe na adabu..
Aliongea hivo kisha akaanza kuondoka..
Police alimzuia kwa kumuita mkuu lakini sasa huyu binti mpaka sasa hivi hajafunguliwa kesi yoyote
Huenda familia yake inamtafuta..Yule mkaka aliwaza kisha akaamuru nifunguliwe kesi..
Ni kesi ya nini??
Itaendeleaaaaaa
Full 1000
WhatsApp 0699286085.