Basi bwana baada ya kuondoa vyombo nikatoka zangu nje nikawa nimemuacha huyo mkaka ndani ametulia tu ,nikasuuza vyombo ,majirani bwana yaan wao akili yao inasema nimevusha bwana aah watajua wenyewe bwana weee ,
"Nilisuuza vyombo nikamaliza nikarudi ndani.. akanifuata huyo mkaka akaniambia naomba niazime simu tafadhali"
"Umemkumbuka mpnz wako???" Nikamuuliza maksudi labda anataka kujua habari za Juddy afu huyo dada mie hata simuelewi yaan ananata mpaka anaboa"
"Hapanaaa nataka kujua simu yangu ilipo ,sijui hata ilianguka wapii"
nikachukua simu yangu nikampa
Akapiga namba zake simu iliita alikuwa ameweka sauti nikasikia halooo sauti ya kike akatoa haraka sauti afu akaweka sikioni😣
"Simu yangu ni muhimu sana naipataje..... nisikilize nahitaji simu yangu tu ndo kitu cha muhimu ..
Embu nielewe basi ....okay endelea na mishe zako nikiwa sawa nitakutafuta namtuma Inno ataijia Vitu vyangu vyote mpatie tafadhali ili tulimalize hili..."
Alikuwa anaongea kwa jazba wee ,mi kimyaa moyoni nasema atakuwa tu Juddy huyoo ,,baada ya kukata simu akapiga namba ingine tena ilikuwa sauti ya mwanaume
"Alex......aah we acha tu....nipo mtaani hapa hapaa....usiwe na shaka inno I'm safe now... nakutumia text ya maelezo kukiwa na shida yeyote piga namba hii naomba nisaidie mshkaji wangu ....poa poa" alikata simu akanitazama kisha akaandika sms .
"Asante!!" Akanipa simu yangu nikamwambia tu sawa nikaichukua hata dakika mbili bado ,iliita nikampatia hakupokea aliikata afu akablock kabisa ile namba akaifuta akanipa simu akasema Samahani nakusumbua nikasema usijali bwana sipendi samahani za muda wote Samahani ndo Samahani huwa sipendi sanaaa ,,
akacheka akanambia afu hujanambia hata jina lako,nikamuuliza we jina langu la nini akasema nambie bwana sio vizuri nikamwambia salma naitwa Salma Omar
akasema jamani napenda mnoo jina la salma ndo mana we mpole sana unajua wenye haya majina hata hawana mambo mengi mi nikawa nacheka zangu tu .
Simu yangu tena iliita namba ngeni nikamwambia simu hii ,sijui ni namba yako akasema tuone nikampatia , akaipokea
"Ndio inno.... ndo hivyo ...achana nae mpuzi tu huyo embu chukua vitu vyangu chukua simu yangu kuna mtu namtuma anaijia msubiri kule kituoni atakuja na boda ....
aisee sina kitu wallet yangu ilianguka sijui wapii ,nipatie pesa pia ...okay poa poa ..." alikata simu akanambia
"Samahani naomba unisaidie kitu!!"
"Sipendi Samahani za muda wote"
"Ha ha ha Sorry , basi nakutuma"
"Haya niagize ila usije sababisha mie nikapigwa wizi bure"
"Hahaha kuwa na amani nitakulinda"
"Wapiii we mwenyewe ulishindwa kujilinda ,mi utaniweza"
"Ha ha ha aiseee sitaki hata kukumbuka jamani"
Akanipa maelezo kuwa niende kukutana na mtu yupo barabarani kabisa yaan kituo cha dara dara akanambia Chukua boda nikasema Fresh .
Nilikutana na huyo kaka , bwana weee ni msupa sio poaaa, yaan kaka wa viwangooo mmmhh
Akanambia naitwa inno huku ananipa mkono aisee ni mzuri hatari afu ana gari kaliii uuuwww
"Nashkuru kwa kumsaidia ndugu yangu"
"Usijali kawaida"
Yaan huyu kaka aisee wanafanana na Alex basi ndo hivo inno baada ya kunishukuru.."
Akawa amenipa simu ,na pesa yaan pesa nyingi kibunda cha misimbazi miekundu tuuu , akanambia nitakulipa siku moja kwa wema wako nikacheka nikapanda zangu Boda nikarudi nyumbani
Ile nashuka pale nje kwenye boda , nasikia naitwa kwa nyuma hee nageuka namkuta juddy na liniii huyu dada akaniita mie??
Huwa tunapishana tu kila mtu na lake sijawahi kuongea nae huyu .
Moyo ulinienda mbio naogopaaa hatari ,alikuwa juu ya piki piki akanambia njoo yaan anaongea kwa nyodo kweli afu anadharau , nikasogea bila shida uso nimeukaza ila moyoni nawasi wasi hatari
"Mambo!!" Akanisalimia yaan kwa kuninyali mh mpaka nikatabasam , moyoni najiuliza au amejua kuwa Bwana ake yupo ndani mwangu ,na lini
"Poa vipi??" Mi nikamjibu huku namtazama kwa mshangao
"Una uhusiano gani na Inno??" Moyo paaah nikasema imekuwaje amtaje inno ameniona nipo nae auu
"Inno gani" nikajifanya nauliza ili nipate muda wa kufikiria zaidi kwamba namjuaje inno , uzuri inno mi tuliongea ndani ya gari yake na hata vitu alinikabidhi humo nikatia kwenye pochi yangu ndo nikaondoka zangu ,
"Kwani we unawajua kina inno wangap"
"Mh we bwana embu mi nakazi zangu" nikageuka zangu kuondoka akanivuta mkono kwa nguvu hata nikaumia nikasema hii ni Serious??
"We kwani unashida gani?? Sitakiwi kuongea na watu au??" Nilimjibu sasa nishapanic na nilikuwa nimepanic kweli kwelii
"Ndi....." sijui hata alikuwa anataka kusema nini lakini nikaona kasita baada ya mie kutazama alipo kuwa anatizama niliona gari ya yule Amos imesimama afu ameshusha vioo anatutizama, Juddy alikuwa kama anawasi wasi mi nikaondoka zangu nikawaacha hata sikutaka kuwafatilia
"Yaan mkojo umenibana salmaaa!!!" Naingia tu ndani namkuta alex anazunguka chumba huku ananesa nesa mkojo umembana😂😂😂
"Nenda tu chooni , hapo nje yupo yule baba uliemuibia sijui ulimuibia niniii mana anaonesha anahamu na wewe balaaa" nikamjibu huku natoa simu yake na pesa kumkabidhi
"Serious nataka kukojoa ujue"
"Njoo ukojoe mdomoni kwangu "
"Haya njoo hapa fanya Aaaahhh"
Alisogea huku anafungua zipu ya suruali ,nikaona huyu kweli dishi anaweza toa kikojoleo chake hapa hapa
"We bwana embu acha ujinga hukoo" Nikamsukuma pembeni huku nacheka , nikachukua ndoo ya kuogea nikaitia maji nikampa
"Ukimaliza uioshe mi naogea hapo" nikatoka nje ili akojoe kwa amani, niliangalia sikumuona Juddy wala yule mzee Amos mmh nikasikitika tu huyu mzee sijui mke wake sa hii anapitia wakati gani jamani hawa wanaume vichomi mpaka wazee basi Tu ...
Usiku Alex ndo akanipa et hela ya kupika jamani nikajikatalisha mwisho nikakubali nikapika masotojo ya ukweli hahahaa
tukala zetu akasema ataondoka usiku wa leo nikamwabia poa karibu sana , akanambia yaan salma sintakuja kukusahau aisee hata sijui nikuambie neno gani tu ujue How i feel ,
nikamwambi hata usijali mwaya nilichofanya mimi angefanya mtu yeyote tu yule kama ungekutana nae ..
Tulipiga story kibao na alex huo Usiku nilijikuta yaan nimemzoe gafla tu kutokana na Kuongea kwake yaan anaongea sana anafurahisha haboi wala nini kaka watu ,
ilifika mida ya saba hivi usiku watu washalala mtaa upo kimyaa akanambia mi naondoka sasa nahisi sasa hivi ni salama dah nyieee😩mwambieni asiondoke basi..
Itaendeleaaaaaa
Full 1000
WhatsApp 0742133100.