JINA ............BAKORA VILLAGE
ART.................KELVIN MLOWE
WHAT..............0699286085
UTANGULIZI
Katika Upande wa magharibi mwa nchi ya Tanzania , palikuwapo kabila moja la kipekee, lililotambulika kama "Wasenezi" jamii ya kipekee yenye asili ya siri, tamaa na mila za maajabu.
Kabila hili halikuandikwa kwenye vitabu vya historia. Hakuna ramani ya Google inayoweza kukuonyesha mahali walipo. kabila hilo lilipatikana katika kijiji kiitwacho Koneso, ambacho wenyeji wa karibu walikiita Bakora Village jina lililotokana na desturi ya kupenda sana yale mambo yetu kuliko hata kula.
Hawakujali sheria za kawaida. Mapenzi kwao hayakuwa jambo la faragha bali ni ibada, ni heshima, ni sadaka kwa miungu yao.lakini kikubwa zaidi ni starehe ...
Na zaidi ya yote, kijiji hicho kilikuwa na siri moja kubwa wanaume walikuwa adimu, na wanawake walizidi kwa idadi mara 5 zaidi.
Hali hiyo ilisababisha njaa ya mapenzi, kiu ya mahaba, na tamaa ya kutisha ya kila mwanamke kutaka mwanaume wake peke yake hata kama nikuiba mume wa mtu wlikuwa tayari ilimradi tu kila mtu akidhi haja zake .
Wanaume walikuwa wachache sana kiasi kwanza hata orodha ya tano haitoshi . Ndio maana mambo mengi yaliweza kutokea huko ikiwa ni kulogana ,kuchepuka na hasa hasa migogoro na chuki baina ya wanawake .
Wengi waliwahi kukitembelea kijiji hicho hawakurudi tena. Wengine walirudi, lakini akili zao zilibaki huko. Wakawa watu wa ajabu, yaani hata huku uswahili wakawa wanazile tabia za kule koneso au BAKORA VILLAGE .
Lakini hii hadithi inamhusu kijana mmoja kwa jina la lucas ambaye ni mmoja ya watu waliweza kwenda kwenye hicho kijji cha koneso kwa bahati mbaya yaliyomkuta tutayajua ......
SEHEMU YA KWANZA:
Lucas ikuwa kijana wa kawaida tu kutoka Arusha ni msukuma mmoja makini sana ambaye mitishamba kwake ni kama bakuri la vitumbua kwa mwanafunzi lakini kipaji chake kikubwa niku piga picha huru, mtafutaji wa matukio ya kipekee kwa ajili ya blogu yake ya utalii wa ndani iliyoitwa "Tembea Mpaka Upotee."
Luca hakuwa na nia ya kupotea.
Alikuwa anatafuta maporomoko ya maji yaliyosahaulika karibu na kijiji kiitwacho Mbwele, lakini hakuwa anajua kuwa hatma yake ilikuwa mbali zaidi ya maji, mbali zaidi ya mipaka ya kawaida.
Hadithi inaaanza Luca, akiwa na kamera yake ya bei ghali shingoni na begi la mgongoni lililosheheni powerbank, chupa ya maji na kitabu cha “Survival Tips in the Wild,” alikuwa na hamasa ya kupiga picha poromoko ya Lugwila Falls maporomoko ambayo hata Google haikuweza kuyaweka vizuri kwenye ramani.
Lakini safari haikuwahi kuwa rahisi kwa wapenda maajabu.
Alianza kutembea akifuata ramani ya kidigitali. Ilimwonyesha njia kupitia mti mkubwa wa miombo, kisha bonde dogo, kisha kuchukua mkato kushoto kuelekea mtoni. Ilikuwa saa nane mchana.
Lakini mara…
Ramani iliganda.
Alifuta jasho, akacheka kicheko cha kutojali. “Ah, signal tu hii.”
Akasubiri sekunde 30.
Dakika moja.
Akiangalia ramani bado haifanyi kazi, lakini moyo wake ukawa bado na matumaini.
“Naweza kujua tu mashariki ni kule,” alijisemea.
Akaendelea mbele, akanyaga jani moja lililoanguka, halafu lingine, hadi akajikuta anapita njia ambayo hakuipanga.
Mara akaanza kusikia ngoma zikipigwa na watu wakiimba lakini kila alivyopiga hatua kwenda mbele aligundua watu wanaoimba ni wanawake . Kuhusu lugha ndo kabisa yeye haelewi ila aliamini wangemwonyesha.
Kama akipata nafasi ya kuongea nao...
Lakini ghafla akasita akasema " mmmmh naenda huko pengine ni wauaji? Hakuna alama zozote zinazoonyesha huko kuna kijiji chochote.hawa ni wakina nani?
Alipojaribu kurudi nyuma alikuta miti aliyoipita awali haipo tena vile alivyokumbuka.
Ilikuwa kama misitu imebadilika.
Kila hatua aliyopiga iliongeza ukimya mzito, na kwa mbali akaanza kuona k mlango mkubwa, wa kipekee, wenye maandishi haya
" BAKORA VILLAGE"
Akasogea.
Kila hatua ilikuwa ngumu.
Miguu yake ilianza kuwa mizito, kana kwamba ardhi ilikuwa inamvuta chini.
“Karibu Koneso…”
Sauti hiyo ilisikika ndani ya kichwa chake, si kwa masikio.
Alipofika mbele ya lango, hakukuta mlinzi, hakukuta mtu yeyote – lakini alihisi wazi kuwa alikuwa anaangaliwa.
Alipiga hatua kwenda mbele , japo alikuwa anaogopa lakini alijipa moyp huenda mambo yataenda sawa huenda kuna watu wema yaani anaenda ila hajuwi ndani kuna nani? Roho zao zikoje ? Ni kama kujitoa sadaka ....
Mara ghafla akakutana na m
Mrembo.
Mwembamba.
Macho yake mazuri sana na kamdomo kamekaa vizuri unaweza kusema ana sinzia ila wapi mtoto kama malaika ana nyele ndefu na kavalia mavazi ya kiasili yaliyocha baadhi ya sehemu za mwili nje .....
Yule mwanamke alitabadamu na kusema "Hujapotea. Umechaguliwa." Kisha akamkonyeza .....na kumshika mkono.