Mwandishi: Kelvin Mlowe
Nilielekea taratibu kwenye mlango wa mbele, moyo ukipiga kama ngoma ya vita. Mikono yangu ilitetemeka niliposhika kitasa cha mlango. Niliufungua polepole... na pale mlangoni alisimama Askari wa doria.
“Ndugu usiku mwema,” alisema kwa sauti ya ukakamavu. “Tunaendesha doria za kawaida. Tumepita tu kuhakikisha kila kitu kiko salama.”
Nilipumua kwa nguvu, nikijaribu kuficha hofu na msisimko uliojaa mwilini.
“Shukrani sana afande. Kila kitu kiko sawa,” nilijibu.
Alinitazama sekunde kadhaa, kisha akasema, “Tukirudi tena usiku wa manane, tutapita hapa tena.” Aligeuka na kuondoka.
Nilifunga mlango kwa haraka. Niliegemea mlango huo, nikavuta pumzi ndefu. Mara nikasikia mlango wa chumba cha wageni ukifunguliwa tena. Niligeuka ghafla.
Sabrina alikuwa amevaa nguo fupi ya kulalia, nyeupe, nusu ya mapa... yake yalionekana wazi. Macho yake yalikuwa ya hatari zaidi ya mtego wa chatu. Alinitazama bila haya.
“Nilifikiri ni mkeo,” alisema kwa sauti ya kukwaruza.
“Sabrina… acha mchezo huu,” nilisema, nikisogea mbali. “Unaelewa kabisa hi ni nyumba ya dada yako. Si sawa hata kidogo.”
Alinisogelea tena, akishika mkono wangu na kuusogeza kwenye kifua chake. “Unajua kitu gani? Wanawake hawajali sana kama mwanaume anatosheka au la. Wanajali kazi, hela, vikao, marafiki zao. Lakini mimi… naweza kukutunza hata kwa saa moja tu, ukasahau kila huzuni.”
Niliachilia mkono wake kwa nguvu, nikarudi nyuma hatua tatu. “Sabrina, nisikilize vizuri. Najua hujaamka tu na wazo hili bila sababu. Labda kuna kitu kinakuumiza, au unahitaji mtu wa kukusikiliza. Lakini siwezi kuwa huyo mtu kwa njia unayotaka.”
Akatabasamu. Lakini ulikuwa ni tabasamu lenye uchungu. “Sawa,” alisema polepole. “Lakini kumbuka... si kila mwanaume ana bahati ya kupewa ofa kama hii bila kuomba.”
Akaingia chumbani na kuufunga mlango kwa fujo kiasi.
Nilikaa kwenye sofa, kichwa kikiwa cha moto. Simu yangu ililia. Ilikuwa ni mke wangu.
“Hello... samahani mpenzi wangu,” sauti yake ilisikika ikitetemeka. “Leo tumekuwa na ajali ndogo na gari ya hospitali. Nipo salama lakini nimetoka kwenye shock kidogo. Nakuja sasa hivi, tuko njiani.”
Macho yangu yalijaa machozi. Kosa dogo lingeweza kugharimu kila kitu. Kama ningeshindwa kujizuia...
Lakini swali ni, Sabrina atakaa kimya? Au mchezo huu ndio unaanza?
Je, uendelee SEHEMU YA TATU?.