FINAL DESTINATION BLOODLINES....
Mbona kama professor wa kitaa nimeshikwa na filamu hiii ... Mbona nimeiona ni filamu yenye story ya kuvutia kuliko hata zile za nyuma???
Oya mzigo huu unaitwa FINAL DESTINATION BLOODLINES,.... Filamu inamuhusu Bibie Stefani ambaye kila muda alikuwa akiota njozi ya Bibi yake Iris ambaye hakuwahi hata kumuona...
Njozi hiyo ilikuwa ni Stefani anaota Bibi yake na Babu yake wakifa kwenye mnara pamoja na watu wengi waliokuwepo hapo ... Stefani aliota ndoto hiyo kwa miezi miwili hadi kumpeleka kufeli darasani...
Stefani kama binti anaamua kumtafuta Bibi yake ambaye ni kama Ukoo ulisema " huyu kwetu kafa na ni kichaa".....
Stefani anakutana na Bibi yake Iris na kumulezea kuhusu ndoto... Bibi anamwambia " mjukuu wangu hiyo sio ndoto nikweli mimi nilikuwepo eneo la tukio hilo lakini nilizuia ... Maana ndoto hiyo ilikuwa unabii " ...
Mbaya sana Bibi anasema alikuja kujua kila ambaye alikuwepo eneo la tukio alikufa yeye na uzao wake baada ya yeye kuwakomboa kwa kuwaambia watoke kwenye jengo lile ...
Maana kama walikimbia vifo basi na familia zao hazitakiwi kuishi .... Maana maisha yao ilibidi yasimame siku ile .....
Binti Stefani anaambiwa na Bibi muda wangu umeisha .... Bibi anasumbuliwa na Cancer na alikaa muda mrefu eneo la pekee yake akizuia kifo kutoka kwenye jinamizi hilo la kifo .....
Binti anamuona Bibi ni kichaa ... Bibi anamwambia yeye ndiye mwenye nafasi ya kuikomboa familia baada ya yeye kuishi miaka mingi ...
Stefani anogoma mno na Bibi anatoka nje ya eneo la usalama na kumwambia Stefani " Seeing is Believing" ...Na hapohapo Bibi yake anakufa kwa ajali mbaya mbele ya Stefan....
Sheria ya kifo cha ukoo ... Anaanza mkubwa na anafata mdogo... Kwahiyo Bibi alikuwa na watoto wawili na Stefani alikuwa mjukuu wa mtoto wake mdogo....
Kwahiyo mzunguko unaanza kwa Baba yake mkubwa na kila mtoto wake alafu unaenda kwenye tumbo la Stefani... Stefani ataweza kuiokoa familia yake ... Familia pia haiamini hicho kitu ....
FINAL DESTINATION BLOODLINES 🥶.