ANAANDIKA FARHAN JR.
.
YOUNG AFRICANS, Waneni husema usiwahadithie Watu ndoto yako ya jana usiku ila hii wacha tuiseme, hii ni simulizi ya muuza Madafu wa Ikulu ndio Yanga wanagawa wastani kwa idadi, Mnyonge wake kala mbili na Mbabe wao kala mbili, unawaita Yanga Afrika ila sisi tunawaita Lecturer wa SAUT Mwanza, wametoa mark up na wamegawa matokeo kwa usahihi Wanafunzi wasichekane, una uhakika wa kupishana na Yanga ila huna uhakika wa kupishana nae wakati wote.
Enyi mlioamini semeni kweli ijapo ni chungu, imebebwa Toyota Cup kule Afrika Kusini, Imebebwa Ngao ya Jamii mbele ya Simba, Imebebwa Muungano, imebebwa Ligi Kuu mbele ya Simba na limebebwa CRDB CUP mbele ya Singida, weka kumbukumbu sawa na wapange Wanafunzi wasiigizie, kama unahisi kuna Mtu anaonewa basi nenda wewe, mesaage to the future the Green and Yellow mean business, ndoo nne kwa heshima, kunja mkono simama wima.
Clocked in and clocked out like a disgruntled Team, lakini walifahamu dhahabu safi hukoshwa kwa moto na almasi hunawiri kwa msukumo, Kwa Mkapa hajatoka Mtu na Amaan hajapona Mtu, ndani ya siku kadhaa tu, another parade incoming, hatua mpya na Njaa mpya, rekodi nyingine visiwani kwa medali za Benki ya Kijani CRDB kwenda kwa Jeshi la Kijani Young Africans, ndoa iliyofungwa peponi, raha na starehe kuitazama kama tendoni.
Young Africans wanaumwa ugonjwa unaitwa Mafanikio, wengine wanaumwa Ukame wa Makombe, Yanga anazidi kujenga daraja refu kama Kigongo na Busisi, anataka kuirudisha Ligi zama za Kale, Wasukuma na pori, Wapogoro na vichaka, Maasai akichomeka mkuki kaa nje, Ladies and Gentlemen kila mmoja atafungwa na Yanga panga mstari fuata mtiririko..