MTUNZI; LIZY MICA
Endelea ๐ป
Sultana alisita kidogo baada ya kuona watu wote wanamtazama yeye.
Moyo wake ulishtuka mara elfu moja pale alipomuona Sona, mwanzo alihisi ni ndoto lakini kadri alivyozidi kumtazama alimtambua mdogo wake wa pekee ingawa ni miaka 10 imepita
"Kwanini uko hapa...." Sona alimtupia swali Dada yake akijitia hamjui
"Nilijua hili ni hekalu, na hata ni kaona inapendeza Mimi kutubu dhambi zangu kabla jua halijazama, ila nikiangalia muonekano wa mazingira apata picha kuwa haya ni makazi ya watu na si hekalu.... naomba radhi" Sultana aliongea kwa unyenyekevu
"Bila shaka wewe ni Mgeni Jijjni Odes, watu wengi hulifananisha Jumba hili na hekalu....mara ya kwanza Sona kutia miguu yake Jijjni Odes aliingia pia mahali hapa akihisi ni sehemu ya kufanya maombi....kuwa na amani" Bi. Fatma aliongea huku akionesha kufurahishwa na muonekano wa Sultana
"Kama hamtajali naomba nifanye maombi kwa dakika chache kisha nitaondoka...." Sultana aliongea baada ya kuiona sanamu ya tembo ukutani
Bi. Fatma alimpa ishara ya kukubaliwa ombi lake.
Sultana aliachia tabasamu kwa kupatiwa ruhusa, dimpozi zilizokuwa mashavuni kwake zilibonyea na kumfanya aonekane mrembo maradufu.
Liam alijikuta akiduwaa kumtazama, kitendo hiki hakikumfurahisha Sona hata kidogo
Sultana alifanya maombi yake kwa dakika kumi, baada ya kumaliza alivua bangili pamoja na hereni zake akaziweka mezani kama sadaka
"Hukuwa na haja ya kuweka sadaka, hili si hekalu...." Bi. Fatma aliongea
"mungu tembo amepoteza muda wake kusikiliza maombi yangu....ni jukumu langu kutoa sadaka kama sehemu ya shukurani" Sultana aliongea kisha akaondoka
Watu wote walibakia kumsindikiza kwa macho na hata wakasahau kama wapo kwenye kumbukumbu ya kifo cha Marmar
"Huenda akapotea njia kama ilivyokuwa kwangu mara ya kwanza kufika Jijini Odes.... nitakuwa msaada kwake" Sona aliongea kisha akaelekea nje
Sultana akiwa anashuka ngazi alisimama baada ya kuhisi kuna mtu nyuma yake, hakuishia kusimama aligeuka nyuma
"Sona....." Aliita huku machozi yakimlenga
"Jiji la Odes ni tofauti na Kijijini kwetu, kwa kuwa umeshaniona naomba urudi....sitarajii tukutane tena" Sona aliongea, hakuonesha dalili ya kumfurahia Dada yake
"Ni miaka 10 imepita bila sisi kuonana, unawezaje kuniambia hivi" Sultana aliuliza
"Mimi ni yatima nisiyekuwa na Dada wala wazazi.....iwe mwanzo na mwisho kujitia unanifahamu undugu wetu uliisha ile siku nimeondoka, Wanaume wa huku si wajinga kama wa Kijijini kwetu hivyo kuwa makini...." Sona alishauri kisha akaondoka
Sultana aliachia tabasamu.... kitendo cha kumuona tu mdogo wake ilikuwa ni faraja kwake. Alijifuta machozi kisha akaendelea na safari yake
Sona anarudi ukumbini kuendelea na ibaada, alishangaa sana baada ya kumuona Bi. Fatma kavaa bangili na hereni za Dada yake zilizotolewa kama sadaka. Alitamani kujua sababu ya kufanya hivyo lakini hakuwa na ujasiri huo
๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป
Mida ya usiku Bi. Fatma akiwa chumbani kwake alijikuta akilikumbuka tabasamu la Sultana
"Huyo ni malaika aliyeletwa na mzimu wa Marmar.....uzuri wake unatosha kuipendezesha nyumba hii bila kuweka mapambo ya gharama..." Bi. Fatma aliongea
"Una maanisha nini...." Ali (dreva wake) aliuliza
"Sijamaanisha chochote, lakini kama ikitokea nimekutana naye nitakuwa wa kwanza kujipendekeza kwake kwa ajili ya Liam" Bi. Fatma aliongea
"Vipi kama ni mke wa mtu?" Ali aliuliza
"Mke wa mtu hawezi kutoa bangili na hereni zake kama sadaka, acha kuwa na maswali mengi..... ikitokea umekutana naye kabla yangu hakikisha unajipendekeza kwa ajili yangu" Bi. Fatma aliongea
Ali aliishia kujikuna kichwa chake hakuwa na neno la kusema
Upande wa Sona akiwa nyumbani kwake alikunywa pombe kali ili asahau maneno magumu aliyomueleza Dada yake lakini haikusadia kitu.
Michezo yote waliyocheza utotoni ilijirudia kichwani kwake.
"Najua kama si kupoteza usichana wako Mimi ningekufa.....lakini pamoja na yote haya ulipaswa utimize ndoto zako na si kuwa kahaba" Sona aliongea pekee huku akilia
Alitamani kujua Dada yake anaendeleaje, alitamani kusikia hadithi za Kijijini kwao.
Lakini hakuwa tayari kumpa nafasi kwa sababu kashaamua kusahau kila kitu kuhusu wao.
Kulivyo pambazuka asubuhi, Sultana alifungasha virago vyake.... alihitaji kurudi Kijiji Odes. Alifanya malipo yake dirishani kisha akaondoka
Wanaume wengi walimgeukia, wengi walitamani kummiliki lakini kwa namna macho yake yalivyokuwa makali sawa na ya Simba jike walipoteza ujasiri wa kumuongelesha
Kabla hajaenda stendi aliingia kwenye hoteli ya gharama sana kula.
Hakuwa mtu wa njaa.....kwa kipindi chote alichofanya kazi ya kuuza mwili wake alijikusanyia pesa ya kutosha.
Aliagiza chakula kisha akaanza kula bila kujivunga....dakika tano zilikuwa nyingi sahani ilikuwa nyeupe
Mhudumu alimletea chakula kingine
"Sijaomba kuongezewa chakula...." Sultana aliongea
"Boss pale kakulipia...." Mhudumu aliongea huku akionesha kwa kidole
Sultana aligeuza shingo yake amuone mtu aliyemnunulia chakula
Itaendelea ๐ฅ.