mmoja avuja damu kama yai la kienyeji! 😳🕊️
✍🏽 Imeandikwa na: Almasi Nillan
Leo India kumechemka kama sufuria ya chai ya kijijini! Katika tukio la kushangaza ambalo limewafanya watu wajiulize kama hii ni kweli ama ni sehemu ya sinema ya Bollywood, ndege wawili (moja akiwa wa Air India, mwingine akiwa na mbawa tu) wamegongana angani kwa kasi ya ajabu! 😵
Picha inayoenea mitandaoni inaonyesha yule ndege mwenye mbawa (samahani sio ndege ya chuma – bali ni yule wa "kuku wa angani" a.k.a dege wa kawaida) akigongana uso kwa uso na ndege ya abiria kana kwamba alikuwa anadai deni! 💥
Ripoti za awali zasema kuwa rubani alishtuka sana hadi akadhani ni shambulizi la UFO, kumbe ni mzee kasuku aliyepotea njia. Kichwa chake kilipigwa “head-on” hadi damu ikasambaa kwenye pua ya ndege – tena hapo mbele kabisa penye nembo ya "Air India", kama matangazo ya nyama choma!
🚓 Polisi wa anga tayari wako kazini, wanasema:
“Tunaendelea na uchunguzi kujua kama dege huyu alikuwa na nia mbaya, au alikuwa tu anachunguza hali ya anga bila kibali.”
Mashahidi wanasema waliona dege huyo akipiga mlio wa “kraaah!” kabla ya tukio, ishara ya mwisho kabla ya kugongana – wengine wanaamini huenda alikuwa amekasirika kwa kupigwa picha bila ruhusa.
Rubani alitua salama, lakini inasemekana alitoka na damu kwenye dirisha la cockpit huku akisema:
“I swear I saw a bird with a suicide mission!” 🧑🏽✈️🐦
🛑 Polisi wanatoa tahadhari kwa ndege wengine wa porini:
“Tafadhali mtumie air traffic control kabla ya kuingia anga za ndege. Ajali haina kinga – hata ukiwa na mbawa!”
🤣🤣🤣
📢Wakenya tuwe makini pia – kama mabuu wa nyumbani wanaeza panda ndege kimakosa, tutarajie lolote!
🔁 Share kwa rafiki yako ambaye huwa anaogopa ndege – hii itamhakikishia kuwa hofu yake si ya bure!
Follow Almasi Nillan😁😁.