Mlango uligongwa nikaanza kutetemeka😩😩niliinuka nikaenda kuchungulia kwa bahati nzuri aliegonga hakuwa yule niliemdhania..
"We salmaaaa" ilikuwa sauti ya zakia ndo waga namazoea nae hapo mtaani kidogo yamezidi" dah nilijua ni juddy mtaa mzima ungejazana pale kwangu"
"Ingia bwana nawewe aah" nilimjibu huku nasema afadhali hata akija huyo kiswaswadu tutamdunda wawili😂😂" .
"Zakia aliingia ndani akaniambia nimeboeka nyumbani nikasema nije kukuona mana kazi umeacha sijui shemu anakutunza vizuri "
"Ha ha ha Umeanza umbea wako nawewe"
"Eeh mwenzangu umbea sunna dadaaa, kwanza nimekumbuka hapaaa "
"Shost wa mtaa sasa"
"Yupi tenaa"
"Si huyo anajikuta Queen "
Mhuuu nikajiweka sawa bila shaka ni judy huyo ,,nikamwambia nipe Ubuyu shost
"Naskia anahamishwa na Mzee Amos ,tena naskia mke wake ameondoka mana huyo baba hajifichi kabisa siku hizi kahamia pale kwa Juddy nyumba ndogo ,
Juddy nae unaambiwa hamtaki mzee amos ila ndo hana jinsi kwasasa mana yule benten wake kamuacha hataki hata kumsikia kwahiyo hana tenaa wa kumtambisha mjini ndo anajibana bana kwa amos hapoo "
"Heee!!! We umeyasikia wapiii??"
"Eeeh karagabaho shoga angu unajifungia ndani , update kama hizi huwezi zipata mwenzio gazet"
"Hahahh kwakweli wewe ni Gazeti ,kwahiyo amekwisha hamaa???"
"Bado ila naskia ni siku yeyote anahamishwa hapa ndo kashakuwa mke mwenzie na mama Jefu"
Mmmh nyie wanaume ,nikasema afadhali ahame bwana wee aah , simu yangu ikaita tena ilikuwa namba hiyo hiyo ambayo niliongea na juddy ,nikasema huyu nae sijui anataka nini tena nikapokea
"Toa namba yangu kwenye block nahitaji kuzungumza na weww" heee ndo nikakumbuka kwahiyo ile siku ,alex alimpigia Juddy ndio mana judy aliipata namba yangu eh"
"Basi baada ya kuwaza hivo nikamwambia Sikujui mie"
"Lol akapandisha hasira we mpuzi acha kujifanya mjinga nitakufata hapo hunijui wewe yani nitakujazia watu hutoamini"
"Nyoo usiniletee mimi hasira zako za kuachwa njoo uone kama sijamfata huyo mzee wako nikampa habari zako , afu nikacheka nikakata simu sikutaka zakia aelewe kinachoendelea"
Basi mimi na zakia Tulipiga story nyingi sana hiyo siku akanipa habar nyingi za Judd mpaka nikashangaa moyoni nasema hapa hata mimi usikute mtaaa unahabari zangu na sijui😂😂
Baada ya zakia kuondoka mi nikaendela na mishe zangu, mida ya sambili usiku simu yangu iliita namba ilikuwa ngeni ,nikapokea kwa woga mana hizi namba ngeni naziogopa hatari
"Njoo hapa nyuma kwa Esta" uuh sauti ilikuwa ya yule yule Judy huyu dada amenikalia kooni nikajuta kupokea simu hiyo ..
Nawaza niende au nisiende, na kwanini nisiende ye si anataka kujua mi najuana vipi na Alex au kuna kingine, nilijifikiria sanaa nikaona embu acha tu niende tutajuana huko huko mbele ya safar kwanini nimuogope kwanza wakati mi bwana ake sina hata chochote nae ??
Nikachukua kijora changu nikajitupia mtoto wa kinyamwezi , taratibu nikasogea hapo kwa esta huwa Kuna saluni ya huyo mdada afu pembeni kuna ki njia kipo giza giza ndo huko alisema Tuonane ,
Nilimkuta amesimama kama kawaida yake amejiremba kama anaenda kwenye party kumbe anakuja kuongea na mie
"Naomba uniambie ukweli salma , Unamjua vipi alex ,na ile siku alipo tumia simu yako alikuwa wapii"
Alishusha sauti akawa anaongea kwa huruma kweli ,nikawaza sijui nimwambie tu ukweliii ,sawa nikafanya maamuzi wacha nimwambie kuwa alijificha ndani kwangu ile siku
Bila hiyana mie nilimuahadithia kila kitu kasoro pesa tu kunipa ,ndio sikulisema
"Eeh mungu asante,hakuumia popote"
"Walaa alikuwa tu mzima"
"Kwahiyo hata ule mda nimekufata hapo nje alikuwa yupo ndani kwako"
"Ndio"
"Eeh mungu ungenambia salma sie wote ni wanawake jamani"
"Sikujua"
"Naomba umpigie simu salma please nahitaji sana kuzungumza na Alex nampenda ,nahitaji kurekebisha nilipo mkosea salma nakuomba"
"Mi sina namba yake hata hivyo"
"Nakupatia mie ninayo ,ongea nae muombe muonane nitakwenda kuonana nae mie please nisaidie "
Alinipa namba mtoto wa watu sina makuu nikapiga simu iliita ya kwanza bila kupokelewa nikarudia ikapokelewa
"Salmaaaa!!! Nilikuwa nampango wa kukucheck kesho umeniwahi!!"
Mmh alianza kwa kuchangamka kabla hata mie sijaongea kitu
"Mmmh umenijuaje??" Hapo nilikuwa nimeweka sauti kubwa Judy anasikiliza kwa makini sana
"Khaa mrembo wewe kwanini nisikujuee"
"Hahaha Umeanzaa mambo yako" mi tena si nikasahau kazi niliyopewa mwenzio ,nikajiachia kuongea na alex yaan kama nilihisi kummiss sanaaa, afu na vile alivyonichangamkia nikajikuta namsahau juddy 😂😂"
"Wooooh ,hahaha lakini salma ukweli nimeku mis mnooo" Judy akanipokonya ile simu afu akaikata jamani mi mwenzie tena nikajisahau kama ni bwana wa mtu hivyo😂😂"
"Umetembea na Alex wewe???" Hee nikatoa macho yaan aliongea kama ana uhakika kuwa nimetembea nae"
"We unaongea nini , kwani sikukuambia kama nilimsaidia tu"
"Alex hana mda wa kushaukia mtu wala kucheka cheka nae ,niambie ukweli alex ameku🙄 eeeh ??"
"Hahah afu we bwana embu nipe hiyo simu " nikataka kuichukua simu yangu nikashangaa akaivuta kwa nguvu kweli hee huyu vipi wakati huo ilikuwa inaita nikahisi anapig huyo huyo alex"
"Mwambie mkutane leo sasa hivi,Rose hotel " afu akaipokea et akaniwekea sikioni ,mi nikabaki kimyaa baada ya kuita haloo haloo kimya alex akakata simu"
Jud akaandika jumbe kumtumia alex nikaona kama wanajibizana hivi kwenye msg baada ya muda ,akanambia nakujaa huku anaondoka tenaa alikuwa na haraka haraka kwelii
"Nipe simu yangu"
"Nakuletea muda sio mrefu"
Nikabaki nimeshangaa hata uwezo wa kumfanya kitu nikawa sina kabisa nimedorolaa yaan namuona huyo anaishia akiwa na simu yangu ..
Nikajivuta zangu kurudi ndani kichwa kina mengi mpaka nacheka mwenyewe
"Yaan mi akili zangu bwana, sa kwanini nimemuacha ameenda na simu??" Nilikua najiuliza huku nacheka kwa uchungu aisee ,nilivyofika nyumbani nikabamiza li mlango kwa hasira nikapanda kitandani,"
Moyo wangu unawaza simu yangu afu najiuliza sasa kwanini kwanza nimemuachia simu , kwanini ndo namuogopa sasa??
Mda ulizidi kwenda judy hakuja , baada ya muda sana kwenda ilikuwa usiku kama sa nne hivi sikuwa hata na saa nilikisia tu kwa uzoefu wangu ,
mlango wangu uligongwa ,akili yangu ikasema Juddy huyo huku najiinua kitandani haraka haraka .
Kichwani hapo napanga maneno ya kumwambia, sitaki mazoea nae anikome sitaki kabisa tena sitaki , nikafungua mlango huku nimejipanga kumkabili mjinga huyu
Baada ya kufungua mlango mungu wangu😳nilishangaa😳😳😳 huyu kafikaje hapa?? Mi nilizania ni juddy ndo kaniletea simu ghafla nakutana na mzee baba afu ni
KWETU morogoro.