Wakati jeshi la Waislamu na jeshi la Wafursi (Waajemi) yalikuwa yakijiandaa kwa vita, ghafla Waislamu wakashangazwa kuona kwamba Wafursi walikuwa wameleta simba aliyezoeshwa kupigana vitani!
Katika uwanja wa vita bila onyo lolote, simba alianza kukimbia kwa kasi kulielekea jeshi la Waislamu huku akinguruma kwa nguvu na akionyesha meno yake ya kutisha.
Lakini kutoka katika jeshi la Waislamu, ghafla akatokea mwanaume mmoja mwenye moyo wa simba. Akakimbia kwa ujasiri mkubwa kuelekea kwa simba yule tukio la kutisha lisilowezekana kufikirika.
Ni nani huyo ambaye anaweza kukimbilia simba mkali badala ya kukimbia kumkimbia simba?
Haijawahi kutokea katika historia kwamba mtu anakimbilia simba anayekuja kwa hasira.
Majeshi yote mawili – la Waislamu na la Wafursi – yalikuwa yakitazama kwa mshangao mkubwa. Wakiwa wameshikwa na butwaa yaani ni vipi mtu, hata awe na nguvu na ujasiri kiasi gani, anaweza kumkimbilia na kupambana na simba?
Lakini shujaa wetu alimkimbilia kama upepo kuelekea kwa simba, bila kuogopa. Kifuani mwake kulikuwa na izza (heshima), imani na ushujaa wa Muislamu ambaye haogopi chochote isipokuwa Allah pekee, Kwa hakika, inaonekana kana kwamba simba ndiye aliyepaswa kumuogopa.
Kisha alipomfikia Simba akamrukia simba kama vile simba mwingine anavyorukia kiwindwa chake, kisha akamchoma kwa mapigo kadhaa ya mkuki hadi alipomuua.
Hofu kubwa ikatanda kwenye nyoyo za Wafursi: “wakaanza kujiuliza tutawezaje kupigana na watu ambao hawaogopi hata simba?!”
Waislamu wakawashinda Wafursi kwa nguvu zote.
Kisha, Sa’ad bin Abi Waqqas (radhi za Allah ziwe juu yake) alimwendea shujaa wetu na akambusu kichwa chake kwa heshma na kumpongeza.
Lakini shujaa huyo, kwa unyenyekevu mkubwa wa kweli wa mashujaa, akainama na kumbusu miguuni Sa’ad bin Abi Waqqas, akamwambia:
"Mtu kama wewe hustahili kubusu kichwa changu – bali mimi ndiye ninayepaswa kubusu miguu yako."
Akionyesha heshma kwa kiongozi wa Jeshi ambaye ni Sa'ad bin Abi Waqqas
Je, mnajua Shujaa huyo aliyepambana na Simba na kumuua?
Ni Haashim bin Utbah bin Abi Waqqas – muuaji wa simba.
Hawa ndio watu wetu wa kuigwa!
💥Ikiwa umemaliza kusoma, usiondoke bila kufanya jukumu lako kwa Mtume Mustwafa (rehma na amani zimshukie yeye na Aali zake na Maswahaba wake wote).
Kwa hadithi zaidi nzuri za Manabii, jinge nami kwa kugusa jina langu kisha Follow Sufian Mzimbiri.