MTUNZI: LIZY MICA
Endelea 🌻
Sona akiwa amevalia sare za Polisi alitoka ndani ya lifti akiwa na wenzake, kama kawaida yake alivunga hamfahamu Sultana badala yake alianza kuongea na Liam
"Kuna changamoto ilitokea hapa, hivyo sisi kama Polisi tulifika kuweka mambo sawa....sina uhakika kama mtapata huduma siku ya leo kwa sababu jengo hili linatakiwa kufungwa kwa ajili ya upelelezi" Sona aliongea
"Kitu gani kimetokea...." Liam aliuliza
"Watu wawili wamepatikana wamekufa.....bahati mbaya ni Raia wa Israeli, nadhani unaelewa balaa lilipo kama wahusika wa mauaji haya hawatapatikana. Kwa siku kadhaa hakutakuwa na huduma ya usafiri..." Sona aliongea kisha akaondoka na wenzake
"Mahali hapa hapafai tena... tuondoke" Liam alimuambia Sultana
Kwa pamoja waliingia kwenye gari, Sultana alijikuta akidondosha machozi... ndani ya moyo wake alifurahi kuona mdogo wake katimiza ndoto yake.
Mavazi ya Kipolisi yalimpendeza kupita kiasi....
"Kwanini unalia...." Liam alimuuliza
"Mimi pia ni mgeni Jijini Odes, nimejikuta tu ni kiwahurumia wageni waliopatikana wamekufa...." Sultana aliongea
"Nitakutafutia sehemu nzuri ukae mpaka pale huduma ya usafiri itakapo rejeshwa, ni sehemu salama kuliko hata nyumbani kwangu" Liam aliongea
Sultana alitikisa kichwa kuashiria ameelewa.
Haikuwa shida kwa Liam kumpangishia mrembo huyu hoteli iliyo mgharimu shilingi milioni moja kwa siku.
Huduma za Burj Al zilikuwa nzuri sana hasa kwa mtu anayeamua kufanya makazi mahali kwa siku kadhaa
"Hapana, siwezi kukaa hapa...unakoelekea utaniomba mk*ndu, niache nijitafutie mwenyewe sehemu ya kulala" Sultana alishtuka baada ya kuoneshwa makazi yake ya muda
Liam alijikuta akicheka kwa maneno aliyoambiwa
"Naomba ukue kiakili....ni aibu kuudhalilisha urembo wako kwa kuongea maneno bila kutumia tafsida" Liam aliongea
"Yule Polisi wa kike ni nani yako...." Sultana alijikuta akiuliza
"Ni rafiki wa familia yangu.....ni Polisi pekee anayeogopeka hapa Jijjni Odes, hivyo hata hili tukio lililotokea atalikamilisha kwa muda mfupi utaweza kurudi Kijijini kwenu, yeye pia ni mzaliwa wa Odes Kijijini" Liam aliongea
Sultana aliachia tabasamu habari hizi zilimvutia na hata akasahau kama yupo Burj Al
Liam alitaka kuondoka lakini Sultana alimzuia
"Naomba nijue unafanya kazi gani....kama nilivyokuambia Mimi ni Kahaba ninaye tegemea mwili wangu kujiingizia kipato. Naomba nijue pia kuhusu kazi yako....unatumia pesa vibaya sana niambie unazitoa wapi" Sultana aliuliza
"Ninafanya biashara nyingi sana, nikianza kukutajia moja baada ya nyingine jua litazama nikiwa naongea....." Liam aliongea
"Nitajie japo moja vinginevyo sitalala hapa...." Sultana alitishia
"Namiliki Kampuni la utengenezaji wa Meli linalojulikana kama Star ships" Liam aliongea kisha akasepa kuna mahali alionekana kuwahi
Sultana alidumu kwenye mshangao, amezoea kukutana na Wakulima lakini kwa mara ya kwanza katembea na CEO wa Star ships
🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
Upande wa Sona akiwa kazini kwake alijikuta akipoteza focus hasa akikumbuka namna alivyomuona Dada yake akiwa na Liam.
Tabia za Sultana anazifahamu hivyo alikuwa na uhakika wawili hawa tayari wamekutana kimwili
🩸Niliwaona wakiingia Burj Al hotel....lakini Liam kaondoka nina uhakika yule mrembo atakuwa pale🩸 Ujumbe uliingia kwenye simu ya Sona
Alifunga ofisi kisha akaondoka, dakika 15 zilikuwa ni nyingi alifika Burj Al
Aliulizia chumba kilicho chukuliwa na CEO wa Star ships
Baada ya kufahamishwa aliingia kwenye lifti
Sultana akiwa anahesabu pesa, mlango wake uligongwa.....sura ya Sona ilionekana kwenye TV ndogo.
Sultana alisimama akaenda kufungua mlango....kama kawaida yake aliachia tabasamu lakini Sona alimkazia
"Ulikuja Jijjni Odes kwa ajili yangu au kutafuta Wanaume!.... umewezaje kutembea na Liam, ulipaswa kuniuliza Mimi na yeye tuna uhusiano gani kabla hujamuonesha uchi wako" Sona alifoka
"Ndiyo Mimi ni Kahaba....lakini pua zangu zinajua kunusa yupi ni Mume wa Sona wangu na yupi si wake.....Liam hana uhusiano wowote na wewe ndio maana nilikubali kufanya biashara naye, nimesikia wewe ni rafiki wa familia yake ni kawaida kumlinda sababu ya tabia zangu.... usiwe na hofu pindi huduma ya usafiri itakapo rejeshwa nitaondoka..." Sultana aliongea akiachia tabasamu
Muonekano wa uzuri wake ulimkwaza Sona..... taratibu alijishika mfukoni mwake
Sultana hakuamini alichokiona
Itaendelea 💥.