Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

DOCTOR NITIBU NA HUKU KUNAWASHA 🌹🌹❤️❤️❤️🌹 sehemu ya 01

1st Jul, 2025 Views 67



.... kwa majina naitwa Nasra.naishi zangu hukuu Vingugwe mbagala ndani ndani hukoo kwetu mabondeni ,nimejipangia zangu chumba nafanya vibiashara vyangu,miaka yangu now ni 27 sina mtoto wala sijawahi kuolewa🤦‍♂️ hao wanaume kutwa kuniacha yaan mimi naachika kwa mwezi hata mara mbili aisee mwanaume nikifunga miezi mitatu naoga maziwa🙌😄 sio kama napenda hapana mwenyewe kuna muda nahisi kama nisharogwa hivi na wananzengo
Okay kuna muda niliwaza au niachane tu na mapenzi sijaumbiwa mimi ?? Au basi nipate hata wa kuzaa nae tu umri unaenda aisee lakini sikuwahi kupata ,nakumbuka wakati huu nilikuwa ndo nimeachana na kibwana changu tu nilikifumania na shoga angu ambae tunafanya nae biashara moja ,nikaona embu acha nijipende zangu tu mwenyewe🥰
Nikaanza kununua viwalo ili niwe mdada wa kisasaa yaani niachane na Uchoko wa mabondeni😜..

Tuachane na hayoo siku moja bwana nilipigiwa simu na ndugu yangu mdogo wangu amepelekwa hospital maana alikuwa mjamzito kwahiyo tarehe zake zimefika ilikuwa asubuhi nikajiandaa fasta kuwahi , nikachukua boda mpaka pale nyumbani kwake, yeye amejaariwa ndoa na anawatoto yaan hiyo mimba ilikuwa ni ya 3 ,basi tukajiandaa mpaka pale Roundtable, hospital moja hivi ipo kizuiani huko huko mbagala , tulifika mida kama ya 6 hivi tukaambiwa mgonjwa bado tukampa chakula tukazuga zuga pale tukarudi hom ,jioni tena tukapeleka chai lakini hali ya mgonjwa ilikua sio nzuri ...

Asubuhi tulipo enda tukaambiwa mgonjwa anatakiwa kuhamishiwa Temeke hospital mana hawawezi kujifungua kawaida mpaka Op na Hapo wamempima wamemshindwa , matumbo joto tukaambiwa inasubiriwa Ambulance apelekwe Temeke hospital nilikuwa na ndg yangu mwingine tukasema sie tutangulie temeke mgonjwa atatukuta huko basi tukachukua boda mpaka kituoni tukapanda magari ya Temeke ,
Tulifika hospital ilikuwa sa tatu hivii asubuhi tukauliza kuhusu mgonjwa anaetoka Roundtable tukaambiwa bado ,tukajivuta zetu mpaka kwenye bench pale la kusubiri .

Mida ya sa 5 hivi ndo ambulance iliingia moja kwa moja mgonjwa akaingizwa Kwenye Op si tukaa kusubir nje pale ..
Majira ya sa kumi akatolewa mgonjwa wetu akiwa tayari mama sasa🥰🥰 alikuwa amewekwa kwenye kile kitanda sasa mtoto hatukuwa tunamuona mi nikamuuliza mwenzangu mbona mtoto hayupo akanambia embu tufate nyuma ,tukawa tunawafata wale manes ambao wanamvuta kwenye kile kitanda mpaka kwenye Wodi ..

Tukauliza vipi mtoto wakatuambia mtoto yupo kule juu amezaliwa anashida basi tukamsalimia mama wa mtoto ,wakatuambia twende kule juu kumuona mtoto ,tukaaga tukaondoka wakati tunatembea nikakumbuka pale nahangaika kulipia lipia huduma niliona ma doctor wengi kweli afu vijana wazuri mpaka raha basi nikawa namwadisia ndugu yangu kuna mmama hivi alikuwa nae njia moja na sisi akaingilia maongezi yetu akanijibu ni wale wa sudani hao yaan wanajali wagonjwa hadi rahaa ...oooh ndo mana wanavirangi vizuriii yaan wadada wao ni wazuri wamkaka jamani adi raha afu wakarimu hata mimi nimeona , tukaenda tunapiga story za hao madoctor wa Sudani hao mpaka tukafika kule juu ambapo ndio tuliambiwa tukatizame mtoto ...

Nikaingia mimi maana walisema anatakiwa kuingia mtu mmoja,,mule ndani nikakuta jamani madoctor kama wote wa sudani nyiee wakaka wacheshi mpaka raha
"Mtoto anaitwa nani??" Doctor mmoja akaniuliza mi nikacheka tu
"Jaamani mtoto ndo kwanza kazaliwa sa hivi hata jina bado "
" mi najua mtoto anakuwa na jina tayari hata kabla hajazaliwa akizaliwa tu anapewa" mwingine akadakia huku anacheka
Nikataja jina la mama ake wakanionesha sehemu alipo huyo mtoto nikasogea kuona hee bonge ya toto kizurii ka mama ake mkubwa🤩🤩 Nikatamani hadi kuzaa wakati huo huo 😋🤗
Basi nikaambiwa mtoto anatakiwa pempas na dawa mana anashida kidogo nikaandikiwa Dawa nikanunue na kulipia File lake
Wakati natoka kuna doctor mmoja akaniita ye alikuwa kimya muda mwingii afu ndo alikuwa anamuhudumia dogo
"Samahani dada naweza kukuagiza nje please " aliniomba kwa upole huku ananitazama kwa makini kumtazama si ndo Yule yule msudani aiyaaa😅 nyie huyu mkaka alikuwa mzuri nahisi kuzidi wasudani woteee🙌🙌 anavyoongea sasa kwa pozi haloo!!! Basi nikajikuta mpaka nababaika
"Ndi ..ah oh haina shida " nikajibu huku najichekesha chekesa 😄
"Naomba unichukulie maji ya baridi na Peps take away " alitoa afu tano akanipa ki hela kinanukia hatari

ITAENDELEA......

SEHEMU YA 02

basi wacha nitembee huku nanusa nusa ile hela yaan inanukia harufu ya kipoaji yaan sio zile harufu za bodyspray ya afu 5,5 Tumezoea hapa ..

Nikaenda kulipia dirishani baada ya kuchukua Nikaenda kwenye dawa process zilikuwa nyingi nikafanikiwa kupata dawa ,nikatoka nje ya geti nikachukua maji na peps tena nikimuhimuza muuza nataka vya bardiiiiii,sitaki kumkwaza yule kaka😄😄 nikarudi zangu chaap ,nikaingia mule ndani kwenye chumba cha watoto yaan kuna watoto kibaoo wengi pre_mature na waliozaliwa afya kidogo inashida ndo wanawekwa huko basi nikawa nimesimama na yale maji na peps alienituna yaa yupo bize hatari sijui hata kama alikuwa ananiona , yule doctor mwingine alonituma dawa ye akachukua nikabaki nimesimama kumsemesha naogopa afu mule ndani mimi tu ndo raia wengine wote ma doctor kulikuwa na nesi mmoja yeye alikuwa anasoma majina ya watoto ambao bado hawajahudumiwa
Nikamwambia dada maji haya hapa akanijibu et kwani mi ndo niliokutuma khaa wabongo bwana😡alinikera afu akaendelea kuwa bize basi kuna mkaka mwingine ye alikuwa anapanga dawa ndo alisikia akanitazama afu akageuka kule ambapo ma doctor wapo bize bize yaan hapo nimesimama karibu lisaa jamani hata nimechoka afu unajua kusimama sehemu wewe sio muhusika wala watu wa kawaida hawarusiwi kuwa hapo inaboa😥
"Abbas ,Abbas .... vitu vyako huku bwana" yule kaka akaongea huku ananionesha kwa kidole yaan vitu nilichukua vya baridiii lakini mpaka yamekuwa ya moto aah
"Oh nakuja sasa hivi eeeh" alinigeukia aakanambia huku anatabasam ,nikapata na nguvu za kuendelea kusimama huwezi amini😀
Alipo maliza kupanga na kuwahudumia watoto akanifata
"nisamehe sanaaa dada angu" akanambie huku ananyoosha mkono kuchukua mfuko
"Usijali..." nikampa vitu vyake
"Chenji yanguu" hee huyu nae anadai vi chenchi kama vile nilisema simpi wakati nilikuwa navitoa nilipo vichimbia
"Hii hapa"
"Mungu akubariki sana ,Mwanao ni yupi hapa"
Nikaonyesha yule mtoto wa mdogo wangu
"Ooh huyu kumbe faili lake ninalo mimi"
"Anashida gani kwani "
"Huyuu yaan sijui nikuelekeze vipi kwa kiswahili kidogo inanisumbua ,Si ulishazaa"
"Mmh bado"
"Weee kweli???"
"Ndio "
"Kwanini sasa???"
"Sijajaaliwa bado.??"
"Aaah hujajaaliwa au wewe ndo hujaamua??"
"Sijajaaliwa nilishaamua kitambo"
"Una umri gani??"
"27 "
" fanya maamuzi bwana sawa" tulijikuta tu mjadala umekuwa mrefu uso wake ulionesha yaan mshangao wa wazi kabisa kuwa sijazaa , akanambia basi hapa ushamaliza kila kitu unaweza tu kwenda nikamuuliza
"kwahiyo shida ake sio kubwa lakini??"
"Aah siwezi kusema kubwa au ndogo ,unajua kila kitu mungu ndie anapanga eeh muhimu tumuombee tuu ....Ezee!!!"
Aligeuka akamuita kaka mwingine alikuwa doctor m_bogo tu akaja akamwambie hivi akataja Neno hata silijui mimi akamuuliza kwa kiswahili wanaita nini
Yule eze akanambia ni mtoto alikunywa maji wakati anazaliwa khaa sasa hilo ndo la kushindwa kulisema kweli😀 Nikasema sawa nikatoka zangu yaan hapo jioni kabisa nikamkuta ndugu yangu bado anang'aa macho nje hao tukasema zetu home .....

Ikabidi sasa tujipe zamu ya kwenda hospital mana tulikuwa wawili mmoja aende asubuhi mwingine jioni ile asubuhi ya siku ya pili ikabidi aanze yule ndg yangu mi nikasema jioni
Nikaandaa vya kupika mapemaaa nikaenda kuchukua nguo za mtoto sox na kofia pempas tulinunua pale pale wanauza
Jioni huyo mpaka temeke wakati naingia pale getini si nikakutana na yule Msudani yeye ndo anatoka hee afu kavaa nguo za nyumbani aisee ni m_gentleman wa maana anaki body cha kuvalia nguo anavyotembea sasa aiyaa nikatazama pembeni haraka haraka yaan kama vile simjui nikajikausha ndo tunapishana nikasikia mtu ananiita "ma mkubwaa!!!" Hee nikajikausha mana nilijua ni yeye huyuu mana ile jana aliniuliza uhusiano wangu na mtoto nikamwambia alojifungua ni mdogo wangu akanambia kwahiyo wewe ni mama mkubwa eeh nikasema ndio , sasa nikalegeza mwendo ila sikugeuka akaita tena Uvumilivu ukanishindwa ah kwanini nimtese nikageuka huku najitabasamisha kinafk , yeye alikuwa kasimama ilibidi namimi nisimame akaja nilipo
"Habari...naona upo kwenye majukumu " akanambia wakati huo alikuwa anasogea nilipo nami nilikuwa nasogea pembeni kutoka pale getini
"Mh nakwambia ni hatari mambo"
"Poa tu,leo nimeona kaja mtu mwingine kabisaa nikataka kumuuliza jaman mamkubwa uuguzi umeshinda" aliongea huku anacheka ana vidimple kwa mbalii basi ndo kisura kinavutia Aii👌
"Hapana bwana ,yule ni ndugu yangu tumepeana zamu ulikujipa muda wa kupumzika" nikamjibu huku nacheka cheka basi hapooo
"Kwahiyo sa hivi unashuka kwa mzazi mana ni muda wa kunyonyesha ukamchukue aje huku juu" nikasema kumbe utaratibu ndo upo hivyo basi akawa amenielekeza vizuri nikasema poa akanambia naomba basi nami nimuone mdogo wako au siruhusiwi ,wee kutembea na mkaka wa maana hivi afu ni doctor afu msudani aii watajua wenyewe hata wakisema ametoroka vita😀😀 mi navimba zangu bwanaaa👌 tukaenda wote mpaka kule wodi ya wazazi akamsalimia mdogo wangu akampa pole kwenye begi akatoa juice ya matunda akampa basi tukapiga story wakati huo tunatembea taratibu mana mzazi hana speed ya kutembea na anatakiwa kwenda kunyonyesha basi Yule kaka akasema naona hata mam kubwa hanitambulishi jaman ngoja nijitambulishe mwenyewe mi nikacheka sasa namtambulishaje mana hata mimi mwenyewe simjui jaman jana tumekutana bahati mbayaa akamwambia mi naitwa Abbas ni Rafiki ake na mamkubwa si ndio mamkubwa?? Nikacheka kweli nikamwambia mi mwenyewe nashkuru kukufahamu maana hata jina nilikuwa bado sikujui basi tukafika kule juu Wakati tunapandisha ngazi si tutakutana na kile kidada jana kiliniropokea alivyomuona yule kaka akashangaa et hee abbas kuna kitu umesahau?? Mi nikajua sa hii unakaribia kwako!!!. Akamjibu hapana nimekuja tu na yangu mwaya.. basi yule dada akanitazama juu mpaka chini hee mpaka nikajiskia vibaya nilikuwa nimevaa zangu Kijora habari mie sina viatu vyangu vya afutano Tandika , sa nivae viwalo kuja hospital jamani hapana nilijitundika tu kijora changu ...

ITAENDELEA....

SEHEMU YA 03

Yule dada akatupita si tukabaki pale nje yaan mimi na Abbas sasa hapo namjua jina ,mzazi akaingia ndani kunyonyesha ,nikamuuliza kwan we ushamaliza akanambia ndio mi nimepunguza majukumu yangu mpaka kesho tena ,,,hali ya mtoto lakini vipi,,,mtoto yupo vizur ashukuriwe mungu kesho akiwa hivyo hivyo mnaweza kuruhusiwa ,,,,asante mungu daah ,,,, ndo basi hapo sikuoni tena..
Yaan swali lake kwanza lilinistaajabisha nikabaki kama vile nimepigwa butwaa yaan hanioni tenaa ki vipi?? Wakati mi mwenyew najua hapo ndo hatuonani tena au yeye anataka kuonana tena yaan nikawa bado sijaelewa anamaana ganii?? Sec hiyo hiyo akarudi yule dada Sijui ni nesi au doctor atajua yeye kwanza, akafika pale
"Haya tuondoke Doctor" akamwambia Abbas kama vile alimpa taarifa za kumsubiri hapo
"Aah mi bado nipo Martha we tangulia" "bwana embu twende upo unafanya ninii" akawa anamvuta mkono kumuinua abbas nae hata hainuki anatoa tu mkono ,hapana Martha we nendaa,,,, ndo upo na huyuuu???. Akageuka kuntazama na hivi anajicho la mapozi huyo dada mmh embu nikae kimya akambembeleza wee lakini abbas alikataa akasema ye ana issue zake basi yule dada akaondoka ila uso wake ulikuwa umekunjamana na hasira kwelii
Mzazi akatoka alikuwa amemaliza abbas akamuuliza uliza maswali pale wakati tunamrudisha wodini baada ya kuhakikisha amefika ndo tukawa tunaondoka yaan nilikuwa siamini huyu kaka kama anaambatana na mimi sa kwanini?? Nikajikuta mpaka ile kujiamini inapotea kabisaa nababaika tu hata akiniuliza swali mi kujibu mtihani simu yake iliita akapokea ndio martha .. nikajua tu ni yule mdada yule hajaridhika kaona apige simu
Aah hayo yako sasaa bwana ......sio kweli ...embu tulia nitakucheck
Akaikata simu muda huo huo ,tukatoka nje ya geti akanisindikiza mpaka kituoni kila gari likija naona uzito kuondoka ukweli nilikuwa najisikia fahari mno yule kaka kuwa pembeni yangu ni mwanaume mwanaume kwelii, anapendeza machoni jaman kuanzia nywele, ndevu kifua japo kipo kwenye shart 🥰🥰 lakini so mwwwah😘😋 mpaka alipo niuliza naishi wapi nikamwambia mi naenda mbagala akanambia basi tupande wote mi nikashukie kwa azizi ally mana kuna mshkaji nataka nikamuone mitaa hiyo,mmh nikasema moyoni mshkaji wapii wakati martha😀Et nikasikia wivu tena!!🤔 tukaenda zetu nauli akanilipia sasa jee🤗 venye ananukia sasa na hivi tulikaa siti moja jaman tumebanana nikatamani hata nipige self ya ukumbusho 😀

Akashuka kwa Azizi roho ikaniuma hiyo aah basi nikaenda zetu hukoo nilipo fika nikampa ubuyu yule ndugu yangu akanambia basi kuna Doctor huyo huyo ndo naelewa hapa alikuwa ananiangalia asubuhi daah mpaka nikawa najishtukia nikajua labda kavutiwa na mimi kumbe alitaka kuniuliza naona akashindwa ,,we kuvutiwa tenaaa embu usinipasue moyoo😀😀 ,,,we mjinga kwelii sa kwani bwana akoo ,,,sio lakin nampenda jamani huyo kaka mmmh sio poa😥,,, mwambie siku hizi tupo dunia ya uwazi funguka ,,,aah siwezi kufanya huo ujinga mimi hata siku moja mwenzangu yaan siwezi kwanza yule kaka sio hata hadhi yangu mi kutwa nanuka jasho afu ye alivyo vile,,, wewe sio hadhi yako si kwa vile wapo tu hapa kuna amani hao ukiwakuta kwao hata kuoga hawaogi muda wote wananuka damu wanaimbia kimbia hovyo muda wa kuoga unafikiri wanao ,hizo pafyumu si wamezijulia hukuu,,,,,, hee shoga angu mbona kama unamchamba tenaa shemeji yako😀,,,,,hahah shemeji yangu bongoo...

Tukacheka hiyo siku msudani ndo alikuwa mda mpaka tunalala kesho yake asubuhi kama kawaida alienda yule ndugu yangu mi nitaenda jioni, kabla ya jioni tulipigiwa simu mchana tukaambiwa haina haja ya kwenda jioni maana kapewa Ruksa wanafanya utaratibu wa kutoka , hiyo siku alienda mumewe mwenyewe akafanya process zote mpaka sa moja jioni inafika walikuwa tayari nyumbani, basi mwenzanu hata usiku sikulala nikawa nakumbuka tu yule kaka alivyonambia kwahiyo sintakuona tenaa afu nikikumbuka sikumjibu hilo swali roho inaniumaaaa😥 najiuliza alikuwa na maana gani sasa jamani?? Au alitaka tuwe tunaonana mara kwa mara?? Basi hata majibu sipati jamani....

Basi tukawa tunahudumia mgonjwa hapo hapo kwake kipindi chote sikuwahi kurudi hata kwangu wala biashara zote nilisimama ,mpaka ikafika 40 hata mawazo na yule kaka tena nilijikuta yamepotea yaan nilikuwa nishaachana nae kwa sababu najua siwezi au hatuwezi tena muonana mimi nayeye ..

Ilifika siku ya 40 tukafanya na hakika siku hiyo hiyo ,tukashauriana kesho yake twende tukafatilie cheti cha mtoto ili tumalize kabisa
Siku yenyewe tukaamka asubuhi mpaka temeke tukaandikisha tulipewa cheti muda huo huo yaan mpaka sa nne tushamaliza tunaondoka zetu kurudi om wakati tunatoka pale nje ya geti nikamwambia mdogo wangu wakati huo mtoto wake anajina teyari mama salma nikamuomba anisubiri nikachukue maji mana koo lilinikauka balaa , wakati nipo pale kwa muuzaji akaja mteja mwingine alikuwa kwa nyuma angu hata sikumtazama ila nilihisia kuna mtu nyuma na yule muuzaji alikuwa amekwenda kuniangalizia chenchi
"Vipi dada yuko wapi" nilisikia sauti kwa nyuma angu
"Amekwenda kuta........" nilimjubu huku nageuza shingo kumtazama haa si niliishiwa pozii baada ya kumkuta Abbas aisee ye mwenyewe hakuamini
"Mam kubwaa" yaan aliniita kwa shangwee mpaka nikabaki nachekaa
"Dah yaan sisi kweli pipo jaman tumekutana hayaa za kunikimbiaaa"
"Basi hata nilikukimbia walaa sema tu ile siku baada ya kupata taarifa anatoka ilibidi aje shemu mwenyewe ili kulipia na gharama zote"
"Aiyaa basi hata kusema ngoja nikamsalmie kaka anguu au mimi sio kaka ako ndo mana unanitenga hivyo"
"Jamani hata sio hivyo mi hata sijakutenga" akaniuliza kama nilikuja Pale hospital nikamwambia tulikuja kufuatilia cheti cha kuzaliwa aah aliskitika "kwahiyo ndo ulikuwa unaondoka hivyo?? Bila hata kunisalimia jamani vibaya mamkubwa mungu hapendi nisingesikia kiu ndo basi daah " alilalamika mpka nikawa naona aibu sasa mbona ananifanya mimi kama special sana wakati sina la mbele wala nyuma jamani
Basi mi nikachukua chench yangu nae akachukua maji tukawa tunatembea huku tunapiga story mpaka nilipo muacha dogo,, akampa hongera kwa kukuza mwali akatoa noti ta elfu kumi akampa mtoto kama zawadi basi akaniomba anamba ya simu sa hizo mbio za kumnyima au kusema sina simu nazitoa wapi??😀 nilitaja huku nina tetemeka hatari yaan mimi na umaraya wangu wotee haki tena sijawahi kupapatikiwa na mkaka handsome boy kama huyu japo ma bwana zangu nilikuwa nawaona wazuri lakini wote kumbe miamba tu yaan sura mbaya pesa hayana kunisumbua tu akili aah🙌
Basi ye akaingia getini si hao mpaka kituo cha dala dala tukapanda zetu basi mdogo wangu akawa ananitani hapoo et nimepata bwana doctor akaenda kuwaaadithia mpaka nyumbani yaan mtu hata sijatongozwa basi kunitia tu roho juu ...
Hapo muda wote natazama tu simu yangu labda takuta hata ka sms ka hi !!!

.........
Full sh 1000
Njoo WhatsApp 0781858056.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

DOCTOR NITIBU NA HUKU KUNAWASHA 🌹🌹❤️❤️❤️🌹 sehemu ya 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/doctor-nitibu-na-huku-kunawasha-sehemu-ya-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

GIGY MONEY DAH😭

majario rewards 100 Comments 0
 

YOUNG AFRICANS,

majario rewards 100 Comments 0
 

BAKORA VILLAGE

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 7...8

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA EPISODE 2

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE...5...6

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 3...4

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA 1

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈21

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈20

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 8

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 7

majario rewards 100 Comments 0
 

Life in a Year (2020)

majario rewards 100 Comments 0
 

Kenya, Tanzania, Congo

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 40

majario rewards 100 Comments 0
 

POSHY QUEEN:

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 39

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈19

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈18

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈17

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈16

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈15

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 05 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 04 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 03 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 02 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 01 ❤❤.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 34

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TUWASHUKURU KINA BABA

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest