Hakikisha unamfollow STORY ZA Zamrata kwa simulizi tamu na za kusisimua ......share, comment, like ...... Kwa sababu simulizi ni haki yako ndo maana uko hapa ....
SEHEMU YA 12
Baraka alitoka kwa kasi kana kwamba alikuwa anakimbia vita. Mikono yake ilishikilia gongo huku akihema na ukichululia yeye ndo kidume mule ndani, macho yamemtoka na moyo unapiga kama ngoma ya jando🤣.
Alikuwa amevaa boxer tu, akasahau hata kuvaa shati. Nywele zake zimetapakaa jasho kama mtu aliyekuwa anakimbizwa na mbwa wa kijiji.
"Nyoka yuko wapi? Nyoka yupi? Na nyoka nani? " Baraka alipaza sauti akiwa tayari kuchomoa gongo bila kuuliza mara mbili.
Aziza alijilaza sakafuni, akijifanya anatetemeka kama mtu aliyekutana na pepo akisubiri maombi ya buludozaaaaa.
Macho yake yamemtoka kama mala kaona wallet , lakini hakukuwa na hata ishara ya uwepo wa nyoka. Alikuwa kaandaa mchezo mzito wa kutibua mahaba ya chumbani.
Neema naye alitoka kwa kasi akiwa amejifunga kanga tu, uso wake ukionyesha hofu mchanganyiko na kero.
"Nyoka yuko wapi jamani!?"
Aziza alijikunja kama mtoto mchanga. "Niliona kitu cheusi kikitembea pembeni ya friji, nikapiga kelele. Samahani kama nimewasumbua... nilishtuka sana."
Baraka alitazama sakafu. Hakukuwa na hata dalili ya utelezi, wala alama ya mnyama. Alishusha pumzi kwa nguvu. "Aziza, usitufanye wajinga. Hapa hakuna nyoka, ulituamsha tu bure."
Neema alimwangalia Aziza kwa jicho la udadisi, kisha akamwambia Baraka, "Nenda kavae nguo zako kwanza. Unaonekana kama umetoka kutengeneza bomba la maji kwa mate."
Baraka aligeuka kwa aibu na kuingia chumbani. Neema akabaki akimtazama Aziza kwa macho ya mashaka.
"Wewe dada, una hakika ulikuwa umeona nyoka au ulikuwa umelala ukaota kuna nyoka ?"
Aziza alitikisa kichwa kwa aibu, "Naomba radhi dada... nadhani nilishtuka tu. Nimekuwa na mawazo sana siku hizi."
"Mawazo gani tena? Unahitaji mapumziko?"
"Hapana dada... ni hali tu ya kiakili. Itapita."
Neema hakusema mengi. Aliingia chumbani akamkuta Baraka anakaa kitandani huku akiwa amevalia bukta na tisheti.
Alimtazama kwa jicho la uchungu mchanganyiko na kujaribu kutabasamu.
" Akijisemea mpaka kitumbus changu hakitaki bakora tena ila huyu dada mandoto ya kijijini yatamuua ajue hapa ni mjini.
"Mume wangu, hivi haya mambo ya Aziza yanakuingia akilini? Maana huyu msichana sijawahi kusikia analalamika juu ya nyoka wala mawazo kabla. Leo tu ghafla?"
Baraka aling’ata ulimi wake. Alijua Aziza ametibua kila kitu. Moto wa mapenzi umezimwa kama mshumaa kwenye upepo wa ghafla.
"Wacha tumpumzishe kesho nayo siku . Tutamuacha Aende sokoni peke yake, apate hewa ya nje. Labda atakuwa sawa."
Neema alikubali hilo lakini moyo wake ukawa umeanza kuchimbika na hofu isiyo na jina. "Mwanamke akianza kuona miujiza ndani ya nyumba yako, tambua moto upo jikoni."
USIKU ULIPOFIKA
""""""""""""""""""""""""""""""
Aziza alikaa kitandani kwake akiwa hajalala. Alikuwa amevaa dera la buluu lililoambatana na kanga aliyojifunga kiunoni.
Aliweka mkono wake kifuani, akisikia moyo wake ukidunda kwa kasi ya ajabu. Kelele za mahaba alizozisikia kabla hazijatibuliwa bado zilikuwa zikicheza kichwani mwake kama muziki wa mduara.
"Baraka ni wa Neema. Lakini kama kweli moyo wake unaniwaza, kama kweli ni wa kwangu... atanifuata tu."
Aliamka na kufungua kitenge na kukiweka pembeni.kisha akatingisha ta..... Akaanza kulisasambua kisha akasema ...
"Leo nimewasha moto na nikauzima. Si kwa sababu nimedhamiria kuharibu, bali kutuma ujumbe kuwa nami nipo.
Neema hatakaa aelewe kilichofanyika leo... lakini moyo wa Baraka sasa umegawanyika Sasa Nitaamua ama anipende, ama akae mbali kabisa. Siwezi tena kuvumilia kuishikama kivuli cha mke wa mtu."
SAA MOJA ASUBUHI
""""""""""""""""""""""""""""""""""'''"""
Majira ya asubuhi alipoamka Aziza ,alifanya usafi na mwisho akawa anaosha vyombo taratibu alichukua katani. Na kuanza kuosha vyombo taratibu anapaka sabuni kwenye katani na kuvisugua vyombo huku akiimba nyimbo ya benwill - najitoa
Mtoto anasauti ambayo ilimfanya baraka aamke kitandani na kumuacha Neema aliyeonekana kachoka na mizunguko .alijifikicha macho huku akipiga miayo
Akawa anapiga hatua kuifuata sauti.alinyata mpaka jikoni kisha akasogea mpaka nyuma ya Aziza taratibu akaipitisha mikono na kushika kiuno taratibu
Alishtuka " aaaaaaaagh"
ITAENDELEA ........