Baada ya kufungua mlango😳😳 nilishtuka kumkuta mzee amos ndo yupo mbele ya mlango wangu ,nusu nianguke huu mwaka mbona wangu
"Kaa...k..shikamoo " nilipata hadi kitete cha mdomo kwanza
"Marahabaaa!! Juddy yupo wapi??" Kwanza aliitikia kama kanisusia vile ,akaniuliza huku amenikazia macho🥺"
"Mi sijui!!!" nikamjibu bila hata wasi wasi"
"We ndo ulikuwa nae mara ya mwisho, na mpaka sasa hajarudi nyumbani, na tangu lini umekuwa na amazoea na judi?? Na yupo wapi wewe ndio unajua"
Sasa aliongea sauti ya ukali ,mwili ukaanza kutetemeka walai mtu anaweza kufa ukapewa kesi ndo mimi hapa ,mbona nimechukua mitihani hivi jamani
"Mi sijuiii!!!" Nilimjibu sasa huku woga unazidi kupanda "
"Hunijui we bint, ulikuwa nae hukuwa nae" nikabaki kimyaa niseme nini ?? "
"Ulikuwa nae hukuwa naeee???" Aliniuliza kwa sauti kali mpaka akanirushia mate usoni🗣"
"Mi ..mi ..ye aliniacha pale"
"Anhaa kwahiyo ulikuwa nae??"
"Ye alikuja kuniuliza"
"Kwamba???"
Nikawa kimyaa akaniuliza tena nikabaki kimyaa alinitikisaaa hee mpaka nikataka kukimbia
"Sipendi niongee mtu yupo kimyaaa" akafoka kwa saut hata wapangaji walio kuwa ndani wakatoka niliona aibu sana
"Alikuwa anamtafuta alex mi kaondoka sijui kaenda wapii"
"Anhaaa kumbe wewe ndie kuwadi wake ,sasa utanipeleka alipo huyo alex wako" akanivuta mkono kwa nguvu mana nilikiwa nimesimama mlangoni kwangu akanivuta mbele afu akanisukuma kwa mbele yake😭😭 "
"Tangulia unioneshe alipo mly wewe unajifanya unaujua ukuwadi??" Nilijikuta machozi yanatoka , sijui mpaka sasa mie nimekosea wapii hata sielewi nini cha kufanya hapo majirani wote wananitazama mie, huyu baba anaongea kwa sauti kubwa maneno yote anamaliza haoni hata aibu jamani daah"
Nikawa napiga hatua ndogo ndogo huku nafuta machozi mana mie hata sijui nielekee wapi kwa huyo alex .
Nilikuja kushtuka nipo chini nimeanguka baada ya huyu baba kunisukuma kwa nguvu et nitembee haraka😭😭 .....
nilianguka chini halafu kulikuwa na tope ,Roho iliniuma nikatamani kulia kwa nguvuuu
"Embu inuka haraka mly weeee" daah nilimtazama kwa uchungu nikatamani nimrukie nimuume meno ya puaa mpuzi huyu baba hajiheshimu hata kidogo"
"Bwana Amos kuna niniii??" Alitoka yule baba mwenye nyumba yetu akamkuta ananivuta pale chini kwa nguvu huku ananitokomeza maneno"
"Mtoto mpuzi yaan anamkuwadia mke wangu wanau me???" Huyu baba aliongea mkavuu hata aibu hanaa et juddy mke wake jamani ajabu afu li baba kubwaa watoto wake wengine wapo sawa na huyo Judy"
"Salma mama shida ???" Baba mwenye nyumba aliniuliza huku ananipa mkono kuinuka pale chini ,nikainuka najifuta futa matope yaan hata sielewi nini cha kufanya"
"Mi hata si..." nilisita kuendelea kuongea baada ya kuona kuna gari inakuja kwa kasi uelekeo ilipo nyumba yetu , ilipiga break za nguvu kila mtu akabaki anaishangaa ile gari😳😳"
Gafla ndo akashuka Alex yaan namuona Alex yuleee , sijui hata kilio kilitokea wapiii mie ,nilikiangua kilio hicho😭😭
afu nalia kwa sauti unajua ile iiiiiih iiiiih haaaa iiiih, hahaha leo nacheka kama mazuri , Alex alikuja haraka akanikumbatia vile vile na matope yangu ndo nilizidi kuliaaa😭😭
nahisi mtaa mzima ulisikia ile sauti mana watu niliona wameongezeka gafla..
"Salmaaaa shida ninii , uko sawa ?? Salmaa umeumiaa , embu ,embu nione"
Alex alikuwa amehamanika ananikagua kila sehemu ,mi nalia tu hata kuongea siwezi ,ule uchungu wotee nikahisi unataka kutokaa"
"Alex huyuu mzee ameninyanyasa mie sina hata kosaaa" nakwambia nilimshtaki huyu mzee kama mtoto mdogo😂😂afu et namshitakia kwa Alex dah🤣🤣
Tena nikanyoosha na kidole kumuonesha ,alex aligeuka akamtazama Mzee Amos ,sasa sijui alikuwa hajamjua mana alivyomtazama kama alishtuka🥵
"Mzee Amos alimrukia Alex akamuuliza wewe mpuzi hujakoma kuuzoea huu mtaa"
"Oyaa we mzeee!! Sina shida na yule mly sawa ,afu leo mara ya kwanza na iwe ya mwisho marufukuu na usije tena kumsogelea huyu mwanamke umenielewa🥺🥺"
Alex alikuwa kachefukwa🥵🥵alimtupa huko mzee amos watu wakabaki wanamcheka..
"Twende ndani" akanishika mabega ananitembeza taratibu tunaenda ndani ,mzee Amos akamvuta nyuma kwa nguvu kama Alex angekuwa lege lege yaan alikuwa anaanguka bonge la mweleka ,
shart yake ilichanika ila hakuanguka mzee amos akataka kumpiga ngumi alex akaikwepa ,baba mwenye nyumba akawahi kumvuta mzee Amos nyuma na wanaume wengine wakamvuta alex
"Kijana muhni huyu mzee ndapo acha nimfundishe adabu, anakuja kuharibu amani ya mtaa" mzee amos alikuwa anahangaika kujitoa mikononi kwa baba mwenye nyumba huku anaongea ,
"Mzee amos tafadhali sitaki balaa kwenye nyumba yangu ,naomba mkasubiriane huko nje akija ndo mpigane kwangu sitaki " baba mwenye nyumba akawa mkali ,moyoni nikasema yaan mzee amos kila mtu kashamzarau sasa hivi"
Alex akacheka tu kama kawaida yake afu akanishika mie tukaingia ndani hapo tena kile kilio kimeisha mana nilikuwa nalia kilio cha kudeka na kweli nilionewa kilio changu kilikuwa cha uchungu kweli kweli .
"Kwani imekuwajee??" Alex aliniuliza baada ya kufika ndani kabla sijamjibu aliitoa simu yangu"
"Ilikuwaje yule mpuzi akatumia simu yako??" Nikamuelezea ilivyokuwa kuanzia judy kunipigia baada ya namba yang kubaki nayo ile siku yeye amepiga , aliniomba msamaha kweli nikamwambia hata sijaona kosa lako"
"Kwahiyo ulikuwa unajua tangu mwanzo!!!?" Akaniuliza nikatikisa kichwa kukubali yaan nilikuwa najua kuhusu yeye na judy"
"Naelewa sasa, Nisamehe mie salma"
"Usijali, alex mi hata sijaona ulipo nikosea"
Moyoni nilikuwa nawaza huyu kama kaletwa na mungu kwangu dah"
Hivi ingekuwaje kama asingekuja sa hivi ningekuwa wapii mie au yule baba angefanya nini maana alikuwa na hasira na mie kweli
"Mwanamke mpuzi sana yule ,yaan anakutumia kwa nguvu ili kunipata kanikera sanaaa, Embu inuka kwanza ukaoge" alichukua kanga akanipa akachukua ndoo akaenda kuweka maji mi nikajifunga nguo nikatoa kile kijora kilikuwa na tope kweli"
"Haya inuka maji tayar" nikajikuta mpaka nacheka et maji kanipelekea bafuni , nilienda kuoga huku najichekea mwenyewe sijawai kupelekewa maji bafuni mie maisha yangu yote ilikuwa ndio mara ya kwanza .."
Nikajimwagia chap nikatoka,ile natoka bafuni nikashangaa kumkuta alex yupo pale nje anamalizia kusuhuza dera langu🥵😳lililokuwa na matope😢🥹❤️,
kwanza nilisimama hata siamini namtazama yupo bize anaanika hapo naangalia vizuri naona na blazia nayo anaikamua baada ya kuanika kijora ha ha ha nikajikuta nacheka kwa sauti et kafua mpaka bla yangu🙈🙈
"Ooh umemaliza" akaniuliza huku anakuja akachukua ndoo ile ya kuogea"
"Twenzetu"
"Sa kwanini umefua??" Nilimuuliza kwa aibu mwenzangu 🙈🙈"
"Hee nimeamua tu"
"Bwana usingefua ningefua tu mwenyewe "
"Au ndo unataka nitoe zote kabisa nikafue sasa hiviii??"
Tukawa tunacheka hapo teyar tupo ndani nishasahau yaliyotokea dakika chache nilikuwa natamani nimuulize imekuwaje baada ya kuonana na Juddy mpaka akaichukua simu yangu afu akaja nyumbani kwangu ila nahofia kuwa mbea akuu nikamezea tu . .
"Umekula??"
"Aisee ndo nakumbuka hapa leo sijala hata"
"Haya inuka huwezi kulala bila kula"
"Usiku sa hizi magenge yashafungwa"
Mi tena na kuwawaza mama ntilie ,huo muda ulikuwa kama sa 6 kasoro hivi akanambia we inuka lazima ule ,
Na kijora changu akanifungulia mlango wa gari nakwambia mie huyu salma sijawahi kupanda gari kali kali kama hizi mie na dala dala zangu maisha yanaenda .
Tulitoka safari ilienda kuishia mbali mbali huko na nyumbani, Ilikuwa ni sehemu ya chakula pamechangamka mpaka raha waweza sema sa mbili usiku kumbe sa sita hiyo na dakika zake tayari
Kulikuwa na wazungu wengi wanakula yaan pakishua sio poa watu wamependeza afu mie nina kijora jamani😂😂
Baada tu ya kukaa akaja muhudumu akatukaribisha vizuri tu mie tena hata sielewi natoa tu macho sio poa
"Kuna nini hapa??" Alex akauliza huku anamtazama yule dada usoni , yule dada hakujibu kwa mdomo alitoa kitabu kilichokuwa kimeandikwa akampa ,alex nae akanipa mie"
"Angalia hapo utapendelea kula nini??" Mie kusoma sijui ,nikawaza hapa nafanya nini afu si nilimwambia mie kusoma sijui huyu kaka au ??
Nikampa ile kitabu mbele ya yule dada"
"Kwani sikukuambia mie sijui kusomaa??" Nilimwambia huku namrudishia ,Alex akaanza kucheka kama kawaida yake"
"Okay dada embu tupe maziwa na pizza usisahau sosej ...ooh embu njoo embu weka na Catless sawa eeh "
Yule muhudumu akawa ameondoka, mi nikawa zangu bize kubinya binya vidole vyangu, nimeinama tu chini,
nilihisi kama naangaliwa sanaaa nikainua macho ,Alex alikuwa ananitazama afu uso wake ulikuwa makini kweli juu yangu ,nikajikuta nina babaisha macho yangu
Tulipo kutanisha macho akatabasamu afu akaniuliza ...."
Itaendeleaaaaaa
KWETU morogoro.